Inflammatory: CHADEMA hawako kwa maslahi ya taifa, they are just another tool

Mkuu pole kwa kutumia references nyingi!!
ILA UKWELI NI KWAMBA!!
Mchambuzi yeyote au mtu yeyote anapofanya research lazima ufanye references lakini mwishoni lazima uje na mawazo ya kulinganisha yale uliyoandika na mazingira au hali halisi ya sehemu ulipo...DONT COPY, JOIN AND PASTE!!!....after that unatakiwa ufanye recomendation kama model inaweza kuwa applicable.
Sasa kwa hali halisi ya Tanzania mkuu mi nadhani CUF hawafai tena kuitwa wapinzani....tofautisha muungano wa serikali ya umoja wa kitaifa katika utawala na mungano wa serikali ya kitaifa katika upinzani.

Ushauri.
CDM waungane na chama chochote cha upinzani kinachotaka muungano lakini siyo CUF.
 
Kiini cha ukweli huiwezi kukikwepa hata kwa maelezo yanayojaza kitabu,lazima cuf wakiri kwanza 2005 hawajaunda kambi ya pamoja ya upinzani kwa kupenda ila ni kwakuwa walikuwa hawajatimiza vigezo vya kuunda kambi ya upinzani peke yao,na mfano mzuri tu,cuf wametangaza kuwa wataandamana lakini hatutarajii katibu mkuu wao ambae ni makamu wa kwanza wa raisi kuwepo kwenye maandamano ya kuipinga serikali ya jamuhuri wa muungano.
 
Waberoya,

CDM iliungana na CCM huko Kigoma kwenye umeya na huo ndo mfano wa coalition govt, kweli..? Mi si mtu wa Kigoma lkn najua CDM iliongoza kwa kipindi fulani na CCM baadae (or vise versa) kwa kupokezana. Na cjui kama umesoma vizuri muundo wa coalition govts ulizozitaja au umegoogle tu kujua kama zipo na ni zipi. Mi cjawahi kupost thread au comment humu JF lkn hili limeniudhi nikaamua nicomment bila kuwa na itikadi ya chama chochote.

WFM.
 
Waberoya,

Kwanza nianze kwa kusema mimi si mwanachama wa Chadema na katika viongozi wote wa Chadema simfahamu hata mmoja personally. Nawaaona na nakiona Chama kutokea nje. Lakini katika andiko lako hapa, naona emotions zaidi kuliko logic. Kuna mambo ambayo umeyakwepa wazi wazi na haya yanapunguza credibility ya argument zako.
  • Kura zote zilizokwishapigwa Bungeni sasa hivi, CUF ilipiga kura upande wa CCM, pamoja na Chadema Mwanzoni kuonesha kuwa walikuwa tayari kushirikiana na Chadema
  • Kauli ya uongozi wa juu wa CUF kuwataka wabunge wa CUF Zanzibar waiunge mkono CCM bungeni
Hizi facts ndugu Waberoya huwezi kuzifungia chini ya busati kwa hisia tu ya kutaka kuwa na upinzani Mkubwa! Upinzani bungeni wote tunataka uungane, lakini tunataka uungane ili uwe upinzani. Siyo uungane halafu uwe na mtazamo na mwelekeo ule ule wa walioko madarakani.

Hapa umeonesha chuki dhidi ya Chadema tu, na pengine iko clear unafanya kazi ya CCM na huwezi kunishawishi kuwa una nia njema na Chadema. Kwanza lugha iliyotumika haivutii kwa wafuasi wa Chadema.

Kwa watazamaji tulio pembeni tunaona CUF inayotaka kushiriki serikalini, na wakati huo huo kushiriki upinzani!! Mfano wake haupo sehemu yoyote duniani. Reference zote zilizotolewa hapa, zinafaa kuwadanganya watu, lakini si kuelezea ubora wa dhana iliyokusudiwa.
 
Wewe Waberoya,

Mbona kila siku uko KINYUME na CDM. Yaani hawa watu wanakunyima usingizi.

Vile vile kwanini upotoshe ukweli humu kwenye forum? Yote uliyoeleza ni muungano wa vyama kuwa na serikli ya pamoja, hapa swala ni chama cha upinzani, sio kuunganisha vyama kuwa na one goverment. CUF iko kwenye serikali ya mseto na SISIEM VISIWANI kwa mantiki hiyo uhalali wake kuwa opposition party iwe bara au kisiwani umetoweka.

Hawawezi kuwa vinyonga, wakija bara rangi nyingine wakienda Zenji rangi nyingine. Huoni logic hapo, hata mtoto wa chekechea ataelewa. Katibu mkuu wa CUF ni Vice President Zanzibar.(Soma pekundu hapo!!!!!!!) Mkipanga lolote la opposition kabla ya utekelezaji litakuwa limevuja. CDM WANA VICHWA wanaelewa kwa nini wameamuwa hivyo.

UMEELEWA?
 
Waberoya,

Kwanza nataka ufahamu mie si mwanachama wa chama chohote Tanzania na sijawahi kupiga kura hata mara moja kwenye uchaguzi mkuu. huwezi amini ila ni ukweli.

Nakubaliana na wewe kuwa Chadema siyo chama haswaa kinachotakiwa kuwa cha upinzani Tanzania. Ila unalotaka kulisema wewe ni sawa na kumwambia Muislaam, USILE NGURUWE kwa sababu ni HARAMU. Yes ni haramu na inawezekana anawadudu wengi tu hatakiwi kuliwa. Ila tatizo kubwa lililopo ni kuwa HAKUNA CHAKULA kingine chochote. Mtu huyo ana chagua KULA au KUFA kwa njaa.

Cha ajabu, wewe unasema NIMESEMA USILE NGURUWE TU ila sijasema USIFE NJAA. Kwa sasa tuna Chadema tu na hatuna chama kingine na kilichobaki ni KUWASAIDIA Chadema au TUFE NJAA.

Hawa Wazushi wengine watatupeleka kwenye Serikali ya Utaifa na mwisho tuwe na Chama Kimoja tu cha CCM kama Uganda.

Mie ukija na Chama mbadala zaidi ya Chadema, na uwe na malengo na utawala mzuri basi NITAKUUNGA MKONO na kununua hadi Kadi ya Chama. Ila kwa sasa, ngoja tubaki tukiwashangilia Chadema huku tukiwa NJE ya Chadema.

Mengine naona tupo pamoja kabisa na tofauti ni ndogo sana.

oo My God! Huu ndo ujinga uliopo bongo! hichi nacho ni cha kusema wazi kwenye jukwaa la great thinker? hii ni aibu!
 
Waberoya

Sijasoma thread zote kujua walionitangulia wamesema nini, pengine naweza kuwa nimerudia kilichosemwa.

Hoja yako ina maeneo yenye point za msingi CDM kuzingatia wakati huo huo kuna maeneo hukuzingatia uhalisia.
Naona ulikuwa na hitimisho tayari hata kabla hujaanza kuandika, taarifa ulizoweka zilitegemea uhitaji wa hitimisho lako.

Mimi ningependa CDM, CUF, TLP, UDP, NCCR waunde kambi moja kwa kuamini kwamba wao wana uchungu na nchi hii na CCM ni adui yao mkubwa. Lakini nachelea kusupport hoja hii kwa sababu moja kubwa.
HAKUNA TRUST:
- Unamwamini vipi Mrema ambaye kila kukicha yeye ni kumsifia Kikwete tu hata pale sifa hazistahili?? Unadhani atamsikiza nani kati ya Kiongozi wa Kambi yao au rais Kikwete??

- NCCR wameingia kukipinga CDM wakati wa kampeni, nilipata kumsikia Mbatia-ITV akisema watu wanafikiri kugombea urais ni swala la kukurupuka tu kwamba unaamua mwezi wa sita kuweka mgombea. Hapa alikuwa nazungumza namna Slaa alivyoingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais. Ni kama alikuwa anawaombea mabaya CDM, bahati mbaya hayajawapata. Kuamianiana kutakuwepo??

- CUF wao toka bunge limeanza hawakuonyesha ushirikiano hata kidogo ingawa kuna maelezo kwamba Mbowe alonyesha nia ya mazungumzo. Kuna maneno makali, dharau na bad body languange imeonyeshwa na Hamad. Utamwamini kweli huyu mtu??
Mwanza kumefanyika uchaguzi wa meya, CUF wanawaste kura zao kwa CCM wakati wange strike a deal na CDM kwamba kura zetu kwenu lakini mtuachie Unaibu meya. Sasa linatokea hili leo lakini kesho unawaomba hao hao muungane. Get into CDM shoes!!!!!!!!!!!

