Bernard Membe kuongea na Wahariri leo Oktoba 19, 2020

Makumbele

Member
May 9, 2009
65
390
Kuna taarifa za awali zinaonyesha kuwa ‘Kachero Mbobezi’ ndugu Bernard Membe ameamua kufanya ‘maamuzi magumu’ na hivyo asubuhi ya leo mida ya saa 4 anatarajiwa ‘kulipuka’ mbele ya Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar.

Je, tutarajie yepi toka kwa hili ‘joka la mdimu’?

A) Atafanya kama Dk Slaa uchaguzi wa 2015 na kumkataa mgombea wa CHADEMA? Tukio hili hafanyi kwa kushirikisha chama chake cha sasa (ACT-Wazalendo)

B) Atatangaza kumuunga mkono mgombea wa CHADEMA kama ambavyo kiongozi wa chama na mwenyekiti wa ACT wamefanya?

Nitarejea hapa baada ya Membe kuongea
 
Membe ndio nani ? Duh muda unaenda spidi kweli tulishamsahau jasusi mbobezi, hakika atakuwa amemaliza kupiga kampeni, maana yeye kampeni anaipiga nyuma ya pazia, tutarajie kupata ratiba ya tafrija itakoyofanyika pale Hyatt Regency jioni baada ya ushindi :D
 
Kachero Mbobezi BERNARD KAMILIUS MEMBE atakua anataka kutupa Update ya baraza lake la mawaziri aliloliandaa pia kutujulishwa ataapishiwa uraisi magogoni au chamwino.
 
Pamoja na ukachero wake alishindwa kumbaini zitto alichokuwa anatafuta kwake!?
Siku nyingi nimewaambia watu hapa kuwa Membe hajui siasa. Nilimtoa kati ya wanasiasa tangu akiwa anajiandaa kugombea 2015.
Alihojiwa na mtangazaji flani, kwa kujiamini aliongea vitu vya kipuuzi kuwa ana maadui watatu na wajiandae kuhama nchi akiupata urais.
Mtu mjanja na mwenye akili hawezi kuongea hivyo.

Huu ulachero aliupenda lakini ulachero haujawahi kumpenda yeye.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Bernard Kamilius Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, leo Jumatatu saa 4:30 asubuhi atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 
Kuna taarifa za awali zinaonyesha kuwa ‘Kachero Mbobezi’ ndugu Bernard Membe ameamua kufanya ‘maamuzi magumu’ na hivyo asubuhi ya leo mida ya saa 4 anatarajiwa ‘kulipuka’ mbele ya Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar...
Membe ana hali ngumu mno kwani wamefunga A/c zake na A/c za watu wote wanaowaona wakiwasiliana nae hata kama siyo wanasiasa , hana pesa kabsa wamemfirisi, pengine ataongelea hilo au anataka kurejea CCM ili wamrejeshee prsa zake
 
Back
Top Bottom