Je, ulishawahi kula ada ya shule/chuo? Tuambie uliirudishaje

Katika pesa ngumu kuicompensate ni ada. Ada ina laana unaweza sota mpaka mwenyewe ukaenda nyumbani kukiri.
Kila ukiwaza kwb acha niitumie nitairudishia ndio unazidi kujiweka mbal na kupata ela ya kulipia
 
Jamani hela ya ada ni tamu sana

Sema ukishaila,huwa inakuwaga ngumu kuirudisha,,unaweza kujuta

Mimi nlishawahi kutumbua laki tano ya ada ya chuo ya semester ya pili

Niliitumbua kwa shopping tu yanii

Sema sasa nilijuta jinsi ya kuilipa kipindi cha mitihani kilipofika

Thanx to "my papuchi jamani"

Loooooooh inasaidiaga sometime

Jamani msile ada awamu hii ya tano mtatumbuliwa

View attachment 422057
Papuchi Dili inajenga mpaka nyumba
 
mzee wangu mimi alikua ananipa ada then ananisindikiza imagine toka mwanza huko mpaka morogoro njia nzima anasoma risala mpaka kuna kipindi nilitoa pesa yote kwenye begi nikamtupia basi tu abiria wakatusihi niichukue,, mzee alikua na risala mbaya yani anakomaa hii pesa natoa kama mkopo ukipata kazi lazima kila shilingi izae shilingi.. sasa ole wako usimjibu wakati anakusomea alikua mpaka ananikaba shati eti nisaini kwenye notebook yake niji commit kwamba hiyo pesa ntairudisha,,
Mzee katisha
 
Nililamba Tshs 45,000,nafika shule nikataka kulipa nusu,kumbe jamaa anajuana na brother,akamvutia sharubu brother.... Baada ya siku tatu nashangaa naitwa parade nikapewa zangu 12 strokes sita toka kwa Mwalimu Mkuu na sita toka kwa brother... Tangu siku hiyo,nilianza kulipa ada ya shule hata kabla sijafika shule,naenda zangu bank,nalipa zen napeleka pay slip tu....
noma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom