Teknolojia mpya ya roboti wa ai kwenye mwc, barcelona

TTCC_TECNO

Member
Oct 23, 2023
22
10
Upo tayari kujua tunachokuletea leo? TECNO ilitambulisha Dynamic 1, mbwa wa AI roboti, katika MWC pale Barcelona mwaka huu wa 2024 Februari 26. Kwa muundo wake rahisi kutumia na vipengele vya kisasa, inawakilisha dhamira kuu ya TECNO iitwayo "STOP AT NOTHING” Dynamic 1 inalenga kufanya maisha yawe rahisi, kwa upande burudani hadi elimu, ikiahidi mabadiliko makubwa katika teknolojia.
1709639881911.png
1709639899337.png
1709639917390.png

Teknolojia mpya ya kisasa kuboresha jinsi binadamu na mashine wanavyoweza kushirikiana.

Dynamic 1 ni roboti mpya wa TECNO ambayo ni mchanganyiko wa AI na muundo uliohamasishwa na Mbwa aina ya Germany shepherd, mwenye taa maalum zinazomulika pindi anapowasiliana na binadamu. Pia ina mikrofoni nne na ufahamu wa sauti, hivyo ana uwezo wa kusikiliza na kujibu kwa ufasaha.
1709639970666.png
1709639983807.png
1709640003059.png
1709640019472.png

AI Hyper Sense inawezesha mwendo mwepesi wa Dynamic

Jambo bora kuhusu Dynamic 1 ni kwamba inatumia sensori za kisasa na teknolojia ya AI kusonga kwa urahisi na kuepuka vikwazo. Harakati zake zenye nguvu na za haraka zinasukumwa na CPU yenye utendaji mkubwa, ikiruhusu utulivu, kupona haraka, na kasi hadi 3.7m/s. Na uhifadhi wa 64GB na WI-FI 6, inahakikisha utendaji wenye uhakika.

Njia tofauti za kudhibiti Dynamic 1 na utendaji wake endelevu.
Kwa kuongezea, Dynamic 1 inakupa chaguo la kuidhibiti: kupitia programu ya simu, kwa kutumia kiremote, au kwa amri ya sauti. Inatumia betri ya 15000mAh na inaweza kufanya kazi hadi dakika 90. Muundo wake wa modula unakuwezesha kubadilisha betri haraka, na inaweza kuchajiwa wakati unaitumia. Vipengele vya usalama vinahakikisha kuwa inalindwa kutokana na matatizo ya umeme.

Hatimaye, kwa kuanzisha Dynamic 1, TECNO inaonyesha ujuzi wake katika roboti za kisasa na AI. Kampuni hiyo imejitolea kuunda teknolojia ya kisasa kwa watumiaji.
 
Hapana boss ni robot wa AI alietambulishwa na TECNO ambae yupo design ya mbwa anaesaidia kwenye shughuli za kila siku
Mkuu kama unawakilisha TECNO na naamini kwa nchi zetu mtamotivate sana watu kununua hizo AI bot.
Lakini hujaongelea sana features ambazo Hilo bot litakuwa linatumia mfano connectivity, Awareness kwamaana bot litatumia camera n.k

Sasa hizo features kwenye upande wa black hat ilitakiwa tuziangalie.
Mfano kama bot itaweza kuaccess data je awareness ya Hilo bot lilipo kama litatumia camera au gps JE halitaexpose location ya user/admin ?

Maswali ni mengi ya kujiuliza kutoka a na matumizi ya Kila siku, na unawaaminisha vipi wateja kwamba bot wanaweza kuwa nalo hata chumbani isijekuwa ya gi*y.

Hebu kama unatueleza tuelezenii vizuri kwasabu waliosoma quba hata flat hawaweki chumbani.
 
Back
Top Bottom