Ivory Coast Vs Tanzania

Jamani wekeni uzalindo kwanza...ni timu yetu na wengine tunaipenda sana.

Sijui uzalendo upi maana kwenye title ni utata mtupu kwenye content napo utata mtupu....kifupi mleta mada na stress za kupigwa tano bila na wekundu wa msimbazi hivyo leo anatamani timu ya taifa ambayo inawachezaji wengi wa simba ifungwe hata 10 nadhani itafurahi sana....
 
Game nasikia itaonyeshwa,
WITO unatolewa,WITO unatolewa kwa wapenzi wote wa soka Tanzania kuiangalia game kwa umakini,isije baadaye watu tukaja kutoa tathmini zetu hapa zitakazohusisha ranks za performance ya ndani ya pitch watu wengine wakaanza ooh unazi sijui u'tui tutaonana wabaya!
 
Unajua Mkuu hakuna mtu anayeombea mabaya hapa tunaongelea reality.Cote de' Ivoire na Simba Mseto wapi na wapi?
Ni sawasawa na mtu analala katikati ya barabara highway gari zinakuja tunasema yule atagongwa unasema tunamuombe mabaya,kufungwa tunafungwa tena za kutosha,hilo halina ubishi, wee subiria
Mkuu mpira hauko hivyo, mpira sio uwezo tu ni pamoja na bahati, unaweza kuamini kama Ufaransa waliondoka bila kushinda mechi hata moja kombe la dunia 2002 na walikuwa na washambuliaji nyota kabisa watatu wa daraja la dunia, huwezi jua leo bahati inaweza kuwa upande wetu ukashangaa kila cross ya Gervinho Drogba akipiga kichwa inagonga mwamba au inatoka nje au Kaseja anadaka halafu ghafla dakika ya 88 Ngasa akanasa pass ya Salum Abubakar na kukimbia nao huku Samatta akifuatia kwa kasi na mara Ngasa anafyatua Kombora ambalo Barry anapangua na kurudi uwanjani halafu inakutana na Samatta anamaliza kazi. Itakuwaje hapo? lazima uzime TV.
 
Mkuu Masuke acha kubishana na punguwani anae leta ushabiki wa kwenye vijiwe vya kahawa na kuuleta hapa JF.
 
Hivi ikitokea vijana wakatoa sare si unaweza ukavunja computa yako kwamba haikuletei habari za ukweli.

Lazima tuandamane manake timu yetu haina uwezo huo na hata wachezaje wetu pia wanajua hilo wamekula lift mpaka huko tu na selection yenyewe siyo nzuri ni simba tupu.
 
Matokeo ya mechi nyingine za za leo

Kenya 0 - Malawi 0
Afrika ya Kati 2 - Botswana 0
Misri 2 - Msumbiji 0
Cameroon 1 -DR Congo 0 (pen)
 
hahaha, haki ya kweli, inawezekana walipofika pale waliuliizia kwa wenyeji kaama timu yao ina migogoro, wakaambiwa hamna mgogoro wowote, sasa mimi sijui nifanye nini, manake naona moyo utauma sana na mapresha kupanda na kushuka kushangilia timu ambayo najua asilimia mia moja kuwa leo inafungwa....cha kuomba Mungu ni kwamba wafungwe machache basi, na wachezaji wa simba wasiwashangae akina drogba, wacheze booli.

Barcelona na chelsea -uefa ulikuwa unajua kuwa nani atapita? Kuwa mzalendo mpira unadunda acha pumba
 
walitoa ngapi ngapi?

Yaani unataka kuniambia umesahau?,mbona game ya nyuma zaidi ya ile ya 5-0 unaikumbuka vizuri,anyway nitakukumbusha...Simba a.k.a Taifa Stars ya sasa hv ilipigwa 3-0 kwenye regulation time, hlf 9-8 kwenye matuta.
 
Naona timu ndio zinaingia uwanjani,TV RTI 1 ndio inayo onyesha mechi hii

ivory cost imeingiza kikosi kilekile kilichotuumiza

kwa sasa naona bendi ya jeshi ipo uwanjani
 
naona vijana walioshika bendera tatu ndio wanaingia uwanjani na tayari timu zote mbili zipo uwanjani
 
Back
Top Bottom