MwanaKijiji hii ina ukweli ndani yake.
Angalia TRA wamejaa wachagga kweli na wanapendeleana kweli ukienda mzaramu au msukuma na aende mchagga utaona wewe utakavyo kadiriwa kodi ni tofauti na mchagga.
Hata ukikuta mwalimu mchagga atapendelea mchagga naona ndio mafunzo ya kichagga kupendeleana.
Hii ina ukweli chunguzeni.
Mungu hana upendeleo hata kidogoSisi wachagga tunaapa: Tutaendelea kukamata nafasi nyeti serikalini, kwenye siasa, kwenye mashirika ya uma na ya watu binafsi, Tutaendelea kukamata Elimu nzuri, Tutaendelea kuongoza kwenye biashara, Tutaendelea kuoa/kuolewa na watu wenye madaraka makubwa serikalini na kwenye taasisi nyeti, Tutaendelea kujipendelea kila inapowezekana.
Hakuna mtu wa kutuzuia kwa kuwa tumedhamiria na hatutarudi nyuma.
Ahsante Mungu kwa kutupendelea na kuendelea kutubariki.
Wenye wivu na Wajinyonge, lakini Mungu awasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo.
Amina.
A MODEST PROPOSAL
Na. M. M. Mwanakijiji
Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.
Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.
Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.
Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".
Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.
Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.
Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.
Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.
Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.
Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.
Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.
Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.
Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.
Well said kiongozi. Waambie watu waache kulialia hovyo. Waamke wachape kazi.Mwanakijiji; yawezekana wewe ukawa tatizo namba moja. Umewezaje kulitolea jibu swali ambalo halipo au umelianzisha mwenyewe, ukalijadili na kulitolea ushauri mwenyewe! Huo ni upembuzi wa level gani?
By the way huwezi ukamwachia mzembe kiutendaji au ukaachia nafasi ya kazi kwa goigoi ambaye hata sababu za msingi hakuna -eti kujenga mshikamano! Mshikamano upi hasa? Wanaoogopa kujiendeleza waje wasubirie kuachiwa nafasi na wachagga wanaotaka kuendeleza mshikamano?
Wanaoanzisha watoto madrassa na kuwachelewesha kusoma lugha zisizolenga kumpa upanuzi wa akili ndio unashauri wachagga wawaachie nafasi kuimarisha mshikamano na ndio hao hao wanaotangaza kuwa serikali imekuwa ikiwapa nafasi wakristu, hoja ambazo hazina tija?...na pia unataka wachagga waache kusoma au kujiendeleza kwa kuogopa kuja kuambiwa 'wengi wamesoma na hivyo inabidi wawaachie wengine nafasi'?
Na wachaga watakapoacha kujiendeleza au waache kusoma ili ku-balance na waliofanya uzembe kujiendeleza au pale ambapo serikali imezembea kuwaendelea, kwa maana yako - unataka nchi nzima watu wake wote warudi hatua nyuma, wenye elimu warudi nyuma, wasitende kazi ili ku-neutralize perception ya wachache kuwa wataonekana wapo wengi maeneo ya kazi! Huo ni upofu, na dalili za kuelekea kupungukiwa ktk judgement na arguments.
Katika nchi yoyote duniani, hata Marekani, Ufaransa, UK, Canada, Israel na penginepo; kuna makundi ya jamii fulani ambazo ni lazima ziwepo na ndio msingi wa mafanikio na challenge kwa mataifa husika ikianzia na uongozi, biashara, siasa, elimu, technologia na hata maeneo ya majeshi...! Hii haikwepeki au haizuiliki.
Na kama Mwanakijiji umeshindwa kutafakari haya na kupata majibu sahihi, basi dira na mwelekeo wa ujenzi wa Taifa ni finyu au umeshindwa kuupatia mwongozo sahihi kwa nia ya kuwaelimisha wengine. Hapa unawapotosha na kuwaaminisha kuwa Wachagga na 'Uchagga' vinaelekea kuwa hoja ya kitaifa badala la mambo mengine ya msingi. Unawakengeua watanzania ambao wengi wamekombolea kutokana na mafanikio ya Kabila hili, aidha kea ajira, kibiashara, kisiasa, au aina nyingiezo za kijamii.
Kwa taarifa yako, Kisiasa, Mkoa wa Kilimanjaro na Wachagga wenyewe wameanza kujitambua hata kabla ya miaka ya 1870 hadi 1900, wachagga hawakukubali Ukoloni ukanyage ktk ardhi yao kirahisi. Hata Wakoloni walipojiimarisha maeneo mengine ya Tanganyika, ilibidi wafanye mbinu kubwa sana kuwapata watu wachache kuwaelimisha ili hatimaye waje wawtumie kama chambo ili kuingia kuwatawala, au hata kukusanya kodi, mambo ambayo pia walikwama, hadi ilipofika miaka ya 1945 hadi 1960, ndio wakifikia hatua angalau za kusema wachagga wamejigawa kuukubali uhuru wa kuongozwa toka makao makuu ya Tanganyika - enzi hizo, chini ya Governor aliyekabidhi jukumu kwa waziri mkuu Nyerere na hatimaye kuwa Rais.
Kwa dokezo hilo fupi unaweza kutambua kuwa wachagga hawajaanzia 'kuona mbele' ktk tawala hizi za awamu ya pili, ya tatu na ya nne kama unavyoliwasilisha, bali mizizi yao ipo mbali kuliko unavyodhamiria kuliweka watanzania walipokee. Kuna mamia ya Watanzania wameweka makazi Mitaa kibao ya Uingereza, Marekani, Botswana, Kenya nk, hasa utadhani ni kama wenyeji. Na wenginea wanafundisha vyuo vikuu kibao ktk nchi hizo na nyinginezo kibao. Je na hao wakirudi Tanzania utawaambiaje? Waachane na elimu na utajiri wao li wafanane na wengine ili tu kujenga mshikamano? Hapo umepotoka. Hivyo nchi haifiki popote!
Tuijadili hali hii na niliyoyadokeza, hakika tuwe na 'Critical Thinking' na sio 'superficially' -ya kijuujuu tu ili kuwapendeza tu baadhi ya watu. Tanzania inahitaji wasomi, watu wanaoweza kuzalisha, wenye skills na resources mbalimbali ktk kulikomboa taifa na sio mkusanyiko wa watu wanaopenda kuonekana maskini, wanaojirudisha nyuma au waoga, na wanaoona wengine kuwa wamefika mbali ambapo wao kamwe hawatofika - eti wamekata tamaa! Wanabaki kushikilia dhana potofu kama ukabila, udini nk..! La hasha Mwanakijiji!
Naomba kuwasilisha!
Jamani wachagga sio wafanyabiashara ni wachuuzi "petty traders" hawana mchango wowote kwenye uchumi wa nchi. Hakuna mchagga hata mmoja aliyesajiri biashara yake DSE. Hata huko serikalini wamepungua sana na wachache ndo hao akina Mgonja Kweka Mramba Masawe, wameshakuwa wateja wa akina Mkono Magafu Makani!
Mama kwenye hiyo directorate Wachagga wataruhusiwa kuomba nafasi? Je Mchagga ataruhusiwa kuwemo katika nafasi za uongozi wa hiyo directorate? Binafsi nisingependa wachagga wawemo...
Kama nimekuelewa vizuri, umeandika kwa fasihi kubwa sana ukijitahidi kuonyesha jiitihada za jamii fulani, mafanikio na wivu kutoka jamii nyingine. Mwalimu alijaribu kupunguza kasi ya [wakilimanjaro] hasa upande wa sekondari alipoondoa mtihani wa kitaifa ambao nusu ya waliofaulu walitoka mkoa huo. Nafasi zikagawiwa kimikoa, hata ile watu wasiojali elimu walipewa nafasi kujaza idadi. Wakilimanjaro wakaazisha private schools, wakiuza kahawa na ndizi wanasomesha watoto. Wale waliopata upendeleo wa bure watoto wao wakawa hawajishughulishi shuleni, matokeo yake idadi ya wanaoingia chuo kikuu ikawa inatoka kule kule katika private schools.
Ni makosa kuivuta jamii moja nyuma isubiri nyingine isiyo na hamasa. Kulalamika kuwa mchaga ni daktari haina mantiki kwasababu daktari hachaguliwii, engineer hachaguliwii wala mwanasheria au mhasibu. Hadi hapo jamii zingine zitakapoona umuhimu wa elimu na si ngoma au unyago, tuwaache waliiona mbele na watazame.
Hii ni sawa na kumwambia Mwanakijiji asisome vitabu ili asiwe na hoja kwa kumsubiri Nguruvi3 siku atakapoamua kusoma vitabu wawe sawa !!!!!
wachaga waacheni wawe juu na wazidi kuendelea-jamii zote hazwez kuwa sawa-ndio maana ujamaa ulishindikana-ukianza na wachaga leo kesho utakuja na kabila wengine-waacheni wawe juu na wazidi kuwa juu-hata mungu alisema mwenye nacho huongezewa-thus naomba wazid kuongezewa zaid na zaida modest proposal
na. M. M. Mwanakijiji
kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.
Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.
Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya kichagga.
Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "kichagga".
Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya jeshi la polisi) wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.
Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.
Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa taifa letu.
Endapo wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama uceo, ukurugenzi, ukuu wa idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa jamii ya kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima tanzania itaanza kukua katika uongozi.
Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni wachagga au wana asili ya mkoa wa kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.
Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa rombo, na wa kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao wamakua, wamwera, wa ndali, wadigo n.k katika hili wapare hawahusishwi.
Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.
Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa kichagga wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.
Katika kufanya hivyo jamii ya watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.