Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

TAI DUME

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
8,859
23,119
UTANGULIZI
Wakuu habari.

Naandika hii story yangu ikiwa ni mwaka sasa nipo mtaani nikiendelea na harakati za kusaka ajira mpya toka mkataba wangu wa ajira ulipoisha mnamo Desemba 2022. Nimeamua kushea uzoefu wangu kwa mtindo wa Masimulizi (katika episodes) kwa kuamini pengine inaweza kuwa na mafunzo kwa waajiri, waajiriwa au wanaotegemewa kuajiriwa. Naomba moderatoes wa JF wauache huu uzi wangu hapa hapa kwenye Jukwa la Ajira kwani muktadha wa simulizi hii maswala ya kubadilishana uzoefu katika swala la ajira na sio mambo ya entertainment. Twende kazi.

Episode 1: Sikuogopa kujidhalilisha ili kupata reliable connection

Mwaka 2011 nilipomaliza my 1st degree kama ilivo kwa wanachuo wengine, nilikuwa na expectation kubwa sana ya kupata ajira nzuri ndani ya muda mfupi. Hii ilijengwa na kiburi kwamba mwaka mmoja before sijamaliza niliwaaproach ndugu na wadau kwenye network yangu kwamba mwakani namaliza. Kila mmoja alinipromise kunisaidia kupata job au kuniconnect na waajiri mbali mbali. Swala likawa ni kwamba wewe maliza tu chuo then utuambie ili tukafanyie mipango.

Kimbebe kilikuja baada ya kumaliza. Nilitulia kwanza mwezi mmoja then nikaanza kucheki walionipromise job kwamba I am available. Asee nilipigwa dana dana za kutisha na mwishowe wengine wakawa hata hawapokei simu zangu. Nikiwaibukia nyumbani au maeneo yao ya kazi wanaishia kunipa nauli ya kurudia na kuniambia ajira ngumu cha muhimu wewe endelea kumuomba Mungu. It was very disappointing situation at that time na nikafikia hatua ya kuanza kuwachukia bila sababu as if wao ndio wanaonisababishia ugumu wa kuajiriwa, hahahaaa.

Basi nikaanza kuumiza kichwa how to go about finding the job. Nikaaply sana kazi kupitia job adverts za mtandaoni lakini mimi mwenyewe nikaona as a fresh graduate I didn’t have the skills and required experiences. Nikaanza kuona hata elimu yenyewe may be course niliyosoma haina maana bora lile boom ningelitumia kwa kuanzisha hata kimradi cha kuchoma popcorn mtaani.

Hali ilikuwa mbaya to most of the graduates maana kila nikiwacheki wana nao wanalalamika kama mimi tuu isipokuwa wachache sana wenye connection tena za familia zao za kuzaliwa. Hapo nikakumbuka wakati naenda kuanza form 5 way back bro wangu aliwahi kuniambia “dogo huko shule nenda kawe na marafiki wa aina mbili, either wenye akili sana darasani au wale wanaotoka kwenye familia bora”. Nilikuja kumwelewa kipindi hiki ni nini bro alichomaanisha. Kwamba wale wenye akili sana darasani watakuinfluence kufauru na wale wanaotoka maisha bora ni future asset katika connection za ajira.

Sasa mimi kutoka na usela wangu mavi wa teenager sikuwa na hata mmoja kati ya hao. Roho ilikuja kuniuma zaidi nilipogundua nilipokuwa advance niligombana na jamaa mmoja ambaye kwao walikuwa wapo poa sana wa kutokea mkoa wa Iringa, nilipooulizia habari zake nikasikia kwa kipindi kile natafuta ajira alikuwa ni msimamizi wa kampuni ya usafirishaji mizigo(malori) na walikuwa na ofisi zao bandarini (clearing and forwarding). Laiti yule jamaa ningemfanya best friend ukute ingekuwa rahisi kwa yeye kunipa mchongo. Anyway, les forget about him.

Nakumbuka siku moja nikiendelea kusaga visigino katika harakati zangu za kutembeza bahasha, kwenye foleni nikamwona lecturer wangu mmoja hivi, tumuite Dr KJ (PhD ya kihaya hiyo) kwenye shangingi lake akiendeshwa na dereva wake kama kawaida. Huyu lecturer nilimkumbuka kwa sababu alikuwa na sifa sana kwenye vipindi vyake na alikuwa anafundisha somo la project Management.

Yaani huyu Muhaya alikuwa anatumia nusu ya muda wake kwenye lecture kujisifia. Ataanza kuwananga maprof kwamba japo yeye ana PhD ila hakuna prof anaemzidi akili na pesa chuo kizima, kwanza yeye anaendeshwa na mshahara anamlipa dereva wake ni sawa na wa tutorial assistant wa pale chuo. Alikuwa mdhalilishaji sana kwa wanafunzi hususani watoto wa kike au wanaofeli somo lake.

Ila watu walichompendea jamaa alikuwa sometimes anagawa sana maokoto akiwakuta wanafunzi njiani ila ndio mjue mtadhalilishwa. Jamaa alikuwa anatembea na dola au Euro akidai pesa za madafu ni nzito, hatukujua anapata wapi zile dola dola. Nakumbuka kuna semester alimlipia ada jamaa mmoja alikuwa anasoma kwa shida sana alikuwa hana boom. Alimlipia ada ya semester ya mwisho ila yule jamaa cha moto alikiona maana Dr KJ kwenye kila kipindi alichofundisha kwenye madarasa yake lazima amtolee mfano yule jamaa mpaka mlipiwa ada akawa famous chuo hahahaaa.

Basi bhana nilipomwona kwenye foleni Dr KJ vitu vingi vingi vikapita kama mshale kwenye mawazo yangu. Kwamba huyu jamaa anaweza akawa asset lakini anaweza akanidhalilisha vibaya sana na nitamuanzaje yupo kwenye gari. Je atanikumbuka maana wanafunzi tulikuwa wengi sana. Lakini nikifikiria pale geto nadaiwa kodi mwenye nyumba keshanivumilia kama two months (niliamua kukomaa mjini sikutaka kwenda mkoani).

Wakati naendelea kuwaza foleni ikaanza kutembea, asee sijui ni nini kilinikuta nikajikuta naikimbilia ile gari na kwenda kuisimamia kwa mbele nikiizuia isiende huku nikimwonyeshea ishara dereva apaki pembeni. Dereva alipoona anaweka foleni akamuuliza bosi wake wafanyeje hahaaa maana nacheka kama ni mazuri. Basi Dr KJ kwa wasiwasi akamwambia aweke pembeni.

Basi nikasogea upande wa Dr KJ akawa hataki kushusha kioo, akanielekeza niende upande upande wa dereva. Nikajua tuu boss anaogopa labda nitamdhuru so he decided to sacrifice his driver- hahahaa. Basi nikaenda upande wa dereva aliposhusha kioo nikamsalimia.

Mimi: shikamoo Dr KJ

Yeye: Unanifahamu?

Mimi: Ndio wewe ni mwalimu wangu wa somo flani nimemaliza mwaka jana.

Yeye: (Bado akiwa na wasiwasi) Nitaamini vipi na kwanini unanisimamisha kama jambazi?

Mimi: (Bila kujiuma uma) Naomba unisamehe sana Dr, ni kuvurugwa na hapa nimeona kama bahati
kukuona. Dr mimi nipo katika harakati za kutafuta kazi, nimekusimamisha ili nikuachie CV yangu maana naamini wewe network yako ni kubwa pengine unaweza ukaniconnect na wadau wako.

Yeye: (Akacheka sana huku akiniita niende upande wake). Kwa hiyo unatafuta kazi gani?

Mimi: Kwa sasa nahitaji sehemu yoyote ya kujishikiza ili nipate uzoefu, lakini uzuri wewe ni mwalimu wangu wa PM so unaweza ukaona ni wapi zile theory wapi naweza kuziapply.

Akaniangalia sana kisha akaniuliza unajua nini kuhusu project management na principles for effective project management? Nikamshushia madude kwa style ambayo nadhani ilimkamata kisawa sawa. nIkamsisitizia kwamba mimi sijawahi kushikwa kwenye somo lake. Baada ya kumjibu pale akaniambia. Mbona unaonekana una njaa sana? Shika hii nenda kale mimi nina mambo mengi sana na hapa unanichelewesha tuu. Sikupokea kwanza ile pesa ila nikamwambia Sir please just take my CV may you can see how you can help.

Akaniuliza, sasa CV yako umeandika nini wakati hujawahi kufanya kazi popote? Halafu sina muda wa kutembea na makaratazi kwa gari yangu. Akawa anafunga kioo, asee nikaking’anga’ania. Akaniambia unataka nini sasa pesa nimekupa umekataa. Nikamwambia, kama huwezi kutembea na makaratasi basi naomba email address yako ili nikutumie. Akaniangaliaa, kisha akatoa business card akanipa. Mimi nikaicheki nikaona ile biz card sio yake ni ya mdada. Nikamwambia mbona sio yako. Akaniambia “vizuri sana upo makini, mpigie huyo dada simu kesho muda kama huu”. Hiyo ilikuwa ni kama saa tisa hivi. Kisha akanipa ile pesa, akasepa zake.

Mwendelezo=>

Sehemu ya 2

Sehemu ya 3
 
Tuendelee tulipoishia

Basi nikaachana na Dr KJ pale, nikahesabu ile pesa ilikuwa ni elfu 40. Kwanza njaa yote ilikata si unajua tena ukipata hela ambayo hujaitegemea. Nikarudi zangu home. Ile hela nikaclear some bills muhimu za pale geto ikiwemo umeme, maji na kwa mangi nilikokuwa nakopa kopa unga na mchele. Then ikabaki kama 10 hivi jioni nikasogea kijiwe cha kunywa banana nikavimba pale kwa banana zangu tatu, banana moja ilikuwa inauzwa sh 350, kwa msiojua banana ni kinywaji kimoja local kinatengenezwa kwa ndizi, ni kali mno kwa estimation ya ulevi banana moja ni kama safari moja na nusu hahahaaa.

Basi siku ya pili ilipofika saa tisa sharp nikaipiga ile namba. Kama nilivyotarajia akapokea mdada. Mazungumzo yetu yalikuwa:

Mimi: Habari, naitwa TAIDUME nimepewa namba yako hii na Dr KJ alinipa maelekezo nikupigie.
Yeye: Ok sawa nina taarifa zako. Sasa kesho saa 4 asubuhi njoo (akanitajia jengo na ofisi ilipo - Posta Dar)
kwa ajili ya interview.
Mimi: (Kwanza nikapigwa butwaa) Ok dada japo umenishtukiza ila nitakuja kwa wakati. Ila ninaomba
kama hutojali nitumie walau kipeperushi au website ya ofisi ili niweze kupata uelewa wa ofisi coz
ili kesho nikija niwe walau na abcd.

Yeye: Samahani kaka sikupewa hayo maelekezo na boss.
Mimi: Sawa nakuelewa, haina shida kuwa na amani tutaona hiyo kesho saa nne.

Basi nikakata simu pale. Siku hiyo ilikuwa Jumatano wakati napiga simu so nipaswa kesho yake Alhamis niibukie kule ofsini. Sasa nikawa na mawazo mengi sana. Nimeambiwa niende kwenye interview lakini sijui naenda kufanya interview ya position gani mbaya zaidi sijui hiyo ofisi yenyewe inadili na nini? Nikarudia kuisoma ile biz card upya nikaona jina la ofisi anayofanyia yule dada maana cheo chake alikuwa ni personal secretary. Ila lile jina la kampuni au tuite ofisi halikuweza kunipa mwanga wowote labda to predict what can be operational sector. Imagine nilikuwa kwenye wakati mgumu kiasi.

Nikaamua kuyaacha kama yalivyo hayo maswali yangu maana sikuweza kupata majibu. Nikamshukuru Mungu maana ilikuwa ndio mara ya kwanza kuitwa kwenye job interview japo hii ilikaa kimitego sana. Siku hiyo nililala mapema sana kwenye saa tatu tu nikawa nishalala, before nilibrash viatu vyangu na kunyoosha nguo kabisa.

Basi asubuhi nikajidamka saa kumi na moja nikajiandaa pale, mpaka kufikia 12 nishatoka geto nipo kutafuta usafiri. Kwenye saa mbili na nusu nikawa nishafika kwenye jengo lenye ile ofisi. Basi nikatafuta kijisehemu kwa nje wanapouza chai nikapiga tea mdogo mdogo huku nikisubiri subiri muda uende kusubiri saa tatu na nusu ndio niibuke. Ilipofika muda nikamcall yule dada akanielekeza nipande lift mpaka ofisi ilipo. Kweli akanipokea pale na kunikaribisha waiting room. Baada ya muda akanilitea kahawa na maji then akaniambia boss atachelewa kidogo ila ameagiza nipewe vipeperushi nisome wakati namsubiri.

Nikawa nasoma soma pale mpaka ilipofika mida ya lunch boss bado hafika. Nikaletewa lunch pale, ile ofisi wana utaratibu wa wafanyakazi kupewa lunch siku za kazi. Nikagonga vizuri tuu pamoja na wafanyakazi wengine, walikuwa watatu baadae nikaja kujua ni secretary wa boss, mhasibu na mtu wa usafi. Ilipofika saa tisa yule secretary wa boss akaniambia boss hawezi kuja kwa siku ile kwahiyo waliniruhusu niondoke ila watanitaarifu lini nitarudi kwa inyerview. Basi nikashukuru pale nikasepa zangu nikiamini kwa kuwa ilikuwa ni Alhamisi basi kwa vyovyote interview itakuwa next week. So, nikaomba baadhi ya vipeperushi ambavyo sikuvisoma nikasepa zangu.

Ilipofika ijumaa muda wote nilihakikisha simu ipo na chaji maana nilitegemea kupata simu kutoka kwa yule secretary ya kunialika tena kwenye interview. Mpaka Jumatatu jioni ya wiki iliyofata sikupigiwa simu yoyote kutoka kwa yule dada. Dah! Nikawa nawaza sijui nimpigie kumuuliza lakini nikaona haitakuwa busara kwa muda ule labda nisubiri walau ikipita ndio nimpigie. Basi nikaamua kupotezea huku nikijipa hope watanipigia tuu.

Nakumbuka ilikuwa Jumanne saa 2 asubuhi nikiwa napanga ile buku niliyonayo naipangila vipi ili siku ipite mara yule secretary akanipigia simu na kuniambia kama naweza boss atakuwa ofisini saa tano na amepanga kukufanyia interview. Nikamwambia consider this Is done, saa tano sharp nitakuwa hapo. Basi akaniambia haina shida nitawakuta maana boss alikuwa ameshafika na ananisubiri. Mimi nimefika pale by saa nne na nusu nikazama ndani. Basi bosi akaambiwa pale baada ya muda akaniita ofisini kwake.

Kiroho kikawa kinanidunda nikawa nasali sala zote unazozijua wewe, wee acha tu kwenye ile situation niimwachia Mungu tu. Basi ile nachoma ndani kwa boss mara paap namwona Dr KJ yupo pale ndani busy na laptop yake. Kiukweli sikutegemea kabisa kama Dr KJ ndio boss wa ile ofisi, mimi mawazo yangu yalikuwa labda Dr ameniconnect na watu wake na nilipanga kama ningefanikiwa pale kupata job basi ningetafuta namba yake au kumfata hata kule chuo ili kumshukuru.

Basi bhana, nikamsalimia pale. Jamaa akaniitikia kama ndio tunaonana kwa mara ya kwanza. Akawa anaendelea kufanya fanya shughuli zake baada ya kama 10 minutes ndio akaniuliza email address yangu. Then akaniambia niende kwa secretary kuna laptop atanipa kuna email amenitumia niisome then nimjibu. Basi nikapewa laptop na kufungua email. Nikakuta amenifowadia email ilikuwa kutoka kwa wadau wake wamemtumia document.

Sasa nafkiri kwa sababu Dr KJ alikuwa busy hakuweza kuisoma ile doc maana ilikuwa na page nying sana. So alichonitaka ni kuisoma ile doc niielewe then nimwandikie summary isiyozidi page mbili then nimtumie. Wakati mimi naendelea na kuisoma ile doc yeye akawa akawa anaondoka akamwagiza secretary wake kwamba nikimaliza nimtumie then niondoke. Kwa hiyo hakuna interview tena kwa mara nyingine. Basi baada ya muda mimi nikamaliza ile kazi nakumbuka ilikuwa kwenye saa na nane hivi. Basi ukaletwa msosi pale tukagonga then mimi nikaaga. Secretary akaniambia bosi akimwambia chochote atanijulisha. Nikatembea zangu huku nikiamini labda kesho nitajulishwa interview itakuwa lini.

Nikasubiri Jumatano mpaka Alhamisi kimya. Nakumbuka Ijumaa yake kwenye saa 3 asubuhi naona namba ya landline inanipigia, unajua sikuwa nimewahi kabisa kupigiwa na landline basi nikajua labda ni namba kutoka nje ya nchi, wakati huo nilikuwa nimejaribu jaribu kuapply scholarship za kusoma vyuo vya nje masters. Basi nikahisi labda mchongo umetiki hahahaa. Nikapokea huku mwenyewe nikijiandaa kubonga ung’eng’e mara naskia “Kaka TAIDUME mbona hujaja kazini siku mbili hizi, boss amekuja leo amekuulizia na amekuwa mkali sana”. Alikuwa ni yule secretary wa boss.

Kwanza nilishangaa sana na sikuelewa anamaanisha nini. Nikamuuliza anajua anaongea na nani maana mimi sijaaliwa popote. Akaniuliza wewe si ni TAIDUME last week ulikuja kwa ajili ya interview ofisini, kwani hamkuongea na boss? Maana leo ameingia ofsini cha kwanza amekuulizia nilipomwambia haujaja tangu tulipoahirisha interview amefoka sana kwa nini huji kazini. Nikaona sasa haya mashkolo mageni kwangu. Nikamuuliza kwahiyo ina maana kazi nimepata? Na je niende muda huo au boss kasemaje? Akanijibu boss amesema Jumatatu akukute job. Nikamuuliza muda wanaofungua ofsi pale akanijibu, basi tukakubaliana Jumatatu niende zangu ofsini.

Nikawaza sana ina maana ndio nimepata kazi au vipi na kwa nini boss anilaumu wakati mimi sikupewa taarifa yoyote ya interview wala ya kuendelea kwenda kule ofsini. Nikahisi labda nimeboronga ile kazi ilitakiwa niifanye kwa siku mbili. Kwa kuwa nilikuwa na laptop langu niliyokuwa natumia chuo nikafungua ili kuisoma tena vizuri ile kazi aliyonipa boss nikaona mbona ipo sawa tuu. Basi niakaona nisijichoshe bure majibu yote nitapata Jumatatu.

Jumatatu ilipofika nilikuwa wa kwanza kufika pale ofsini, baada ya muda kidogo alikuwa yule mtu wa usafi ni mmama mtu mzima kidogo basi akafungua ofisi pale na kuendelea na majukumu yake. Mimi nikasubiri pale mpaka wafanyakazi wengine walivyofika. Yule secretary wa boss akanitania kwa kuniambia Karibu boss TAIDUME, unaweza kuchagua ofisi hapo kati ya hizo mbili zilizo wazi. Nikamwabia natamani hizo ofisi ila ni mpaka nifaulu interview, ila akaniambia yaani wewe na boss mnanishangaza sana.

