jogoolashamba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 348
- 71
Yawapasa Mwinyi na Membe kuwa wangekuwa wameachia ngazi kwa matukio waliyohusika nayo. Membe kupeleka jeshi Malawi kutangaza vita, na Mwinyi kuharibu silaha za kijeshi.
Membe ana tabia ya kukurupuka ovyo mara nyingi sana na maswala ya kimataifa! Nimemsikia akikataa kwa nguvu sana kuwapa haki mashoga wakati sijaona maandamano ya hao mashoga anaopingana nao. Tanzania ushoga ni kosa la jinai kwa mujibu wa kanuni ya Adhabu, hao mashoga ambao waliopindukia sheria hiyo na kuanza kupambana naMembe ofisini kwake kweli inawezekana. hajaenda polisi kuripoti kuwa anabughudhiwa na mashoga lakini anapanda jukwaani kumlalamikia Cameroon kuwa Tanzania mashoga hawatapewa haki zao. Si kukurupuka huko na kuaibisha Taifa?
Swala la kupeleka majeshi kuzuia ndege za Malawi kuruka juu ya anga ya Malawi lilikuwa la kijinga na la kututia aibu Watanzania. Katika Mataifa ya wastaarabu kama Ulaya Membe angekuwa amekwisha kujiuzulu yeye mwenyewe kwa hiari yake, lakini kwetu Africa ukiwa rafiki wa Bosi hata ukiangamiza kaTaifa kenyewe bado uko huru kuishi na ofisi yako.
Ona Mwinyi alivyolibomoa jeshi,kwanza mabomu yote Mbagala yakalipuliwa, akaanza kwenda kutembelea wahanga sawa na mwizi aliyebomoa usiku asubuhi akaenda kuwapa pole wahanga. Kama aibu hiyo haikutosha kumlazimisha ajiuzulu akaunguza kambi yote ya Gongolamboto. Hakuna askari hata mmoja aliyejeruhiwa, nimeambiwa askari wote waliondolewa kambini kuanzia saa nane mchana. Hata ndege ya SwissAir ilitaarifiwa isishuke mchana saa nane hiyo hiyo. Nasikia SwisAir walishindwa kutekeleza onyo kwa sababu ya dege kubwa lililokuwa limejaza mafuta tele KIA na limeelekeza pua yake chini tayari kushuka, lingejaribu kugeuza pua kuielekeza juu uzito wake ungesababisha likakalia ******. Hivyo dege likalazimika kutua na Mungu Bariki likaruka tena na kuondoka kabla mabomu hayajaanza kulipuka.
Wakazi wa Gongo la Mboto hawakujulishwa wala hakukuwa na maandalizi ya ambulance wala zima moto. Atakayeniambia kuwa mabomu yaliyoanza kulipuka saa mbili usiku yalikuwa ni Accident nitataharuki. Dawa ni mihela ya walipa kodi ipo tele na wahanga wamejengewa mijumba mipya, hakuna hasara. Hata ingekuwa ajali ingemlazimu Mwinyi ajiuzulu, lakini wapi huyooo afya na huko akaenda kumteka nyara Ulimboka, na mpaka leo nchi inajulikana ina wateka nyara lakini hawajulikani, hata watuhumiwa kuhojiwa hakuna lazima. Rafiki wa JK huyo.