Je, ulishawahi kula ada ya shule/chuo? Tuambie uliirudishaje

Mimi nilikula pale MWANZA BABPTIST, sasa ishu ikawa,kulikuwa na mwalimu wa ambaye ni mzungu anaitwa Mrs Giddens..ndio alikuwa mwalim wa darasa aisee alifuatilia hadi aibu.mzee nyumbani anajua ada amemaliza nikaona nitunge uongo kwa mkuu Mwakanemela,nikamkomalia kuwa nimelipa ada yote ila sijapewa risiti...kwa ukweli .mkuu aligoma akasema hajaona ada yangu...sitasahau kabisa huo mwaka 2004,
 
Ilkuwa mwaka 2009 npo form 3 nilkuwa ada lak 3 ili niend kw Madida(afrk kusin) kusak life,nlifanikiw kufk lkn kumbe nlifka kpnd kbaya cha maandaliz y world cup kulkuw n msako wa htr,nlkamatw nkarudishw om,nikashndw kumwangalia mzee uson,ss iv napamban na vyum vy gerej
Poorly
Nililamba Tshs 45,000,nafika shule nikataka kulipa nusu,kumbe jamaa anajuana na brother,akamvutia sharubu brother.... Baada ya siku tatu nashangaa naitwa parade nikapewa zangu 12 strokes sita toka kwa Mwalimu Mkuu na sita toka kwa brother... Tangu siku hiyo,nilianza kulipa ada ya shule hata kabla sijafika shule,naenda zangu bank,nalipa zen napeleka pay slip tu....
 
Natumaini wote ni wazima wa afya

Mnamo 2005 nilipewa ada ya shule laki 8.5 nilivyoishika tu kesho yake nikaenda Ubungo nikachukua bus mpaka Kilimanjaro kwa demu wangu

Nikachukua gesti tukatumbua sana ile pesa tukaenda Arusha kula sana bata, kuja kushtuka mfukoni nina elfu 20 tu akili ikaanza kuyumba nikawa nawaza nitairudisha vipi hii ada na mpaka hapo ilikuwa bado week shule ifunguliwe.

Baada ya siku kadhaa yule demu akanipiga chini nilichanganyikiwa kupita maelezo ada nimekula, demu amenitosa na shule bila ada hakuingiliki.

Nakumbuka nilipata job K/koo kwenye duka la mhindi nilifanya kazi mwezi mmoja na nusu baada ya kupata mshaara wa kwanza 100K wiki mbili zilizofata niliuza laki 7 nikaamua kuiba pesa zote na generator moja nikauza nikarudi shule.
Nikikumbuka nacheka sana..

Vipi wewe uliwahi kupata mkasa wa kula ada ya shule/chuo?
 
Nilikula nikiwa Malangali nakumbuka, nilikula ya form five hadi six na michango yote. Dah baadae wakasema kama hujalipa ada hufanyi mock duh nilipagawa sana then baadae Mwalim nyudike alinipiaga ili Nipige mock.

Demu wangu wakati Huo alikuwa mtoto mmoja hivi Wa Filbertbay secondary.... Dah wapi mtoto Precious
 
Unanitonesha kidonda, mpaka leo sijaenda kuchukua cheti, nadaiwa 1.2M, nyumbn hawaijui hio mana walinipa. Samahan naomb niulize, hv ukiajiriwa ni lazma uwe na vyeti vyote Original? Au wanaangalia tu kile cha mwisho mfn cha chuo?
 
Kama tu unadaiwa 1.2 hiko cha chuo umekipataje???
 
Kwan kuingia chuo ni mpk uwe na chet cha 6?(nilitumia results slip), Chuo sikulipiwa ada na wazazi bali ni bodi, istoshe sijasema cha chuo nimekipata ila najua mwez wa pili kama si wa kwanza nitakipata mana hakihusiani na cha 4m6. Ila kwenye ajira ndo sijui kama lazma niwe navyo vyote au la!
 
Nilikula ada na michongo yote mwenge high school singida na mtoto mmoja mkali wa kinyaturu.2006.nimekomboa cheti juzijuzi kazini walipokomaa na uhakiki
 
Mimi nilikula ada ya format six term ya pili, nakumbuka ada ilikuwa 35000 plus 10000 ya matibabu, km 45000 hivi ila kilichonisaidia mwishoni ni mhasibu alitoroka na kitabu cha risiti akakimwagia maji, hivyo na mimi nilisema nilikuwa nimeshalipa ada jamaa alikuwa hajanipa risiti bado.
 
Habari za wakati huu wakuu,

Naamini wakati unasoma sekondari au 'level ' yoyote ya elimu uliwahi kula hela uliyopewa kwaajili ya ada. Au uliona wengi wakila ada

Kama uliwahi tushirikishe Ilikuaje? Na uliirudishaje?

Msemo wa mtaani" Kama umekula hela ya ada ni ngumu kuirudisha"

Karibuni
 
Sitakaa nisahau nikiwa form six nilikula ada halafu wakati mtihani unakaribia tukaambiwa hatutaruhusiwa kufanya paper,

Daah na hapo home siwezi sema,ikabidi niingie kijiji nikauza godoro,blanket,viatu,nguo,ndoo, maisha yalikua magumu sana mpaka kumaliza shule!
 
Ulitisha asee
 
Nilikulaga ada ya six ishu ikaja kwenye kuchukua leaving...
Nilifanya makeke fulani na Second Master wa wakati huo nikamtoa 30 tu akanipa leaving yangu maisha yakaendelea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom