Jamani naombeni msaada mwenzenu tigo imenishinda!

bado upo kwenye hako kamtandao hata wanafunzi wameshihama umebaki peke yako tuko airtel zantel na voda
 
Kama una line ya tigo kaa nayo tuu lakini mtu akikuomba namba mpe ya voda au airtel hata zantel ya tigo usimpe.
 
hivi huu mtandao wa tigo umekuwaje mbona wanafanya uhuni wa kutuibia waziwazi! Jana nimeongeza salio la 5000,nikaongea dk 3,simu inakata eti salio halitoshi!kuangalia nakuta imebaki sh.2!leo nimeweka sh.2000,sijaongea hata dk moja,kuangalia salio limebaki sh.3!kwa staili hii tigo imenishinda,kwani tcra wako wapi?

tigo ni superb black wizard
 
Nimekua nayo tangu ikiitwa mobitel mpaka leo hii ambapo ikifika kuanzia saa 10 jioni kuliko nipige kwa Tigo hata kama ninae mpigia ni tigo bora nitumie airtel. Siku hizi Tigo ni abiria chunga mzigo wako hasa jioni dakika 2 elfu 1 imeisha. Airtel wananiudhi na temporary internet problem hasa kwenye simu. Kwa kweli hata nikiwa naitumia tigo kwa sasa siwezi kuitetea kuwa ni rafiki kiuchumi.
 
Back
Top Bottom