iSIM ni teknolojia mpya ambayo itaondoa mfumo wa eSIM

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Apple Updates 1 copy.jpg


Teknolojia inazidi kukimbia na kila siku teknolojia mpya inatokea na kubadilika.

Wiki hii katika kongamano la Mobile World Congress (MWC) 2023; teknolojia mpya ya iSIM ilitambulishwa rasmi na kuonyesha ni teknolojia ambayo itakwenda kufuata baada ya eSIM. Ni teknolojia mpya ambayo itakwenda kubadilisha mfumo wa matumizi ya kuweka laini (SIM Card) za mitandao ya simu ndani ya simu. Miaka ijayo mfumo wa iSIM (Integrated SIM (iSIM) utatumika zaidi ya mfumo wa eSIM.

SIM card ni teknolojia ya kutumia laini ya simu na ilianza mwaka 1991. teknolojia hii ilianza kuchukua umaarufu kuanzia mwaka 1997 mpaka 2013. Na mpaka sasa kwa nchi nyingi inatumika sana na imekuwa ikibadilika kwa kupunguzwa kwa ukubwa wa laini ya simu.

Mfano SIM card (1FF) ya mwanzo ambayo ni sawa na size ya kadi ya benki na ilitumika miaka ya kutumia simu za kulipia (mfano TTCL za zamani); mwaka 1996 ikafuata size ya mini-SIM (2FF) ambayo ni SIM card ya laini za simu za vitochi ambazo sio smart phone. Mwaka 2003: ikaanza Micro-SIM (2003) ambayo ni laini ndogo ya kukata. Mwaka 2012 ikaanza line ndogo kabisa ya nano-SIM (4FF) ambayo inatumika kwenye iPhone na Smartphone mpya kwa sasa.

image.png

Mwaka 2016 teknolojia ikahamia katika mfumo wa eSIM. Huu ni mfumo ambao simu inakuwa na modem maalum ambayo inakubali kuwa na mtandao wa aina yoyote bila kulazimika kutumia laini ya simu (SIM Card). Ni teknolojia ambayo bado ndio imeanza na haipatikani kwa watumiaji wengine duniani.

Mwaka 2023; ni mwaka ambao tunashuhudia teknolojia mpya ya iSIM ambapo kirefu chake ni Integrated SIM (iSIM). Hii ni teknolojia ambayo inaelekea kufanana na eSIM kwa sababu haitumii SIM Card (laini ya simu) lakini tofauti yake ni kuwa processor ya simu ndio inakuwa na uwezo wa kupokea mawasiliano badala ya kutumia modem maalum; teknolojia ya iSIM ilianza mwaka 2021 lakini haikuanza kuwekwa katika simu na vifaa vya matumizi ya kawaida.

Faida nyingine ya iSIM haitumii charge nyingi na kumaliza betri ya simu kwa sababu kwa kawaida modem ya eSIM inatumia umeme ukilinganisha na iSIM; lakini iSIM inakwepo kwenye processor ambayo tayari inatumika kwenye simu kama ubongo wa simu. Hivyo hakuna umeme wa ziada unaotumika ni power ile ile ya processor ndio ambayo inatumika kwenye mawasiliano.

Bado utaratibu wa kuunganisha mtandao wa simu na simu yako utafanana na utaratibu ambao unatumika katika simu ambazo zinatumia mfumo wa eSIM. Utaratibu wa kuunganisha iSIM utafanana na eSIM hivyo itakuwa ni rahisi kwa mitandao ya simu kuunganisha na iSIM. Utofauti utakwepo katika teknolojia ya ndani ya simu.

Kwa ufupi, ni kwanini iSIM zitachukua nafasi zaidi ya eSIM:​

  • iSIM inatumia kiasi kidogo cha umeme na nguvu ya simu zaidi ya eSIM. Hivyo inatunza charge inakaa kwa muda mrefu katika simu, zaidi ya eSIM.
  • iSIM inasaidia kupunguza nafasi kubwa ya modem na mfumo wa eSIM hivyo inaweka nafasi ya speaker na vifaa vingine vya simu kupata nafasi ndani ya simu.
  • iSIM ni salama zaidi kwa sababu processor ina uwezo mkubwa wa security na kusimamia mfumo mzima wa mawasiliano
  • iSIM inarahisisha kila simu kuwa na uwezo wa kutumika bila kutumia SIM Card kwa sababu haiitaji modem maalum ya kuunganisha mawasiliano.
Qualcomm imekuwa ni kampuni ya kwanza duniani kuweka mfumo wa iSIM katika ubongo wa simu wa Snapdragon 8 Gen 2. Samsung itakuwa ni brand ya kwanza kuwa na teknolojia hii na itachukua nguvu mpya zaidi ya eSIM.

Chanzo cha Habari
iSIM ni teknolojia mpya ambayo itaondoa mfumo wa eSIM
iSIM (integrated SIM): key features, benefits and perspective (2023)
https://www.qualcomm.com/news/releases/2023/02/qualcomm-and-thales-unveil-world-s-first-gsma-compliant-isim-wit
 
Huku bongo tuko nyuma sana bado bei za bando za internet zinatuhangaisha.. eSIM kibongo bongo naskia ni TTCL pekee ndo walikua nayo hii huduma japo sina hakika mpaka sasa still ipo na wanaitoa hii huduma..........
 
Makafr Yako Mbali Sana Kwa Technology
Acha Watuletee Maajabu Nasi Tutumie Taratibu Sasa Number Za Simu Zinabaki Zile Zile
 
Now Airtel, Vodacom na tiGO washaleta hii huduma..

1. Airtel ku activate ni bure

2. Vodacom ku activate ni 6000

3. tiGO ku activate ni 5000

.............................................................................
 
Back
Top Bottom