Intern doctor kwa Tanzania...

Mhubiri

Senior Member
Feb 12, 2008
180
21
Dada yangu amemaliza masomo yake ya udaktari wa binadamu mwezi huu,nchi moja ya Ulaya.Kuna nchi nyingine amepata nafasi ya kufanya internship lakini mwenyewe amesema,anapenda zaidi kuja kufanya internship yake Tanzania ili apate uzoefu zaidi kwa vitendo kwavile kuna wagonjwa wengi na madaktari ni wachache.

Ana maswali yafuatayo:
1.Kama atakuja mwezi ujao wa November,itamchukua muda gani mpaka atakapoanza kufanya hiyo internship?Yaani mchakato mzima wa kutuma maombi,kukubaliwa nk huwa unachukua muda gani?

2.Ni wapi pazuri kufanya internship na kujifunza zaidi kati ya Muhimbili na hospitali za Wilaya za Dar kama Mwananyamala au Temeke au Hospitali za Mikoani na Wilayani?

3.Kwa siku intern doctor anatakiwa afanye kazi kwa masaa mangapi?Ni jumatatu mpaka Ijumaa au hata weekends?

4.Je kuna posho/mshahara?Ni shilingi ngapi kwa mwezi?

5.Atapata likizo?Kwa mwaka ni wiki ngapi?

Madaktari na wakuu wengine mnaofahamu,naomba majibu tafadhali
 
MAJIBU:

1. Ndani ya wiki moja anaweza kuwa tayari ameshapata sehemu ya kufanya internship. Ila lazima asajiliwe na TCU.

2. Hospitali za Wilaya kama Mwananyamala, Amana na Temeke. Muhimbili kuna overstaff ya specialist ie Maspecialists na Mapostgraduates.

3. Unapofanya Internship dhamira ni kujifunza zaidi, unaweza kufanyakazi 24 hours sometimes if your on call, na zaidi ya masaa 12 kama hupo duty za kawaida.

4. Basic salary ya Daktari.

5. Internship huwa ni period ya one years yaani exactly 12 months. Baada ya hapo unaweza kujipa likizo mwenyewe iwe ya mwaka au miezi sita is up to you.
 
asante mkuu Mahmetkid kwa majibu mazuri.Nitamtumia kama ulivyoandika.Unaweza pia kunitajia basic salary ya Daktari ambayo ndiyo mshahara wa Intern doctor?
 
asante mk
uu Mahmetkid kwa majibu mazuri.Nitamtumia kama ulivyoandika.Unaweza pia kunitajia basic salary ya Daktari ambayo ndiyo mshahara wa Intern doctor?

posho ya intern doctor ni 80% ya basic salary ya daktari...na kama anataka uzoefu zaidi aende hospital za mikoani,,,,hamna likizo
 
mkuu asante..lakini swali lake ni kujua kiasi cha pesa maana hata huo mshahara wa daktari Tanzania hafahamu na binafsi sijui.Unaweza kuandika ni Tshs ngapi?Kwa mfano laki 2 au 4 au laki tano?
 
angalia ur inbox

shukran mkuu kwa majibu yako mazuri..swali la mwisho..kama atafanyia nje internship,let's say Ulaya,halafu akataka kuja kufanya kazi Tanzania kama daktari,atapokelewa na kuanza kazi moja kwa moja au itabidi afanye tena internship Tanzania?
 
Nadhani itabidi arudie ila nimembiwa kuna nchi ukifanya intern ukija bongo ni moja kwa moja ila majority naona wanarudia kufanya wakifika bongo.....ila usitie shaka kurudia maana ni muhimu kujifunza health system ya bongo kabla hujaingia kazini jumla jumla ukizingatia pia atapokea 80% ya mshahara wa daktari si haba...
 
Mkuu La Cosa Mia,nashukuru.Huyu binti pia amepata nafasi ya kufanya internship Ulaya.Lakini baadaye lengo lake ni kurudi Tanzania.
Hizo nchi ambazo akifanya intern hawezi kurudia tena Tanzania,ni za Afrika au hata nje ya Afrika?Unaweza kuzitaja?Lakini kama ulivyosema,hata akirudia tena intern pia si mbaya.Nitamjulisha
 
Sina uhakika kati ya china au russia....mimi mwenyewe nasoma MD nje ya nchi na nitafanya intern huku ila najua na bongo nitarudia pia ila sio mbaya....
 
nikiri leo ni moja ya siku nilizogain vitu vya muhimu,although sisomi medicine but nimejifunza vitu vya muhimu hapa.Asanteni wadau
 
Back
Top Bottom