Talking of Zanzibar GNU: Kaka hakuna anayejua makubaliano ya Seif na Karume. I bet you, not even Kikwete. Uliwahi kutegemea CUF waombe rais Zanzibar aongezewe muda (wavunje katiba), kwa hili hata CCM ikawazidi hekima hata kama ni kwa uroho wa waliotaka hicho kiti
CUF wameshinda uchaguzi 1995 Nyerere (RIP) akashauri waunde serikali ya pamoja CCM wakagoma, leo utasema CCM ya kina Kingunge na Makamba wanawapenda CUF??

Nadhani kwa sasa waache vumbi litulie they can talk in the future baada ya matendo ya kila mmoja kuonyesha kwamba wao ni wamoja.

Lets give it time na Inshallah JF iendelee kuwepo na watu msibadili ID ili tukumbushane haya!!!!!!!!!!!!
 
Waberoya,

CDM iliungana na CCM huko Kigoma kwenye umeya na huo ndo mfano wa coalition govt, kweli..? Mi si mtu wa Kigoma lkn najua CDM iliongoza kwa kipindi fulani na CCM baadae (or vise versa) kwa kupokezana. Na cjui kama umesoma vizuri muundo wa coalition govts ulizozitaja au umegoogle tu kujua kama zipo na ni zipi. Mi cjawahi kupost thread au comment humu JF lkn hili limeniudhi nikaamua nicomment bila kuwa na itikadi ya chama chochote.
WFM.

At least nimekuwa wa kwanza kukugonge senksi Mkuu
 
Tusikariri mambo, sio kila mgogoro unapotokea basi suluhisho ni serikari ya muungano, hili swala la coalition linategemeana na mazingira ya nchi na sera za vyama vya siasa. Kama kuna tofauti kubwa ya kisera ni ngumu sana kuungana.

Kwa mazingira ya Tanzania ukweli ni kwamba chama tawala CCM wameshindwa kusimamia rasilimali za Taifa kwa kukumbatia ufisadi na uzembe wa kiutendaji unaolisababishia hasara kubwa Taifa letu. Asilimia 90 ya watawala wa sasa wana sifa zote za kufikishwa mahakamani kwa kulihujumu Taifa letu. Hivyo basi CCM kwa sasa hawana sifa ya kuunda serikali ya umoja na chama chochote (Kasoro CUF), kwa maana watu waadilifu hawawezi kuungana na watu waovu (CCM), ukiuungana na waovu ina maana unabariki na kukubali maovu yao.

Kwa sasa ni lazima CCM waondoke, wapishe watu wanaoipenda Tz na kuwaheshimu watu wake.

Tumechoka kuongozwa na watu wanaoenda against the interest and rules of our Lovely Land. KATIBA MPYA
 
Mi kwa kweli nimemuelewa huyu jamaa vizuri saana... Lakini kasahau kitu kimoja kutueleza labda kutokana na jazba aliyonayo... Wakati unajenga hoja hata kama umewahi kuandika dissertation ya aina yoyote ile ni lazima uwe na fikra huru zenye mrengo wa kati badala ya lawama.

JAMBO ALILOSAHAU KATIKA THREAD NDEFU AMBAYO HAIJAKAMIKA!!
Umesahau kuelezea katika mifano yako yote kuhusu Coalition Gov hasa ni nani huwa anaingia kambi pinzani.. Kwa mfano hujaeleza Lets Kenya ni chama gani kipo kambi rasmi ya upinzani??!! Pia hujatuelezea kama ukiwa kwenye Coalition Gov kama pia unaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.. Toa mifano katika nchi hizo sio kututisha as if JF imejaa watu wasioelewa ukweli...

MYTAKE:
Naomba uelezee kambi ya Upinzani kwenye Coalition Gov inahusisha vyama vipi?? Pia nielezee ni kwa nini CUF na CCM pekee kule Zanzibar walikubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili hali wamewatenga wafuasi wa vyama vingine?? Je wingi wao ndio chanzo au hulka ******* waliyonayo??

Maelezo dot com
 
good point but let me ask will Chadema capable of going themselves to the parliament.
They are capable. Kinachotakiwa sio wingi ila ni nguvu za hoja na nia njema ya utaifa. Kama wabunge wakiweka pembeni ubinafsi wao wa vyama hata wale wa CCM wataunga mkono hoja nzuri za Chadema kama ilivyokuwa kwenye bunge lililopita.

Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanziba ilikuwa ni lazima kwa sababu siasa za Zanziba sio za sera za CUF na CCM bali ni za Upemba na Unguja. Pemba ilikuwa kama vile imetawaliwa na Unguja hivyo ilikua ni lazima kuwashirikisha kwenye serikali.
 
Naanza hoja yangu kuangalia msimamo wa chadema kwa CUF na kueleza ukweli kuhusu caolition governments

Maana yake:

A coalition government is where two or more political parties join together in parliament/assembly to run the government and agree on a policy programme


Faida zake:
  • Government will be more consensus-based: resulting policies will be broadly approved of

  • Better representation of the electorate's wishes

  • Better quality of policy: enhanced scrutiny and increased attention paid to each policy

  • Increased continuity: election does not lead to dramatic overhaul which can produce fragmented rule2
Hasara zake:


· The most obvious criticism of Proportional Representation is that it could form coalition governments. This is seen by some as a majorly bad thing as it supposedly does not allow ‘strong' government. Having more than one party in charge of decision making could cause a lot of arguments between the leaders of the country as the top ministers may have opposing political ideologies and views. It could also mean that it is very hard to get policy through the governmental process meaning government could be overall less effective in the running of the country.

· It could also cause an overly expanded Cabinet to cater for everyone's needs in the Government, which could lead to much needless expenditure.


· There could also be many arguments, which cause Cabinets to split and some important policy to be suspended to do the impossible task of keeping everybody happy


Mifano ya nchi zinazounda serikali ya umoja wa kitaifa


Europe:

Albania, Andorra, Austria, Belgium, Croatio, Belgium, Czech, Denmark, Finland, Estonia, Germany, Iceland, Ireland, Italy, Kosovo,Latvia, Lithuania, Luxembourg, Monaco, Montenegro, Netherlands, Norway, Poland, Romania, Serbia, Slovakia, Slovenia, Sweden, Switzerland ( has been ruled by a coalition of the four strongest parties in parliament from 1959 to 2008 called the ‘magic formula"), Ukraine and UK

Americas

Chile, Trinidad and Tobago, Suriname, Canada.

Africa:

Algeria, DRC Congo, Gabon, Guinea-Bissau, Kenya, Mali, Mauritania, Mauritius, Morocco,Senegal, Zanzibar Island, and Zimbabwe (was proposed not sure if still exists)

Asia

Armenia,Bangladesh,Cambodia,India,Indonesia,Iraq, Isarel, Japan, Lebanon, Malaysia, Maldives, Pakistan, Sri-Lanka, Thailand, Timor-Leste

Ocenia

Australia, New Zealand, Papua New Guinea, Vanuatu

Kwa nini huwa inaundwa?;

The usual reason given for this arrangement is that no party on its own can achieve a majority in the parliament. A coalition government might also be created in a time of national difficulty or crisis, for example during wartime, to give a government the high degree of perceived political legitimacy it desires whilst also playing a role in diminishing internal political strife. In such times, parties have formed all-party coalitions (national unity governments, grand coalitions)1

Kwa nini nchi nyingi zenye mfumo huu zimeendelea ?