Wewe unasema hujui kama umepata kazi wakati boss kaniambia nikuandalie ofisi ili uendelee na kazi, au mnaniona mimi bibi yenu? Ikabidi nishangae tuu pale. Basi nikaoneshwa ofisi huku sijui nafasi yangu, majukumu yangu ya kazi wala stahiki zangu. Lakini nikasema yoote hayo nitayajua boss akija inaoneka hii ni ofisi ya one man show.

Nimekaa pale huku nikisoma soma docs mbalimbali za ofisi ili kujifamiliarize operations za ofisi. Kwenye saa 6 mchana Dr KJ akanipigia simu kwa kupitia simu ya secretary wake akaniambia amemtuma dereva wake anifate anipeleke alipo kwenye mkutano so nijiandae akanielekeza na doc za kubeba ambazo secretary atanipa, akakata simu. Nikabaki kushangaa tu pale. Mara dereva akaja pale so secretary akanipatia zile docs zinazohitajika tukaondoka.

Njiani nikawa najaribu kumdodosa dereva wa boss mambo general ya ofisi akawa ananipa abcs pale. Tulipofika ilikuwa ni kwenye ofisi za TAMWA, kulikuwa na wadau kutoka NGOs mbalimbali walikuwa wanaadhimisha kuanzisha mtandao unaitwa Jukwaa la Katiba Tanzania ambalo lengo lake lilikuwa kuunganisha Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) za Tanzania ili kudai katiba mpya Tanzania. (Kwa mnaokumbuka lile vuguvugu la katiba mpya Tanzania kipindi cha Kikwete mpaka kuundwa kwa lile bunge la katiba ambapo Mh Rais Samia alikuwa mwenyekiti mwenza, ndio nazungumzia wakati huo) My task was to take notes on the key issues that Dr KJ will need to include in his report.

Basi kikao kilienda vizuri na wakati wa kujitambulisha pale Dr KJ alinitambulisha kama Afisa Program (Program Officer) wa Shirika lake. Nikashtuka kidogo ala kumbe mimi ni program office, japo sikuonesha kwa watu. Na baada ya hapo kuna series ya vikao vya Jukwaa la Katiba nilishiriki ambapo niliweza kujenga network na kufahamiana na wadau wengi wa NGOs au CSOs. Nakumbuka kwenye kupata wawakilishi wa kuwakilisha NGOs na Asasi za kiraia katika bunge la katiba ndipo alipoibuka bwana Polepole.

Mchakato wa kumpata mwakilishi ulihusisha kupigiwa kura ambapo walihitajiki wawakilishi wasiozidi watano kama nakumbuka sawasawa. Huyu bwana Polepole hata mimi nilimkubali sana wakati anagombea uwakilishi maana jamaa alikuwa anajua kupangilia sana hoja zake na alionekana angekuja kuwachallenge vizuri sana wale ambao wangeenda agaist CSOs coalition’s interests.

Turudi kwenye mada yetu sasa. Basi ule mkutano uliisha jioni hivyo boss akaniambia tukutane kesho ofsini kama kawaida. Kesho yake nilifika ofisini kama kawaida na baada ya muda boss alifika. Tukaitwa wafanyakazi wote pamoja na dereva. Officially Dr KJ akanitangaza kwamba mimi ni mfanyakazi mpya wa lile shirika na nafasi yangu ilikuwa ni Program Officer Advocay nafasi ambayo iliniweka kuwa wa pili kimadaraka baada ya bosi kwa usimamizi wa office. Baadae nikapewa mkataba wangu pale ili kuupitia na kufahamishwa majukumu yangu, probation period, kasalali kenyewe na blahblah nyingi za kimkatabata.

Tukutane sehemu inayofata – Episode 3
 
Back
Top Bottom