Inflammatory: CHADEMA hawako kwa maslahi ya taifa, they are just another tool

Naanza hoja yangu kuangalia msimamo wa chadema kwa CUF na kueleza ukweli kuhusu caolition governments

Maana yake:

A coalition government is where two or more political parties join together in parliament/assembly to run the government and agree on a policy programme


Faida zake:
  • Government will be more consensus-based: resulting policies will be broadly approved of

  • Better representation of the electorate's wishes

  • Better quality of policy: enhanced scrutiny and increased attention paid to each policy

  • Increased continuity: election does not lead to dramatic overhaul which can produce fragmented rule2
Hasara zake:


· The most obvious criticism of Proportional Representation is that it could form coalition governments. This is seen by some as a majorly bad thing as it supposedly does not allow ‘strong’ government. Having more than one party in charge of decision making could cause a lot of arguments between the leaders of the country as the top ministers may have opposing political ideologies and views. It could also mean that it is very hard to get policy through the governmental process meaning government could be overall less effective in the running of the country.

· It could also cause an overly expanded Cabinet to cater for everyone’s needs in the Government, which could lead to much needless expenditure.


· There could also be many arguments, which cause Cabinets to split and some important policy to be suspended to do the impossible task of keeping everybody happy


Mifano ya nchi zinazounda serikali ya umoja wa kitaifa


Europe:

Albania, Andorra, Austria, Belgium, Croatio, Belgium, Czech, Denmark, Finland, Estonia, Germany, Iceland, Ireland, Italy, Kosovo,Latvia, Lithuania, Luxembourg, Monaco, Montenegro, Netherlands, Norway, Poland, Romania, Serbia, Slovakia, Slovenia, Sweden, Switzerland ( has been ruled by a coalition of the four strongest parties in parliament from 1959 to 2008 called the ‘magic formula”), Ukraine and UK

Americas

Chile, Trinidad and Tobago, Suriname, Canada.

Africa:

Algeria, DRC Congo, Gabon, Guinea-Bissau, Kenya, Mali, Mauritania, Mauritius, Morocco,Senegal, Zanzibar Island, and Zimbabwe (was proposed not sure if still exists)

Asia

Armenia,Bangladesh,Cambodia,India,Indonesia,Iraq, Isarel, Japan, Lebanon, Malaysia, Maldives, Pakistan, Sri-Lanka, Thailand, Timor-Leste

Ocenia

Australia, New Zealand, Papua New Guinea, Vanuatu

Kwa nini huwa inaundwa?;

The usual reason given for this arrangement is that no party on its own can achieve a majority in the parliament. A coalition government might also be created in a time of national difficulty or crisis, for example during wartime, to give a government the high degree of perceived political legitimacy it desires whilst also playing a role in diminishing internal political strife. In such times, parties have formed all-party coalitions (national unity governments, grand coalitions)1

Kwa nini nchi nyingi zenye mfumo huu zimeendelea ?

Pamoja na hasara zake which is debatable advantages of coalition governments is far million times better than its disadvantages. How and why

1. Kutenganisha siasa na utendaji kazi wa serikali , kwa mfano Japan average ya prime minister kwa mwaka!, karibu kila mwaka wanakuwa na waziri mkuu mpya ambaye ni kama rais wa nchi! Still economic activities are growing up very fast!! Ufike muda tuone utendaji wa kisiasa unakuwa kwenye kushindana ku-implement policies na sio kuingilia professionals. Kwa sababu hii nchi nyingi zimefanikiwa kuendelea pamoja na kuwa coalition governments ina udhaifu wake lakini afadhali kuliko kutokuwa nayo

2. IKIFIKIA level, au wakati kuwa uamuzi wowote mzuri regardleess umetolewa na chama gani unafaa kuungwa mkono then that is a sign and good grounds of endorsing this system. Ifikie muda kila kiongozi anawaza mema kwa ajili ya nchi yake na KUPATA UONGOZI SI KWENDA KUJIONYESHA KUWA WEWE NI RAIS BALI KUTATUA MATATIZO FULANI YA NCHI YAKO KWA LENGO LA KULETA MABADILIKO AMBAYO YATALINDA HESHIMA YAKO.

3. Kuwa siasa sio uadui bali ni ushindanifu wa hoja, malengo, policy na ni hulka kamili ya binadamu kutofautiana na ni jambo la kukusudiwa na kila mmoja kujenga nchi moja pamoja na kuwa mnaweza kuwa na mitazamo tofauti, if we will reach this stage we are through!

Je kuna faida gani au kwa nini serikali ya umoja wa kitaifa ni muhimu hasa kwa nchi za dunia ya tatu ambazo vyama vingi ni vile vya kibeberu.

Kuna solutions mbili kubwa aidha kuwatoa kwa nguvu, maana ballot box cannot do anything! You heard me! But if we inclined to accept evolution not revolution then second option i.e coalition government is another good techniques ya kuwaondoa mabeberu!! Why and how

FAIDA YA serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania

1. Ni kichekesho na uhuni na uvunjivu wa haki za kibinadamu kuwa chama fulani kikipata kura asilimia 60 then wanaongoza nchi yote regardless of those 40% who did support them. Kwa mfano haingii akilini kuwa kikwete alipata asilimia 60 then wengine hawatakiwi kuunda serikali!!! Ambao tulisupport vyama vingine itakuwa rahisi na vizuri tukiwakilishwa serikalini walau kupata wizara kulingana na idadi ya kura zilizopatikana, let say CDM inapata wizara 3 out of 10! Is well and good

2. Serikali ya umoja wa kitaifa inavipa breakthrough vyama vingine kwa kuonyesha uwezo wao wa kiutendaji na kujenga hoja, this is like a continuing evaluation ya kuwa je CDM wamepewa wizara 3 wanafanya vizuri wakipewa urais si ndiyo watafanya vizuri zaidi?

3. Serikali ya umoja wa kitaifa inaviimarisha vyama, inajijenga na kupanua demokrasia ambayo tunaona haipo si kwenye chama tawala hata vya upinzania pia. Kwa mfano tulishuhudia Hilary na Obama wakipambana kwa hoja na sera zao ngali wako chama kimoja na mwisho wa siku wakamaliza vyema!!! Kama tunalipenda taifa we can still argue while we are in the same governments! Hii ni level ya juu lakini ni nzuri

4. KUBWA KULIKO YOTE ni kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itahimiza watu kujitokeza kupiga kura wakiamini kuwa wingi wa kura zao ndio unaipa nafasi kubwa chama chao kushika serikali, MOTISHA YA KUPIGA KURA NI KUBWA SANA KWENYE HZI SERIKALI NA WATU HAWAKATI TAMAA kuwa hata nipige vipi CCM watapita

5. Kufanya maamuzi ya kijinga ya kichama inakuwa ngumu kwenye cabinet

6. Msisahau wanasiasa ni wanasiasa they are born with same parents! Coalition governments inaweka msimamo kuwa hakuna chama kinachoa AMINIWA


Je what can we do now?

Mabadiliko ya katiba yanatakiwa ya accommodate issue nyingi ikiwemo hili

Je CUF na CCM Zanzibar hali ikoje?

Nimekaa Unguja na nimeona mabomu yakipigwa kwa wana CUF, na mimi kuathirika, nimeshuhudia chaos nyingi kwa macho yangu na leo hii natamani nirudi unguja nione hali ikoje!!! Coalition governments was the only solution for that situations! Wanaoibeza CUF idha hawajui maana ya caolition, hawajui kilichokuwa kinaendelea Zenj na wako blindly kuhusu nini maana ya coalition. Ni mwanzo mzuri sana ila inabidi iende mbali zaidi kuzungumzia

Vipi kuhusu tamko la CHADEMA na MSIMAMO WA CHADEMA


I don’t support that tamko kwa sababu hizi

1. Chadema imefail kuwaambia au kujibu hoja ya coalition governments kwa greater heights, wanajibu cheaply kuwa CUF NI sehemu ya serikali!!! Kuwa sehemu ya serikali hakukupi mwanya kuwa usisimamie unachokiamini ndiyo maana USA hatuvitaji Republican kama ni chama cha upinzani!! Tunakitaja kwa majina yao ndivyo walivyo, IFIKIE MUDA TUSEME YULE NI MCHADEMA SIYO KWA SABABU NI MPINZANI KWA SABABU YA YALE UNAYOYASIMAMIA!!!


2. They have depicted high level of ignorance regarding coalition governments, KWANZA KAMA VILE HAZIPO, pili kama vile ni mbaya, same chadema waliungana na CCM huko Kigoma kwenye umeya na that was good example of coalition government –type


3. Kukataa coalition governments kuna onyesha vitu viwili, CHADEMA wana uroho wa madaraka na wanaiona TANZANIA KAMA NYAMA FULANI INATAKA KUDONDOKA NA WAO WANATAKA KUIRUKIA….., Tanzanias are very clever the only thing that CDM will be supported if they can agree that coalition governments is a solution because people don’t trust them either! Believe me humu JF kuna tendency ya kutoangalia ukweli wa kulijenga taifa ila ni ubishi wa kishindani usio na maana kutaka cheap popularity ya ghost members usiowaona, can you stand alone?

4. Chadema imejiwekea wigo wa kujionyesha kuwa they can fight corruption alone and only alone!!! Hii ni hatari sana kwa wapenda mabadiliko , umoja wa kitaifa kupinga yanayorudisha taifa nyuma ni wajibu wakila mtu regardless of which part he belongs. Leo hii ni nadra CDM kuunga mkono CUF kile ambacho hata wao wanakipigania…huu ni utoto na high level of stupidity na ni sumu mbaya sana kwa wapenda maendeleo

5. Chadema ina ona kila wanachokisema kiko sahihi simply kwa kuwa na wabunge 47 kati ya zaidi ya 200! Baadhi ya watanzania na ujinga wao wanaamini CDM inaweza ikafanya maajabu bungeni!!!! Hizi ni ndoto za alinacha

6. CDM baada ya kuchanganyikiwa na matokeo bado haija recover from that shock!!! Maamuzi yake, misemo yake, mienendo yake si ya UTAIFA BALI NI UCHADEMA this is catalysed by the fact that they have money from our kodi (ruzuku) this made them to forget that they are making history today that will be a joke of tomorrow!!!! History is being written kuna vitu in near future itakuwa ni ngumu sana kwa watu kuvimeza kwa sababu ya makosa ya leo,

7. Kama ni kutofautiana na CUF na vyama vingine, is better they use a better language au kutoa sababu zingine na si kuwa CUF NI SEHEMU YA SERIKALI, HUU NI UOZO MKUBWA SANA AMBAO KWA KAMATI KUU YA CHADEMA HAIKUPASWA KUANDIKWA, ni uozo unaoelezea mawazo na nia yao kwenye hii nchi ni nini, kweli hakuna wenye busara wa kunena na kuandika kutokuungana na CUF yet mkatoa sababu zingine na sii kuwavunja nguvu na kutangaza bifu, kwa wengine CUF iko juu mbali zaidi ya CDM na walipofikia Zanzibar is desired most kwa yeyote mpenda mabadiliko-bara HUU NDIO UKWELI!!!!


JE CHADEMA HAWAJUI UKWELI??

Definitely chadema na wasomi wa type ya Slaa wanajua ukweli wanajua faida ya serikali ya umoja wa kitaifa na wanajua you can still abide to your ideology regardless of whether you are in coalition governments or not! CHADEMA WANAWADANGANYA WANACHAMA WAO na hasa JF-Kata, wanawajaza ujinga kiasi cha kuwa leo hii tuwaze tu kuwa na single party governments, YES we may have that lakini sio kwa kukashifu kuwa coalition govern. Ni mbaya!!! Na hawawezi kuungana na CUF Kwa sababu hiyo, huu upupu wa kihistoria utaandikwa kila leo kwa ku-joke chadema, tupo..jamani

Chadema chini yawafanyabiashara wanajua fedha za kambi ya upinzani wanazopata wao ni zao kwa sasa na hazitakiwi kugawanywa! What a selfish!!! Then they tell people cheap reasons why CUF is not among them??


WITO

Yes I know and I believe kuna matusi kibao yatatoka kwa ‘JF-Chadema kata’, kuna wenye hoja watatoa, ‘JF-Chadema wakongwe ‘, kuna hoja na supportive documents zitatoka kwa wote wenye kupenda mabadiliko hawa ni JF-huru!

Jamani taifa hili litajengwa na wote, tukifikia muda wa kugawanyika CCM hatoki na tutaishia kusema tu na mvi zinakuja inakuwa mwaka wa 2015 na 2100 CCM will be in power.

After all CHADEMA they are not so opportunist and influential they can buy what is happening in Mistri, Jordam and Yemen… hawana muda huo wala hawawazi hayo, yet kuna watu mnalilia chadema , kutotaka kufikiri matokeo (results)/output ndio imetufikisha hapa tulipo leo. Hii ndilo linakujwa swali je hawa CDM hawakujua katiba na NEC ina matatizo kabla ya uchaguzi? Walifikiri wataichukua Tanzania watawale kama CCM? Hivi hula za kichadema na ki-ccm kwa namna gani zimetofautiana kwa matendo yao?? Msio taka kusikia shauri zenu ,

CHADEMA STOP THIS NONSENSE OF SAYING THAT CUF ISA PART OF GOVERNMENT GO TO SCHOOL!!!!! we dont trust you either!



References


Read more:
WIKIANSWER
Wikipedia
Tamko la chadema

sitajibu vijembe, matusi, na statement za hasira au zenye conclusion zisizo na tija, count your post wasted or applauded na wafuata mkumbo, nitajibu hoja zilizoenda shule..........


Haya chakula hicho!


umejitahid,lakini upuuuzi wote nonesense.
 
Waberoya!!!Salam

Kwanza kabisa nikupongeze kwa kutuwekea somo zuri kabisa.Nakiubaliana na somo lako laikini pia nakubaliana na hoja zako.

Kimsingi haya yote yanafahamika kwa chama chochote makini cha siasa.Hakuna chama cha siasa hapa nchini kisichofahamu umuhimu wa coaltion na siku zote vyama hivi vya upinzani vimekuwa vikipigana tafu pale inapobidi.Itakumbukwa kuwa CDM,CUF,TLP na NCCR Waliungana huko nyuma ili kushirikiana katika mambo yanayohusu Upinzani na walijitahidi kidogo kuheshimu mashirikiano hayo.Lakini baadaye ushirikiano huu ulikufa kabisa,mpaka sasa sababu za msingi hatujaambiwa ila kila chama kinamtuhumu mwenzake.

Tatizo lililopo ni kuwa vyama vyetu hivi vinaubinafsi sana hatuna dhamira ya pamoja ya kujali maslahi ya taifa kwanza.Tulishindwa kuwa na sauti ya pamoja wakati wa mambo madogo wakati tunashirikiana,leo hii tunawezaje kuungana Bungeni kwenye maslahi ya Taifa?Kuunda Baraza Kivuli la pamoja sio jambo dogo hata kidogo.CUF tayari wanandoa na CCM na ndio maana wakati CDM tunalia hatumtambui Rais wenzetu walikuwa kinyume nasi kwakuwa Maalim Seif alikuwepo kwenye msafara wa Kikwete wasingeweza kumuacha peke yake Bungeni.CUF wanaongoza dola.Ni ngumu sana kushirikiana na chama cha aina hii kwenye masuala nyeti kama kuwa na serikali mbadala.
Mnaandaje bajeti mbadala na chama ambacho kinaunga mkono serikali?Kisera,kisiasa na hata kimahesabu haiwezekani.Kama kuna nchi imewahi kufanikiwa katika hili basi ni kwa kiwango kidogo sana. Natambua umuhimu wa kuunganisha nguvu lakini kwa mazingira ya sasa ya kisiasa ni ngumu.Bado tunaoneana gere,vyama vyetu havijawa na ukomavu wa kujali maslahi ya taifa kwanza,hakuna chama kinachokubali kuona chama chenzake kipata maendeleo.Na hii ni spirit nzuri.Siasa ni Ushindani,tumeshindana tumeshinda lets enjoy our cake.
Lakini pia Waberoya ukumbuke kuwa maslahi ya taifa hayajengwi kwa kuungana kwa vyama kwani kuna sheria inayoibana CDM kwa hilo?kwani wananchi wameomba hilo?kama ingekuwa ni hitaji la wananchi wengi basi tungesema CDM wamekosea lakini sio hivyo,Sio hitaji la wananchi.Sidhani kama kuwa wamoja kwenye Baraza Kivuli ndio kuwa na nguvu.Nguvu Bungeni inajengwa kwenye kujenga na kuchambua hoja.CUF na vyma vingine vilivyoko Bungeni bado vinafursa kubwa za kujali maslahi ya taifa bungeni bila kuwa mawaziri.Kwamfano
Anna Kilango,Selelii,Shelukindo,Kimaro,Mwakyembe,Zitto,Dr Slaa na wengineo walikuwa mawaziri kabla hawajajipambanua kuwa ni makamnda wa kujali taifa kwanza?

Waberoya siasa za wenzetu sio sawa na za kwetu,kwetu siasa ni upepo,leo unavuma huku kesho kule.Literature nyingi za wenzetu zitabaki kuwa theory tu wala hazitekelezeki.Siaza zetu hazieleweki,hazishikiki,hazitabiriki.Zipo tu zinaelea,itakavyotokea ndio hivyo hivyo,ilimradi siku zimekwenda.

BTW:Tangu mwanzo wenzetu walikataa kuwa na sisi wakiamini kuwa wangeweza kuwa na kambi isiyo rasmi Bungeni ila baada ya kuona uwezekano ni mdogo ndipo wakabisha hodi CDM.

Vile vile nimesoma gazeti fulani linasema kuwa Hamad Rashid ndiye aliyabdilisha kanuni za Bunge zilizotoa rum kwa Mbunge yeyote wa Upinzani kuongoza kamati za POAC,PAC na LAC baada ya kushindana na Cheyo na kushindwa.
 
Wabz, you said it well. I have been wondering since I read the press release of Chadema CC's and I see a party trying to run solo. If they do not keep Utaifa mbele, they should forget it!
 
Kwani ajabu nini?

Mazingira yamenifanya nisipige kura hadi leo hii. Si kuwa sitaki, la hasha.

Uchaguzi wa kwanza nilikosa kwa sababu nilikuwa sijamaliza miaka 17 na ilikuwa uchaguzi pekee ningeliweza kupiga kura.

Uchaguzi wa pili, nilikuwa Msange JKT na sikuweza kupiga kura.

Kabla ya uchaguzi uliofuata kufika ambao nilipania haswa kupiga kura, Wazazi wangu walihamia Kathmandu, Nepal ambako hadi leo tunaishi.

Nimejaribu sana kuulizia uwezekano wa kupiga kura kama USA, UK nk ila nimekuwa nikikataliwa.

Sasa hapo ajabu ni KIPI hadi kuandika Oo My God na kutowa mapovu?

Au wewe dunia yako inaanzia Bongo na Kuishia Bongo? Na unajifanya ni Great Thinker kwa kuja na kuandika hapa na kusagia wenzio ambao maisha yamewapeleka sehemu nyingine kabisa na wasiweze kupiga kura?

Naona umekaa sana Kathmandu na akili zako zimekuwa za Kihindihindi. Inatakiwa TUKUKAMATE na kuku-SATI hadi uwe majivu na majivu hayo tuyapeleke kwenye mto Wala, kwenye kijiji cha Kasisi wilaya ya Sikonge, Tabora ili yakaishie kwenye mto Malagalasi.

Siku nyingine angalia unataka kuanzisha Bifu na nani.

Naona leo utarudi kwenu unatamba kuwa "nimerusha bifu na SIKONGE wa JF....."

Ngoja nimalizie kwa lugha ya APACHE, MSULA EVE........... PIECE!!!!!!!!
oo My God! Huu ndo ujinga uliopo bongo! hichi nacho ni cha kusema wazi kwenye jukwaa la great thinker? hii ni aibu!
 
Ha ha haaa!

Easy guys! CUF (kupitia J. Mtatiro) wanatokwa na mapovu kuhusu uamuzi wa CDM. Waberoya anatokwa na mapovu kuhusu uamuzi (Mwenyewe anadai ni sababu) wa CDM.

What is happening?????????????
 
Good move cdm never allow "waswahili" kuja kupata kula na nyie cake yenu ..waache walalame tu for next 5 years ok..

Nilitegemea na nimefurahi wamefanya the same thing..safi sana

CUF acheni kulalama chapeni kazi..kuungana ni dalili ya uvivu,

Besides wananchi wanataka opinions nyingi siyo pro-cdm or pro ccm or pro cuf..we need them all..
 
Weberoya, mtu mwenye akili timamu kwa sasa hawezi kuwashauri viongozi wala wanachama wa CDM kwa kuwa kama ulivyosema mwenyewe bado hawajaamka kutoka katika mshtuko wa matokeo ya uchaguzi, nakushauri save ushauri wako for now watakuja kuutafuta wenyewe kwako, unless unataka matusi endelea.
 
Tukumbuke kuwa CUF kwa sasa ni undefined organ; upinzani wanataka,lakini wakati huohuo wao wanaongoza serikali kwa kushirikiana na CCM, linapokuja swala la maamuzi ya kiutawala watakaa na CCM, Kwa upande mwingine linapokuja swala la kuipinga serikali ya CCM wao pia wanataka washirikishwe na CDM.Hili ni janga la kitaifa kuwa na chama cha aina hii.

Hatuwezi kuwaona CUF kama chama cha siasa, kwani hakina tija kwa watanzania.

Mkuu,
Wazanzibari ni watanzania?
Kama jibu lako ni ndio basi sahihisha maandishi yako.
CUF ina tija kwa watu wa huko Zanzibar lakini pia katika kushape siasa za Tanzania. Mkuu, unakumbuka vizuri tokea siasa za vyama vingi zimeanza NCCR, CUF ndio vilikuwa vyama vya siasa!!??? kwa maana unayoitoa hapa!
Au Tanzania ni Tanganyika tu(Tanzania bara)?
Mkuu, tunachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja, plus ushabiki...
 
It is ok, sibaliki wala silazimishi muungano wa cuf na cdm, japo unaweza kuwa na impact in near future.ninachopinga ni sababu inayotolewa na cdm kuwa cuf ni sehemu ya serikali, hii sababu inaidhalilisha chadema yote kuwa still hawajui upinzani ni ideology sio kuwa against!!!!!!!!!!!!!!!

Waberoya hivi wapi umesikia kamati kuu ya CDM ikibeza muungano wa CUF na CCM? Muungano huo ni muhimu na sijasikia CDM wakibeza kwamba wasingefanya hivo. Huo serikali ya mseto sote tunakubali kuwa ni muhimu kwa amani ya Zanzibar. Tatizo linakuja kwamba CUF hawataki kuelewa nafasi yao sasa baada ya kuunda serikali ya muungano. Waliingia kwenye serikali bila kujua impact yake kisiasa kwao. CHADEMA WAMESEMA CUF NI SEHEMU YA SERIKALI. CCM ndio chama kinachotawala Zanzibar na wameungana na CUF huko kuunda serikali. Haohao CCM wanatawala serikali ya Muungano. Kwa kuwa CCM inaunda serkali zote za Muungano na Zanzibar by implication CUF is part of the government. Hili swala dogo lisilotaka degree inawashindeni vipi kuelewa. Watakuaje sehemu ya serkali ya Zanzibar inayoongozwa na CCM na wawe wapinzani wa CCM bara?
Unamtaka Dr. Slaa atumie lugha gani kueleza nafasi ya CUF kwenye serikali?
Kwa mfano rahisi kusema wanzaibar ni sehemu ya serikali ni kosa. Wanakuja kuwa sehemu ya serkali kupitia serkali ya Zanzaibar ambayo kupitia hapo wanakuwa makamu wa Rais, waziri nk. Je Maalim Seif kwenye itifaki ya ya serkali ya Tanzania hayumo?
Ukiacha ushabiki CUF kuwaita ni sehemu ya serkali si makosa! Manake ndio ukweli kuwa wameungana na CHAMA dola kutawala Zanzibar.
Kwanini walikubali serikali ya kitaifa kama kama kuwaita kuw ni sehemu ya serikali hawataki wakati ndio ukweli wenyewe?
Mshika mbili mmoja humponyoka. Ni vema CUF wakatambua kuwa si rahisi kukubalika kuwa chama cha upinzani wakati wanashirikiana na chama kinachotawala hata kama kushirikiana huko ni kwa manufaa.
CDM wako sahihi kabisa.
 
Waberoya,

Siasa ni kama MAISHA. Siasa siyo hesabu ambazo zina sheria zake. Kwenye hesabu kuna kitu kama MAGAZIJUTO. Ukipewa hesabu yoyote, inabidi ufuate hiyo sheria na ukibadilisha, utapata jibu la ajabu.

Pia unasahau kuwa tuna tofauti kubwa sana katika vichwa vyetu, mahali tunapoishi, mila zetu, utamaduni wetu nk na hao unaotupa mfano.

Mfano kwa USA, Rais hawezi tu kwenda kwenye BoT ya USA na kuchukua hela kwa ajili ya uchaguzi.

Rais hawezi kuingia mikataba ya ajabu ajabu na kuwalazimisha watu wake walipe hayo madeni.

Rais hawezi kuwa anasafiri ovyo ovyo hadi kwenda kuweka Mauwa kwenye kaburi la Mke wa Rais ambaye alikufa miaka kadhaa nyuma.

Rais hawezi kuwa ananunulia Mawaziri na wabunge wake magari/nyumba na baadaye wanauziana kwa bei poa huku wananchi hawana mishahara, wanafunzi hawana hela.

Nchi kama UK, kuna vyombo vya usalama kibao ambavyo hadi vinashindana kunusa uchafu unaotaka kutokea. Wahindi UK walianza kujisogeza na kumwaga hela ovyo hasa kwa chama cha Labour. Utakuwa unakumbuka jinsi yule Mhindi alivyorudishiwa hela zake na wale Ndugu wawili kama sikosei Mithaal wakakataliwa uraia. Mohamed Al fayed pamoja na kuwekeza hela zake nyingi tu, bado walimgomea kumpa Uraia.

Sisi akina Rostam si tu kuwa tunawapa Uraia na uongozi. Tunamwingiza hadi IKULU yetu na kumpa nguvu ya ajabu sana.

Uzinzi kwa uongozi ni jambo la kawaida. Uvivu na tabia nyingne mbaya kwa Tanzania na nchi nyingi za Africa ni jambo la kawaida. Na hapa unakuja na kusema tufuate SIASA kama nchi fulani.......

Unaweza kuwa sahihi sana na ingelikuwa vema iwe hivyo ila tu, ni lazima tujenge kwanza MISINGI ya kuwa kama wao. FMes ameshasema sana kuwa "viongozi wetu ni reflection yetu Watz wenyewe....." Kama hatutabadili tabia zetu kwa sasa, itatuwia ngumu sana kubadili nchi. Ni sawa na kuleta Mbengu nzuri sana shambani ila shamba lenyewe halijalimwa na magugu kibao na kibaya zaidi, wakulima wenyewe ni Wazaramo ambao ndiyo kwanza wanaanza ngoma ya kumtoa mwali.

Tanzania inabidi baadhi ya mambo yapindishwe hata kama hayataleta jibu sahihi ambalo ni 0. Ila kwa siku zinavyozidi, tutaanza kusogelea jibu sahihi. Ni kama kupata area ya umbo lisilo na sura maalumu. Ukiweka vibox vikubwa na kuvihesabu, utapata AREA yake. Ukipungza ukubwa wa vibox au viduara, unapata jibu lililo karibu zaidi na ukweli. Ukipunguza tena na tena na kufanya SUM UP au Integration, utapata jibu lililo karibu zaidi na ukweli ila kuhesabu itabidi utumie computer.

Binadamu si kama Nyumbu ambaye anazaliwa na kutembea. Sisi inabidi muda. Ila amini nakuambia, kuna siku si tu kuwa tutatembea, la khasha. Tutatimua mbio haswa na tukishinda tutacheza kama Usain Bolt, NUH LINGA.
 
Siyo kweli Mkuu.

Ingelikuwa hakuna jinsi, ingelibidi waungane na hao ma Mrs. CCM.

Ila kama hakuna ulazima, basi waendelee tu na Upinzani.

Kama CUF na hao nyumba ndogo nyingine za CCM wakitaka kweli kuwa WAPINZANI, basi waonyeshe hayo kwenye vikao vya Bunge.

Wakutane na CUF na watafute SIKU MOJA ya kufanya maandanamo nchi nzima kwa ajili ya kupinga Dowans kulipwa na shida ya umeme. Waonyeshe kwa mfano kuwa kweli wanataka kuwa Wapinzani na si kulalamika tu kuwa na waon wanataka KEKI na bila kufahamu kuwa KEKI ya Chadema, inakuja na kazi ngumu kabla hujaila.

Zitto alitaka kuila tu bila kuifanyia kazi na tulimwangushia hapa Mvua.

Hamad na Mtatiro, mipovu inawatoka kutaka ulaji. Ila hawako tayari kumwaga jasho hata kidogo. Ni huyu Hamad tulitegemea hata awe na Dr. Slaa kwenye uchaguzi wa Rais ila jamaa akajiona mjanja. Sasa hivi angelikuwa Chadema na labda angelikuwa Chadema pekee Zanzibar na nina imani angelipewa cheo kikubwa sana kwenye baraka kivuli cha upinzani.

Alitandika vibaya kitanda chake, sasa alale na maumivu yake.
Weberoya, mtu mwenye akili timamu kwa sasa hawezi kuwashauri viongozi wala wanachama wa CDM kwa kuwa kama ulivyosema mwenyewe bado hawajaamka kutoka katika mshtuko wa matokeo ya uchaguzi, nakushauri save ushauri wako for now watakuja kuutafuta wenyewe kwako, unless unataka matusi endelea.
 
Mimi nimesoma mambo ya mahesabu. Kimahesabu unachokisema ni hivi
cuf ( ccm + upinzani) = cuf and ccm + cuf and upinzani.
Kwa hiyo no more upinzani kwa sababu siri za upinzani na tawala zinakuwa kitu kimoja na ndipo ukinzani unaanza na kupoteza maana ya upinzani au kwa lugha ya kileo uana harakati. Usipoelewa hapa tena weka kanda ya Bonny Mwaitege ujifariji " Njoo ufanyiwe Maombi"
 
Tatizo lililopo ni kuwa vyama vyetu hivi vinaubinafsi sana hatuna dhamira ya pamoja ya kujali maslahi ya taifa kwanza.

Natambua umuhimu wa kuunganisha nguvu lakini kwa mazingira ya sasa ya kisiasa ni ngumu.Bado vyama vyetu havijawa na ukomavu wa kujali maslahi ya taifa kwanza,hakuna chama kinachokubali kuona chama chenzake kipata maendeleo.

Siasa ni Ushindani,tumeshindana tumeshinda lets enjoy our cake.

Siasa za wenzetu sio sawa na za kwetu,kwetu siasa ni upepo,leo unavuma huku kesho kule.siasa zetu hazieleweki,hazishikiki,hazitabiriki.Zipo tu zinaelea,itakavyotokea ndio hivyo hivyo,ilimradi siku zimekwenda.
.

Aksante Regia kwa kueleza sababu "halisi" ambazo zisingeweza kuwekwa kwenye tamko rasmi la chama kwa sababu za kiintelejensia.
 
Msingi wa hoja ni muhimu sana katika kujenga hoja. Ukishakosea msingi lazima ukosee hitimisho. Na ndivyo alichofanya Waberoya. Hoja ya Waberoya imejengwa katika msingi kwamba CHADEMA hawathamini mwafaka wa Zanzibar, na ndiyo maana hawataki kuungana nao. Na kwa sababu amekosea msingi wa hoja, utakuta kwamba, pamoja na kwamba kaandika maandishi mengi, marefu na mazuri, na kwa kweli katoa elimu nzuri sana kuhusu sababu za vyama kuungana, lakini utakuta kwamba hitimisho lake limipinda kwa sababu msingi wa hoja wa hoja ulikuwa umepinda.

Waberoya ametoa sababu kubwa mbili za vyama kuunda serikali ya pamoja, ambazo ni: i) pale ambapo hakuna chama kilicho na majority bungeni kama ilivyotokea UK kwenye uchaguzi wa juzi. Labda niongeze kwamba vyama vya upinzani vinaweza kuungana pale ambapo hakuna chama kinachoweza kuunda kambi ya upinzani bungeni peke kwa mujibu wa kanuni. Na hiki ndicho kilichotokea katika Bunge letu lililopita-si CUF wala CHADEMA waliokuwa na uwezo wa kuunda kambi rasmi ya upinzani kikanuni peke yao. Hivyo vikalazimika kuunda kambi ya pamoja. Kwa leo hii, sababu hii haipo kwa sababu kikanuni CHADEMA wametimiza masharti ya kuunda kambi peke yao. Kwa hiyo sababu hii haina sababu! Ile ya pili ina nafasi Zanzibar na ndio essence ya mwafaka lakini sio katika upande wa muungano.

Ni vizuri kuweka sawa swala la Mwafaka na CHADEMA ambalo ndio msingi wa hoja ya Waberoya:
i) CHADEMA tunathamini sana mwafaka wa Zanzibar na tulikuwa miongoni mwa taasisi za mwanzo kabisa kuwapongeza vyama vya CUF na CCM na tunaendelea kuwapongeza kwa uamuzi wao uliotanguliza maslahi ya nchi dhidi ya vyama. Tunatambua kwa dhati kabisa kuwa mazingira ya siasa yaliyofikiwa Zanzibar yalihitaji serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kusema kweli hili ni jambo ambalo Mwalimu Nyerere alilisema tangu uchaguzi wa mwaka 1995. Kwa hiyo hoja kwamba CHADEMA hawakufurahishwa au hawathamini mwafaka haina mshika wala maana yeyote na wala siyo hoja ya msingi hapa.
ii) Ukweli ni kwamba kwa mwafaka uliopo Zanzibar, CUF na CCM wameunda Serikali kwa pamoja na kwa hivyo Zanzibar hakuna tena upinzani na ndiyo maana hata Baraza la wawakilishi ilibidi warekebishe kanuni ili kufuta kambi rasmi ya upinzani bungeni. Nidyo kusema hakuna chama cha upinzani rasmi katika Baraza la wawakilishi.
iii) Binafsi na sympathize na wenzetu wa CUF kwa bara na naelewa kabisa hasira za ndugu yangu Julius Mtatiro. Wapo katika a very awkward position. Wanalazimika kuwa nusu chama tawala na nusu chama cha upinzani kwa huku bara. Sasa ni vigumu sana kujenga ushirikiano na chama cha namna hiyo. Kuingia kwenye ushirikiano ni uamuzi mgumu na una consequences zake, ikiwemo kuwa na confused identity. Ili kuwa na clear identity vyama huamua kuwa katika upande moja, ambao ni ule wa serikali. Ndicho ambo Liberal Democrats wamefanya na ndivyo ambavyo CUF wanapaswa kufanya na kusema kweli wamefanya hivyo. Katika chaguzi nyingi za madiwani wameshirikiana na CCM na wala sio CHADEMA.
iv) Ushirikiano wa vyama vya siasa unahitaji mazingira mwafaka na kuaminiana. Hamuwezi mkawa mnasema ovyo kwenye vyombo vya habari halafu mnasema mnashrikiana ili kuwaridhisha wananchi. Ifike mahala unafiki ukae pembeni mwa siasa zetu. Mazingira ya vyama vyetu hayaruhusu muungano wenye tija, na ilibidi tufanye maamuzi magumu kabisa na tutayasimamia kwa sababu tumefanya kwa misingi ya msingi na baada ya tafakuri ya kutosha. It's a tough decision, but politics are about making tough decisions and standing by them and accepting the consequences of those decisions. We believe we did the right thing and we will stand by our decision and for that we're ready to bear the consequences of our decisions, including being nagged and named!
 
Msingi wa hoja ni muhimu sana katika kujenga hoja. Ukishakosea msingi lazima ukosee hitimisho. Na ndivyo alichofanya Waberoya. Hoja ya Waberoya imejengwa katika msingi kwamba CHADEMA hawathamini mwafaka wa Zanzibar, na ndiyo maana hawataki kuungana nao. Na kwa sababu amekosea msingi wa hoja, utakuta kwamba, pamoja na kwamba kaandika maandishi mengi, marefu na mazuri, na kwa kweli katoa elimu nzuri sana kuhusu sababu za vyama kuungana, lakini utakuta kwamba hitimisho lake limipinda kwa sababu msingi wa hoja wa hoja ulikuwa umepinda.

Waberoya ametoa sababu kubwa mbili za vyama kuunda serikali ya pamoja, ambazo ni: i) pale ambapo hakuna chama kilicho na majority bungeni kama ilivyotokea UK kwenye uchaguzi wa juzi. Labda niongeze kwamba vyama vya upinzani vinaweza kuungana pale ambapo hakuna chama kinachoweza kuunda kambi ya upinzani bungeni peke kwa mujibu wa kanuni. Na hiki ndicho kilichotokea katika Bunge letu lililopita-si CUF wala CHADEMA waliokuwa na uwezo wa kuunda kambi rasmi ya upinzani kikanuni peke yao. Hivyo vikalazimika kuunda kambi ya pamoja. Kwa leo hii, sababu hii haipo kwa sababu kikanuni CHADEMA wametimiza masharti ya kuunda kambi peke yao. Kwa hiyo sababu hii haina sababu! Ile ya pili ina nafasi Zanzibar na ndio essence ya mwafaka lakini sio katika upande wa muungano.

Ni vizuri kuweka sawa swala la Mwafaka na CHADEMA ambalo ndio msingi wa hoja ya Waberoya:
i) CHADEMA tunathamini sana mwafaka wa Zanzibar na tulikuwa miongoni mwa taasisi za mwanzo kabisa kuwapongeza vyama vya CUF na CCM na tunaendelea kuwapongeza kwa uamuzi wao uliotanguliza maslahi ya nchi dhidi ya vyama. Tunatambua kwa dhati kabisa kuwa mazingira ya siasa yaliyofikiwa Zanzibar yalihitaji serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kusema kweli hili ni jambo ambalo Mwalimu Nyerere alilisema tangu uchaguzi wa mwaka 1995. Kwa hiyo hoja kwamba CHADEMA hawakufurahishwa au hawathamini mwafaka haina mshika wala maana yeyote na wala siyo hoja ya msingi hapa.
ii) Ukweli ni kwamba kwa mwafaka uliopo Zanzibar, CUF na CCM wameunda Serikali kwa pamoja na kwa hivyo Zanzibar hakuna tena upinzani na ndiyo maana hata Baraza la wawakilishi ilibidi warekebishe kanuni ili kufuta kambi rasmi ya upinzani bungeni. Nidyo kusema hakuna chama cha upinzani rasmi katika Baraza la wawakilishi.
iii) Binafsi na sympathize na wenzetu wa CUF kwa bara na naelewa kabisa hasira za ndugu yangu Julius Mtatiro. Wapo katika a very awkward position. Wanalazimika kuwa nusu chama tawala na nusu chama cha upinzani kwa huku bara. Sasa ni vigumu sana kujenga ushirikiano na chama cha namna hiyo. Kuingia kwenye ushirikiano ni uamuzi mgumu na una consequences zake, ikiwemo kuwa na confused identity. Ili kuwa na clear identity vyama huamua kuwa katika upande moja, ambao ni ule wa serikali. Ndicho ambo Liberal Democrats wamefanya na ndivyo ambavyo CUF wanapaswa kufanya na kusema kweli wamefanya hivyo. Katika chaguzi nyingi za madiwani wameshirikiana na CCM na wala sio CHADEMA.
iv) Ushirikiano wa vyama vya siasa unahitaji mazingira mwafaka na kuaminiana. Hamuwezi mkawa mnasema ovyo kwenye vyombo vya habari halafu mnasema mnashrikiana ili kuwaridhisha wananchi. Ifike mahala unafiki ukae pembeni mwa siasa zetu. Mazingira ya vyama vyetu hayaruhusu muungano wenye tija, na ilibidi tufanye maamuzi magumu kabisa na tutayasimamia kwa sababu tumefanya kwa misingi ya msingi na baada ya tafakuri ya kutosha. It's a tough decision, but politics are about making tough decisions and standing by them and accepting the consequences of those decisions. We believe we did the right thing and we will stand by our decision and for that we're ready to bear the consequences of our decisions, including being nagged and named!

Nakuaminia Kitila
 
Very smart Waberoya, huu ndo ukweli ambao watu humu hawapendi kuusikia. Mara kibao nimejaribu kuongea haya, lakini kwa vile watu wa humu wanaongozwa na upepo, wafata mkumbo, tafakari kwao ni mwiko. Mwenye akili na asikie
Na ikiwa kusema ni dawa basi ni bora kuendelea kusema hata kama watatia vidole na pamba masikioni. Ukweli hautakiwi, unatakiwa kusifia hata kama ni kusifu ujinga!!

Nanukuu semi hapa:

NI HERI NJAA YA TUMBO KULIKO NJAA YA AKILI...

NI HERI UTUMWA WA MWILI, KULIKO UTUMWA WA FIKRA...

NI HERI UMASKINI WA MALI, KULIKO UMASKINI WA ROHO...

ALISEMA MZEE SHAABAN ROBERT ''UTU BUSARA, UJINGA HASARA!" NA Laiti watu wakitafakari basi tunaweza kuifikia nchi ya Kufikirika iwapo tutaweza kuvuka nchi ya KUSADIKIKA!

Kwa waelewa wamenielewa, kwa ambao hawajanielewa "Namaanisha nimeunga mkono HOJA!"

Tubadilike kwa ajili ya Tanzania, Tanzania ni yetu sote na si ya baadhi. na wasijidanganye watu kwamba wao ni wateule dhidi ya wengine..
 
oo My God! Huu ndo ujinga uliopo bongo! hichi nacho ni cha kusema wazi kwenye jukwaa la great thinker? hii ni aibu!
Shhhhhh! ndio haohao wanaosema "KURA ZeTU ZIMIIBWA!!" ukifikiri sana unaweza kulia kama sio kucheka! Hio ndio aina ya kizazi tulichonacho kinachopigania mageuzi na Tanzania ijayo!!
 
kwanini mtu unaliona leo, suala la CDM kukataa muungano na CUF ni issue na hukuona tatizo pale Rashid Hamad aliposema wazi kuwa wanashindwa kuungana na CDM kuunda kambi ya upinzani kwa vile CDM haiimtambui JK ikulu?

je ubora wa CUF na CCM unategemea udhaifu wa CDM?

hii inaonyesha jinsi siasa zetu zinavyotazama zaidi watu badala ya dhana na masuala. Je tutegemee mabadiliko toka miongoni mwa watu wa tabaka la kati? tabaka kigeugeu? hasha, wataogeuza kwa nia njema taifa hili, wapo mitaani, vijijini na hawajui JF

they are comming and they do politics in plain language, and natural laws/ principles
 
mkuu SIKONGE heshima kwako,
sio siri nimekukubali kwa analysis yako ,umezungumzia mambo mazito sana na kila mtu mwenye ufahamu na akili timamu atayafikiria sana
Waberoya,

Wewe na kaka yako mkiishia kuishi kwenye KISIWA fulani na huko kuna Mwanamke mmoja, itabidi muanze kumchangia. Hiyo si kuwa ni wazo zuri ila kwa sababu HAKUNA NJIA NYINGINE.

USA akina Obama walikuwa wengi kwenye mabaraza yao na hawakutaka kusikiliza MJUSI yeyote. Mambo yamebadilika na wengine hata wanasema kuwa itakuwa rahisi kwake kufanya kazi maana Republicans nao sasa wana sauti. Ila kabla ya hapo asingelithubutu kwenda kuwapigia magoti.

Hata CCM wangelikuwa chama cha Maslahi ya TAIFA, basi wangelikuwa wamefanya mengi sana. Ila kwa kuwa ni Wezi na Vibaka wakubwa na wana madaraka makubwa, ndiyo wametufikisha hapa tulipo.

CHADEMA kama wangelikuwa hawana jinsi, ingelibidi waungane na hao Wake WA CCM. Ila kwa hali ilivyo sasa, they can go to hell.

Inatakuwa tu urudi siku Bunge wameanza vikao. Chadema waliachwa peke yao. Hao CUF walipiga kura na CCM kuchagua Spika. Chadema walipoondoka, CUF waliwazomea na kukimbilia viti vyao. Walikuwa kama vile maatahira hivi na huwezi amini MIJITU MIZIMA na akili kichwani ingeliweza kufanya vitu vya kitoto namna hiyo.

Baadaye akaja Dr. Hamad siku ile ya mdahalo. Akamwaga matusi yake na kuonyesha jinsi alivyo Dr. hadi wa kejeli na vijembe utafikiri Kaka pacha wa Khadija Kopa. Akasema wao wataanzisha Kambi ya upinzani isiyo rasmi akitegemea kwa hilo ataendelea kutanua kwa visenti kutoka CCM. Walipomgomea na kumwambia sheria hairuhusu, ndiyo akaja na wimbo wake wa kuingizwa kwenye ngome ya upinzani.

Watu kama hawa wewe ndiyo UNAWATETEA kweli?

Kwako wewe hawa ndiyo wanajali maslahi ya RAIFA?

Kwako wewe ni CCM inajali maslahi ya taifa?

Kama na wewe unataka ndoa na Dr, Hamad Rashid, si uende tu mkafunge?

Au hata NCCR Mageuzi na bwana Kashilila sijui? Kama siyo Mbatia, sisi poa. Hata Mrema ni sawa tu.

Hawa watu kama kweli watabadilika kwa vitendo, basi tutakuwa hapa KUWAPIGIA kelele Chadema wawaingize upinzani ila siyo leo. Waonyeshe kwa dhati kuwa wako kwa ajili ya UTAIFA na si matumbo yao. Kama wewe ndiyo Dr. Hamad basi rusha vijembe vikali na ukimalize basi visome mwenyewe na ndiyo uwe UJUMBE WAKO kwako maana kwa vijembe, Dr wee mkali.
 
Back
Top Bottom