Mzee kinana, CCM ndio kikwazo cha upatikanaji wa katiba mpya sasa ni miaka 10 toka mchakato wananchi tunataka katiba yetu

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,488
2,340
Inashangaza sana kuona CCM haitaki kabisa kuendeleza mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya katiba inayohitajika sana na wananchi. Mchakato huu ulianzishwa na mwenyekiti wa CCM wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete na kuufikisha ktk ngazi ya bunge la katiba na mahafidhina wa CCM wakauvuruga mchakato mzima kwa sababu hawakuta katiba mpya. Leo ni mwaka wa 10 hakuna kinachoendelea juu ya katiba mpya zaidi ya visingizio vya watawala.

Hayati Magufuli yeye alisema wazi kuwa katiba mpya sio kipau mbele cha serikali yake na baya zaidi akasema hana bajeti ya katiba mpya. Mama Samia nae alipoingia wananchi tuliamini ataendeleza pale alipoishia Jakaya Kikwete badala yake akaturudisha nyuma kabisa eti wananchi wakosome elimu ya katiba kwanza jambo ambalo linashangaza sana kwani tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa ya kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya katiba na kuwapatia wananchi nakala za katiba na vipeperushi ili wajisomee. Kutokana na sababu hizo ni wazi CCM haitaki wananchi wapate katiba mpya kwani sasa ni miaka 10 hakuna kinachoendelea juu ya katiba mpya.

Wananchi tuna uelewa mpana wa katiba na ndio maana tuluweza kushiriki kutoa maoni na mapendekezo kwenye rasmu ya tume ya Warioba .

Ushauri kwa viongozi wa CCM hii nchi ni yetu sote na katiba ni ya wananchi na wananchi ndio wanataka katiba mpya

Hivyo ni kosa kwaCCM kuwacheleweshea katiba mpya wananchi.
 
Back
Top Bottom