Rais Samia azindua Jengo la Kitega Uchumi Pemba, leo Januari 9, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation - Pemba visiwani Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima wa karafuu kuacha kuchepusha na kuza kwa magendo zao la karafuu.

Rais Samia amesema hayo leo mara baada ya kufungua jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation (ZSTC) Chake Chake kisiwani Pemba.

Aidha, Rais Samia amesema serikali inatarajia kuleta wawekezaji wa zao la karafuu ili kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao hilo katika soko la dunia.

Rais Samia pia amewataka wakulima kuendelea kulima karafuu kwa wingi na kwa tija zaidi ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuinua uchumi wa buluu.

Vile vile, Rais Samia amesema serikali itaendelea kutafuta fursa za kuongeza tija na uzalishaji bila kuathiri viwango na thamani ya karafuu katika soko la kimataifa.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa ZSTC kutatua kero za wakulima pamoja na kuwa na kanzidata ili kutunza kumbukumbu za zao hilo na wakulima zitakazowezesha kuratibu mipango endelevu.

Hali kadhalika, Rais Samia amewataka ZSTC kutumia ipasavyo jengo lililozinduliwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kukusanya mapato yatakayosaidia kujiendesha yenyewe na kupunguza gharama kwa serikali.

GDZPBsHXMAAJGvV.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba

GDZSBTZXoAAGLZ3.jpeg
Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba
GDZRAKHXgAAvU-v.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma ya Kibati ikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi
 
Back
Top Bottom