Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Webs,
Salaam popote ulipo.
Naamini uwezo wa kufikiri na siwezi kuhoji elimu yako. Naijua.
Kwanza kabisa mimi ni MwanaCDM na nitachangia kama mmoja wa wale ambao umewashutumu kwamba hakuna wanachokifanya na hawana tofauti na CCM.
Naamini kwamba kuna mengi ninayoyafanya kwa nchi yangu na siko kama CCM hata kidogo.
Hii nchi imefika hapa ilipofika kwa sababu yako wewe. Wewe ndie wa kulaumiwa.
Kwa wepesi wa kutia moyo umeweza kutoa hasira zako. Sio kwa sababu huipendi nchi yako bali hujui jinsi ya kuisaidia. Kwa elimu yako na uzoefu wako ningetegemea ulione hilo.
Wewe na wengine wengi ambao mmekaa pembeni, hamshiriki katika uongozi wa vyama vya siasa wa serikali badala yake mnakuwa wepesi kulaumu 'vyama' ndio wakulaumiwa. kulaumiwa sana. CDM, CUF, CCM, NCCR etc ni vyama Waberoya. Ni vyama vinavyoundwa na watu. Viongozi wa taifa wa CHADEMA hawafiki mia moja (100)!! Viongozi wa Mikoa na Wilaya zote hawazidi mia tano (500). Wengine wote ni watanzania. Sasa unaposema watanzania hao hawafanyi lolote hivy 'tuwafute' halafu nani afanye sasa?? Is this not contradictory??
Ukweli unaoupinga kwenye nafsi yako ni kwamba CDM na vyama vingine havina wafuasi Milioni sita. Hakuna wanachama milioni 6 wa CDM wala CUF. Wananchi watu wazima wapo zaidi ya Milioni 20. Sasa hata ukivifuta CDM na CUF inakuwaje?
Nisaidie, nisaidie kufikiri, je ni wana CDM na wana CUF walichagua CCM? Unapotushambulia kosa letu ni nini? Kuichagua CCM au kutoichagua CCM.........hoja hii nitaianzishia thread yake ili ichangiwe vizuri. Ila tafadhali nijulishe.
Kwa muda wote utaoendelea kuwa 'mimi sina chama chochote vyama vyote ni kama CCM' basi nchi hii itaendelea kuwa kama ilivyo. Hasira unazopata wewe ukiwa pembezoni ni robo ya hasira ninazopata mimi niliyeko ndani ya uozo huo unaosikia harufu yake kwa mbali. Sogea karibu uusikie vizuri tufanye kazi ya kuondoa. Kupiga kelele huko pembezoni hauna tofauti na CDM au CUF waliokimya!!
Ukimya na kelele za pembeni ni kitu kilekile.
Otherwise, tutaendelea kujadili.