Salaam, Shalom!!
Nimelazimika kupandisha mada hii baada ya kusoma comment ya mdau wa JF aitwaye Voice of Tanzania alipokuwa akichangia mada katika thread isomekayo,
Ni Lini Serikali ya CCM itanunua laptop Kwa Kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?
Nilipotoa mfano wa Nchi ndogo ya Rwanda kuweza kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata laptop za kusaidia kujifunza darasani Ili kuendana na Kasi ya mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa Elimu na teknolojia ya mawasiliano, alijibu kuwa, jambo Hilo limewezekana sababu Nchi ya Rwanda ni ndogo!!
Nilipohoji, ikiwa Udogo wa Nchi ya Rwanda ni fursa kupeleka maendeleo na mabadiliko ya kimfumo wa ELIMU nchini mwao, ikiwa nasi tutaigawa Nchi yetu vipande vidogo vidogo vyenye kulingana na ukubwa wa Rwanda, tutaweza kuwafikia na kuwapita kimaendeleo katika sekta mbalimbali, Elimu ikiwamo?
Pia, nimewahi kumsikia kiongozi mmoja mkubwa akijenga HOJA kama ya ndugu Voice of Tanzania kwamba,
Mwalimu Nyerere katika utawala wake, aliweza Kutoa chakula mashuleni na huduma nyingine kirahisi sababu tulikuwa idadi ndogo kulinganisha na sasa tumeongezeka sana.
Maswali ya kujiuliza Watanzania,
1. Je, ni Kweli ukubwa wa Nchi yetu, ni kikwazo Kwa Serikali yetu kushindwa kupeleka maendeleo Kwa haraka?
2. Je, ni Kweli wingi wetu wananchi walipakodi ni kikwazo kikuu ya Serikali yetu kushindwa kutuhudumia wananchi?
Karibuni 🙏.