NSSF yalipa mafao ya bilioni 56 kwa Miezi 6

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umelipa shilingi bilioni 56.689 kama mafao ya wastaafu katika kipindi cha miezi sita iliyoanzia mwezi Julai mpaka Disemba 2023.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omari Mziya amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Makao Makuu ya NSSF, Jengo la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, amesema Mfuko umeandaa mpango mahususi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wanachama na tayari mpango huo unaendelea kutekelezwa kwenye ofisi mbalimbali za NSSF kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

Bw. Mziya amesema NSSF inawathamini wanachama wake, hivyo inawaomba waajiri wote wa sekta binafsi kutimiza wajibu wao kwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kila mwezi ili kuwaondolea usumbufu watakapostaafu waweze kulipwa mafao yao kwa wakati.

Amesema Mfuko unaendelea kulipa pensheni kwa wastaafu, ambapo katika kipindi cha mwezi Januari 2024, imelipa shilingi bilioni 9.93.

Amebainisha kuwa Mfuko upo katika zoezi la uhakiki wastaafu ambalo lilianza tarehe 1 Februari na litaendelea mpaka tarehe 30 Aprili, 2024, ambapo alitoa wito kwa wastaafu na wategemezi kutumia kipindi hiki kufanya uhakiki kwenye ofisi zote za NSSF zilizopo Tanzania Bara na waliopo Zanzibar wafike katika ofisi za ZSSF.
 
Back
Top Bottom