Je, ulishawahi kula ada ya shule/chuo? Tuambie uliirudishaje

Nakumbuka nilikua mkoa wa mara musoma vijijini huko kuna mahala panaitwa majita uko, shule iliitwa BWASI ni ya wasabato , nikiwa form3 nilipata binti flani wa kisukuma anaitwa Elina Manyusi aisee yule binti yule,shidaaa yani mbantu haswa kiuno dondora af mzurii na macho yake ya kulembua alinikosha haswa.

Nikiwa ndio nimefika kutoka dar nilipewa ada nikalipe account yao ya NBC badala ya kumaliza transaction mapema nikajisahaulisha kuwa ile ni ada, bwana nafika musoma mjini pale nisha mpanga mtoto namsubiri pale nikafikia kuna hotel wanaita afrilux kama sijakosea ni muda kidogo,

Wakati ule ada ilikua laki 6 na 80 boarding sasa ile ndio ilikua awamu ya pili nna laki 3 na 40 na pocket money ef 50 lakini nilimaliza pesa yote kwa anasa nakuja kustuka nna ef 74,000 tu na niko kwenye BUKWAYA narudi shule huku mawazo kibao.

Aisee nilipofukuzwa ada nikarudi kijiji flani kinaitwa BUKIMA nikawa najichanganya na wavuvi niliitafuta pesa kama miezi miwili na nikafanikiwa kupata kama 275000. Nikamrudia second master wangu alinielewa vizuri na maisha ya shule yakaenda jumlisha na shida za hapa na pale kulia lia shida uwongo mwingi wa wanafunzi home wakarusha laki na nusu na nilipo clear hilo tatizo nilijifunza kuwa pesa inatafutwa kwa uchungu hivyo unaitajika umakini zaidi kwenye kuifuja
 
uon
Umenikumbusha mbali aisee, 13yrs ago nilijimegea dola 7200 nikazamia huko dunia ya kwanza. Ziliisha kabla sijapata kazi nusra nipate kichaa, nilipoteza miaka miwili bila kusoma. Ujana shida sana.
uongo mtupu
 
Nilikula ada ya Chuo nikajisemea nitailipa nikipata boom. Baadae boom linatoka na lenyewe nikalikandamiza. Kuja kujishtukia ni paper linakaribia,nilichanganyikiwa. Home huwezi kuwaambia chochote,ikabidi nimpigie uncle wangu akanitoa kidogo then nikamkamata braza angu nikamueleza ukweli akanifokea kwingi lakini alinimalizia! Siku kama mbili hivi kabla ya paper Aisee acha kabisa. Nilienda kwa Princpal kubembeleza mpaka akanikubalia kufanya paper wakati wengine washaanza kitambo,lakini niliambulia Supplementary nzito!
 
Jamani hela ya ada ni tamu sana

Sema ukishaila,huwa inakuwaga ngumu kuirudisha,,unaweza kujuta

Mimi nlishawahi kutumbua laki tano ya ada ya chuo ya semester ya pili
Niliitumbua kwa shopping tu yanii

Sema sasa nilijuta jinsi ya kuilipa kipindi cha mitihani kilipofika
Thanx to "my papuchi jamani"
Loooooooh inasaidiaga sometime

Jamani msile ada awamu hii ya tano mtatumbuliwa View attachment 422057
Inaonekana unauza,ni PM hua natoa hela nzur sana kwa makahaba huwez amin
 
mzee wangu mimi alikua ananipa ada then ananisindikiza imagine toka mwanza huko mpaka morogoro njia nzima anasoma risala mpaka kuna kipindi nilitoa pesa yote kwenye begi nikamtupia basi tu abiria wakatusihi niichukue,, mzee alikua na risala mbaya yani anakomaa hii pesa natoa kama mkopo ukipata kazi lazima kila shilingi izae shilingi.. sasa ole wako usimjibu wakati anakusomea alikua mpaka ananikaba shati eti nisaini kwenye notebook yake niji commit kwamba hiyo pesa ntairudisha,,
 
Nilikula mzigo wa form six mkwawa mpaka Leo sijalipa na vyeti sijachukua maana sekta binafsi nilipo UHAKIKI hauna nafasi na kama mtu haamini nilisoma form six basi anijibu nilifikaje chuo .
Utakuwa ulihonga au kuna mtu kwenye sistim alikuunganishia kibongobongo.
 
mzee wangu mimi alikua ananipa ada then ananisindikiza imagine toka mwanza huko mpaka morogoro njia nzima anasoma risala mpaka kuna kipindi nilitoa pesa yote kwenye begi nikamtupia basi tu abiria wakatusihi niichukue,, mzee alikua na risala mbaya yani anakomaa hii pesa natoa kama mkopo ukipata kazi lazima kila shilingi izae shilingi.. sasa ole wako usimjibu wakati anakusomea alikua mpaka ananikaba shati eti nisaini kwenye notebook yake niji commit kwamba hiyo pesa ntairudisha,,
Hahahah! Mkuu nimecheka sana,vipi ushamrudishia mzee hela yake? Vipi saini mlizotiliana?
 
Nakumbuka nilikua mkoa wa mara musoma vijijini huko kuna mahala panaitwa majita uko, shule iliitwa BWASI ni ya wasabato , nikiwa form3 nilipata binti flani wa kisukuma anaitwa Elina Manyusi aisee yule binti yule,shidaaa yani mbantu haswa kiuno dondora af mzurii na macho yake ya kulembua alinikosha haswa.

Nikiwa ndio nimefika kutoka dar nilipewa ada nikalipe account yao ya NBC badala ya kumaliza transaction mapema nikajisahaulisha kuwa ile ni ada, bwana nafika musoma mjini pale nisha mpanga mtoto namsubiri pale nikafikia kuna hotel wanaita afrilux kama sijakosea ni muda kidogo,

Wakati ule ada ilikua laki 6 na 80 boarding sasa ile ndio ilikua awamu ya pili nna laki 3 na 40 na pocket money ef 50 lakini nilimaliza pesa yote kwa anasa nakuja kustuka nna ef 74,000 tu na niko kwenye BUKWAYA narudi shule huku mawazo kibao.

Aisee nilipofukuzwa ada nikarudi kijiji flani kinaitwa BUKIMA nikawa najichanganya na wavuvi niliitafuta pesa kama miezi miwili na nikafanikiwa kupata kama 275000. Nikamrudia second master wangu alinielewa vizuri na maisha ya shule yakaenda jumlisha na shida za hapa na pale kulia lia shida uwongo mwingi wa wanafunzi home wakarusha laki na nusu na nilipo clear hilo tatizo nilijifunza kuwa pesa inatafutwa kwa uchungu hivyo unaitajika umakini zaidi kwenye kuifuja
Umenikumbusha kijiji kimoja knaitwa makojo, daaaah hilo jina lilikua linanipa shida kulitamka mkawa najua nakosea aisee
 
Nakumbuka nikiwa Mwaka wa Tatu Chuo Semetre ya 6 nilitumiwa Ada muda huo nikiwa Bar naangalia match ya Arsenal na Man U na timu yangu ikashinda,kilichotokea hapo sitasahau tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom