Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Kutokana na mlolongo wa matukio yanayotokea nchini, nimekuwa nikijiuliza Sana, je kipaumbele Cha CCM, ni kuendelea kubaki madarakani au ni kuwaletea maendeleo watanzania?
Kipaumbele Cha utawala wowote wa serikali ni kuwaletea maendeleo wananchi wake na kama wasipofanya hivyo, watajikuta wanapigwa chini katika uchaguzi unaofuata.
Hali ni tofauti Sana nchini kwetu, Kwa kuwa ndani ya nchi hii, katika utawala wa CCM kipaumbele Chao kikubwa ni kuhakikisha kuwa chama Chao Cha CCM kinaendekea kubaki madarakani, Kwa njia zozote zile, ziwe za haramu au hallali, lakini kubaki madarakani, ndiyo priority no one kwao!
Ipo mifano mingi, mmojawapi wa mifano hiyo ni kuwa Kwa kutumia vyombo vya dola, kuhakikisha kuwa chama kilichopo madarakani, kinaendekea kusalia madarakani miaka yote.
Hiyo hali haihitaji ushahidi, Kwa kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, enzi za utawala wa Mwendazake, Hayati Magufuli, Dkt Bashiru Ally, aliwahi kulikiri waziwazi, mbele ya vyombo vya habari kuwa chama chale Cha CCM, kitaendelea kutumia vyombo vya dola wakati wote, kuendelea kusalia madarakani!
Hebu tujiulize ni kwanini serikali ya CCM inapata "kigugumizi" kikubwa Sana kutengeneza Katiba mpya itakayoendana na mfumo wa vyama vingi?
Jibu liko wazi, kuwa kutengeneza Katiba mpya, itakayokidhi mfumo wa vyama vingi, itakuwa sawasawa na kujitia kitanzi wenyewe CCM!
Siyo Siri tena kuwa Katiba yetu ya nchi ni ya mfumo wa chama kimoja.
ni kwanini CCM iendelee kupata "kigugumizi" kuibadilisha Katiba hiyo?
Jibu liko wazi, wao CCM wanajua kuwa wakiobadilisha Katiba hiyo na kuleta Katiba itakayokidhi mfumo wa vyama vingi, ndiyo itakuwa mwisho wa utawala wao wa kidikteta.
Hebu tujiulize, inakuwaje Rais aliyeko madarakani, ambaye pia ndiyo Mwenyekiti wa chama tawala Cha CCM, kupewa madaraka makubwa mno ya kiuteua viongozi mbalimbali wa vyombo vya dola, kama Mkuu wa Jeshi nchini, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jaji Mkuu, Wakuu wote wa Mikoa, wakuu wote wa wolaya, wakurugenzi wote wa wolaya (ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa chaguzi mbalimbali kwenye maeneo yao)
Hivi Kwa kumpa madaraka makubwa kiasi hicho, ambayo ni sawasawa na kumfanya Mkuu huyo wa nchi awe dikteta, hivi nchi hii itawezaje kuifanya ipate maendeleo enddlevu?
Ndiyo maana siyo jambo la kishangaza hata kidogo Kwa nchi yetu, pamoja na kuwa tumepata huru wetu toka Kwa mkolloni zaidi ya miaka 60 hivi Sasa, nchi yetu Bado inakuwa na ukosefu wa mahitaji ya msingi wa Binadamu, ya Maji na Umeme!😎
Vyombo vya habari binafsi, ambavyo ndiyo tegemeo pekee lililokuwa limebaki Kwa watanzania, navyo vimetiwa "Kabali" na watawala na vinaelekezwa nini Cha kuripoti!
Kwa hali hiyo unategemea watawala wetu watulletee maendeleo sisi watanzania?
Jibu langu ni big NO.
Ni wazi kuwa watawala wetu, kipaumbele Chao Cha kwanza ni kuendelea kubaki madarakani FOR ANY MEANS