Ijue Asili ya jina Taifa Stars

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
652
Majira ya saa mbili usiku wa leo, timu yetu ya taifa, Taifa Stars, itakuwa na kibarua dhidi ya Morocco kwenye AFCON.

Wakati tunaisubiri mechi hiyo muhimu, si vibaya tukafahamu asili ya jina la TAIFA STARS.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Paul West Guivaha, ndiye aliyetunga jina la timu yetu ya taifa, la Taifa Stars.

Hii ilikuwa mwaka 1973 kwenye mashindano ya michezo ya Afrika (All Africa Games) yaliyofanyika Lagos Nigeria.

Tanzania ilifuzu kwa mara ya kwanza, huku yeye akiwa kocha.

Waandaaji wa mashindano yale kule walihitaji majina ya utani timu zote ili yaingizwe kwenye nyaraka kuwarahisia kazi watangazaji.

Ilipofika zamu ya Tanzania, akaulizwa kocha Paul West Guivaha.

Hadi hapo hakukuwa na jina la utani la timu ya taifa ya Tanzania, lakini yeye akaropoka tu kwa kusema, TAIFA STARS.

Jamaa wakaliandika jina hilo na kuanza kulitumia hapo hapo.

Mechi ya kwanza jina hili kutumika ilikuwa dhidi ya Algeria, Januari 8, 1973. Tanzania ilipoteza 4-2.

Bahati mbaya hadi anafariki, hakuwahi kuulizwa alilipata wapi, lakini linahusishwa na muundo wa mashindano yetu ya ndani wakati huo.

Taifa Cup yalikuwa mashindano makubwa sana, yakihusisha timu za mikoa na yalitoa wachezaji wengi kwenye timu ya taifa.

Hata ligi yetu ilikuwa ikiitwa mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya taifa, siyo ligi kama ilivyo sasa.

Kwa hiyo yawezekana kujirudia rudia kwa TAIFA kukamkaa kichwani na kujikuta akiropoka tu, Taifa Stars.

Baada ya kutoka Nigeria, timu ya taifa ikarudi nyumbani na jipya la Taifa Stars.

Hata hivyo, katuachia jina zuri sana!

FB_IMG_1705496254351.jpg
 
1972 kulikuwa hakuna tshirt ?
 
Sio kweli, haiwezekani timu iende kwenye mashindano makubwa ya all african games ikiwa haina jina tayari,
Hembu hii kitu ipelekwe
Jamii check
Tupate uhakika
 
Hii mechi sijui niangalie! Sijui nijilaliage zangu mapema, ili kesho nikiamka nichungulie tu kwenye mitandao kuona tumefungwa goli ngapi!!!
 
Sio kweli, haiwezekani timu iende kwenye mashindano makubwa ya all african games ikiwa haina jina tayari,
Hembu hii kitu ipelekwe
Jamii check
Tupate uhakika
Soma tena vizuri utamwelewa.Mwandishi kasema lilitafutwa jina la utani,kwahiyo inawezekana ilikua inaitwa Tanzania ila hiyo Taifa stars ilizaliwa hapo na sasa ndio jina rasmi linaloitambulisha timu ya Taifa ya tanzania.kama nimemwelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom