Januari ashangaa wabunge wengine wamefikaje Bungeni?

Ninauliza kwanini serikali isichukuwe hatua ikatafuta hela ikanunua mitambo mipya ya kuzalisha umeme ikawa mali ya serikali? Kama serikali ina 94B za kuilipa Dowans..........inashindwaje kutafuta hela zingine wajazie 94B hata kwa kukopa ikanunua mitambo brand new? Haingii akilini rais, waziri mkuu na waziri husika wanachokifanya......eti wameridhia Tanesco iingie mkataba mpya na DOWANS!!! Hivi inawezekanaje kuingia mkataba na mwizi ambaye amekuibia na bado una kesi naye? Hawa wakuu wa nchi wanaona ni bora waingie mkataba na mwizi kuliko kutafuta hela ikanunuliwa mitambo mipya ambayo itakuwa vumbuzi la tatizo na mali ya serikali.

Hata jamaa anayejiita mtoto wa mkulima naye ameona ni bora kuingia mkataba na mwizi........hivi nyie wakubwa hamumogopi Mungu? Kwanini mnawafanya na kufikiri watanzania ni wajinga sana? Tatizo la umeme mkuu wa nchi amekiri ni la miaka mingi......sasa ni hatua gani amefanya tangia ameingia madarakani ili kumaliza tatizo lenyewe? Kumaliza tatizo la umeme halihitaji kuwa na digrii hata kijana wa form six anaweza kuweka mipango dhabiti na kumaliza swali hili mara moja! kwa mfano serikali inaweza ikaamua kuuza hisa kwa wazawa wakasimamia hili shirka vizuri mno kwani biashara ni wateja na Tanesco inawateja kila kukicha.

Mimi naona huu ni mradi wa watu fulani wa kujinufaisha ndo maana kila mwaka tatizo la umeme linazidi eti kisingizio ni ukame..........nchi ina miaka 50 ya uhuru bado inatatizo la umeme!! kweli adhabu ya watanzania hamtaikwepa.

Kwa makusudi mmefanya kila njia kumuweka mtoto wa fisadi kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge - nishati na madini eti mnatudanganya JM atatetea watanzania........sisi siyo watoto wa baby class, JM anatetea mafisadi na mpango ni ufanyike mkataba kati ya DWNS na Tanesco, huu mpango unaelekea kufanikiwa kwani hata huko Bungeni hatuna spika wa watanzania bali ni spika wa mafisadi!! Anna makinda kwa muda mfupi tu tumekuona unavyopeleka bunge kwa maslahi ya serikali na mafisadi, sasa sisi watanzania tunakuomba ubadilike usimamie bunge kwa utashi wako otherwise ukiendelea kama ulivyoanza mambo yatakuwa mabaya na yatakugharimu!! Nyie viongozi wa serikali endeleeni kuona watanzania ni wajinga na waoga!! siku zinakuja watanzania watafanya maamuzi! kama mmeshindwa kutambua kuwa mawingu ndiyo huleta mvua basi subirini mafuriko halafu mje myazuie kwa mikono!!!!
 
Amesema kama mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini tayari ameshaanzakazi ya kushughulikia tatizo la umeme nchini kwa maarifa zaidi, ari zaidi, nguvu na kasi zaidi.

Kwa kuanzia wamefanya ziara bwawa la mtera na baadaye watakuwa na kikao cha kamati DSM kwa wiki nzima baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge.
Kweli hii ni kasi, ari na nguvu zaidi, nilitegemea wataanza utekelezaji kwani hawaendi kuangalia kitu kipya. Taarifa zote walizoenda kutembelea zipo.
Huko mtera na vikao ni utafutaji wa posho tu
 
huyo mbona ze comedy tu kama babayake,wala asikuumize kichwa muda uliobaki ni mrefu sana alakini tutatoboa na kuwaonyesha kua nguvu ya umma ni noma.
 
Lazma ashangae wenzie wamefikaje manake yeye kapelekwa pale.. Tehetehe.. Kuiga kwengine bwana.. Kamuiga obama kwenye speech yake ya illinois avokuwa seneta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom