January, Mnyika wapendekeza kutumika kwa mitambo ya Dowans kupunguza mgao wa umeme

halafu huyu JM alikuwa PA wa mkwere huyu....saa nyingine akili zake sizielewe elewi. Ukimkuta asubuhi utafikiri yupo upande wetu, baada ya chakula cha mchana, anaanza kuonekana kama vile anaelekea alipotoka.
 
Kuna watu walikuwa wanamsifia January pale alipoandika ile barua kwa Ngeleja...ila kuna watu wakasema hilo ni changa la macho..mtaona...huyu ni pandikizi la RA. YAMETIMIA
 
kama ikiwahswa kutakuwa na implications gani na kesi iliyoamuliwa na icc? na je wakikaa chini na dowans tutaepuka kulip ile tuzo ya icc to dowans?
 
Heri tu waiwashe. mimi nimechoka kulala giza
Mwenzangu hata mimi naona ni bora tu waiwashe maana haya mambo hata hayaheleweki.
Mara Dowans mwenyewe hajulikani,mara hooo hii ni kampuni ya mfukoni,mara hoo hata mimi
wenyewe siwajui na sina haja ya kuwajua na sina ubia nayo( kikwete) Leo hii mara wabunge
wamepewa mil.90 za kufanyia anasa za dunia. Mimi nasema bora iwashwe tu tupate umeme.
Nchi hii ukimuondoa Dr slaa,waliobaki wote ni wanafiki pamoja na mie mwenyewe. Nasema
washeni tu hiyo Dowans tufanye shughuli zetu za maendeleo zitumiazo umeme. Nchi hii ina laana!.
 
mbona ile mitambo kampuni ya DOWANS walishaiuza kwa kampuni moja ya Cyprus ..... labda hiyo kampuni ya Cyprus waingie nayo mikataba ...yatakuwa yale yale .... richmond kamrithisha dowans mkataba...halafu dowans kauza mitambo kwa kampuni ya Cyprus..je aliyenunua sio tapeli...?

Nilisoma sehemu hapa hapa JF kwamba hiyo mitambo imeuzwa na aliyeuziwa ataingia mkataba.....Am I dreaming or this was sometime posted here....Mungu mwenye nguvu na rehema...watanzania wana akili kweli.....
 
Embu tujikumbushe ushauri wa Zitto

huyu dogo (mlamba miguu) anasema the same anaonekana eti hero..shame on you
 
Simpendi Mdudu Dowans!
Nafikiri ataifishwe tu na abadilishwe Jina kwani kila nisikiapo jina lake naumia sana! Wataalamu wa sheria liangalieni hili kwa kina na hatua ichukuliwe mara, vijana tupo nyuma yenu!
 
January na Rostam this time imekula kwenu.

Kwanza kabisa suala la upungufu wa umeme march ni myth. Kuna mitambo ya gas ambayo ina matatizo na by march itakuwa imeshafanyiwa ukarabati na kuongeza 100MW kwenye grid. Mafuta ya IPTL yamenunuliwa na kuanzia week hii another 80MW zinakuja kwenye grid.

Sababu mitambo ya Dowans iko ubungo na kinachotakiwa ni kuiwasha tu, hakuna haja ya mkataba sasa hivi hata kufikiriwa. Tusubiri hiyo May kama kweli kutakuwa hakuna mvua na Mtera, Kidatu nk kuzimwa, ndio tuanze kuongea huu upuuzi.

Engineers wa Tanesco wameni brief kuwa ni almost 95% chance by May tatizo la mgao litakuwa halipo na ndio sababu watoto wa mjini wanaahaha kutisha umma kuwe na contract na hao majambazi.

January, this time hamtupati kabisa, kwa sababu baada ya contract ya Richmond kusainiwa kwa EMERGENCY ya uongo, mvua zilianza na umeme wa Richmond ulikuwa hauna kazi hata kama ungefungwa in time.
 
Leo nimeona kutoka tbc kwamba serikali imetangaza rasmi kwamba hali ya umeme ni mbaya na wanajipanga kuchukua hatua za dharura. Hivi sisi ni watu wa dharura tu miaka yote hatuna utaratibu wa kuiona dharura kabla haijafika? Au tunataka kutengengeneza DOwans nyingine!!!!
 
Kwa hali ilivyo ya mkanganyiko wa mambo,nionavyo ni comflict za interest tu...kuna namna tunahujumiwa ili wabariki mitambo yao mufilisi ya DOWANS...
 
Mh. Sitta yuko wapi? Mbona yuko kimya kwenye hili? Au halimhusu?
 
Ni umafia unataka kutendeka hapa, lakini MUNGU wetu ni mwema, atafunua yote hata baada ya miaka. Natamani kujilipua!!
 
Mzee wa intelejensia Criminal Mwema kwani hakuwatahadaharisha na Intelejensia yake kuwa kutakuwa na daharura ya umeme au Intelejensia yake ilikuwa imezidiwa nguvu na Mabwana wake Mafisadi? Toa Intelejensia zako Mwema kama wewe kweli hizo Intelejensia zinafanyakazi au Intelejensia zako zinafanyakazi pale watanzania wanaposimama na kugombania haki yao ndio unakuja na mabomu kuwapiga? Upo wapi criminal Mwema? :coffee:
 
kampuni fake ya mfukoni lakini inaweza kuisaidia nchi kubwa kama hii.....ama nchi yetu ndiyo fake zaidi ya kampuni hii!!!!????????
 
Back
Top Bottom