Jeshi la Polisi lipongezwe kwa kazi nzuri kwa Dk. Ulimboka ~ Nicholaus Mgaya

mlanguzi

Senior Member
Jul 15, 2012
181
10
TUCTA nao wamo
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (Tucta) limelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtu anayedaiwa kumteka na kumpiga kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dk Steven Ulimboka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kuwa, hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo inaleta matumaini ya kuwabaini watu wengine waliohusika na vitendo hivyo, jambo ambalo linaweza kurahisisha uchunguzi.

Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuendelea na uchunguzi ili waweze kuwabaini wahusika wengine na kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambalo limesababisha kutokea kwa hisia tofauti katika jamii.

"Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi ili waweze kuwabaini watuhumiwa wengine na kuwachukulia hatua za kisheria," alisema Mgaya.

SOURCE: MWANANCHI
 
Mgaya asifikiri kwa kuwa ni kiongozi wa wafanyakazi basi ataaminika kwa kauli hiyo ya kipuuzi, hiyo ni kauli yake haihusiani na kauli ya chama, tangu apigwe mkwara na JK pale alipoitisha mgomo wa wafanyakazi amekuwa mpole na mjinga kiasi kikubwa na hapo alipo ana kadi ya CCM kwa lengo la kugombea Ubunge naomba hilo jimbo analotaka kugombea wamuogope kama Ukoma kwani ni mnafiki hasiye faa kuwa kiongozi na naomba watumishi wa TUCTA wajiunge kwa pamoja ili kumuondoa mtu huyu.
 
I remember the great, late Rwegasira who unlike Mgaya and Mukoba was walking the talks.

Hawa ni vinyonga (chameleons) watupu.
 
namshangaa mgaya kujikosha naona huyu achunguzwe uwezo wake wa ku baini uongo na ukweli ,anaona maiguzo kuwa ni kweli watanzania wa leo si wakuletea maigizo kama haya ,huyo anayedaiwa kumtemka Dr Uli kama ametubu awtaje walomtuma ,ama anataka kutuambia kwamba Dr Uli ndiye mtu wa kwanza kwa yeye kutaka ku muua si uongo mtupu,wangapi amewaua kwa nini hakutubu huko kenya .mgaya huna jipya
 
I remember the great, late Rwegasira who unlike Mgaya and Mukoba was walking the talks.

Hawa ni vinyonga (chameleons) watupu.

Kwenye red: Nini kilimuua huyo bwana?

As for Mgaya, once a traitor always a traitor. I hope anapata usingizi usiku.
 
Naye katibu wa Tucta ni sehemu ya tatizo. Kama siyo udhaifu wake hayo yasingetokea na watumishi tusingekuwa tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi, {laki mbili na milioni ishirini}? Hastahili Kuwa katibu wa Tucta kwani maisha magumu kwa watumishi yanazidi yeye akiwa ndiye mtendaji mkuu wa shirikisho la wafanyakazi. Mgaya yeye badala ya kuwa mtetezi wa wafanyakazi amekuwa mtetezi wa serikali. Hatuoni juhudi zake kuwatetea watumishi.
 
Mgaya,plze nenda Milembe kisha ndo urudi uanze kuumba maneno kama utakavyo!!! inatia kichefuchefu na hasira sana!!! Hivi unafikiri umma wa Watanzania wa leo hii wanadanganyika kirahisi hivyooo!!!
 
TUCTA nao wamo
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (Tucta) limelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtu anayedaiwa kumteka na kumpiga kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dk Steven Ulimboka.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kuwa, hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo inaleta matumaini ya kuwabaini watu wengine waliohusika na vitendo hivyo, jambo ambalo linaweza kurahisisha uchunguzi.
Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuendelea na uchunguzi ili waweze kuwabaini wahusika wengine na kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambalo limesababisha kutokea kwa hisia tofauti katika jamii.
“Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi ili waweze kuwabaini watuhumiwa wengine na kuwachukulia hatua za kisheria,” alisema Mgaya.

SOURCE: MWANANCHI

Huu ni uthibitisho kuwa vyama vya wafanyakazi vinatumiwa na TIS au UWT. Haiwezekani kiongozi mkuu wa shirikisho la wafanyakazi kusifia sinema ya polisi kuhusu aliyehusika na utekaji na utesaji wa dr. Ulimboka. Kama Mgaya anasifia uchafu wa jeshi la polisi na UWT, nakubaliana naye.
 
Huu ni upuuzi.
Watu hawapongezwi kwa kufanya kazi waliyo ajiriwa kuifanya.

Mkuu Msalambwe,
Polisi hawajafanya kazi waliyopaswa kuifanya kwa kutumia kodi ya wananchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa umma. Polisi wamefanya kazi waliyopewa na watawala dhaifu; ambao wameshindwa kudumisha utawala wa sheria badala yake wamegeuka watesaji na wauaji.
 
Mgaya is a puppet, hypocrite, bribed long ago, lier, evil,
he was/is/will not working for workers union INTERESTS....
wanakula na serikali kikombe kimoja... hafai... tumpuuze...
mgaya has expired long ago, hulishwa fedha... na kufunga mdomo... utafikiri hajui namna Dr. Uli alivyo tekwa na police & serikali inahusika 100%, hovyo kabisa
 
Mgaya is a puppet, hypocrite, bribed long ago, lier, evil,
he was/is/will not working for workers union INTERESTS....
wanakula na serikali kikombe kimoja... hafai... tumpuuze...
mgaya has expired long ago, hulishwa fedha... na kufunga mdomo... utafikiri hajui namna Dr. Uli alivyo tekwa na police & serikali inahusika 100%, hovyo kabisa
Hii ni comment yake Kama Mgaya au ndiyo maoni Kama kiongozi wa tucta?
 
Mgaya akiyasoma magazeti ya kesho sijui atakavyojisikia. Akiendelea kuwapongeza hawa majambazi wa Mwema nitaamini naye ni mwanasiasa
 
Utalipongezaje jeshi la polisi? Wewe ukitimiza majukumu yako nani hua anakupongeza?
Msaliti wa wafanyakazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom