Kinamama waache kuendekeza kisingizio cha "Baba yako alitutelekeza", si kila baba alitelekeza mtoto

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
1. Mwanamke kapigwa mimba na mwanaume X anaenda kumtegeshea mimba Mwanaume Y, hapo unakuta Mwanaume Y kategeshewa sababu anajiweza kiuchumi, Mwanaume Y anakuja kugundua mchezo anaachana na mwanamke aliebeba mtoto ambae si wake, wala sio kutelekeza mtoto, ajabu ni kwamba mama anaona aibu kumwambia mtoto kwamba baba yake ni mwanaume X, mtoto maisha yake yote anajua Mwanaume Y aliwatekeleza.

2. Tamaa za mama - hasa kwa mabinti wa mjini type za masista duu na slay queens wanaazuzuka na vitu badala ya utu, mwanamke kajifungua ila baada ya muda anaenda kuishi na mwanaume mwengine na kumkana kabisa baba wa mtoto hataki kuishi nae, atatumika huko kisha anatemwa, atambrainwash mtoto kwamba baba yake aliwatelekeza.

3. Maksudi - hasa kwa wanawake wanaojiweza hupandikiza hii sumu kwa watoto ili wamchukie baba, hata baba akija kuona mtoto anafichiwa mtoto, baba anatuma pesa ila mtoto haambiwi, baba anatuma zawadi mama anasema kamnunulia yeye.
 
Sio kila baba anatelekeza watoto ni sahihi lakini pia wababa wengi wanatelekeza watoto wao.

Hili wala halihitaji utetezi, tena inaanzia pale mna mahusiano vizuri unapata mimba anakwambia toa, ukigoma anakwambia utalea mwenyewe na kweli halei mtoto, huyu hajatelekeza?
 
pole
 
Nakubaliana na wewe, ila kuna muda huwa mnakuaga chanzo ni ninyi mabinti. Kwa hilo ulilosema kama kweli mwanaumebanasema hayo hapo yy ni chanzo, ila kuna tu binti tu ngese sana. Kuna wanaume wanazaa na wabinti na wanahudumia vyema tu. Siku ya siku utakuta ka ugomvi kadogo unaanza kutolewa maneno "una uhakika gani kama huyu mtoto ni wako" mkuu hili lisikie tu, hata kama ulipanga mazuri kwa mama na mtoto lazima urudi nyuma kujipanga upya.

Baada ya muda utakuta anakuambia zilikua hasira tu. Yaani mkuu chanzo anaweza kuwa me au ke. Kuna jamaa zangu wawili yaliwakuta kuulizwa na kebeiwa kuwa mimba sio zao. Au kuna mazingira unakuta huyaelewi, binti hajatulia unashindwa kujua ni yako kweli au umegeuzwa chuma ulete tu.
 
Back
Top Bottom