Je, Ukubwa wa Nchi yetu Tanzania ni kikwazo katika kuwafikia na kuwahudumia wananchi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,619
Salaam, Shalom!!

Nimelazimika kupandisha mada hii baada ya kusoma comment ya mdau wa JF aitwaye Voice of Tanzania alipokuwa akichangia mada katika thread isomekayo,

Ni Lini Serikali ya CCM itanunua laptop Kwa Kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?

Nilipotoa mfano wa Nchi ndogo ya Rwanda kuweza kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata laptop za kusaidia kujifunza darasani Ili kuendana na Kasi ya mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa Elimu na teknolojia ya mawasiliano, alijibu kuwa, jambo Hilo limewezekana sababu Nchi ya Rwanda ni ndogo!!

Nilipohoji, ikiwa Udogo wa Nchi ya Rwanda ni fursa kupeleka maendeleo na mabadiliko ya kimfumo wa ELIMU nchini mwao, ikiwa nasi tutaigawa Nchi yetu vipande vidogo vidogo vyenye kulingana na ukubwa wa Rwanda, tutaweza kuwafikia na kuwapita kimaendeleo katika sekta mbalimbali, Elimu ikiwamo?

Pia, nimewahi kumsikia kiongozi mmoja mkubwa akijenga HOJA kama ya ndugu Voice of Tanzania kwamba,

Mwalimu Nyerere katika utawala wake, aliweza Kutoa chakula mashuleni na huduma nyingine kirahisi sababu tulikuwa idadi ndogo kulinganisha na sasa tumeongezeka sana.

Maswali ya kujiuliza Watanzania,

1. Je, ni Kweli ukubwa wa Nchi yetu, ni kikwazo Kwa Serikali yetu kushindwa kupeleka maendeleo Kwa haraka?

2. Je, ni Kweli wingi wetu wananchi walipakodi ni kikwazo kikuu ya Serikali yetu kushindwa kutuhudumia wananchi?

Karibuni 🙏.
 
Kikwazo ni chadema na vibaraka.
 
Nchi haina mipango. Inajiendea tu kama gari bovu.
Sasa nadhani nawe unaweza ona hatari ya akili ndogo kuongoza akili kubwa,

Tubadili viongozi wenye upeo mdogo wa kufikiri,

Watalitumbukiza Taifa letu shimoni tukiwa tunaona.
 
Ngumu kumeza.

Sisi ni walafi/viongozi ni walafi wanatia mdomoni chakula kingi zaidi ya uwezo wa mdomo kutafuna.

Waasisi wa Taifa Hili ni walafi pia, ndiyo maana tunaendelea kuwa walafi .

Sera na mikakati yetu ya kimaendeleo imejaa ulafi
 
Nchi ni KUBWA sana,( 900,000 plus KM za mraba), alafu hatuna bahati ya kuzichuma na kuzitumia rasimali vizuri. Tulipokuwa na idadi ya watu ndogo, tulitakiwa tusikosee Kufanya maendeleo, kama Botswana, Norway, Sweden, Finland na nyingine, lakini kwa sasa ni shida, idadi ya watu ni KUBWA, nchi ni kubwa, uongozi ni goigoi,tutateseka mpaka basi.
 
Population Sio kikwazo Cha maendeleo.
Mwalimu aliweza sababu aliachiwa pesa nyingi sana na wakoloni wakati ule ndizo alizozitumia kusaidia Uhuru nchi zingine na kupigana vita vya kagera.
Kuwapa wote laptop Sio ndio kutaboresha elimu.
Kama hizi nyimbo za kipumbavu zinaweza wafikia hadi vijijini vichakani huko, kwann wasiamue kupata Elimu bora.
Suala ni uamuzi na utashi tu wa watunga sera ndio uleta maendeleo.
Zanzibar ni ndogo mbona imeshindwa kuendelea kama Rwanda kielimu.
 
Are we really free?

Uhuru aliouleta Mwalimu ni upi?

Uhuru wa Nchi na siyo Uhuru wa wananchi?

Free to roam around but not free to think and decide for ourselves?

Tunarithishwa nini sasa, tupo hapa ulimwenguni Kwa muda kidogo Sana lakini ni muda mrefu , vIzazi na vIzazi vyetu vitakuwepo hapa. Je! Mambo Haya tunayoyaona hayafai tutawarithisha wanetu?

Tutawarithisha umaskini?

Chuki? Utumwa wa fikra?

Kufanyiwa maamuzi?

Mpaka lini ?
 
Back
Top Bottom