Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 12,965
- 21,878
It was expected......Wasafi walikuwa wanaitest Mamalaka inayojifanya nafiki nafiki......sasa Wasafi wamejua Ubaya sio Lissu bali.......Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.
Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM
---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X
Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.
Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.
Updates
Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi