Innocent Killer (The Revenge)

STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA TISINI

SONGA NAYO................

Upande wa gereza la Segerea majira hayo ya asubuhi, iliingia gari mpya kabisa ambayo haikuwa hata na plate number. Bmw X7 ndiyo gari ambayo ilionekana hayo maeneo, kwanza walishangaa sana gari inatembeaje barabarani huko bila kuwa na plate number? Hakuna mtu ambaye alikuwa na jibu juu ya hilo jambo ila nadhani walikuwa na imani kwamba mhusika mwenyewe alikuwa hapo kwa ajili ya kuwapa majibu sahihi kabisa kwamba ni kipi ambacho kilikuwa kinaendelea.

Kumbuka hilo tukio lilikuwa linaonekana moja kwa moja kutoka upande wapili. Jason ndiye mtu ambaye alishuka kwenye hiyo gari ya kifahari ambayo bei yake sio chini ya milioni miamoja za kitanzania. Mwanaume huyo baada ya kushuka aliiweka suti yake vyema na kuanza kujongea kuelekea lango la kuingilia ndani kabisa, hakuwa na wasiwasi na hiyo gari yake ndiyo maana aliiacha kwenye eneo ambalo hakuwa na imani na usalama wake ila alijua hakuna mtu ambaye anaweza kuigusa.

Alijongea taratibu mpaka langoni, kitu cha ajabu ambacho huenda kwake yeye hakikuwa kigeni sana ni kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye alimkagua pale, alipita kama vile alikuwa ni raisi wa nchi, alitabasamu kwa mbali sana kwa sababu alikuwa anaelewa kitu ambacho kilitakiwa kufanyika humo ndani. Kitu ambacho kwake na kwenye mahesabu yake hakikuwa sahihi kabisa, ni kwamba hakujua kama hilo tukio Monalisa anaweza kuwa analiona moja kwa moja japo alielewa kwamba kuna watu ambao waliutengeneza huo mchezo walikuwa wakishuhudia kila hatua mambo yanavyo kwenda.

Jason baada ya kukata kona kadhaa alikutana na maskari mbele ambao walikuwa wa kutosha huku wakiwa wanaongozwa na mkuu wa gereza hilo ambaye alikuwa katikati, kiburi kikiwa sehemu ya maisha yake kwani yeye ndiye mtu pekee ambaye alikuwa na mamlaka ya juu zaidi hilo eneo.

“Bwana mdogo nasikia umekuja hapa kumuona ndugu yako, mtu ambaye inasemekana umekuja kumuona ni mtu ambaye ana kesi nzito sana ya mauaji ya watu wakubwa sana ndani ya nchi hii, sasa vipi kama nawewe tukianza kukuhisi kwamba huenda mpo kundi moja na huyo mtu ambaye alikuwa anajificha kweye vazi la polisi halafu kumbe ni mshenzi tu?” Jason alimwangalia sana huyo mzee ambaye alikuwa na kitambi kikubwa sana, rushwa ilionekana kumkubali sana kwenye mwili wake.

“Una mtu yeyote ambaye anakutegemea wewe ili aishi?” Jason aliongea kwa sauti nzito mno mikono yake ikiwa kwenye suruali ya suti yake safi ya bei ghali.

“Haahhaah hahahaha upo kwenye himaya yangu halafu unataka kuleta jeuri? Nisikilize bwana mdogo hapa kuna mambo ambayo mimi ndiye nayapanga, ninaweza kukufanya ukutane na huyo mtu wako au usikutane naye na vile vile ninaweza kukukamata kwa kukupa kesi ya kukosa nidhamu kwa mkuu wa gereza ukajikuta unaishia pabaya sana”

“Nenda kwenye ofisi yako ukae pembeni uwe mbali tu na haya mambo yanavyo endelea, najua umewekwa tu hapo kama toi na hujui chochote kuhusu haya mambo wala haunifahamu kwamba mimi ni nani. Jina lako unaitwa Mr Kasisi, una watoto saba, watatu umezaa na mkeo wa ndoa na hao wanne umezaa na wanawake wa kwenye madanguro. Hii ni siri ambayo hautaki ijulikane popote pale kwa sababu ya kukwepa aibu kubwa ambayo itakufanya utolewe kwenye hiyo nafasi yako, sasa utaamua mwenyewe kama ufunge mdomo wako kwa amani ili uiokoe nafasi yako au uendelee kunipigia makelele na kunipotezea muda hapa ili niziweke video zako hadharani kila mtu ajue namna watu kama nyie mlivyo wachafu” Jason aliongea kitu ambacho kilimshtua sana mzee huyo, aliogopa mno.

Hizo ni moja ya siri nzito sana ambazo alizifukia yeye kama yeye kwenye moyo wake ila leo kuna watu ambao hata yeye mwenyewe hajuani nao na walikuwa wana habari zake zote, mkurugenzi wa usalama wa taifa atashindwaje kuzipata taarifa zake? Pole kwake huenda hakujua aliye simama mbele yake alikuwa ni nani.

Mzee huyo na hao askari wake waliondoka wakiwa na hasira kali sana, yeye ndiye alikuwa kiongozi wa hilo gereza ila kuna watu walikuwa wanaweza kumpangia cha kufanya na kipi cha kuto kukifanya bila hata kumheshimu. Hakuwa na namna nyingine ili kuokoa kibarua chake ilimlazimu afanye maamuzi ya kuondoka japo moyoni alikuwa na hofu kubwa mno na hasira ambazo hazikukwepeka.

Jason aliendelea kusonga mbele bila wasiwasi wowote ule, alikunja kona mbili alikutana na uwanja mkubwa sana, alitakiwa kuumaliza huo uwanja ndipo aingie upande wa pili ambako bila shaka alikuwa ana maelekezo kwamba alikuwa amefungwa huko IGP. Hilo eneo lilikuwa kimya sana kwa sababu haikuwa muda wa wafungwa kuwa nje ila alikuwa anaona mtu mmoja mmoja akiwa anaotea jua kwenye hilo eneo. Kuna baadhi ya wanaume walikuwa wanafagia fagia maeneo ambayo kiuhalisia hayakuwa na uchafu wowote ule, miili yao tu ilisadiki walikuwa ni watu wa mazoezi haswa.

Alijongea hatua kumi, kuna mwanaume akampamia kiasi kwamba alikuwa amekosea njia kwa bahati mbaya, ila mwanaume huyo alibeba funguo kwenye mfuko wa Jason, alitabasamu kwa sababu alikuwa ametambua tangu mtu huyo anafika hilo eneo. Watu wote ambao walikuwa kwenye hilo eneo walianza kusogea upande ambao yeye alikuwepo wakijifanya kwamba kila mtu alikuwa ana safari zake.

Alisimama na kuikunja suti yake kidogo kwenye upande wa mikono, aligeuka na kuangalia kwenye moja ya pembe ambayo ilijificha vyema, alijua hiyo sehemu lazima ilikuwa na kamera ndiyo maana alisimama hilo eneo na kugeuka, alitabasamu kwenye kamera hiyo na sura yake ilionekana kwa usahihi sana kiasi kwamba kama kuna mtu alikuwa anaangalia upande wa pili basi angemuona kwa usahihi sana. Na hicho ndicho ambacho yeye alikuwa anakihitaji wamuone vyema ila bahati mbaya sana hakujua kwamba Monalisa analiona hilo tukio moja kwa moja.

Kisu kikali kilirushwa kwa nguvu kuelekea upande wake na mwanaume mmoja ambaye alijifanya kwamba anasukuma toroli la takataka huku yeye akiwa anafuata kwa nyuma kwa kasi ya ajabu sana, kisu hicho kilidakwa kwa vidole viwili tu na Jason ambaye alirudi nyuma hatua mbili tu. Yule mwanaume wakati anakaribia kufika Jason alidunda chini kwa mguu mmoja na kujigeuza kama tairi likiwa kwenye mwendo kwa kasi kubwa sana ambayo ilikuwa mara mbili ya yule mwanaume aliyekuwa anakuja nayo.

Alitua kwenye kifua cha mwanaume huyo kwa goti huku akishuka naye chini, akiendelea kushusha ngumi kwenye uso wa huyo mwanaume. Walitua chini mtu huyo akiwa kwenye hali mbaya sana, kisu ambacho alikuwa nacho kwenye mkono wake alikizamisha kwenye shingo ya mwanaume huyo na kukuzingushia upande wa pili.

Huo ukatili kuna watu walikuwa wanauona moja kwa moja kwenye televisheni, mwanaume huyo aliuliwa kwa sekunde ambazo hata kumi hazikuisha. Sasa hakukuwa na haja ya kujificha tena kwani mgeni wao tayari alikuwa ameshajua kwamba hilo eneo watu walikuwa wanamtaka yeye na wanamsubiri kwa hamu. Walijitokeza wanaume kumi na wawili wakiwa kwenye hizo nguo za gerezani.

Hawakuwa na silaha yoyote ile ya moto zaidi ya panga zao kwenye mikono yao, ni yule mmoja tu wa kwanza ndiye ambaye alikuwa na kisu kidogo ila hao wengine wote walikuwa na panga kwenye mikono yao. Waliangaliana kwa muda kidogo kisha akajisogeza mbele mwanaume mmoja ambaye mwili wake ulikuwa umekomaa mno anapokuwa anaikaza misuli yake kwa nguvu.

Hata yeye alikuwa jeuri vile vile, aliuvunja ule upanga wake kwa mikono yake miwili kuonyesha ubora wake kisha akamuita Jason kwa mkono wake mmoja kwa dharau. Mwanaume aliikunja mikono yake mpaka ile suti ilichanika kwenye mikono kwa namna mikono hiyo ilivyo vimba, kwake ilikuwa ni dharau kubwa kijana kama huyo kumuita namna hiyo.

Alisogea kwa nguvu sana, ilivyo bakisha hatua moja kumfikia huyo mtu, alisita kwanza na kutulia, hesabu za yule mwanaume alikuwa amezipiga kwamba Jason anajipeleka moja kwa moja hivyo alirusha ngumi tano mfululizo na lengo lake alihitaji zimpate Jason ila zote hazikufika popote kwani ziliishia kwenye hewa. Sasa Jason alijivuta mpaka alipo mwanaume huyo alijibinua kama anataka kushuka na teke mwanaume huyo akaikinga mikono yake lakini alidanganywa haikuwa hivyo, Jason alijigeuza kwa sarakasi moja na kutua chini kisha akautuma mkono wake wa kulia ambao ulienda kutua kwenye eneo la moyo la mwanaume huyo.

Mtu huyo alianza kuhangaika baada ya kushindwa kuhema, ngumi hiyo iliusimamisha moyo kufanya kazi, alihangaika akizunguka kwa sekunde kadhaa mpaka alipo zidiwa na kuanza kushuka chini ila hakupewa hiyo nafasi, mwanaume alijigeuka kwa double kiki moja ambayo ilitua kwenye shingo ya mwanaume huyo alienda kujibamiza kwenye mavyuma ambayo yalitoboa vibaya sana kichwa chake.

Iliwalazimu kila mtu kugeuka ili aweze kuona mwenzao huyo alikuwa kwenye hali gani, walijikuta wanamgeukia wote Jason kwa hasira sana na kuanza kumfuata wakiwa na mapanga kwenye mikono yao, kwa sasa walikuwa wamebaki kumi na moja tu pekee.

Jason hakuwa na haraka nao, alikuwa na kasi ya ajabu sana kwenye kukwepa hizo panga. Kuna upanga ambao ulirushwa kwa kasi kuelekea kwenye shingo yake, alisogea pembeni na kuudaka ukatua kwenye mkono wake. Alitingisha kichwa chake kuonyesha kusikitika maana unyama ambao alikuwa anaenda kuufanya na huo upanga wake mkononi hata yeye alikuwa anaogopa na kuwaonea huruma watu ambao walikuwa wanaangalia kwa upande wa pili.

Mwanaume ambaye aliurusha upanga huo, alikimbizana na kasi ya huo upanga ili amfikie Jason ila alikuwa amechelewa sana, kwani kuja kwake kwa pupa na ngumi za hasira, kulifanya ngumi yake ilkutanishwe na upanga huo ambapo kiganja kilidondoka chini, alipiga kelele za kuomba msaada ila tayari alifika kwenye mikono ya simba mla nyama. Upanga ulizamishwa kwenye jicho lake, likafuatia buti kali ambalo lilimdidimizia kwenye huo upanga.

Jason aliuchomoa na kuurusha kwa spidi kali sana huku naye akiruka juu na kuwakwepa wale wanaume ambao walikuwa wamemkaribia alipo. Wale wa mbele waliukwepa ule upanga ukaenda kumkita yule wa nyuma kabisa ambaye ndiye Jason alimfikia kifuani, aliuchomoa ule upanga kwa nguvu kisha akampiga mtama mkali mno, mwanaume huyo wakati anashuka chini alishindiliwa na buti lililo fanya mvunjiko wa kifua chake kusikika kwa kila mtu.

Ile hali ilianza kuwatia hofu sana ila walikuwa wamechelewa pakubwa kwani kushangaa kwao walishangaa mwenzao mmoja akiwa anaenda chini, hawakuelewa huo upanga ulirushwa muda gani ila ulizama sehemu ya moyo wake, akadondoka. Walikuwa kama wamemchokoza simba mwenye njaa kali kwa kumpitishia swala mbele yake.

Ndani ya dakika tatu tu pekee walikuwa wamesimama wanaume wanne tu mbele yake wakiwa wanasukumana yupi atangulie na yupi asiende. Jason kwenye mkono wake alikuwa ameushika upanga ambao ulikuwa unavuja damu. Aliutupa chini ili kuwapa wanaume hao nafasi ya kumjia pale alipo, walipata nguvu na kuja wote kwa pamoja baada ya kuona kauachia upanga huo.

Alilala chini wakampita ila alifanikiwa kumdaka yule wa nyuma kabisa, alimkutanisha na ngumi moja ya uti wa mgongo kisha akaushika uti wa mgongo huo kwa nguvu na kuugawanyisha sehemu mbili tofauti. Hawakuuona kwa macho ila namna ulivyokuwa unavunjwa kila mtu alisikia, mwanaume huyo alibaki ameganda tu mwili hauna mawasiliano tena kwani unategemea zaidi uti wa mgongo ili ufanye kazi.

Mwingine baada ya kuona hilo jambo alirudi na upanga kwa nguvu, upanga huo ulidakwa kwenye makali na kuvunjwa na mkono, Jason alimgonga na viganja viwili vya masikio huyo mwanaume ambaye aliishia kupiga sana makelele ila kelele zake zilipelekea Jason kuzamisha vidole kwenye macho ya mtu huyo kisha akamvuta kwa nyuma na kumpigiza shingo yake kwenye kiatu chake kwa mbele, shingo ya mtu huyo ilitoboka akafariki hapo hapo.

Walikuwa wawili ambao walikuwa wanakuja wote kwa pamoja, Jason alijipapasa kwenye kiuno chake na kutoa bastola yale kisha akaikoki kwa spidi kwa kuipigiza kwenye kiatu chake, aliachia risasi tatu ambazo zilipasua kichwa cha mmoja kati ya wale wanaume wawili. Mmoja aliyekuwa amebaki alisimama huku akipiga kelele za uoga maana aliona kichwa cha mwenzake kinavyo pasuliwa, aligeuka na kuanza kukimbia na huyo ndiye ambaye alichukua ule ufunguo wa gari kwa mara ya kwanza kabisa.

Hakufika mbali, alidondoka chini baada ya kupigwa risasi ya paja kwa nyuma huku funguo ikimdondoka kutoka kwenye mfuko wake, aliendelea kujiburuza huku akiwa anajivutia eneo ambalo lilikuwa karibu na geti la senyenge. Jason alisogea taratibu na kuiokota funguo yake mkononi kwake akiwa na jeraha dogo wakati ule anaudaka ule upanga, alimsogelea mtu huyo na kuinama pale alipofikia, mwanaume huyo alikuwa anaomba sana msamaha mtu huyo amuache salama kwani yeye pale aliagizwa tu halikuwa lengo lake kufika.

Jason hakuongea naye chochote kwanza zaidi ya kumpiga tena mwanaume huyo risasi ya goti hali iliyo pelekea goti hilo kupasuka vibaya sana, mwanaume huyo alilia mara moja kwa makelele ila alitulizwa.

“Shiiiiiiiiiiii” hakutakiwa kupiga makelele kabisa kwani eneo hilo hakuna mtu yeyote ambaye alimlazimisha yeye kuwepo mpaka wakati huo, kama angekuwa anaona maisha yake ni ya mhimu sana basi alikuwa na nafasi kubwa sana tangu mwanzo wa kuyaokoa maisha yake. Sasa ametiwa mbavuni anaanza kumlilia nani? Alitakiwa kuumaliza mchezo ambao karata amezichanga yeye.

Rasmi Jason ameamua kuyaishi maisha ya watu ambao walitaka kuthibitisha kwamba ni kweli yeye siyo wa kawaida hata siku moja, sasa itakuwaje na wamesha mjua? Kumbuka mchungaji John Mwituka aliahidi kumuua kama akiwa na uhakika kama ni yeye. Usisahau Monalisa kwa mara ya kwanza alikuwa anaushuhudia unyama wa mtu huyo ambaye kwake alikuwa ni kijana legelege sana, atafanyaje huyo mrembo?.....90 naweza nukta hapa panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam
Bux the storyteller.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Shukrani mkuu tupe na bonus leo
 
Am here
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA TISINI NA MOJA

SONGA NAYO................
“Una miaka mingapi?” Jason alimuuliza yule mwanaume pale akiwa chini kwenye maumivu makali mno

“26”
“Mbona bado mdogo na unakubali vipi kufanya kazi za hatari namna hii?” mwanaume huyo hakujibu kitu chochote zaidi ya kumwaga machozi kwa kuvunjiwa goti lake na paja ambalo lilikuwa linamwaga damu kwa wingi sana kwenye mguu wake. Jason alisimama na kumrushia kijana huyo bastola ambayo ilikuwa kwenye mkono wake.

“Hiyo bastola ina uwezo wa kubeba risasi sita, risasi tatu nimempiga mwenzako pale nyuma, risasi mbili nimekupiga wewe hapo hivyo imebakia moja humo ndani. Hizo sehemu ambazo nimekupiga zitakuletea maumivu makali sana kadri muda unavyo zidi kwenda na watu ambao wamekutuma hii kazi wakikuona kwenye hii hali hawawezi kukusaidia tena kwani utakuwa huna msaada wowote ule kwao hivyo kiufupi lazima watakuua tu tena kwa mateso maana umeshindwa kuifanikisha kazi yao kama walivyo kuagiza”

“Cha kukusaidia itumie vyema hiyo risasi moja ambayo imebakia humo ili usipate maumivu makali sana” mwanaume alitamka kwa msisitizo mno huku akiwa anatoka hilo eneo na kwenda kulifungua lango la chuma mbele yake ambalo lilikuwa wazi, huko ndiko ambako alikuwa amehifadhiwa Lusubilo Mtindika ambaye aliyekuwa ni IGP wa nchi ya Tanzania.

Kijana huyo ambaye alipatiwa hiyo bastola pale nje alibaki analia sana akiwa anaitazama silaha hiyo kwa umakini mkubwa sana, aliibeba kwa mkono wake wa kulia huku akiwa anainyanyua kwa uchungu mkubwa, aliiweka kichwani kwake na kujiua yeye mwenyewe.

Monalisa hayo mambo ambayo yeye alikuwa anayashuhudia kwenye hiyo runinga yalimtisha kiasi kwamba alibaki kama vile ni mtu ambaye hakuwa hata akielewa kwamba yeye mwenyewe ni nani, aliamua kusimama na kuisogelea tv hiyo ili amuone kwa ukaribu huyo mtu ambaye alidai kwamba hawezi kuishi bila yeye kwenye maisha yake yote.

Hakuwa na uhakika kama mbele yake alikuwa ni mtu wa kawaida au roboti ndilo lilikuwa limetumika kuifanya hiyo kazi huku wakiiweka sura ya huyo mwanaume ambaye yeye alimjua kama mpenzi wake. Alichoka sana na kukaa chini huku akitokwa na machozi kwa uchungu mkubwa mno, ubora wa kamera hizo ulimfanya amuone vizuri kabisa mpenzi wake tena hakusimuliwa, alishuhudia yeye mwenyewe mwanaume huyo akiwaua kikatili sana wanaume walio shiba mazoezi magumu kwa sekunde za kuhesabu tu.

Moja ya matukio ambayo yalimtisha sana ni ile kushuhudia huyo mpenzi wake akiwa anaudaka upanga kwenye makali kwa mkono wake mmoja na huku upanga huo ukaishia kumuumiza sehemu ndogo tu, kila sekunde moja ilivyokuwa inahesabu alikuwa anazidisha maswali kwenye kichwa chake kuhusu mtu huyo mpaka alihisi kama kichwa chake kinataka kupasuka.

John Mwituka alichukua tablet yake kubwa na kumrushia binti yake pale ambapo alikuwa amekaa, juu ya tablet hiyo ilikuwa inaonekana picha kubwa sana ya familia ya jaji mkuu marehemu Markvelous Japhary, Jason akiwa pembeni akiwa mwingi wa tabasamu tena la kutosha. Aliendelea kuangalia picha zingie za mbele ambazo zilikuwa nyingi sana, kuna baadhi ya picha alimuona Jason akiwa Ikulu na raisi ambaye naye alikuwa ameuliwa Shadrack Okoe.

Lakini haikuishia hapo tu aliona mpaka video za watu hao mpaka siku ambayo alikuwa anarudi kutoka Marekani, picha ziliendelea mpaka siku ya msiba namna mwanaume huyo alivyokuwa amejifunga ndevu za bandia ili asiweze kujulikana kwa watu ambao huenda walikuwa na baadhi ya taarifa zake. Monalisa angekuwa na swali gani na kila kitu alikuwa anakiona kwa macho yake? Alimgeukia baba yake machozi yakiwa yanamshuka mpaka mdomoni kwake, huyo mwanaume alikuwa ni kila kitu kwenye moyo wake na tangu wafahamiane amekuwa akijua yeye ndiye ambaye ana jukumu la kumlinda lakini kwa alicho kishuhudia je alikuwa na hiyo nafasi kweli?

Kabla hajamuuliza chochote baba yake alikumbuka vyema siku ambayo alimfuatilia Professor Michael ndani ya nchi ya Marekani ambapo alifika sehemu akakutana na mtu aliye jitambulisha kama Dr Morgan. Hilo halikuwa na umuhimu sana kwake ila kitu kilicho mpeleka kwenye yale mawazo ni wakati anapigana na yule kijana ambaye alimwambia kwamba kama asingekuwa anamjua basi siku ile ile angemuua. Sasa swali, ina maana haya yote yana uhusiano na Jason? Kama ni kweli kivipi jambo kama hilo liwezekane?.

“How?” Monalisa aliuliza kwa ukali akiwa anamwangalia baba yake kwa macho makali sana utadhani aliye muona kwenye hiyo video ndiye baba yake mzazi.

“Dunia imegawanyika kwenye makundi makubwa mawili. Kundi la kwanza ni wale ambao wanaamini kwenye mambo ya kusadikika au kuaminika ila huwa yapo kweli na kundi la pili ni lile ambalo linaamini kwenye kundi la vitu vinavyo onekana. Kundi la kwanza huwa linaendeshwa na hisia zaidi pamoja na imani lakini kundi la pili, ni kundi ambalo linaamini zaidi kwenye ushahidi wa macho”

“Hili kundi la kwanza la hisia huwa lina watu wenye akili zaidi wengi na wenye maono ya mbali sana na mara nyingi huwa linabeba viumbe vya kutisha tofauti na la pili. Wewe hapo upo kwenye kundi la watu wanao hitaji ushahidi wa macho ndiyo maana unaweza ukawa unachelewa sana kwenye mambo mengi hapa duniani na hilo ni jambo la hatari sana” mzee huyo alinyanyuka huku akiwa anasogea pembeni na kuiwasha sigara kwenye mdomo wake. Halikuwa jambo la kawaida kwani mzee huyo hata siku moja hakuwahi kuvuta sigara mbele ya mtoto wake maana alikuwa hazipendi kabisa, mpaka kufikia hatua ya kuvutia mbele yake mambo hayakuwa ya kawaida na hilo Monalisa alilielewa mapema sana.

“Kama huyo mwanaume ulikuwa mpaka unalala naye na haukuwahi kuona utofauti wowote kwenye mwili wake na namna mwili wake ulivyo komaa, mwanangu utaweza kujilinda kweli kwenye hii dunia ambayo haina hata huruma siku nikiwa sipo?” mzee huyo aliuliza huku akiwa anaangalia dirishani ambapo palikuwa wazi na upepo wa bahari ulikuwa unapiga kwa mbali na kuifanya harufu hiyo ya sigara isisambae humo ndani. Mwanamke huyo hakuwa na cha kuongea maana alihisi kama kwenye roho yake kuna kitu kinamkaba sana na kumletea hasira isiyokuwa na kipimo, basi ilibidi mzee huyo aendelee.

“Kwenye maisha yako inatakiwa hisia zako ziwe zinafanya kazi zaidi ya akili yako ila maamuzi yako yanatakiwe yatokane na akili yako na siyo hisia zako. Hii sentensi huwa wanaielewa watu wachache sana ndiyo maana huwa hawawezi kuifanyia kazi na huenda hata wewe usiielewe leo hii mpaka pale ambapo utakuja kuwa kwenye matatizo mazito sana. Hisia huwa zinampatia mtu ukweli wa namna mambo yalivyo, ndiyo sababu hata kwenye mapenzi wengi huwa wanapotea kwa sababu hisia huwa zinawapa ukweli wa kwamba ni yupi mtu anampenda lakini wakati wa kufanya maamuzi wanasahau kutumia akili tena wanaacha hisia zile zile ndizo zitumike kufanyia maamuzi na hapo ndipo huwa unaanza mwisho mbaya”

“Mimi wakati nikiwa kijana mdogo nilikuwa napenda sana wanawake, nafsi yangu ilikuwa ikitulia zaidi pale ninapo lala na mwanamke. Hiyo ilitokana na kwamba nilikuwa ninaendeshwa sana na hisia kuliko kutumia akili ila nilikuja kuachana na haya maisha ya kutumia hisia kufanya maamuzi baada ya kukutana na mwanamke mmoja huko Dubai ambaye alitaka kutoka na roho yangu, nilishoboka na nikawa kwenye mahusiano naye, nilijikuta nakuwa kama mtumwa kwake maana nilimpenda isivyo kuwa kawaida”

“Siku ambayo nilipona kufa kutoka kwenye mkono wa yule mwanamke ndipo nilikuja kugundua kwamba napaswa kutumia zaidi akili kuliko hisia japo hisia zinatakiwa kufanya kazi zaidi na sio kwenye kufanyia maamuzi. Yule mwanamke alikuwa ni ajenti wa KGB, siku ambayo alipanga kuniua ni siku ambayo hisia zangu zilinisaidia maana niliona kama kazidisha mapenzi sana halafu ghafla sana, usiku nilijifanya nimelala sana, kweli nikaona mtu anakuja na kisu kwenye mkono wake ili akizamishe shingoni, siwezi kukusimulia nilicho mfanyia ila nilimfanyia kitu kibaya sana na tangu siku ile niliacha kabisa kuwaamini wanawake”

“Kwenye ulimwengu ambao wanaishi hawa viumbe kama huyo bwana mdogo ambaye umemuona hapo, huwa wanatumia sana hisia kama mlango wa sita wa fahamu, hivyo wakati wewe ukiwa unalala sana na kujua kwamba kuna milango mikuu mitano ya fahamu wenzako wanajua kwamba ipo sita. Kwa ule uwezo ambao nimemuona anao, basi huyo hata kama hatari ipo mita zaidi ya mianne mbele ana uwezo wa kujua kwa kutumia hisia zake”

“Hata mimi sijawahi kumjua kwamba yupo hivi japo baada ya kutajiwa nafasi ambayo anayo nilishtuka sana hivyo ilibidi tuandae huu mtego ili nithibitishe kile ambacho nilikuwa naambiwa na ndo kama hicho ambacho umekiona. Je unataka kumjua kwamba yeye ni nani sasa baada ya kujionea namna alivyo?” mzee huyo alivuta moshi mwingi kwa nguvu na kuutolea nje kisha akakirusha kipisi kidogo cha sigara ambacho kilibakia kweye mkono wake nje na kumgeukia binti yake ambaye mpaka wakati huo alikuwa kama vile amechanganyikiwa. Namna tu alivyo mwangalia baba yake ilikuwa ni ishara tosha kwamba alimruhusu mzee huyo aendelee na maelezo yake.

“Huyo ndiye mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Tanzania” hiyo kauli ilimfanya amwangalie baba yake kwa umakini mkubwa na mzee huyo hakuwa na tatizo aliirudia tena kauli yake kama alivyokuwa ameitamka mwanzo. Monalisa alielekea kabatini na kuchukua pombe kubwa sana ambayo aliiweka mdomoni bila hata kumimina kinywaji hicho maana mambo ambayo alikuwa anambiwa yalikuwa yapo kinyume na matarajio yake na nafsi yake isingeweza kabisa kuyahimili.

“What is going on in this world? (Ni kipi kinaendelea kwenye hii dunia?)” aliuliza akiwa anahema kwa nguvu sana huku akiwa anaitazama picha ya Jason kwa hasira kwenye tv kubwa ambayo ilikuwa ukutani kijana huyo akiwa kwenye tabasamu zito sana. Baba yake alisogea sehemu ambayo alikuwepo binti yake, akaweka picha moja ambayo walikuwa wanaonekana wanaume wawili ambapo mmoja alikuwa ni mzee na mwingine alikuwa ni Jason mwenyewe, wote wakiwa kwenye suti za blue.

“Unamjua huyo mzee” mchungaji huyo alimuuliza mtoto wake akiwa anaweka nne kwenye miguu yake. Sura ambayo ilikuwa inaonekana hapo mbele haikuwa ngeni kabisa kwa Monalisa, huyo alikuwa ni Professor Michael ambaye alikuwa anamjua kama moja ya wahadhiri wake huko Havard sema kulikuwa na mpishano mdogo sana wa hiyo sura ila haikuwa tatizo yeye kumjua mwanaume huyo.

Alishangaa sana na alipigwa na butwaa kwamba hao watu walikuwa na ukaribu gani? Alivuta taswira namna Jason siku ile alivyo potelea kwenye ofisi ya mtu huyo halafu leo anaambiwa Jason ni mkurugenzi wa usalama wa taifa? Aamini kipi? Alichanganyikiwa.

Na mimi niseme tu mpaka hapa sehemu ya 91 sina la ziada panapo majaaliwa tutakutana tena wakati mwingine.

Wasalaam

Bux the storyteller.View attachment 2773921

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu tunashukuru ila ungewekahata vipande viwili vitatu hivi kufidia aisee, but kazi yako ni njema sana, muundo, mtindo, wahusika, matumizi ya lugha na mandhari vimekaa poa sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom