Je, Rais Magufuli anatafuta kiki kupitia mikopo ya wanafunzi?

Kwenye kilele cha miaka 55 ya UDSM mtaambiwa hakuna mikopo.Wanafunzi wafanye kazi tu.CCM haikuleta umaskini katika familia za hao wanafunzi wanaolilia mkopo.
 
Sawa Mkuu...ongereni kwa kuongoza kwa kutengeneza matatizo na kuja kutoa tamko la utatuzi mbele ya kadamnasi ili kupata kiki.

Hata mkulu alipompigia Gambo simu kumpongeza kwa kitendo chake cha kutaka kuzuia maendeleo ya wananchi wa ARUSHA...alimwambia ampe mtu aliyekaribu naye simu eti ili ajue watu wajue kuwa Gambo alikuwa anaongea na rais....what a simple mind.??

Na Gambo mwenyewe alivo kichwa panzi wakati anaongea na wafanyabiashara wa ARUSHA akamwaga mzigo kama ulivo...najua alikuwa anatafuta kiki kama kawaida yenu...ila kwa mtu mwenye akili ilikuwa ni udhalilishaji mkubwa kwa kiongozi wa nchi.

Na Lumumba mlivo vichwa panzi mkawa wa kwanza kuleta sehemu ya mazungumzo ya Gambo na wafanyabiashara hapa JF akijisifu kupigiwa simu na rais..

Mmebaki kufanya siasa za kui-preempty serikali ila mnachotakiwa kujua ni kwamba mwisho wa siku Serikali itaibuka kidedea haijalishi ilitenda kwa kuamua au kwa sababu mlisema nyie. Mtakuwa mmekumbuka shuka kumekucha
 
Salam Wanabodi,
Tujitwike mzigoni.

Ikiwa zimepita siku chache tangu serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu Mh. Stella Manyanya kutoa taratibu mpya juu ya utoaji wa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu, zimesikika kelele na vilio vya watoto wa Kimaskini juu ya hatma yao Masomo.

Watu wengi wamelaani taratibu hizo kuwa siyo rafiki kwa wanafunzi hao. Pamoja na hayo ni wanafunzi wachache tu ndiyo wamebahatika kupata mkopo katika awamu ya kwanza.

Nimekua nikijiuliza sana hii ina maana gani ikiwa Mh Rais John Pombe Magufuli aliahidi kuwa wanafunzi wote wenye sifa ya kusoma chuo kikuu wanapatiwa mikopo. Mbona ahadi yake na hali halisi hazilandani kabisa?

Je,ni kweli serikali imekosa fedha za kuipatia Bodi ya Mikopo ili wawapatie Wanafunzi? Je,ni katika harakati za Serikali kubana matumizi ili kizidisha kile wanachokiita maendeleo?

Kati ya hayo maswali yangu hapo,siamini kabisa kwamba Serikali haina fedha za kuwapatia wanafunzi. Pili,serikali haiwezi kubana matumizi mpaka kufikia hatua ya kuwanyima baadhi ya wanafunzi mikopo.

Kelele nyingi zimepigwa na wadau wa elimu,Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu,wahanga wa tukio lenyewe na watu wengi mtaani wanasikitika.
Jambo hili limekua ndo mazungumzo makuu mitandaoni na hata mitaani. Yaani limeteka sana hisia za watu wengi. Hata serikali pia inalitambua hili kuwa hali si nzuri.

Nikionacho ni kwamba Serikali ya awamu ya 5 inajaribu kutafuta attention ya watu ili baada ya muda mfupi watoe mikopo kwa wanafunzi wengi baada ya hapo serikali itasifiwa na kupewa sifa za kutosha.
Kwa nilichokisikia ni kuwa Mh Rais anaweza kuwa mgeni rasmi kwenye sshughuli ya kusherehekea miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Je,ni hapo ndipo atakapopandisha mizuka na kusema wnafunzi wote wapatiwe mikopo kisha kushangiliwa na Umati wa wanafunzi watakaohudhuria?
Hii siyo kiki kweli?

TUSUBIRI TUONE.
Na kweli na tunamsubir kwa hamu kubwa
 
How do we expect to have a developed and
industrialized country if we don't educate the
very same people who we expect to propel us
there?
 
Duh duh nyie vijana wa digital hatari sana mnadukuwa hadi kwenye ubongo!!
Single haijatoka studio ishavuja !!
 
Just keep praying hard for our beloved president, what you question will one day happen miraculously.

How do we expect to have a developed and
industrialized country if we don't educate the
very same people who we expect to propel us
there?
 
Ila mumemchoka dah nimecheka mpaka nimelia yaani anatafuta kiki kwenye maisha ya watoto wa wenziwe kwa sababu jesca yupo Dodoma anapelekwa na gari na kurudi Ikulu kwa hiyo wakihangaika wa wenzake hayamhusu
 
Sidhani kama wanatafuta kiki. Wizara na bodi wamekuja na yao lakini wadau wa elimu wameamua vinginevyo. Hivyo sitashangaa watu wakiamkia pabaya hivikaribuni. Huwezi kutafuta kiki kwa issue kama hii ni hatari. Nguvu ya wanafunzi si ya kupuuza hata siku moja haswa wakiungwa mkono na jamii. Bunge lipo au nalo ni kibogoyo? Stay tuned.
 
Salam Wanabodi,
Tujitwike mzigoni.

Ikiwa zimepita siku chache tangu serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu Mh. Stella Manyanya kutoa taratibu mpya juu ya utoaji wa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu, zimesikika kelele na vilio vya watoto wa Kimaskini juu ya hatma yao Masomo.

Watu wengi wamelaani taratibu hizo kuwa siyo rafiki kwa wanafunzi hao. Pamoja na hayo ni wanafunzi wachache tu ndiyo wamebahatika kupata mkopo katika awamu ya kwanza.

Nimekua nikijiuliza sana hii ina maana gani ikiwa Mh Rais John Pombe Magufuli aliahidi kuwa wanafunzi wote wenye sifa ya kusoma chuo kikuu wanapatiwa mikopo. Mbona ahadi yake na hali halisi hazilandani kabisa?

Je,ni kweli serikali imekosa fedha za kuipatia Bodi ya Mikopo ili wawapatie Wanafunzi? Je,ni katika harakati za Serikali kubana matumizi ili kizidisha kile wanachokiita maendeleo?

Kati ya hayo maswali yangu hapo,siamini kabisa kwamba Serikali haina fedha za kuwapatia wanafunzi. Pili,serikali haiwezi kubana matumizi mpaka kufikia hatua ya kuwanyima baadhi ya wanafunzi mikopo.

Kelele nyingi zimepigwa na wadau wa elimu,Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu,wahanga wa tukio lenyewe na watu wengi mtaani wanasikitika.
Jambo hili limekua ndo mazungumzo makuu mitandaoni na hata mitaani. Yaani limeteka sana hisia za watu wengi. Hata serikali pia inalitambua hili kuwa hali si nzuri.

Nikionacho ni kwamba Serikali ya awamu ya 5 inajaribu kutafuta attention ya watu ili baada ya muda mfupi watoe mikopo kwa wanafunzi wengi baada ya hapo serikali itasifiwa na kupewa sifa za kutosha.
Kwa nilichokisikia ni kuwa Mh Rais anaweza kuwa mgeni rasmi kwenye sshughuli ya kusherehekea miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Je,ni hapo ndipo atakapopandisha mizuka na kusema wnafunzi wote wapatiwe mikopo kisha kushangiliwa na Umati wa wanafunzi watakaohudhuria?
Hii siyo kiki kweli?

TUSUBIRI TUONE.
mkuu umeharibu kila kituu, KIKI inatafutwa hapa!
 
Maisha yamekuwa vululuvululu kutokana na maamuzi ya kukurupuka...haikubaliki sisi tulipe kodi alafu watu wachache wakatae kuwakopesha wanetu ili wasome kwa vigezo vyao wao. Serikali ya watu lazima iwe kwaajili ya watu Sasa ukitofautiana nawatu inakuwa ndo uchwa...wenyewe. Tunataka viwanda lkn hatutaki kusomesha vijana,aibu ajabu.
 
Back
Top Bottom