kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Lawama la kushindwa kwa Taifa stars AFCON kwanza liende kwa TFF kabla ya sehemu nyingine. Timu zetu kubwa kwenye ligi haziandai Wachezaji wa kuichezea timu ya taifa kwakuwa wamepewa ruksa ya kutafuta wachezaji 12 nje ya nchi. Hii inasababisha vijana kama Mzize na wengine wasipate muda wa kukosea na kusahihisha makosa Yao ndani ya timu zao. Timu za Simba, Yanga na Azam Zina miundombinu na mabechi mazuri ya ufundi, ndizo zingepaswa kutoa washambuliaji wazuri kwenye timu Yao ya Taifa lakini wapi wee, wanawatumia wageni ambao wanatufunga tunapokutana nao kwenye mashindano ya CAF.
Lawama ingine kubwa iende kwenye uteuzi wa timu, tumeteua wachezaji kutoka nje wengi ambao hatuwajui vizuri na kuwaacha tunaowajua vizuri akina Mwenda, Mzize, kyombo na wengine. Hawa vijana wangeenda kule wangejifunza mengi sana.
Lawama ingine ni wizara ya michezo, inaonekana zaidi wakati wa mashindano zaidi kuliko wakati wa maandalizi ya wachezaji. Hi serikali haioni kuwa wachezaji 12 kila timu inaiua timu ya Taifa? Viwanja vyetu vingi ni vya CCM na vibovu, viwanja vya serikali vizuri viko wapi? Kwanini serikali haihoji timu kubwa kukosa viwanja au kwaajili ya conflict of interest ña viwanja vya CCM na uwanja wa taifa dhidi ya viwanja vya timu? Maana wanajua kama kila timu ikimiliki uwanja wake viwanja vya CCM vitabaki vya kichezea magwaride ya sherehe za muungano. Vijana wa makocha wazuri? Vitaru vya watoto viko wapi? Sera ya michezo ipo? shule Zina viwanja?