mlanguzi
Senior Member
- Jul 15, 2012
- 181
- 10
TUCTA nao wamo
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (Tucta) limelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtu anayedaiwa kumteka na kumpiga kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dk Steven Ulimboka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kuwa, hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo inaleta matumaini ya kuwabaini watu wengine waliohusika na vitendo hivyo, jambo ambalo linaweza kurahisisha uchunguzi.
Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuendelea na uchunguzi ili waweze kuwabaini wahusika wengine na kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambalo limesababisha kutokea kwa hisia tofauti katika jamii.
"Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi ili waweze kuwabaini watuhumiwa wengine na kuwachukulia hatua za kisheria," alisema Mgaya.
SOURCE: MWANANCHI