Jamani, kwani lazima?

Akili za ziada ni kitu cha maana sana!!! Akili za paulina ukijikuta nazo bora ungekua mnyama tu.
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-22

ILIPOISHIA
Paulina alirudi nusu saa baadaye na kukuta sebule changuchangu, hakuna kitu kilichokaa kwa mpangilio wakati si kawaida ya nyumba yake hiyo…
“Stela,” aliita.

“Abee.”
“Baba alitoka leo?”
“Hajatoka.”
SHUKA NAYO SASA…

aulina alikazia macho kwenye masofa na kutingisha kichwa cha masikitiko huku Stela akimwangalia kwa macho yaliyojaa woga wa kila aina…
“Kwani nini mama?” Aliuliza Stela…
“Hamna kitu.”

Paulina aliondoka sebuleni akili yake ikimwambia kwamba kulikuwa na makasheshe kwenye viti hviyo ndiyo maana kuko changuchangu lakini sasa atathibitishaje mawazo yake hayo?
Aliingia chumbani ambako alimkuta mume wake amejilaza kitandani kwa ajili ya kupumzika. Alisalimia Paulina lakini katika hali ambayo hakuitarajia, alijikuta akiitikiwa kwa ukali na maneno makali pia…
“Sina haja na salamu yako wewe. Kamsalimie baba Riziki.”
“He! Bado unayo?”

“Ungekuwa wewe ungekuwa huna?”
“Lakini si niliomba tuongee?”
“Nilisema siwezi kuongea, kwani ukweli si unajulikana? Unataka uanze nyuma wakati nimeshajua mbele?”

Paulina hakuwa na la kusema zaidi ya kufunga bakuli lake, yaani kinywa chake! Angesema nini sasa wakati nafsi yake ilishamwambia kila kitu? Akabaki ameduwaa!
“Looh! Hii kali,” alisema moyoni Paulina akiwa amekosa nguvu ndani ya nafsi.

***
Asubuhi kulikucha, mume wa Paulina alitamani sana kuwa na msichana wake wa kazi, Stela. Angefanyaje sasa? Aliamua kuendelea kulala kama vile haendi kazini…
“Leo huendi kazini?” Aliuliza Paulina.
“Siendi.”
“Una nini?”

“Nimekwambia siendi, we vipi?”
“Kha! Jamani si nimeuliza tu?”
“Na mimi si nimekujibu kwamba leo siendi.”
Paulina alitoka na kufanya shughuli zake nyingine akiwa bado na picha ya jana yake ya kukuta vitu sebuleni viko vululuvululu huku na kule. Kwa kuwa mumewe alitangaza haendi kazini hivyo na yeye akaamua asiende kazini kwake ili kulinda au kufuatilia nyendo zake.

Mpaka saa nne asubuhi, mumewe alijua mkewe hatoki, akaoga akajiandaa kutoka.
Akiwa anakunywa chai, alimtumia meseji msichana wa kazi…
“Nataka kukutana na wewe lakini hiki kimeo kipo, itakuwaje sasa?”
“Mimi sijui, nakusikiliza wewe tu,” alijibu Stela.
“Muage, mwambie unakwenda hospitali hujisikii vizuri.”

“Sawa.”
Stela alioga, akavaa, akamfuata dada yake jikoni…
Dada naomba niende hospitali, sijisikii vizuri.”
“Unajisikiaje kwani?”

“Tumbo kama limevimba tena linakata, mwili hauna nguvu halafu macho nahisi yana kizunguzungu.”
“Oke nenda, una nauli?”
“Nauli ninayo, sina fedha ya matibabu.”
“Mwombe baba.”
“Sawa.”

Wakati Stela anakwenda sebuleni, Paulina alitembea kwa kunyata ili asikie mazungumzo yao…
“Baba mama kaniambia unipe pesa ya kuendea hospitali.”
“Shilingi ngapi?”
“Sijui.”

“Sasa kama wewe ndiyo hujui nani anaweza kujua? Nikikupa shilingi elfu mbili je?” Alisema mwanaume huyo huku akisimama kuelekea chumbani kuchukua pesa.
Kwa mbali, Paulina aliondoa wasiwasi kati yake na msichana wake wa kazi na mumewe…
“Angekuwa na uhusiano naye asingemjibu vile,” alisema Paulina.

Stela, baada ya kupokea pesa alimuaga Paulina anakwenda sasa…
“Sawa, pole sana.”
“Asante sana.”
Dakika kumi baada ya Stela kuondoka, mume wa Paulina naye aliondoka bila kuaga mtu. Paulina alisikia mlango ukifunguliwa na kufungwa tu…paa!

“Mh! sijui anakwenda wapi naye? Au ana ahadi na Stela?” Alijiuliza mwanamke huyo.
Hatua kumi na tano mbele, mume wa Paulina aliweka simu sikioni na kuwasiliana na Stela…
“Haloo baba,” aliitika Stela…
“Uko wapi?”

“Huku kwenye duka la Mangi Mrefu.”
“Unaijua Mchepuko Gesti?”
“Ndiyo, si hii hapa jirani na kwa Mangi Mrefu?”
“Ingia hapo sasa, mimi nakuja.”
“Sawa.”

Stela alikwenda kwenye gesti hiyo na kuzama ndani kwa wasiwasi…
“Naomba chumba.”
“Shilingi elfu kumi na tano.”
“Anakuja kulipa mzee.”
“Sawa.”

Stela alipewa chumba, akazama humo na kumsubiri bosi wake.
Mume wa Paulina alifika, akaulizia mgeni wake, akajibiwa chumba alichoingia, akalipa!
Mume wa Paulina hakutaka shoo isiyokuwa na maana, hivyo alivyozama tu akaanza mpambano kwa kumvua nguo zote Stela, akaomba na yeye avuliwe, akafanyiwa hivyo.

Baada ya muda, wote wawili walikuwa katiikati ya maraha wakiburudika, Stela licha ya kuwa hausigeli lakini akatumia nafasi hiyo kumchezesha kwata mwanaume huyo hadi akampa ahadi kibao…
“Yule Paulina atatoka, utakaa wewe kama mama mwenye nyumba, sawa?” Je, unajua nini kiliendelea?
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-23

ILIPOISHIA
Baada ya muda wote wawili walikuwa katikati ya maraha wakiburudika, Stela licha ya kuwa hausigeli lakini akatumia nafasi hiyo kumchezesha kwata mwanaume huyo hadi akampa ahadi kibao…
“Yule Paulina atatoka, utakaa wewe kama mama mwenye nyumba, sawa?”
SASA ENDELEA…

“
Sawa, lakini umwambie,” alisema Stela.
“Nimwambie nini sasa?”
“Kwamba yeye atatoka mimi nitakuwa mama mwenye nyumba.”
“Khaa! Sasa wewe kwa akili zako huoni kwamba nikimwambia tutakuwa tumetibua kila kitu, we ngoja atoke kama kujua atajua siku za usoni.”

Mume wa Paulina alikolea kwelikweli, akashangazwa na mapigo hayo, akaamini ule msemo usemao usiyemjua usimdharau, hakumjua Stela kabla kwa hiyo kumbe hakutakiwa kumdharau wakati yeye awali alimchukulia kama mfanyakazi wake wa ndani tu…
“Stela,” aliita kwa kigugumizi.
“Abe…”

“Kumbe na wewe umo?”
“Niponipo kidogo,” Stela alikuwa muwazi hata kwa mambo ambayo hakutakiwa kuwa muwazi kama hilo. Angekuwa mwingine pengine asingejibu. Mchezo ulikwenda sawasawa hadi wakafika kwenye sherehe za kuhitimu safari yao ambapo wote walipongezana kwa chereko za mahaba.

Waliendelea kudumu ndani ya gesti hiyo kwa dakika nyingine thelathini ndipo walipoamua kuondoka lakini walikubaliana kwamba, aanze kutoka mume wa Paulina ambapo baada ya kuangalia hali ya hewa ampigie simu Stela naye atoke kurudi nyumbani akijifanya anatoka kliniki.

***
Nje ya gesti hiyo alikuwa akipita mwanamke mmoja anaitwa mama Jumanne, pia ni jirani na Paulina lakini si kwa muda mrefu. Mama Jumanne anamjua msichana wa kazi wa Paulina, Stela lakini hakuwa akimjua mume wa Paulina.
Sasa akiwa anapita akamwona Stela anatoka baada ya kupigiwa simu na bosi wake kwamba sasa anaweza kutoka tu.

“Mh! Yule si Stela?” alijiuliza mama Jumanne huku akimtumbulia macho msichana huyo ambaye alionesha dhahiri kuwa alikuwemo ndani ya gesti ile kwa muda mrefu sana.
“Ni yeye, anatokea wapi sasa?” aliendelea kujiuliza mwanamke huyo huku akiwaza jinsi atakavyomfikishia Paulina taarifa ya Stela kutoka gesti.

Stela ndye aliyeanza kufika nyumbani na kumkuta Paulina akiendelea na kazi za ndani kabla ya kutoka kwenda kwenye shughuli zake za kila siku…
“Umetibiwa?”
“Ndiyo.”
“Tatizo nini?”

“Wamesema nisifanye kazi ngumu sana kama zamani.”
“Unaona sasa Stela? Mimi nasema lazima uende kwa mwanaume aliyekupa hiyo mimba, hapa huwezi kunifaa,” alikuja juu Paulina.

Kwa kauli ile, Stela alitamani kumwambia ukweli bosi wake huyo lakini akaishia kusema moyoni…
“Niende wapi wakati mwenye mimba anaishi kwenye nyumba hii?”
“Sasa mama, baba si alisema nitaishi hapa kwa sababu hata yule mwanaume hajiwezi?!”
“Alisema yeye nilisema mimi?”
“Alisema yeye.”

“Sasa yeye ndiyo mimi?”
“Kwani kila mmoja ana nguvu yake ya kusema?”
“Wee! Sikiliza nikwambie, wewe ni mtoto mdogo sana kwa hiyo huna ubavu wa kuniuliza maswali ya kijinga.”

“Hodi,” mama Jumanne alibisha hodi kwa Paulina...
“Ingia, pita,” alijibu Stela bila kujua ni nani!
“Karibu, pita unamjua ni nani aliyebisha hodi?”
“Atakuwa mgeni.”

“Ah! Mama Jumanne, karibu sana,” alikaribisha Paulina.
“Asante, leo nimekuja kukutembelea.”
“Nashangaa, lazima kutakuwa na heri,” alisema Paulina…
“Tegemea pia lisilo na heri,” alisema mama Jumanne huku akiachia tabasamu. Paulina alijikaza kutabasamu lakini kutoka moyoni alikuwa na hali ngumu sana kwa kauli ya mama Jumanne kumwambia pia ategemee lisilo na heri…

“Ina maana kaja ana kitu kikubwa cha kuniambia mimi siyo?” alijiuliza Paulina kwa uso wenye tabasamu feki.
Baada ya mama Jumanne kukaa kwenye kochi, Paulina alimruhusu Stela kwenda kuendelea na shughuli zake…

“Afadhali ameondoka maana kilichonileta kinamhusu huyo msichana wako wa kazi,” alianza kusema mama Jumanne huku akikaa sawasawa...
“Enhe? Niambie…”
“Nimemwona akitoka gesti,” mama Jumanne alisema huku akimsogelea Paulina kwa ishara kwamba hakutaka asikike na Stela…

“Umemwona anatokea gesti?”
“Ndiyo mwenzangu.”
“Wapi?”
“Ile gesti pale jirani na kwa mzee Kwatelo.”
“Mh! Pale kwenye kisima cha maji?”
“Palepale.”

“Alikuwa na nani?”
“Hapo ndipo kwenye mtihani kwangu. Sikumwona mwanaume yeyote akitoka. Pengine alikuwa ndani au alishatangulia.”
Paulina alitamani amuite Stela palepale huku mama Jumanne akiwepo lakini alipomuuliza mwanamke huyo akagoma…

“Utamuuliza mkiwa wenyewe. Tena mimi naondoka zangu, yangu yalikuwa hayo tu,” alisema mama Jumanne na kuondoka zake. Ye alishalisanua basi, roho yake ilikuwa kwatuuu!
“Stela,” aliita Paulina kwa sauti ya ukali…
“Abee mama.”
“Njoo haraka sana.”
 
Back
Top Bottom