Je, ITV ni Huru ama inatumiwa na wanasiasa?

Njaa mbaya ndugu zangu,ona vijana wasomi wa kitanzania wanavyojitia aibu,..Ni aibu kwa mtu kusimama na kusema Vyama vya wanaharakati vinafadhiliwa,wakati huna ushaidi,pili kama ni kweli kwanini hivyo vya vya wanaharakati visifutwe au kusimamishwa maana si wanaushahidi..hebu waache kuvishushia hadhi vyama kutetea haki za watz,..pia huyu Mkambala anadominate sana mjadala,HAFAI...
 
na wewe toa ushahidi kuwa hawafadhiliwi
Njaa mbaya ndugu zangu,ona vijana wasomi wa kitanzania wanavyojitia aibu,..Ni aibu kwa mtu kusimama na kusema Vyama vya wanaharakati vinafadhiliwa,wakati huna ushaidi,pili kama ni kweli kwanini hivyo vya vya wanaharakati visifutwe au kusimamishwa maana si wanaushahidi..hebu waache kuvishushia hadhi vyama kutetea haki za watz,..pia huyu Mkambala anadominate sana mjadala,HAFAI...
 
sijui wachangiaji wanaogopa magwanda pale mbele.wapo kama wabunge wa ccm mjengoni
 
Kuna jamaa kanipigia simu anasema anawasiliana na yule mama wa midahalo Rose Mwakitwange na Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima wafanye mdahalo wao kuhusu mada hiyo hiyo, lakini wachangaiji waende kwa hiari yao, siyo kuchaguliwa, na polisi wakitaka pia waende wakahenyeshwe kwa hoja.

Wanatarajia kurusha kipindi hicho Star TV ingawa huenda kikapigwa mkwara na serikali.

Hata hivyo mnashangaa nini kwa ITV kufanya hivyo? ITV si inatumika na CCM na JK?ITV ni CCM damu, na wanamuona JK kama vile God, hawaamini eti naye ni fisadi!

Isitoshe mnakumbuka ITV ilivyofanya katika uchaguzi wa mwaka 1995 walipotoa footage ya mauaji ya Rwanda kwa ajili ya kutisha raia wasipigie kura upinzani?

ITV ni kituo kimoja ambacho kazi yake kubwa ni kuchelewesha ukombozi wa Watanzania!
 
mada ya alhamisi ya tarehe 1/3/2012 ya kipindi cha kipimajoto iliyokuwa ikisema " Polisi kuua raia kwa silaha za moto wakitawanya maandamano, je wanaheshimu na kulinda haki za binadamu?" mada hiyo ilionekana kuchakachuliwa ndani ya ukumbi na wachangiaji. Mada iligeuzwa na kwa "wanaharakati kushawishi raia kuandamana, wanaheshimu haki za binadamu?". Nasema hivyo kwa sababu zaidi ya asilimia tisini ya wachangiaji waliwashambulia wanaharakati kwa kuchochea wananchi kuandamana na kuchochea vurugu. Haihitaji mtu kuwa na PhD kutambua kwamba watu walioalikwa kwenye kipindi hicho walikuwa mamluki walioenda kutetea polisi na serikali kwa ujumla. Jambo hili linathibitishwa na makofi mazito yaliyokuwa yakipigwa mara watetezi hao wa polisi walipokuwa wakichangia mada. Neno wanaharakati halikuwepo kwenya mada husika lakini ndilo limetawala mjadala wa leo kwa kutajwa na wachangiaji wengi wakiwemo maafisa wa polisi walioalikwa kwenye kipindi hicho kilichokuwa kinarushwa na televisheni ya itv.
 
kwa hiyo ulitaka wachangie kile unachotaka wewe?

Acha ukahabu wa kuwapenda wanaume polisi hao ni wababa wenye wake zao. Unajipendekeza kwao ili iweje, watafute raia wenzako watatosha kukupa starehe ya kutosho unayoitafuta kutoka kwa hao mapolisi wauuaji.
 
Mnakumbuka walitikiswa ile mbaya na akina Mkuchika wakati wa mafisadi papa. Aliyewàokoa ni JK kupitia Yusuf Makamba! Hivyo lazima aufyate kwa CCM! Ni adui mkubwa kwa Wananchi wanaotaka kujikomboa!
 
Hee! Hamjui Mengi anatumiwa na CCM? sijui anajipendekeza nini kwao, kwani walishamliza kwenye dili ya Kilimanjaro Hoteli. Nashangaa bado anawalamba tu miguu yao!
 
asante sana lakini avatar yako nimeipenda sana,sijui wapi naweza kukuona
Acha ukahabu wa kuwapenda wanaume polisi hao ni wababa wenye wake zao. Unajipendekeza kwao ili iweje, watafute raia wenzako watatosha kukupa starehe ya kutosho unayoitafuta kutoka kwa hao mapolisi wauuaji.
 
Sasa hapo itv na mengi wameingiaje?huo mjadala umechangiwa na wale wananchi,unadhani ni kazi rahs kuwacomfront hao jamaa tena tv!ila salum mkambala,kaniudhi sana leo.
 
Kipindi cha Malumbano ya hoja kilichorushwa na ITV leo usiku kimenishangaza sana. Ni wazi kabisa kuwa wachangiaji waliandaliwa, na pia wale wana harakati waliohudhuria waliingizwa mkenge bila kujua.
Hoja ilikuwa inahusu Mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji.
La kusikitisha na kushangaza, katika kipindi hicho zaidi ya 80% ya wachangiaji waliunga mkono Polisi kuua raia. Amini usiamini. Ndiyo hivyo. Aidha zaidi ya 90% ya wachangiaji waliwaponda sana wanaharakati na kusema wanataka kufanya nchi isitawalike kwa kudai kuwa wanafadhiliwa na nchi za ulaya, jambo ambalo sio la kawaida kusemwa na mchangiaji wa kawaida.
Hata uendeshaji wa kipindi chenyewe ilikuwa wanaposimama wanaopinga ubabe wa polisi mwendesha kipindi anawakatisha maelezo yao. Na wanapoongea wanaopinga maandamano na kuunga mkono uhalifu wa polisi wanaachwa waongee mpaka wakamilishe maelezo yao.
Nadhani ITV inapoteza maana kwa kukubali kununuliwa na mafisadi waoga wa maandamano
 
hivi ukiondoa wageni rasmi walioalikwa hivi huwa unatumika utaratibu gani kuwapata wachangiaji wengine?
 
yaani kipindi cha leo ni full propaganda ya polisi,, watoa mada wote walikua au ni waajiriwa wa polisi au wamenunuliwa kupotosha mada na jeshi la polisi

angalizizo,, kila chenye mwanzo kina mwisho
 
Watu wanapaswa kujua kuwa hata taifa la Marekani limesimama lilipo kutokana na harakati za miaka mingi iliyopita. Tunapaswa kupigania vizazi vijavyo
 
I'm deeply disappointed, kumbe watanzania tumesha gawanyika, kama inafkia watanzania wanashangilia na kupiga makofi dhidi uwaji wa raia unaofanywa na jeshi la polisi. Itv-hofu ni yanini? Hamulipi kodi? Watu wana andamana kwa sababu ya kupuuzwa. Kama maandamano yana poteza ,je mbona kila leo tunajipanga barabarani kisa anapita Pinda ,Mkama,Mama salima ,Rais, Rc,Nape. Acheni kuziba watanzania midomo na kufundisha watu jinsi ya kuongea. Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom