Je, kuna somo ambalo hutakuja kulisahau kwa jinsi lilivyokutoa jasho?

Abstract algebra, ilinikimbiza kiasi chake, ila mwisho wa siku nilitoboa.
 
Kila mtu ana somo ambalo halikuwahi kuwa rahisi kwake. Labda kwa wachache ambao ni exceptional wanaweza wasiwe walikutana na hii situation.

Nimekumbuka enzi zangu nipo chuo. Katika harakati zangu za kuijenga future yangu nikabahatika kutua kwenye chuo kimoja wapo kikubwa hapa nchini kwa course ya miaka 3.

Harakati zikaanza, siku zikaenda nikafanikiwa kuingia mwaka wa pili hapa sasa ndipo nilikutana na ugumu na kuiona elimu ngumu...

Sitakuja kulisahau somo moja linaitwa ECONOMETRICS. Kwa wale waliosoma Economics au course zenye uhusiano na economics watakuwa wanalielewa hili somo. Kwa course yangu na department yangu nilipokuwa. Hili ni moja wapo ya masomo ambayo huwa 'yanawakamata' watu wengi sana.

Ingawa nilibahatika kulifaulu vizuri chamoto nilikiona na nilinyoosha mikono juu.

Physics Advanced level, ilinisumbua nikakonda hadi nikawa kama nimeathirika na ugonjwa wa kisasa. Mungu si Mzee Mkumba, NECTA nikatusua vibaya sana. Kwa chuo Pathology ilinisumbua sana, hadi nikajutia na kuilaana siku niliyochagua kusoma course yenye hilo somo, lakini Mungu akanisaidia nikatoboa kiulaini kama unyoya
 
pole mkuu

l
 
Back
Top Bottom