Ivory Coast Vs Tanzania

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Mechi hii ya kwanza ya kuwania kufuzu kombe la dunia 2014, itachezwa saa 2:00 usiku (EAT) kwa mujibu ESPN Soccernett katika uwanja wa kumbukumbu ya Felix Boigny mjini Abidijan.
Updates nitaomba ziwekwe hapa pamoja na link za kutazama game. Na kama kuna anayefahamu kituo cha televisheni kitakachoonesha mechi hiyo kwa hapa nyumbani atuambie.
 
jamani, na mimi natamani kuangalia hii mechi, pamoja na kwamba mimi sio mwana simba, naamini leo watacheza vizuri ili kujilinganisha na wenzao wa yanga waliokuwa at least hawafungwi bao nyingi sana...nasema hivi kwasababu kipindi cha nyuma wengi wa wachezaji walitoka yanga, sasa wanatoka simba sasa hawa wekundu wasijefikiri wanacheza na yanga iliyokuwa kwenye migogoro ikaamua ifungwe tano bila kwa makusudi, na simba nao wameridhika kuona kama wao wanaweza sana mpira, kumbe simba wamefanyika kiboko cha wanayanga kuuuchapa uongozi mubovu......Mungu ibariki Tanzania, Mungu isaidia Taisfa stars:lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel:
 
Naomba kujua mechi ya mwisho kati ya Yanga na Simba matokeo yalikuwaje....kama hujui usini jibu....!?
 
Naomba kujua mechi ya mwisho kati ya Yanga na Simba matokeo yalikuwaje....kama hujui usini jibu....!?
ilikuwa ni tano bila, lakini yanga walifanya makusudi, walizembea makusudi kama adhabu ya kuwaadhibu viongozi wao kutokana na mgogoro uliopo....ni kama vile unaenda kuwinda, afu digidigi anakuja home kwako anaingia ndani anakaa sebuleni, utakachofanya pale wewe hutumii ujuzi wowote, wala ile mitego uliyozoea anayokusumbuaga kule porini, unaingia ndani unachukua kisu unamchinja,...lakini ni mteremko....kama kusingekuwa na mgogoro, simba ingefungwa na yanga kama ilivyo kawaida yao.....yanga oyeeeeeeeeeee
 
Tuwe wastaarabu kidogo, timu ya Taifa imeshachaguliwa. Sioni kama kuna busara kuiita ya Tanganyika au Simba. Badili hiyo heading toka Tanganyika weka Tanzania. Na mambo ya utani wa Simba na Yanga yasijadiliwe kwanza, au muanzishe thread nyingine.
 
Na hiyo ndo timu ya Taifa tuliyonayo, vyovyote itakavyokuwa hiyo ndo Taifa Star na bendera waliyopewa kwenda nayo ni ya Taifa, jezi zao zina nembo ya TFF na rangi za bendera ya Taifa, mimi mwenyewe nimepiga uzi wa Taifa star hapa nilipo nasubiri kuangalia vijana wa Kim Poulsen kuona watakavyopeperusha bendera ya Taifa, Kila la heri Taifa star: kwa kumbukumbu kikosi kinaweza kuwa: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris, Shaban Nditi, Sure boy, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.
 
Tuwe wastaarabu kidogo, timu ya Taifa imeshachaguliwa. Sioni kama kuna busara kuiita ya Tanganyika au Simba. Badili hiyo heading toka Tanganyika weka Tanzania. Na mambo ya utani wa Simba na Yanga yasijadiliwe kwanza, au muanzishe thread nyingine.

Nakubaliana na kila ulichosema Hapo wanaoandika hivyo ndio wachocheo wa ujinga na kukosa elimu na bila kuona mbele mazara yake Elimu ni muhimu lasivyo mtashindana ubishi wa kijiweni mpaka kesho.
 
ilikuwa ni tano bila, lakini yanga walifanya makusudi, walizembea makusudi kama adhabu ya kuwaadhibu viongozi wao kutokana na mgogoro uliopo....ni kama vile unaenda kuwinda, afu digidigi anakuja home kwako anaingia ndani anakaa sebuleni, utakachofanya pale wewe hutumii ujuzi wowote, wala ile mitego uliyozoea anayokusumbuaga kule porini, unaingia ndani unachukua kisu unamchinja,...lakini ni mteremko....kama kusingekuwa na mgogoro, simba ingefungwa na yanga kama ilivyo kawaida yao.....yanga oyeeeeeeeeeee
haya maelezo hayafanani na hali halisi,huwezi kuchafua historia ili kumkomoa nchunga. Tatizo la yanga,! Ni kuamini kuwa kila timu inayofungwa na Simba ni mbovu, sasa imetokea kwao na hawataki kukubali kuwa ni wabovu wanaanza visingizio , ooo... Wazee waliamua timu ifungwe ili kumkomoa nchunga. Mlifungwa sababu timu ilikuwa haina uwezo uwanjani.
 
Back
Top Bottom