Pamoja na hasara zake which is debatable advantages of coalition governments is far million times better than its disadvantages. How and why

1. Kutenganisha siasa na utendaji kazi wa serikali , kwa mfano Japan average ya prime minister kwa mwaka!, karibu kila mwaka wanakuwa na waziri mkuu mpya ambaye ni kama rais wa nchi! Still economic activities are growing up very fast!! Ufike muda tuone utendaji wa kisiasa unakuwa kwenye kushindana ku-implement policies na sio kuingilia professionals. Kwa sababu hii nchi nyingi zimefanikiwa kuendelea pamoja na kuwa coalition governments ina udhaifu wake lakini afadhali kuliko kutokuwa nayo

2. IKIFIKIA level, au wakati kuwa uamuzi wowote mzuri regardleess umetolewa na chama gani unafaa kuungwa mkono then that is a sign and good grounds of endorsing this system. Ifikie muda kila kiongozi anawaza mema kwa ajili ya nchi yake na KUPATA UONGOZI SI KWENDA KUJIONYESHA KUWA WEWE NI RAIS BALI KUTATUA MATATIZO FULANI YA NCHI YAKO KWA LENGO LA KULETA MABADILIKO AMBAYO YATALINDA HESHIMA YAKO.

3. Kuwa siasa sio uadui bali ni ushindanifu wa hoja, malengo, policy na ni hulka kamili ya binadamu kutofautiana na ni jambo la kukusudiwa na kila mmoja kujenga nchi moja pamoja na kuwa mnaweza kuwa na mitazamo tofauti, if we will reach this stage we are through!

Je kuna faida gani au kwa nini serikali ya umoja wa kitaifa ni muhimu hasa kwa nchi za dunia ya tatu ambazo vyama vingi ni vile vya kibeberu.

Kuna solutions mbili kubwa aidha kuwatoa kwa nguvu, maana ballot box cannot do anything! You heard me! But if we inclined to accept evolution not revolution then second option i.e coalition government is another good techniques ya kuwaondoa mabeberu!! Why and how

FAIDA YA serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania

1. Ni kichekesho na uhuni na uvunjivu wa haki za kibinadamu kuwa chama fulani kikipata kura asilimia 60 then wanaongoza nchi yote regardless of those 40% who did support them. Kwa mfano haingii akilini kuwa kikwete alipata asilimia 60 then wengine hawatakiwi kuunda serikali!!! Ambao tulisupport vyama vingine itakuwa rahisi na vizuri tukiwakilishwa serikalini walau kupata wizara kulingana na idadi ya kura zilizopatikana, let say CDM inapata wizara 3 out of 10! Is well and good

2. Serikali ya umoja wa kitaifa inavipa breakthrough vyama vingine kwa kuonyesha uwezo wao wa kiutendaji na kujenga hoja, this is like a continuing evaluation ya kuwa je CDM wamepewa wizara 3 wanafanya vizuri wakipewa urais si ndiyo watafanya vizuri zaidi?

3. Serikali ya umoja wa kitaifa inaviimarisha vyama, inajijenga na kupanua demokrasia ambayo tunaona haipo si kwenye chama tawala hata vya upinzania pia. Kwa mfano tulishuhudia Hilary na Obama wakipambana kwa hoja na sera zao ngali wako chama kimoja na mwisho wa siku wakamaliza vyema!!! Kama tunalipenda taifa we can still argue while we are in the same governments! Hii ni level ya juu lakini ni nzuri

4. KUBWA KULIKO YOTE ni kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itahimiza watu kujitokeza kupiga kura wakiamini kuwa wingi wa kura zao ndio unaipa nafasi kubwa chama chao kushika serikali, MOTISHA YA KUPIGA KURA NI KUBWA SANA KWENYE HZI SERIKALI NA WATU HAWAKATI TAMAA kuwa hata nipige vipi CCM watapita

5. Kufanya maamuzi ya kijinga ya kichama inakuwa ngumu kwenye cabinet

6. Msisahau wanasiasa ni wanasiasa they are born with same parents! Coalition governments inaweka msimamo kuwa hakuna chama kinachoa AMINIWA


Je what can we do now?

Mabadiliko ya katiba yanatakiwa ya accommodate issue nyingi ikiwemo hili

Je CUF na CCM Zanzibar hali ikoje?

Nimekaa Unguja na nimeona mabomu yakipigwa kwa wana CUF, na mimi kuathirika, nimeshuhudia chaos nyingi kwa macho yangu na leo hii natamani nirudi unguja nione hali ikoje!!! Coalition governments was the only solution for that situations! Wanaoibeza CUF idha hawajui maana ya caolition, hawajui kilichokuwa kinaendelea Zenj na wako blindly kuhusu nini maana ya coalition. Ni mwanzo mzuri sana ila inabidi iende mbali zaidi kuzungumzia

Vipi kuhusu tamko la CHADEMA na MSIMAMO WA CHADEMA


I don't support that tamko kwa sababu hizi

1. Chadema imefail kuwaambia au kujibu hoja ya coalition governments kwa greater heights, wanajibu cheaply kuwa CUF NI sehemu ya serikali!!! Kuwa sehemu ya serikali hakukupi mwanya kuwa usisimamie unachokiamini ndiyo maana USA hatuvitaji Republican kama ni chama cha upinzani!! Tunakitaja kwa majina yao ndivyo walivyo, IFIKIE MUDA TUSEME YULE NI MCHADEMA SIYO KWA SABABU NI MPINZANI KWA SABABU YA YALE UNAYOYASIMAMIA!!!


2. They have depicted high level of ignorance regarding coalition governments, KWANZA KAMA VILE HAZIPO, pili kama vile ni mbaya, same chadema waliungana na CCM huko Kigoma kwenye umeya na that was good example of coalition government –type


3. Kukataa coalition governments kuna onyesha vitu viwili, CHADEMA wana uroho wa madaraka na wanaiona TANZANIA KAMA NYAMA FULANI INATAKA KUDONDOKA NA WAO WANATAKA KUIRUKIA….., Tanzanias are very clever the only thing that CDM will be supported if they can agree that coalition governments is a solution because people don't trust them either! Believe me humu JF kuna tendency ya kutoangalia ukweli wa kulijenga taifa ila ni ubishi wa kishindani usio na maana kutaka cheap popularity ya ghost members usiowaona, can you stand alone?

4. Chadema imejiwekea wigo wa kujionyesha kuwa they can fight corruption alone and only alone!!! Hii ni hatari sana kwa wapenda mabadiliko , umoja wa kitaifa kupinga yanayorudisha taifa nyuma ni wajibu wakila mtu regardless of which part he belongs. Leo hii ni nadra CDM kuunga mkono CUF kile ambacho hata wao wanakipigania…huu ni utoto na high level of stupidity na ni sumu mbaya sana kwa wapenda maendeleo

5. Chadema ina ona kila wanachokisema kiko sahihi simply kwa kuwa na wabunge 47 kati ya zaidi ya 200! Baadhi ya watanzania na ujinga wao wanaamini CDM inaweza ikafanya maajabu bungeni!!!! Hizi ni ndoto za alinacha

6. CDM baada ya kuchanganyikiwa na matokeo bado haija recover from that shock!!! Maamuzi yake, misemo yake, mienendo yake si ya UTAIFA BALI NI UCHADEMA this is catalysed by the fact that they have money from our kodi (ruzuku) this made them to forget that they are making history today that will be a joke of tomorrow!!!! History is being written kuna vitu in near future itakuwa ni ngumu sana kwa watu kuvimeza kwa sababu ya makosa ya leo,

7. Kama ni kutofautiana na CUF na vyama vingine, is better they use a better language au kutoa sababu zingine na si kuwa CUF NI SEHEMU YA SERIKALI, HUU NI UOZO MKUBWA SANA AMBAO KWA KAMATI KUU YA CHADEMA HAIKUPASWA KUANDIKWA, ni uozo unaoelezea mawazo na nia yao kwenye hii nchi ni nini, kweli hakuna wenye busara wa kunena na kuandika kutokuungana na CUF yet mkatoa sababu zingine na sii kuwavunja nguvu na kutangaza bifu, kwa wengine CUF iko juu mbali zaidi ya CDM na walipofikia Zanzibar is desired most kwa yeyote mpenda mabadiliko-bara HUU NDIO UKWELI!!!!


JE CHADEMA HAWAJUI UKWELI??

Definitely chadema na wasomi wa type ya Slaa wanajua ukweli wanajua faida ya serikali ya umoja wa kitaifa na wanajua you can still abide to your ideology regardless of whether you are in coalition governments or not! CHADEMA WANAWADANGANYA WANACHAMA WAO na hasa JF-Kata, wanawajaza ujinga kiasi cha kuwa leo hii tuwaze tu kuwa na single party governments, YES we may have that lakini sio kwa kukashifu kuwa coalition govern. Ni mbaya!!! Na hawawezi kuungana na CUF Kwa sababu hiyo, huu upupu wa kihistoria utaandikwa kila leo kwa ku-joke chadema, tupo..jamani

Chadema chini yawafanyabiashara wanajua fedha za kambi ya upinzani wanazopata wao ni zao kwa sasa na hazitakiwi kugawanywa! What a selfish!!! Then they tell people cheap reasons why CUF is not among them??


