Je, Taifa Stars ni mali ya TFF au Serikali?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,130
7,900
Unajua moja ya shida ya nchi hii ni serikali na wanasiasa kuwaonea donge watu na taasisi binafsi pale zinapoonekana kupata ushawishi, umaarufu na nguvu kuwazidi wao. Hili limekuwa ni tatizo kubwa kuliko wengi wanavyodhani au kufikiri. Matokeo yake wamekuwa wanatumia nguvu kubwa kutengeneza watu ili wakipata umaarufu wapate kuwa karibu nao huku wakiweza kuwacontrol. Pale mtu au taasisi inapochipuka ambayo haiko mikononi mwao, watajaribu kila njia kuimiliki na wakiona hawana control nayo sana, huyo mtu au taasisi ategemee mambo yake kukwama.

FIFA walifanya makusudi kabisa kutenganisha mpira na shughuli za serikali. Pamoja na kwamba ushirikiano wa serikali katika masuala ya michezo unahitajika mfano kwenye masuala ya kusaidia vibali vya wachezaji wa nje, ulinzi na usalama wakati wa mechi, nk. ili shughuli za mpira ziende, ila FIFA wanataka uendeshaji na maamuzi yanayohusiana na mpira yabaki mikononi mwa chama husika ambapo kwetu ni TFF na hili linasisitizwa kwa maslahi ya mpira wenyewe.

Tulipoambiwa serikali imejitolea kumlipia mshahara kocha Amrouche na benchi la ufundi wengi walipongeza, chawa wakashangilia tulipoambiwa kuna goli la mama ingawa cha kushangaza na kuchekesha, mbinu za kocha zimekuwa siyo kutafuta magoli bali kujilinda. Wengine tulijua haya yote yatakuja na gharama zake.

Kwa nini nimeleta mada hii?

Kwa serikali kuonea gere umaarufu wa timu za Simba na Yanga na kujaribu kupenya huko ingawa kelele huwa zinaibuka pale wanasiasa wanapozidisha, serikali ni kama imeamua kugeukia timu ya taifa kwa mgongo wa kuwa ni "timu ya taifa" kwa hiyo wana mamlaka nayo. Hili nataka kuwakumbusha siyo sahihi na litakuja kuwa na matokeo mabaya huko mbele. Kuna maamuzi yanaweza kufanywa au yanafanywa kwenye timu ya taifa ambayo yanaweza kuwa yasiwe na maslahi kwa timu ila yenye nia ya kuifaidisha serikali na watawala.

Juzi juzi hapa malalamiko yalizidi kwamba ushawishi wa serikali na wanasiana umekuwa mkubwa mno katika timu ya taifa hadi kuanza kugawa watu katika misingi ya kisiasa. Tuliona mabango ya kusifu wanasiasa yanazidi viwanjani, tuliona kila jambo tunaambiwa huyu ndiyo amewezesha. Timu ilipopata kipigo dhidi ya Uganda na watu kama kuwazodoa wale waliokuwa wanasifu na kuabudu, ikapelekea kama serikali kususa na kutaka kuiweka timu mbali na wananchi ili tukose wote. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa wachezaji kuitwa kimya kimya. Tumeendelea hadi sasa hivi tunaletewa wajukuu wa Kawawa. Tutegemee sasa kuona wajukuu wa John Komba, Msekwa, Mangula, Wassira na makada wengine wa CCM waliozaliwa huko ughaibuni wakijazwa katika timu ya taifa na hao kutumika kama chapuo katika majukwaa ya kisiasa.

Tunajua serikali imehusika sana katika kuishawishi CAF kuleta AFCON ukanda huu. Msaada wa Serikali wa hali na mali ni muhimu katika kuifanikisha Taifa Stars katika mashindano yake yote kama walivyofanya juzi kwa kutoa ndege ilipokwenda Morocco na ni budi uendelee ila tusipokuwa makini hamu na tamaa yao ya kuimiliki Taifa Stars itaenda kuiangamiza na kuigawa timu katika misingi ya kisiasa. Tunajenga upya uzalendo kwa timu yetu kwa hiyo kila tunachofanya lazima tuwe makini sana, hivi hivi tutaendelea kila siku kununuliwa tiketi za bure ili kushawishi watu waje viwanjani. Kawaida katika mechi za Simba na Yanga, uwanja mzima unajaa kwa rangi za jezi ila juzi ungeweza kuhesabu watu waliovaa jezi za Taifa Stars na wengi waliovaa hawajatoa pesa zao kuzinunua.

Kwa kumalizia, ingekuwa vizuri tuanze kupewa wasifu na background story ya hawa wachezaji wanaotafutwa huko nje na kuingizwa katika timu ya taifa. Ukiangalia nchi kama Marekani na Ufaransa ambazo zimekuwa na utamaduni wa kuchukua wachezaji wenye asili ya nje au ambao wazazi wao walikuwa wahamiaji, huwa wanakuwa wawazi kutoa taarifa zao kuhusu asili ya hao wachezaji na wazazi wao. Ni muhimu sana tufanye hivyo.
 
Umepiga palepale panapouma. Ila Sawa tu maana tunasiasisha hata visivyo vya siasa.
Timu ya Taifa lolote lililo chini ya FIFA ni Mali ya Chama cha Soka cha nchi husika. Hata membo kifuani ni ya Chama cha Soka na siyo Taifa. Tuchukue mfano wa timu ya Taifa ya Nigeria. Bendera ya Taifa la Nigeria ina rangi nyeupe na Kijani, lakini nembo ya Timu ya Taifa ya Nigeria ina ndege Tai kuhanikiza jina Lao la utani la Green Eagles. Nembo kifuani Kwa jezi ya Taifa stars ni ya TFF.
Kuna kitu umekisema cha maana Sana, wala tusifiche CCM wanapenda kudandia meli zinazovuma. Diamond, Ali Kiba, Harmonize, Marioo nk umaarufu wao hauna mchango wa CCM hata sh.100/- lakini Kila siku utaona kujishebedua eti ni CCM iliyowafikisha hapo.
Ukiwa maarufu tu wewe ni Mali ya CCM Kwa hiari au Kwa lazima.
Dr Shika
Pierre Liquid
Mwakinyo
Mbwana Samata.
 
Taifa Stairs ni timu ya TFF
Niliuliza swali huku kimsingi jibu ninalo. Lengo langu lilikuwa kutoa hoja zangu kama nilivyofanya katika mada.

Kama ulivyosema Bila bila kudandia treni kwa mbele kwa serikali yetu na kupenda kutafuta attention na sifa kama wanazopewa wasanii na wanamichezo kutokana na kazi zao ni shida kubwa inayohitaji tiba mbadala.
 
Nilikuelewa vzr, mkuu wabongo mpira hawajui,tunakurupuka, mbaya sasa wameingia watu wa siasa ktk mpira ,tatizo ndio hili sasa
 
Unajua moja ya shida ya nchi hii ni serikali na wanasiasa kuwaonea donge watu na taasisi binafsi pale zinapoonekana kupata ushawishi, umaarufu na nguvu kuwazidi wao. Hili limekuwa ni tatizo kubwa kuliko wengi wanavyodhani au kufikiri. Matokeo yake wamekuwa wanatumia nguvu kubwa kutengeneza watu ili wakipata umaarufu wapate kuwa karibu nao huku wakiweza kuwacontrol. Pale mtu au taasisi inapochipuka ambayo haiko mikononi mwao, watajaribu kila njia kuimiliki na wakiona hawana control nayo sana, huyo mtu au taasisi ategemee mambo yake kukwama.

FIFA walifanya makusudi kabisa kutenganisha mpira na shughuli za serikali. Pamoja na kwamba ushirikiano wa serikali katika masuala ya michezo unahitajika mfano kwenye masuala ya kusaidia vibali vya wachezaji wa nje, ulinzi na usalama wakati wa mechi, nk. ili shughuli za mpira ziende, ila FIFA wanataka uendeshaji na maamuzi yanayohusiana na mpira yabaki mikononi mwa chama husika ambapo kwetu ni TFF na hili linasisitizwa kwa maslahi ya mpira wenyewe.

Tulipoambiwa serikali imejitolea kumlipia mshahara kocha Amrouche na benchi la ufundi wengi walipongeza, chawa wakashangilia tulipoambiwa kuna goli la mama ingawa cha kushangaza na kuchekesha, mbinu za kocha zimekuwa siyo kutafuta magoli bali kujilinda. Wengine tulijua haya yote yatakuja na gharama zake.

Kwa nini nimeleta mada hii?

Kwa serikali kuonea gere umaarufu wa timu za Simba na Yanga na kujaribu kupenya huko ingawa kelele huwa zinaibuka pale wanasiasa wanapozidisha, serikali ni kama imeamua kugeukia timu ya taifa kwa mgongo wa kuwa ni "timu ya taifa" kwa hiyo wana mamlaka nayo. Hili nataka kuwakumbusha siyo sahihi na litakuja kuwa na matokeo mabaya huko mbele. Kuna maamuzi yanaweza kufanywa au yanafanywa kwenye timu ya taifa ambayo yanaweza kuwa yasiwe na maslahi kwa timu ila yenye nia ya kuifaidisha serikali na watawala.

Juzi juzi hapa malalamiko yalizidi kwamba ushawishi wa serikali na wanasiana umekuwa mkubwa mno katika timu ya taifa hadi kuanza kugawa watu katika misingi ya kisiasa. Tuliona mabango ya kusifu wanasiasa yanazidi viwanjani, tuliona kila jambo tunaambiwa huyu ndiyo amewezesha. Timu ilipopata kipigo dhidi ya Uganda na watu kama kuwazodoa wale waliokuwa wanasifu na kuabudu, ikapelekea kama serikali kususa na kutaka kuiweka timu mbali na wananchi ili tukose wote. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa wachezaji kuitwa kimya kimya. Tumeendelea hadi sasa hivi tunaletewa wajukuu wa Kawawa. Tutegemee sasa kuona wajukuu wa John Komba, Msekwa, Mangula, Wassira na makada wengine wa CCM waliozaliwa huko ughaibuni wakijazwa katika timu ya taifa na hao kutumika kama chapuo katika majukwaa ya kisiasa.

Tunajua serikali imehusika sana katika kuishawishi CAF kuleta AFCON ukanda huu. Msaada wa Serikali wa hali na mali ni muhimu katika kuifanikisha Taifa Stars katika mashindano yake yote kama walivyofanya juzi kwa kutoa ndege ilipokwenda Morocco na ni budi uendelee ila tusipokuwa makini hamu na tamaa yao ya kuimiliki Taifa Stars itaenda kuiangamiza na kuigawa timu katika misingi ya kisiasa. Tunajenga upya uzalendo kwa timu yetu kwa hiyo kila tunachofanya lazima tuwe makini sana, hivi hivi tutaendelea kila siku kununuliwa tiketi za bure ili kushawishi watu waje viwanjani. Kawaida katika mechi za Simba na Yanga, uwanja mzima unajaa kwa rangi za jezi ila juzi ungeweza kuhesabu watu waliovaa jezi za Taifa Stars na wengi waliovaa hawajatoa pesa zao kuzinunua.

Kwa kumalizia, ingekuwa vizuri tuanze kupewa wasifu na background story ya hawa wachezaji wanaotafutwa huko nje na kuingizwa katika timu ya taifa. Ukiangalia nchi kama Marekani na Ufaransa ambazo zimekuwa na utamaduni wa kuchukua wachezaji wenye asili ya nje au ambao wazazi wao walikuwa wahamiaji, huwa wanakuwa wawazi kutoa taarifa zao kuhusu asili ya hao wachezaji na wazazi wao. Ni muhimu sana tufanye hivyo.

Labda jiulize kwanza TFF ni mali ya nani na ipo nchi gani? Ukipata jibu utakuwa umejijibu kila kitu na kufuta uzi wako!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom