Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30

nchi hii kuna tatizo la investment economics .... huu mradi haukufanyiwa investment/project appraisal ... miradi mingi haifanyiwi appraisal

ujinga uliofanyika ni kufanya market reseach ambayo ilionesha kunaa wamachinga wengi sana na watakuwa ndiyo wateja

swali ambalo hawakujiuliza ambalo lipo kwenye investment appraisal ni.. je wakijenga machinga complex wamachinga watakwenda kukodisha sehemu za biashara katika jengo hilo? ... kama hapana ... je nikwanini hapana?
 
Katika hizo gharama za ujenzi viongozi wa jiji walikula kiasi gani? Haya ni matokea ya wakubwa kushinikiza miradi ambayo haina faida ulaji ulianzia NSSF hadi jiji; ukweli kabla mkopo haujatolewa NSSF waliupitia mradi ili kuona namna gani wataweza kurudisha pesa zao ulaji uliwafanya wafumbe.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.
ritz kama vya kufugia paka!

Duh hela yanguuuu! Mimi ni mwanachama wa NSSF hivyo hiyo ni hela yangu.
 
Last edited by a moderator:
Kwanini jiji isifumee vizimba vyote na wajenge kama apartment? Kupangisha apartment,vyumba viwili,jiko,sebule,na choo ambayo mtu anaweza kulipa laki tatu!
 
Katika hizo gharama za ujenzi viongozi wa jiji walikula kiasi gani? Haya ni matokea ya wakubwa kushinikiza miradi ambayo haina faida ulaji ulianzia NSSF hadi jiji; ukweli kabla mkopo haujatolewa NSSF waliupitia mradi ili kuona namna gani wataweza kurudisha pesa zao ulaji uliwafanya wafumbe.

Chama
Gongo la Mboto DSM
chama amini usiamini huenda gharama za mradi huo ni robo tu ya gharama ambazo tunaambiwa. Nchi hii imefika pabaya.
 
Last edited by a moderator:
White Elephant ili jengwa kukidhi matakwa ya kisiasa,pension za watu zinagaragazwa tu......Copy and Paste Mbaya sana.

Mytake:Needs Assessment ni muhimu sana katika issue kama Machinga Complex coz haiishii Kuweka Stucture tu inambatana na mambo mengine.
 
Lile jengo ni monument to ulevi wa madaraka!

Mtu aliyeshauri lijengwe soko ambalo wamachinga watawekwa na wateja wawafuate ni mtu ambaye haelewi ABC ya biashara

Watu wananunua vitu kutoka kwa wamachinga siyo kwa sababu ni wamachinga, bali kwa sababu machinga anakuletea bidhaa mahali ulipo. Inaweza ikawa wakati uko kwenye foleni ya magari, au wakati unapata soda mbili tatu pale Nguruko, na hata wakati uko nyumbani kwako umekaa barazani. Hili ni hitaji lililo endelevu na ambalo limefanya hata hii dhana ya umachinga ikaweza kudumu - vinginevyo kusingekuwa na hitajio, ingekufa kifo cha kawaida.

Sasa unapowachukua wamachinga na kuwaweka pale Ilala, hivi kweli kuna mteja gani atayeondoka nyumbani kwake, apite maduka yote ya maana, apite magulio yote, apite Mlimamni City, halafu aende pale Ilala, ambapo anauhakika kuwa watamvunjia gari lake akilipaki eti akanunue sticker ya Arsenal?
 
Hiyo ni bad investment na waliobuni huo mradi walipishwe hiyo hela, huko ndiko kuwajibika,hakuna kingine. The least they could do ni ku-redesign kituo kimoja kiikubwa cha mabasi na kueka small-scale departmental shopping centres , isingejalisha how big the investment is, because after 20 years I am pretty sure mradi ungeshajilipa. Hii nchi ina mijitu ya ajabu sana.
 
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.

Ritz Ukisikia uvivu wa Viongozi kufikiria ndiyo hule.....hivi ukiwauliza hao waliotengeneza hivyo vizimba waliwasiliana na hao wamachinga kama walikuwa wanavihitaji au lah!utasikia.
 
sera mbovu za ccm utazijua tu. Bilioni 12 si zilitosha kuboresha miundombinu katika baadhi ya vijiji na kuwafanya vijana kubaki huko wajiajiri? Hata hivyo bado hawajachelewa wala kupata hasara. Lile jengo walibadili kwa kuliwekea parking za kukodisha pamoja na ofisi na kumbi za kukodisha. Hiyyo biashara ya machinga haitakaa ifanyike hapo kwa ufanisi.

Tatizo haki haikutendeka ktk kuvigawa kwani walipewa wenye nazo na mwisho wake wakavifungia wakisubiri biashara ichangamke ili waje kuvifungua kumbe ndo yazidi kudorora na sasa inakula kwa manispaa badala ya kuchukua maamuzi ya haraka ya kuwapatia ambao wangepaendeleza na sasa pangekuwa pamezoeleweka na wanunuzi, tatizo la yote ufisadi
 
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?

Na mimi nimejiuliza sana hili swali. Maanake ni kama hawana strategy. Wanasubiri wanasiasa wawaamulie halafu wanapeleka pesa zetu kwenye miradi ya ajabu.

