je wanafunzi walioandika matusi kwenye mitihan ya taifa wanastahili adhabu ya miaka 3?

thinka

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
334
148
Ni kwel kitendo walichokifanya hawa wanafunzi sio cha kuvumilia lakin je hii adhabu ya kufungiwa miaka mitatu hawa wanafunzi itawajenga au ndo itazidi kuwabomoa?
 
Ni kwel kitendo walichokifanya hawa wanafunzi sio cha kuvumilia lakin je hii adhabu ya kufungiwa miaka mitatu hawa wanafunzi itawajenga au ndo itazidi kuwabomoa?

Itawajenga!!Lakini inabidi wakipimwe akili zao kama hazijapungua!
 
wacha iwabomoe katika kundi kubwa la wanafunzi wakikosa wao hakuna hasara.hawana adabu.
 
Hahaha! Na kweli kufeli kwao tu haitoshi, kunahitajika discipline aisee. Sasa hata wa vyuo vikuu wasije wakaanza kuandika matusi wakiona ngoma imebamba!
 
nadhani hao watoto walidhamiria kutukana na kuandika madudu kwenye mitihani .. je unadhani baada ya miaka minne wameandika madudu hayo sasa hata kama ukiwapa mwaka hawawezi kubadilika ... kwa maana nyingine tukubali hatuna kitu cha maana kwa hao watoto
 
Inawafa,hawa epiq nation generatio wajinga kweli
Ni kwel kitendo walichokifanya hawa wanafunzi sio cha kuvumilia lakin je hii adhabu ya kufungiwa miaka mitatu hawa wanafunzi itawajenga au ndo itazidi kuwabomoa?
 
hii adhabu inawafaa, si rahisi kwa mtoto hasiyejua anachofanya akabadilika kwa siku mmoja, acha wakae kwanza miaka mitatu na wapate muda wa kusoma then watafanya mitihani
 
kuna tofauti gani kwa aliyeandika bongo flava kwenye mtihani na aliyepata division 0.bora aliyeshusha mistari akamburudisha msahihishaji kuliko aliyeandika madudu na mwishowe akaangukia 0
 
kuna tofauti gani kwa aliyeandika bongo flava kwenye mtihani na aliyepata division 0.bora aliyeshusha mistari akamburudisha msahihishaji kuliko aliyeandika madudu na mwishowe akaangukia 0

mhh malimwengu ya walimwengu makubwa.
 
Hiyo adhabu inawafaa kabisa ila adhabu iongezekeke kidogo, wapelekwe jela angalau miezi sita, siku anaingia anachapwa viboko 6 na siku anatoka anapokea vingine 6, hakika hatakaa arudie na itakuwa fundisho kwa wengine wanaofikiria kufanya hivyo
 
waloandika bongo fleva serikali iwasaidie kuendeleza kipaji chao.
MP.
 
Sema tatizo la Nchi kama ya TZ ni kukosa utawala wa sheria na kutoa updates kwa wananchi, Kwa kweli tumesikia kupitia baadhi ya vyombo vya habari kuhusu hili swala ila jambo la kusikitisha nimkwamba adhabu waliyopewa niu ndogo sana wala haiendani na kosa walilolifanya. Hivyo ingetakiwa angalau wapigwe jela miaka mitano na adhabu zao ziwe zinaonyeshwa kwa Wanafunzi wenzao ili waew ni mfano bora wa kuigwa na jamii inayowazunguka.
 
kuna tofauti gani kwa aliyeandika bongo flava kwenye mtihani na aliyepata division 0.bora aliyeshusha mistari akamburudisha msahihishaji kuliko aliyeandika madudu na mwishowe akaangukia 0
hili nalo neno maana wote wamefeli
 
kufutiwatu matokeo niadhabu tosha maana ataendelea nachuo gani?labda madarasa au sundayschools,hapo ramani yao yakuajiriwa imekufa mwishowe wataishia uchangudoa na ujambazi
 
Back
Top Bottom