MWANA WA UFALME
JF-Expert Member
- Sep 10, 2010
- 578
- 144
Kwani hapakuwa na business plan. In modern society hivi bado kuna kampuni zinafanya biashara za kombolela.
Mnapiga makelele bureee kuhusu NSSF lakini kulingana na hali ya Dra sasa hivi NSSF ndiye ataibuka mshindi. Jengo lile halikujengwa vibaya bali wamegawa vipande ambavyo hata kuviondoa haitawagharimu kiasi kikubwa. Jengo hilo linaweza kubadilishwa na kuwa Mall au hata ofisi za mashirka binafsi na kadhalika, hivyo NSSF wamejipatia kiwanja na jengo bila hata kutoka jasho. Hasara ni kwa manispaa ya Ilala, hii inaonyesha uongozi mbaya wa Manispaa hiyo kujiingiza na kubariki swala la Umachinga.
Walichotakiwa wao kujiuliza ni kwa nini vijana wengi wamechukua Umachinga kama njia ya kujipatia ajira na wataweza vipi kupambana na Umachinga ikiw ni kero kwa Taifa naq vijana wenyewe. Hivyo, kilichotakiwa ni kupambana na nacho na sio kukipa uwezo zaidi. Kwanza, ni manispaa kuzalisha kazi nyinginezo ambazo zinaleta maendeleo zaidi kwa manispaa na vijana wenyewe.
Pili, wananchi wengi wanapenda kununua mali zao kwa Machinga kwa sababu hakuna sehemu moja kama Mall ambayo unaweza kupata kila kitu ukitakacho. Na kutokana na msululu wa magari Dar, traffic jam mtu huwezi kwenda mjini ukapata kila kitu, huwezi kwenda Kariakoo ukapata kila kitu, huwezi kwenda soko la Ilala ukapata kila kitu lakini unaweza pata vitu vingi kwa machinga barabani wakati ukielekea nyumbani au kazini..
Suluhisho ni kujenga Malls au sunday market kila manispaa ambapo wafanyabiashara wenye maduka ya vitu vya Machinga ndio wapewe sehemu hizo za duka ili kurahisisha wanunuzi kuweza kwenda jengo moja na kupata vitu vyote wavitakavyo.. One stop shopping waingereza wanasema. Na hao Machinga, wapeni kazi ya kusimamia parking za magari, kusafisha barabara, kuweka matangazo, kuchimba mitaro na kadhalika.. Ni muhimu kwa manispaa kufikiria kazi za kuwawezesha vijana wao waondokane na Umachinga na sio kuwabariki ktk umachinga..
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?
Huu sio "uwekezaji" wa NSSF, bali mkopo, liability ya NSSF iko hedged with collateral ya ardhi ya Jiji.tumeona issue ya uwekezaji wa NSSF Dodoma na huku kwingine; nadhani watu wanatakiwa kuwa waangalifu hasa mifuko hii inaposukumizwa kuwekeza
Huu sio "uwekezaji" wa NSSF, bali mkopo, liability ya NSSF iko hedged with collateral ya ardhi ya Jiji.
Kwenye "uwekezaji" the capital is not collateralized.
Lets get the issues right, please.
wrong. Serikali inasema ni uwekezaji! au hujasoma ripoti ya CAG uone wanavyopishana kati ya Serikali na NSSF. Ingekuwa mkono kungekuwa na mkataba wenye kusema hivyo...
Mwanakijiji na wengine humu mimi naomba kuuliza:
Hivi yule kijana wake Dau hapa JF yuko wapi siku hizi?
here we go again .... mwanakijiji vs NSSF ... Dr. Dau kakufanya nini..?
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?