Kwenye nchi zilizoendelea, hii mifuko huwekeza kwenye Amana na Hisa tu, period. Na hata hizo hisa ni ambazo zimethaminiwa na ma-analyst kuwa zinalipa. Siyo kusubiri busara za mwanasiasa
 
Hii 'movie' kama naiona inapoelekea vile! Jiji 'wanashindwa' kulipa mkopo, NSSF wanaamua kuuza hilo jengo pamoja na mali nyingine za jiji zilizowekwa kama collateral, waliofanya jiji lishindwe kulipa wanajitokeza kununua majengo na mali hizo kwa bei wanayotaka kwa kutumia pesa ya mkopo kutoka NSSF tena! . Dili limekamilika. Jiji limepoteza na NSSF pia inapoteza kwa kushindwa ku recover sehemu ya mkopo na riba! Maisha yanaendelea. Nani kasema bongo si tambarare!!!!!?
 
here we go again .... mwanakijiji vs NSSF ... Dr. Dau kakufanya nini..?

Mkuu Njiwa hata Mwanakijiji akisema kweli wewe unaona ni bifu? Hizo ni hela za walalahoi wa tz lazima zihojiwe. Natamani itungwe sheria itakayofanya kujiunga na hii mifuko isiwe lazima ila hiyari maana inaonekana imekuwa magenge ya wezi tu wanaoiba kupitia miradi ambayo wachangiaji wa fedha hizo hawapati faida yoyote. Wakurugenzi wa mifuko hii wanaishi katika dimbwi la utajiri huku wanachama wao wakikosa mlo wa siku!
 
Ritz Ukisikia uvivu wa Viongozi kufikiria ndiyo hule.....hivi ukiwauliza hao waliotengeneza hivyo vizimba waliwasiliana na hao wamachinga kama walikuwa wanavihitaji au lah!utasikia.
Ahadi ni majengo matano mengine kama hayo ktk mikoa mingine mikubwa !
 
uwekezaji mwingi wa vitu vya umma siasa inatangulia maslahi na hii ndio shida. uwekezaji wa ujenzi wa gharama ile kwa kutegemea kodi ya 60,000 kwa kizimba ndio ilipe deni pamoja na riba haiwezekani. ni muhimu mifuko hii inayotumia fedha zetu ktk uwekezaji usio na tija isimammiwe na chombo huru kischo na mrengo wa kisiasa. la sivyo itakuwa ni kuridhisha wakubwa tu au kutumika kisiasa
 
Inaongozwa na utashi wa kisiasa na ushkaji.....

Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?
 
Kimahesabu kwa wapangaji 5000 @TShs 60,000= 300,000,000 kwa mwezi hii inafanya jumla ya TShs. 3.6 billion kwa mwaka. Assume gharama za kusimamia jengo ni 10% i.e. 30,000,000 Halmashauri ya Jiji ina uwezo wa kulipa si chini ya TShs. 250,000,000 kwa mwezi.

Deni linalipika ndani ya miaka kumi; unless pesa zinaingizwa kwenye kulipana posho.
 
Hii 'movie' kama naiona inapoelekea vile! Jiji 'wanashindwa' kulipa mkopo, NSSF wanaamua kuuza hilo jengo pamoja na mali nyingine za jiji zilizowekwa kama collateral, waliofanya jiji lishindwe kulipa wanajitokeza kununua majengo na mali hizo kwa bei wanayotaka kwa kutumia pesa ya mkopo kutoka NSSF tena! . Dili limekamilika. Jiji limepoteza na NSSF pia inapoteza kwa kushindwa ku recover sehemu ya mkopo na riba! Maisha yanaendelea. Nani kasema bongo si tambarare!!!!!?

Great Thinker, na utasikia Manji ameshinda tenda na ananunua jengo hilo na mali nyingine ... Lakini sidhani kama hili ndio ilikuwa nia yao! NSSF huenda ilikuwa na nia njema kabisa na wamachinga, tatizo wale walopewa vile vibanda sio wamachinga, na ukifuatilia sana utaona, kibaya zaidi wameshindwa kufanya biashara pale lakini hawataki kupaachia. hii ndio Bongo. Lakini pia wakati umefika sasa wa NSSF kufanya Analysis kwanza kabla ya kukurupuka. kama ulivosema hapo juu, ni kununua HISA za makampuni ENDELEVU na sio ya kubabaisha baada ya muda yanakufa, kuna Treasury Bills na Bonds za Benki Kuu kila siku tunasikia zinauzw akwanini hawawekezi huko na kuna riba nzuri tu, kuna mabenki yente uhakika yamejaa kila kona na sometimes wana overnight interest rate ya 27% wanatakiwa watafute Treasury na kuna Systems sasa hivi ambazo zinaweza kuwasaidia kuwa online kwenye deals ,... hivi ndio vitu vinatakiwa vifanywe na NSSF, sio ofisi za Bunge, Chuo cha Dodoma, MAchinga Complex, what if wakishindwa kulipa hayo madeni CHENJI YETU TUTAIPATAJE TUKISTAAFU.
 
Kimahesabu kwa wapangaji 5000 @TShs 60,000= 300,000,000 kwa mwezi hii inafanya jumla ya TShs. 3.6 billion kwa mwaka. Assume gharama za kusimamia jengo ni 10% i.e. 30,000,000 Halmashauri ya Jiji ina uwezo wa kulipa si chini ya TShs. 250,000,000 kwa mwezi.

Deni linalipika ndani ya miaka kumi; unless pesa zinaingizwa kwenye kulipana posho.

Uyasemayo ni kweli, tatizo vile vibanda wamepangishana wenyewe! mafisadi! kama umesoma vizuri wale wamachinga hawakupangishwa hapo! wao wameachwa pale Karume na badala yake wamepewa wenye nazo na ndio maana pamedoda hapo na hawataki kurudisha hivo vibanda.
 
Back
Top Bottom