January, Mnyika wapendekeza kutumika kwa mitambo ya Dowans kupunguza mgao wa umeme

Wakiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo asubuhi, J.Makamba kama m/kiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini na Mnyika kama waziri kivuli wa nishati, wamependekeza ni lazima maamuzi magumu yafanyike ili kuwezesha mitambo ya Dowans kuwashwa ili kupunguza makali ya mgao.

Kwa mujibu wa Makamba, mitambo ya dowans inazalisha MW 120 na itasaidia kupunguza makali ya mgao kwa 60-70%.Wote wametambua uwepo wa swala la dowans mahakamani.

Mnyika: Mnyika amependekeza sheria ya uhujumu uchumi itumike katka swala la dowans. Huku akisema kuwa hawezi kwenda deep zaidi, Mniyka alimaanisha kuwa mitambo ya Dowans inapaswa kutaifishwa sbb ya ukweli kuwa mkataba wa dowans/richmond ni wa kitapeli na huwezi kuwa na mgao wakati mitambo iko pale imezimwa.

Makamba: Makamba emependekeza kuwa usainiwe mkataba wa muda mfupi (hata wa miezi 3) na hao wenye mitambo ili kuwezeshwa mitambo kuwashwa maana kama hakutakuwa na mvua, basi Mtera itazimwa by March. Amependekeza uangaliwe utaratibu ambao hauta athiri kesi iliyopo

Wote wawili Mnyika na Makamba wameonyesha kuwa utakuwa ni uzembe na kichekesho kwa nchi kuingia gizani au kuathiriwa na mgao wakati iko mitambo ambayo imezimwa huku viongozi wa juu wakikaa kimya na kushindwa kuchukua maamuzi magumu.

Wadau hizi hoja mnazionaje?

Mbwa karudia matapishi yake!Nawapa pole sana vijana hao. Wameshindwa kabisa kuona mbali.Lakini naomba waelewe kwamba kwa kukubali kutumia mitambo hiyo, wameipa Dowans legitimacy.Dawa ni kuisusia kabisa.Tuko tayari kukaa gizani kuliko kuwaangukia mafisadi.Au mafisadi wameshawalainisha?
 
Kuna ufumbuzi wa muda mrefu sema tu wanasiasa wanaubania. Nimewahi kusikia ishu ya Steigler's Gorge huko kusini ya tanzania. Kwamba palikuwa na mradi wa kuzalisha mw 2100 wakati mahitaji ya nchi ni kama mw 800, hivyo kungekuwa na ziada ya umeme nchini. Watu wameupiga chini wakisema ni gharama na pia utachukua miaka mingi kukamilika. Ishu ya kuwasha mitambo ya dowans tusianze kumpinga makamba. Hata zitto alipingwa kwa ishu kama hii. After all mvua zimeanza kunyesha. Hope ndani ya miezi 2 mabwawa yatajaa. Kuanzia hapo tuanze kuangalia ufumbuzi wa kudumu
 
Nauliza haya maswali nikiwa na uchungu; naomba ndugu zangu watanzania munielewe na kunieleza ukweli.
  1. Hivi kwa kuendelea kuamini kuwa suluhu la tatizo la umeme ni MITAMBO YA DOWANS (100MW) sisi tuna akili nzuri kweli?
  2. Hivi watanzania tunajua maana ya dhalura?
  3. Hivi sisi tunatunza kumbukumbu ya yaliyopita, mbona Idrisa alituaminisha kuwa njia pekee kunusuru taifa ilikuwa kununua hiyo mitambo la sivyo nchi ingeingia gizani! Mitambo haikununuliwa na giza halikuwapo. JE TANESCO WAMEFANYA NINI TOKEA HAPO?
  4. Kama tuna akili nzuri tunatakiwa tujue kuwa kama mtera na kwingine kukifungwa kwa kukosa mvua, na tukawasha IPTL, Dowans na Songas bado tutakuwa na mgao mkubwa sana
  5. Hivi ni kazi ya wabunge kuamua mikakati ya shirika la Tanesco?. Ningependa wabunge wajadili mipango inayopendekezwa na tanesco na si wao kuwaeleza tanesco na wizara wafanye nini!
  6. Hivi uko mbele ikijulikana kuna matatizo katika huu mkakati wa dharura, je hawa wabunge watawajibishwa na nani?
USHAURI:

  • Hiyo kamati badala ya kuangaika na kuiamulia Tanesco kukodi mitambo ya Dowans, iwaulize tokea kipindi wamezuiwa kununua mitambo hiyo muda wote walikuwa wanafanya nini mpaka leo tena kuna dhalura?
  • Wawaeleze Tanesco hivi; kama tanesco inaamini njia ya kunusulu taifa ni kuwa na mitambo ya 100MW (like dowan) basi wanunue hiyo mitambo wakaenayo standby hapo ubungo!

Naomba kuwasilisha kwa uchungu...........!
 
Here we go again!

The problem with us waTZ and mostly our leaders and politicians usually prefer to take re-active approach to problem solving! We don't usually solve problems but we only cure them!

Pro-active approach to problem solving is the best method to apply. We should solve problems,not only curing them. We should ask ourselves why such problems occur,and then we solve the 'why'.

For the case of power shortage. A lot of pro-active solutions to the problem have been suggested but it is sad that our politicians still persist with their re-active measures.

What shall we do?! Countrywide protests to force the government to take pro-active measures(which usually offers long term solutions) to solve the shortage. If the government fails to hear our concern,then we proceed with protesting to oust the regime.

It is possible,we just need courage and confidence.

AMANDLA!
 
Serikali kama ikiamua kilivalia njuga suala hili najua tz litakwisha bt they are not serious ndio mana hatuoni utendaji ukifanyika zaidi ya taarifa kwamba makali yataongezeka mara dufu sijui mtera itafungwa, hii ni aibu!
 
Haina neno kama kamkataba hako ka miezi 6 katakuwa ni ka bure...kinyume cha hapo nitamuona na Mnyika kesha haribikiwa.

Hawa wa upande wa pil (ccm)i sina matatizo nao kwani tangu mwanzo mkakati wao unajulikana ni kutununuza mitambo ya dowans kwani wameshamlipa fidia. Swali langu kwa mh Mnyika je? ni kwanini aliingizwa kwenye mjadala unaoihusu dowans ambayo shauri lake liko mahakamani? Ni vipi ameweza kufanya hivyo kwenye TV na yeye na chama chake wameshindwa bungeni? Chadema kama chama wanaonaje tabia hiyo ya Mnyika wanaiunga mkono au la? Kama wanamunga mkono mbona kwenye bunge hawa kufanya juhudi zozote za kuana dowans inajadiliwa baada ya kuambiwa suala hili liko mahakamani? tuliwategemea watoke nje ndio staili yao. Kama hawamuungi mkono watamchukulia hatua gani ndugu Mnyika za kinidhamu maana kakizalilisha chama chake.
 
Nauliza haya maswali nikiwa na uchungu; naomba ndugu zangu watanzania munielewe na kunieleza ukweli.

  1. Hivi kwa kuendelea kuamini kuwa suluhu la tatizo la umeme ni MITAMBO YA DOWANS (100MW) sisi tuna akili nzuri kweli?
  2. Hivi watanzania tunajua maana ya dhalura?
  3. Hivi sisi tunatunza kumbukumbu ya yaliyopita, mbona Idrisa alituaminisha kuwa njia pekee kunusuru taifa ilikuwa kununua hiyo mitambo la sivyo nchi ingeingia gizani! Mitambo haikununuliwa na giza halikuwapo. JE TANESCO WAMEFANYA NINI TOKEA HAPO?
  4. Kama tuna akili nzuri tunatakiwa tujue kuwa kama mtera na kwingine kukifungwa kwa kukosa mvua, na tukawasha IPTL, Dowans na Songas bado tutakuwa na mgao mkubwa sana
  5. Hivi ni kazi ya wabunge kuamua mikakati ya shirika la Tanesco?. Ningependa wabunge wajadili mipango inayopendekezwa na tanesco na si wao kuwaeleza tanesco na wizara wafanye nini!
  6. Hivi uko mbele ikijulikana kuna matatizo katika huu mkakati wa dharura, je hawa wabunge watawajibishwa na nani?
USHAURI:

  • Hiyo kamati badala ya kuangaika na kuiamulia Tanesco kukodi mitambo ya Dowans, iwaulize tokea kipindi wamezuiwa kununua mitambo hiyo muda wote walikuwa wanafanya nini mpaka leo tena kuna dhalura?
  • Wawaeleze Tanesco hivi; kama tanesco inaamini njia ya kunusulu taifa ni kuwa na mitambo ya 100MW (like dowan) basi wanunue hiyo mitambo wakaenayo standby hapo ubungo!

Naomba kuwasilisha kwa uchungu...........!

Kuna mahusiano ya hali ya maisha ya watanzania wengi na selfishness ya viongozi/wanasiasa....Ku solve matatizo ya wananchi ni kupunguza income sources za viongozi/wanasiasa. Kwakuwa selfishness ndiyo determinant kwa vyovyote vile ni bora watanzania wale majani, wakae gizani, wafe na maradhi ya uzembe na ujinga ili sisi na wanetu tuendelee kuwa watukufu na wenye kusaza maana tukigawana haitoshi na tukiwawezesha hatutaendelea na mbingu yetu; hapo ndipo tatizo lilipo....Kila anayeingilia himaya hii anaalikwa kwenye karamu na kwa vile selfisheness na motives ndiyo attitude ya watanzania it does not matter anatoka upinzani au chama tawala. Inasikitisha na kusononesha moyo!
 
Mbwa karudia matapishi yake!Nawapa pole sana vijana hao. Wameshindwa kabisa kuona mbali.Lakini naomba waelewe kwamba kwa kukubali kutumia mitambo hiyo, wameipa Dowans legitimacy.Dawa ni kuisusia kabisa.Tuko tayari kukaa gizani kuliko kuwaangukia mafisadi.Au mafisadi wameshawalainisha?

Mkuu Mnyika anasema tapeli kaleta sukari kumbe ni mchanga nasi tumpe pesa feki achimbe kuna tatizo gani?
mitambo itaifishwe wananchi tupate umeme. na iwe funzo kwa wasanii wengine.
 
Wana JF
Rekodi zilizopo zinaonesha Dowans ilikuwa ikizalisha umeme megawati mia kwa kila siku, ule ambao uliingizwa gridi ya taifa na kuuzwa kwa bilioni 1.52 kwa ujumla wake kwa hesabu hii unapotoa gharama za uzalishaji ambazo ni wastani wa sh. milioni 750 kwa siku na bei ya unit moja sh.74.84, kiasi kilichobaki milioni 752 kwa siku inayoingia, na kutoka wataalamu wa hesabu wanena baada ya kutoa milioni 152 ilokuwa ikilipwa kampuni hiyo (Capacity Charge) Serikali kupitia Tanesco ilikuwa ikivuna milioni 600 kwa siku jambo ambalo kamati ya Bunge, Sita wala Mwakyembe wamekuwa na kigugumizi kueleza watanzania ukweli..
Tujadili
 
Ungependa source? Bunge, magazeti..anza na mwananchi..

kwanza aliandika kitabu on Bumbuli, mara akapewa ubunge wa Bumbuli. Alafu akaandika barua kwa waziri wa nishati, mara akapewa uenyekiti wa kamati ya nishati... Huyu mtoto wa Makaamba, mwana wa kaatibu wa chama ambacho RA kakiweka kapuni, je tunaweza kuwa na imani nae?

Na inakuaje wkt bado tuna sakata la tulipe au la, ati tunasema tukodishe au kutaifisha mitambo? Naona mazingaombwe zaidi ya maamuzi ya kisheria au kitaaluma! Umeenda wap uzalendo, wa hiari au kulazmishwa? WAKE UP PEOPLE!?
 
Be informed that JANUARY MAKAMBA is another RICHBUMBULI a.k.a. RICMONDULI in a making.

Take it from me Januari Makamba AMETUMWA RASMI NA IKULU KWENDA KUITETEA DOWANS by hooks and crooks.
Januari Makamba ametumwa kupitia mgongo wa Rostam Azizi/J.Kiwete kwenda kusafisha njia au hali ya hewa kwa DOWANS baada ya Watanzania kupiga kelele za kuzuia malipo ya 94b/=Tshs.

Kile ambacho Watanzania milioni 45 waliaminishwa na Bunge lililopita chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Spika SITA kuwa DOWANS ilikuwa ni Kampuni ya kitapeli/kifisadi sasa Watanzania hao hao wanataka KUSHAWISHISHIWA KUWA HUO ULIKUWA NI UONGO NA KWAMBA DOWANS NI KAMPUNI POA AMBAYO PEKE YAKE NDIYO INAWEZA KUTATUA MATATIZO YA UMEME TANZANIA.

Nawasikitikia Watanzania wenzangu kuwa tu wapole kupita kiasi kiasi cha kuonekana kama ni wajinga. Ingelikuwa nchi zingine kama kwa hao ndugu zetu walioamua kuingia mitaani kuzing'oa serikali zao madarakani kutokana na ufisadi TAYARI WATU WANGELIKUWA MITAANI KUPINGA KUWASHWA UMEME WA DOWANS maana DOWANS siyo kampuni pekee inayoweza kutatua matatizo yetu ya umeme.

Poleni sana Watanzania.
 
Wana JF
Rekodi zilizopo zinaonesha Dowans ilikuwa ikizalisha umeme megawati mia kwa kila siku

Rekodi gani hizo; walianza kuzalisha lini?

ule ambao uliingizwa gridi ya taifa na kuuzwa kwa bilioni 1.52 kwa ujumla wake kwa hesabu hii unapotoa gharama za uzalishaji ambazo ni wastani wa sh. milioni 750 kwa siku na bei ya unit moja sh.74.84, kiasi kilichobaki milioni 752 kwa siku inayoingia, na kutoka wataalamu wa hesabu wanena baada ya kutoa milioni 152 ilokuwa ikilipwa kampuni hiyo (Capacity Charge) Serikali kupitia Tanesco ilikuwa ikivuna milioni 600 kwa siku jambo ambalo kamati ya Bunge, Sita wala Mwakyembe wamekuwa na kigugumizi kueleza watanzania ukweli..
Tujadili

Sijakuelewa; kuwa Dowans walikuwa wanaidai serikali (Tanesco) milioni 600 kwa siku?
 
Mitambo ya Dowans ni ya kutaifisha hakuna haja ya kununua wala kukodisha kwani hata serikali ikununua mitambo ya Dowans bado si suruhisho la kuondoa tatizo la mgao wa umeme, machine zitafanya kazi siku moja mbili watasema zimeharibika na wao wanaendelea kulipwa za bure.
Solution ni kungalia chanzo kingine cha umeme na kuhakisha taratibu za kununua na kuanza kuzalisha tayari utafiti na paper zilishaandikwa na wataalamu kwa vyanzo vifiatavyo
1. umeme kwenye bonde la rufiji (stiglas Gourge) hauitaji mvua)
2. umeme wa makaa ya mawe - Kiwira ipo tayari
3. umeme wa upepo
4. umeme wa mkonge

Mkuu ni kweli usemayo yaani viongozi wetu hawa wameamua kwa makusudi kuihujumu nchi yetu. Kuhusu mradi wa Stiegler's Gorge, jamaa wa Rubada mwaka jana walisema tayari Wachina tena kwa pesa zao walishakuja tayari kwa ujenzi wakawekewa mizengwe bila sababu yoyote. Na Mradi huo ulitarajiwa kuzalisha MW 2100 kwa maana hiyo mgao wa umeme ungekuwa historia. Inaonekana ni kweli kama alivyosema Kafulila kuwa mgao wa umeme ni mradi wa watu. Wanatufanyia makusudi.
Kuhusu umeme wa mkonge jamaa wa Katani LTD kule Tanga tayari wanazalisha umeme wao kutokana na biogas wanayoitengeza kutoka na "waste" zitokanazo na Mkonge. Viwanda vya sukari pia vinazalisha umeme wao kutokana na "baggase" (waste products ya miwa) na kuna kipindi walitaka wazalishe zaidi ili ziada waiuzie TANESCO kama sikosei pia waliwekewa mizengwe. Kwahiyo unaona wazi kabisa kuwa viongozi wetu hawana nia ya dhati ya kutatua tatizo la umeme, wanafanya makusudi na huu ni mradi wa mafisadi, akina RA na kundi lake.
 
Ninakumbuka BWM ktk awamu yake aliintroduce ruzuku kwa Tanesco kila inapofikia misimu ya namna hii na JK alipoingia aliiondoa huku wapambe wakatamalaki eti wameondoa ulaji wa net group lakini wakasahau kuwa 2002-05 mgao ulusahahauliwa nchini. Kwa hiyyo ni kukosekana kwa ujasiri wa maamuzi magumu kuchukuliwa na wauu. Lingine wanasiasa waacha unafiki....
 
Hehehe bongo bwana. Ikanikumbusha mwaka jana nillitwa kwa emergency kwenye nyumba ya tajiri mmoja alikua kapata cardiac arrest. Kufika pale tukahangaika kumpa CPR. Ndugu zake mda wote wanahangaika na kusema ?mpigieni Dr John ni daktari wake mda mrefu, anadawa spesho anampa jamani, mpigieni aje hawa ma docta wengine hawatamweza huyu!!"
Sisi tukabaki kuangaliana na kushangaa,huyu Dr John tunamjua, ni Rural Medical Aid, yani hata sio Clinical Officer acha General Practitioner imekueje awe mtaalam wa moyo wa huyu jamaa??
Anyway 15 mins kaingia Dr John, tukamuuliza haraka Docta ulikua unampa dawa gani akiwa katika situation hii, tusaidie. Jamaa kwa aibu akasema nilikua nampa DICLOPAR tu anatulia, navuta hela yangu naondoka. 2 months later yule jamaa akafariki kutokana na complications za moyo ambazo zingekwepeka kama angefwata utaratibu wa cardiologist. Nani awajibishwe?

Sasa ndio kama Tanzania yangu. Ina ugonjwa wa moyo lakini inapewa Diclopar, ikija kufa nani atawajibishwa??
 
Back
Top Bottom