WITO

Yes I know and I believe kuna matusi kibao yatatoka kwa ‘JF-Chadema kata', kuna wenye hoja watatoa, ‘JF-Chadema wakongwe ', kuna hoja na supportive documents zitatoka kwa wote wenye kupenda mabadiliko hawa ni JF-huru!

Jamani taifa hili litajengwa na wote, tukifikia muda wa kugawanyika CCM hatoki na tutaishia kusema tu na mvi zinakuja inakuwa mwaka wa 2015 na 2100 CCM will be in power.

After all CHADEMA they are not so opportunist and influential they can buy what is happening in Mistri, Jordam and Yemen… hawana muda huo wala hawawazi hayo, yet kuna watu mnalilia chadema , kutotaka kufikiri matokeo (results)/output ndio imetufikisha hapa tulipo leo. Hii ndilo linakujwa swali je hawa CDM hawakujua katiba na NEC ina matatizo kabla ya uchaguzi? Walifikiri wataichukua Tanzania watawale kama CCM? Hivi hula za kichadema na ki-ccm kwa namna gani zimetofautiana kwa matendo yao?? Msio taka kusikia shauri zenu ,

CHADEMA STOP THIS NONSENSE OF SAYING THAT CUF ISA PART OF GOVERNMENT GO TO SCHOOL!!!!! we dont trust you either!



References


Read more:
WIKIANSWER
Wikipedia
Tamko la chadema

sitajibu vijembe, matusi, na statement za hasira au zenye conclusion zisizo na tija, count your post wasted or applauded na wafuata mkumbo, nitajibu hoja zilizoenda shule..........


Haya chakula hicho!

Your article is good but you missed the point from the beginning.....CHADEMA and CUF is not a coalition government...they are not in power....what CHADEMA is saying is that technically CUF is not an opposition party but a governing party through the coalition with CCM in the Isle governent. So, by them joining forces with CCM it means their ideology is somehow similar to CCM's. Therefore, they cannot critisize or srutinize goverment's programmes or policies when they are in on decision-making table. In the parliament, if it was set up like the british parliament where will CUF MPs sit? On the opposition side or on the goverment side?

I present to you
 
MI nahisi mtoa mada hayupo nchini pia hajui kinachoendelea kwenye taifa hili then...hajui nisababu ipi inafanya CDM wawakatae CUF

coz hata hiyo mifano ya nnchi alizo tolea mifano mambo yao nitofauti kabisa na mzozo kati ya CDM na CUF

IN SHORT CUF na CCM ni kama mke na mume...sasa mke anatumwa na mumewe .......kwa manufaa ya mume.
 
may be you are right my dear, lakini nimetoa definition kwa kile ninachokisema...hujaona? that definition may stand as assumption, and it defending me! hayo mengine hayana tija , kama definition iko wrong then that is debatable.....

sorry I am not CUF fans, jaribu kuwa huru mkuu, usione kila mpinzani wa chadema ni cuf, na kila anyetetea chadema ni mchadema!!! that is very wrong, uache hii tabia labda kama unaweza kujitetea kama nilivyojitetea awali.

Umejitahidi sana kujitetea, nimependa jinsi ulivyotoa angalizo kuwa si mmoja wa CUF fan na si kila anyetetea chadema ni mchadema. Lengo langu kuu kukutaka ujielimishe zaidi lilikuwa kukurudisha ktk mstari pamoja na kuwa ww ndio mleta hoja hapa. Kukurudisha ktka mstari kuwa hoja yako ni uundwaji kambi ya upinzani bungeni. Ungekuwa unafahamu kuwa CDM kisheria wanaqualify kuunda (peke yao) kambi ya upinzani kutokana na kuwa wametimiza vigezo. Pili hoja ya kuvishirikisha vyama vingine haina msingi wowote kwani CDM wametimiza masharti ya kuunda kambi hiyo kisheria. Kama utayafahamu haya utajua kuwa uwezo wa vyama vingine kuunga mkono hoja za CDM ndani ya bunge uko palepale.Hivyo hoja ya kulazimisha CDM kuviingiza vyama vingine hususani CUF ndani ya kambi yao haina msingi wowote. Having said that kinachobaki ni kuwa motive ya CUF na vyama vingine vinavyolazimisha kuwa kambi ya upinzani ni finance tu. Pesa (pamoja na umaarufu) watakayopewa CDM kama kambi ya upinzani ndio inawasumbua kina Hamadi na Kafulila, vinginevyo fursa yao kama vyama vya upinzani (excluding CUF) yako palepale.
 
Hivi nyie watu wa JF mlitaka watu wa zanzibar wafanyeje labda?

Labda walitaka wawalambe miguu wafalme wa Chadema. Wamesahau siasa ni mitazamo yenye kuwavutia watu. Sasa kama hawajawakubali mlitaka mshirikishwe katika serikali umoja pasina kuwa na wawakilishi??? Mie sijui lakini nahisi wivu au ubaguzi umewajaa wanachadema.
 
Hivi nyie watu wa JF mlitaka watu wa zanzibar wafanyeje labda?

Hakuna mwenye ugomvi na serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar na hususan kwa cuf kuwepo serikalini.
Na kwa muktadha wa thread hii, kisichokubalika ni cuf kutaka kupitia mlango wa nyuma kuingia kambi ya upinzani ili kukamilisha kazi watakayokuwa wanatumwa na ccm.
Duniani kote hakuna chama kinachoshiriki kuunda serikali na wakati huo huo kuunda kambi ya upinzani. Sasa kama mnataka kufanya majaribio hapa kwetu hiyo kitu haikubaliki.
 
Hivi nyie watu wa JF mlitaka watu wa zanzibar wafanyeje labda?

Nafikiri kuendelea kuangalia mambo kutokana na mitizamo ya vyama si sahihi na hapa JF si mahali pake. Mimi nashauri watu tuwe objective kama kuna hoja ya msingi inakuja hapa basi inajadiliwa kwa uelewa wa hali ya juu na si kishabiki. Swali lako limenitatiza kidogo, I would expect ww kufahamu vizuri sana kuwa it was not CUF idea kushirikishwa ktk serikali ya CCM. CUF walikuwa na malengo mazuri tu ya kahakikisha wanzanzibari wananufaika na nchi yao kwa ujumla wao ktk nyanja zote ikiwa ni pamoja na kiuchumi na si kunufaika kwa watu wachache. CCM waliliona hilo na ndio wao waliokuja na wazo la kuwashirikisha CUF serikalini (kukata mzizi wa fitina) ili wasijeng'olewa na CUF. CUF wamenasa ktk mtego huo wa CCM ndio imefika hapo ilipo. Sasa wanaJF wanacho-argue ni kuwa si kweli kuwa siku zote hizo CUF ilikuwa inafight kushirikishwa serkalini bali ilikuwa ina-vita vikubwa zaidi kisiasa, kiuchumi nk ambayo kwa bahati mbaya imeshindwa vita hiyo. Kama ni mfuatiliaji utagundua kuwa pamoja nakushilikishwa kwa CUF serikalini manifesto inayotumiwa kuongoza nchi si ya CUF bali ni ya CCM meaning ideas zote nzuri za CUF zinakuwa vigumu kutekelezeka.
 
JK hivyo unasema kuwa Chadema problem ya udini haiwatafuni? basi nimeshindwa mimi ila utafiti wangu mdogo tu nilioufanya unaonyesha udini unawatafuna Chadema kama hawajaligundua basi nawatakia kila la kheri.

Propaganda ya problem za udini ndani ya Chadema na hata kwa jamii ya watz zinaenezwa na CCM ili kuwatisha watanzania. CCM wanamtumia Zito kueneza propaganda hizo ndani ya CDM na ndio maana baada ya kushtukiwa Zito amekaa kimya. CCM waliona hawana hoja ya msingi ya kuwaeleza watanzania ikabidi wakimbile kwenye dini ili ku-divert attention ya watu.
 
Back
Top Bottom