Inflammatory: CHADEMA hawako kwa maslahi ya taifa, they are just another tool

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
Naanza hoja yangu kuangalia msimamo wa chadema kwa CUF na kueleza ukweli kuhusu caolition governments

Maana yake:

A coalition government is where two or more political parties join together in parliament/assembly to run the government and agree on a policy programme


Faida zake:
  • Government will be more consensus-based: resulting policies will be broadly approved of

  • Better representation of the electorate's wishes

  • Better quality of policy: enhanced scrutiny and increased attention paid to each policy

  • Increased continuity: election does not lead to dramatic overhaul which can produce fragmented rule2
Hasara zake:


· The most obvious criticism of Proportional Representation is that it could form coalition governments. This is seen by some as a majorly bad thing as it supposedly does not allow ‘strong' government. Having more than one party in charge of decision making could cause a lot of arguments between the leaders of the country as the top ministers may have opposing political ideologies and views. It could also mean that it is very hard to get policy through the governmental process meaning government could be overall less effective in the running of the country.

· It could also cause an overly expanded Cabinet to cater for everyone's needs in the Government, which could lead to much needless expenditure.


· There could also be many arguments, which cause Cabinets to split and some important policy to be suspended to do the impossible task of keeping everybody happy


Mifano ya nchi zinazounda serikali ya umoja wa kitaifa


Europe:

Albania, Andorra, Austria, Belgium, Croatio, Belgium, Czech, Denmark, Finland, Estonia, Germany, Iceland, Ireland, Italy, Kosovo,Latvia, Lithuania, Luxembourg, Monaco, Montenegro, Netherlands, Norway, Poland, Romania, Serbia, Slovakia, Slovenia, Sweden, Switzerland ( has been ruled by a coalition of the four strongest parties in parliament from 1959 to 2008 called the ‘magic formula"), Ukraine and UK

Americas

Chile, Trinidad and Tobago, Suriname, Canada.

Africa:

Algeria, DRC Congo, Gabon, Guinea-Bissau, Kenya, Mali, Mauritania, Mauritius, Morocco,Senegal, Zanzibar Island, and Zimbabwe (was proposed not sure if still exists)

Asia

Armenia,Bangladesh,Cambodia,India,Indonesia,Iraq, Isarel, Japan, Lebanon, Malaysia, Maldives, Pakistan, Sri-Lanka, Thailand, Timor-Leste

Ocenia

Australia, New Zealand, Papua New Guinea, Vanuatu

Kwa nini huwa inaundwa?;

The usual reason given for this arrangement is that no party on its own can achieve a majority in the parliament. A coalition government might also be created in a time of national difficulty or crisis, for example during wartime, to give a government the high degree of perceived political legitimacy it desires whilst also playing a role in diminishing internal political strife. In such times, parties have formed all-party coalitions (national unity governments, grand coalitions)1

Kwa nini nchi nyingi zenye mfumo huu zimeendelea ?

Pamoja na hasara zake which is debatable advantages of coalition governments is far million times better than its disadvantages. How and why

1. Kutenganisha siasa na utendaji kazi wa serikali , kwa mfano Japan average ya prime minister kwa mwaka!, karibu kila mwaka wanakuwa na waziri mkuu mpya ambaye ni kama rais wa nchi! Still economic activities are growing up very fast!! Ufike muda tuone utendaji wa kisiasa unakuwa kwenye kushindana ku-implement policies na sio kuingilia professionals. Kwa sababu hii nchi nyingi zimefanikiwa kuendelea pamoja na kuwa coalition governments ina udhaifu wake lakini afadhali kuliko kutokuwa nayo

2. IKIFIKIA level, au wakati kuwa uamuzi wowote mzuri regardleess umetolewa na chama gani unafaa kuungwa mkono then that is a sign and good grounds of endorsing this system. Ifikie muda kila kiongozi anawaza mema kwa ajili ya nchi yake na KUPATA UONGOZI SI KWENDA KUJIONYESHA KUWA WEWE NI RAIS BALI KUTATUA MATATIZO FULANI YA NCHI YAKO KWA LENGO LA KULETA MABADILIKO AMBAYO YATALINDA HESHIMA YAKO.

3. Kuwa siasa sio uadui bali ni ushindanifu wa hoja, malengo, policy na ni hulka kamili ya binadamu kutofautiana na ni jambo la kukusudiwa na kila mmoja kujenga nchi moja pamoja na kuwa mnaweza kuwa na mitazamo tofauti, if we will reach this stage we are through!

Je kuna faida gani au kwa nini serikali ya umoja wa kitaifa ni muhimu hasa kwa nchi za dunia ya tatu ambazo vyama vingi ni vile vya kibeberu.

Kuna solutions mbili kubwa aidha kuwatoa kwa nguvu, maana ballot box cannot do anything! You heard me! But if we inclined to accept evolution not revolution then second option i.e coalition government is another good techniques ya kuwaondoa mabeberu!! Why and how

FAIDA YA serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania

1. Ni kichekesho na uhuni na uvunjivu wa haki za kibinadamu kuwa chama fulani kikipata kura asilimia 60 then wanaongoza nchi yote regardless of those 40% who did support them. Kwa mfano haingii akilini kuwa kikwete alipata asilimia 60 then wengine hawatakiwi kuunda serikali!!! Ambao tulisupport vyama vingine itakuwa rahisi na vizuri tukiwakilishwa serikalini walau kupata wizara kulingana na idadi ya kura zilizopatikana, let say CDM inapata wizara 3 out of 10! Is well and good

2. Serikali ya umoja wa kitaifa inavipa breakthrough vyama vingine kwa kuonyesha uwezo wao wa kiutendaji na kujenga hoja, this is like a continuing evaluation ya kuwa je CDM wamepewa wizara 3 wanafanya vizuri wakipewa urais si ndiyo watafanya vizuri zaidi?

3. Serikali ya umoja wa kitaifa inaviimarisha vyama, inajijenga na kupanua demokrasia ambayo tunaona haipo si kwenye chama tawala hata vya upinzania pia. Kwa mfano tulishuhudia Hilary na Obama wakipambana kwa hoja na sera zao ngali wako chama kimoja na mwisho wa siku wakamaliza vyema!!! Kama tunalipenda taifa we can still argue while we are in the same governments! Hii ni level ya juu lakini ni nzuri

4. KUBWA KULIKO YOTE ni kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itahimiza watu kujitokeza kupiga kura wakiamini kuwa wingi wa kura zao ndio unaipa nafasi kubwa chama chao kushika serikali, MOTISHA YA KUPIGA KURA NI KUBWA SANA KWENYE HZI SERIKALI NA WATU HAWAKATI TAMAA kuwa hata nipige vipi CCM watapita

5. Kufanya maamuzi ya kijinga ya kichama inakuwa ngumu kwenye cabinet

6. Msisahau wanasiasa ni wanasiasa they are born with same parents! Coalition governments inaweka msimamo kuwa hakuna chama kinachoa AMINIWA


Je what can we do now?

Mabadiliko ya katiba yanatakiwa ya accommodate issue nyingi ikiwemo hili

Je CUF na CCM Zanzibar hali ikoje?

Nimekaa Unguja na nimeona mabomu yakipigwa kwa wana CUF, na mimi kuathirika, nimeshuhudia chaos nyingi kwa macho yangu na leo hii natamani nirudi unguja nione hali ikoje!!! Coalition governments was the only solution for that situations! Wanaoibeza CUF idha hawajui maana ya caolition, hawajui kilichokuwa kinaendelea Zenj na wako blindly kuhusu nini maana ya coalition. Ni mwanzo mzuri sana ila inabidi iende mbali zaidi kuzungumzia

Vipi kuhusu tamko la CHADEMA na MSIMAMO WA CHADEMA


I don't support that tamko kwa sababu hizi

1. Chadema imefail kuwaambia au kujibu hoja ya coalition governments kwa greater heights, wanajibu cheaply kuwa CUF NI sehemu ya serikali!!! Kuwa sehemu ya serikali hakukupi mwanya kuwa usisimamie unachokiamini ndiyo maana USA hatuvitaji Republican kama ni chama cha upinzani!! Tunakitaja kwa majina yao ndivyo walivyo, IFIKIE MUDA TUSEME YULE NI MCHADEMA SIYO KWA SABABU NI MPINZANI KWA SABABU YA YALE UNAYOYASIMAMIA!!!


2. They have depicted high level of ignorance regarding coalition governments, KWANZA KAMA VILE HAZIPO, pili kama vile ni mbaya, same chadema waliungana na CCM huko Kigoma kwenye umeya na that was good example of coalition government –type


3. Kukataa coalition governments kuna onyesha vitu viwili, CHADEMA wana uroho wa madaraka na wanaiona TANZANIA KAMA NYAMA FULANI INATAKA KUDONDOKA NA WAO WANATAKA KUIRUKIA….., Tanzanias are very clever the only thing that CDM will be supported if they can agree that coalition governments is a solution because people don't trust them either! Believe me humu JF kuna tendency ya kutoangalia ukweli wa kulijenga taifa ila ni ubishi wa kishindani usio na maana kutaka cheap popularity ya ghost members usiowaona, can you stand alone?

4. Chadema imejiwekea wigo wa kujionyesha kuwa they can fight corruption alone and only alone!!! Hii ni hatari sana kwa wapenda mabadiliko , umoja wa kitaifa kupinga yanayorudisha taifa nyuma ni wajibu wakila mtu regardless of which part he belongs. Leo hii ni nadra CDM kuunga mkono CUF kile ambacho hata wao wanakipigania…huu ni utoto na high level of stupidity na ni sumu mbaya sana kwa wapenda maendeleo

5. Chadema ina ona kila wanachokisema kiko sahihi simply kwa kuwa na wabunge 47 kati ya zaidi ya 200! Baadhi ya watanzania na ujinga wao wanaamini CDM inaweza ikafanya maajabu bungeni!!!! Hizi ni ndoto za alinacha

6. CDM baada ya kuchanganyikiwa na matokeo bado haija recover from that shock!!! Maamuzi yake, misemo yake, mienendo yake si ya UTAIFA BALI NI UCHADEMA this is catalysed by the fact that they have money from our kodi (ruzuku) this made them to forget that they are making history today that will be a joke of tomorrow!!!! History is being written kuna vitu in near future itakuwa ni ngumu sana kwa watu kuvimeza kwa sababu ya makosa ya leo,

7. Kama ni kutofautiana na CUF na vyama vingine, is better they use a better language au kutoa sababu zingine na si kuwa CUF NI SEHEMU YA SERIKALI, HUU NI UOZO MKUBWA SANA AMBAO KWA KAMATI KUU YA CHADEMA HAIKUPASWA KUANDIKWA, ni uozo unaoelezea mawazo na nia yao kwenye hii nchi ni nini, kweli hakuna wenye busara wa kunena na kuandika kutokuungana na CUF yet mkatoa sababu zingine na sii kuwavunja nguvu na kutangaza bifu, kwa wengine CUF iko juu mbali zaidi ya CDM na walipofikia Zanzibar is desired most kwa yeyote mpenda mabadiliko-bara HUU NDIO UKWELI!!!!


JE CHADEMA HAWAJUI UKWELI??

Definitely chadema na wasomi wa type ya Slaa wanajua ukweli wanajua faida ya serikali ya umoja wa kitaifa na wanajua you can still abide to your ideology regardless of whether you are in coalition governments or not! CHADEMA WANAWADANGANYA WANACHAMA WAO na hasa JF-Kata, wanawajaza ujinga kiasi cha kuwa leo hii tuwaze tu kuwa na single party governments, YES we may have that lakini sio kwa kukashifu kuwa coalition govern. Ni mbaya!!! Na hawawezi kuungana na CUF Kwa sababu hiyo, huu upupu wa kihistoria utaandikwa kila leo kwa ku-joke chadema, tupo..jamani

Chadema chini yawafanyabiashara wanajua fedha za kambi ya upinzani wanazopata wao ni zao kwa sasa na hazitakiwi kugawanywa! What a selfish!!! Then they tell people cheap reasons why CUF is not among them??


WITO

Yes I know and I believe kuna matusi kibao yatatoka kwa ‘JF-Chadema kata', kuna wenye hoja watatoa, ‘JF-Chadema wakongwe ', kuna hoja na supportive documents zitatoka kwa wote wenye kupenda mabadiliko hawa ni JF-huru!

Jamani taifa hili litajengwa na wote, tukifikia muda wa kugawanyika CCM hatoki na tutaishia kusema tu na mvi zinakuja inakuwa mwaka wa 2015 na 2100 CCM will be in power.

After all CHADEMA they are not so opportunist and influential they can buy what is happening in Mistri, Jordam and Yemen… hawana muda huo wala hawawazi hayo, yet kuna watu mnalilia chadema , kutotaka kufikiri matokeo (results)/output ndio imetufikisha hapa tulipo leo. Hii ndilo linakujwa swali je hawa CDM hawakujua katiba na NEC ina matatizo kabla ya uchaguzi? Walifikiri wataichukua Tanzania watawale kama CCM? Hivi hula za kichadema na ki-ccm kwa namna gani zimetofautiana kwa matendo yao?? Msio taka kusikia shauri zenu ,

CHADEMA STOP THIS NONSENSE OF SAYING THAT CUF ISA PART OF GOVERNMENT GO TO SCHOOL!!!!! we dont trust you either!



References


Read more:
WIKIANSWER
Wikipedia
Tamko la chadema

sitajibu vijembe, matusi, na statement za hasira au zenye conclusion zisizo na tija, count your post wasted or applauded na wafuata mkumbo, nitajibu hoja zilizoenda shule..........


Haya chakula hicho!
 
nathani i thought uko smarter than Wikianswer! Serikali ya umoja wa kitaifa huwa siku zote siyo kitu kizuri maaana kufanya decisions huwa mpaka muanze consensus ambapo mara nyingi huchukua muda kufanya maamuzi! Hivi kwanini tusikubali kushindwa? mbona US mara nyingi chama hushindwa kwa percent ndogo? na hukubali kukaa pembeni? Au siasa za Africa mpaka uendeshe serikali ndo mtu unaridhika?
 
Coalition govt walio-form CUF na CCM ina maana gani? Ni sawa na coalition govt ya uingereza na New zealand? Tungefurahi kama ungeweka memorandum za understanding walizokubaliana ili tujue kwa undani! Maana tunaweza tukawa hatuongelie coalition govt ya aina moja!!
 
Thread ndefu lakini ungesema na ukweli kidogo basi. Umesahau kuwa CDM walimuunga mkono Prof Lipumba mwaka 2000? Utasemaje eti CDM hawawezi kuunga mkono CUF kwa lolote? Acha hizo. Upinzani sio lazima mtu awe waziri kivuli, jenga hoja tu za kutetea maslahi ya watanzania nasi tutakuhesabu. Kuandika mi-thread mirefu kwa minajili ya kupigia spidi pesa ya kambi ya upinzani bara wakati visiwani unavuta ya serikali ni bure kabisa!
 
Very smart Waberoya, huu ndo ukweli ambao watu humu hawapendi kuusikia. Mara kibao nimejaribu kuongea haya, lakini kwa vile watu wa humu wanaongozwa na upepo, wafata mkumbo, tafakari kwao ni mwiko. Mwenye akili na asikie
 
Muleta thread hii amejieleza vizuri lakini sijui imekuwaje. akafikia kwenye hitimisho lisilokuwa sahihi. suala la chadema kukataa kuungana na cuf kwenye kambi ya upinzani liko wazi kabisa wala haliitaji maelezo mengi; hata tukichukua nchi zote hizo alizozitoa kama mfano, haijawahi kutokea, chama kikashiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa, na wakati huo huo kikaunda kambi ya upinzani! Hata Zanzibar kwenyewe imebidi kuvunja kambi ya upinzani kwasababu vyama vyote viwili vyenye wawakilishi kwenye baraza vimeungana.
 
Mkuu kuna Baadhi ya Mambo umeayaeleza yakiwa na muelekeo mzuri, lakini labda kuna kitu hujakizingatia, siasa za sasa ni tofauti na za zamani kabisa, tulipokuwa tunasema socialist tulikuwa tunamaanisha hivyo na kulikuwa na theory za socialism

Siasa za sasa huwezi kuzungumzia Australia kwa sababu wako kwenye Coalition basi na Tanzania tunaweza kuwa kama hivyo!
Nchi nyingi Zimeingia kwenye Coalition kwa sababu ya Demokrasia Imewaforce (Hakuna majority), lakini ni kesi tofauti kabisa na ya Tanzania Zanzibar, Pale ni ukweli usiopingika kuwa CUF walishinda ule uchaguzi same as Uchaguzi wa kwanza wa Vyama Vingi Visiwani, Kwa hiyo Coaliation ya Zanzibar haikuwa influenced na Demokrasia bali ni Coalition iliyokuwa na sababu za Kibinafsi zaidi (Uzanzibar na Utanganyika),

Kama Demokrasia haikushape coalition ya CUF na CCM zanzibar, hao Cuf watawezaje kuipinga serikali ambayo nao wapo ndani kwa maslahi yao Binafsi,
Hivi Mkuu Waberoya, unataka kuniambia miaka yote CUF walichokuwa wanapigania ni hiki cha Seriakli ya Umoja? ina maana watu wote walikuwa wankufa Zanzibar hii ndio outcome yake?

So far Hakuna mtu anayejua CUF wanataka nini?, Hakuna hata mwanachama mmoja wa CUF anayeweza kukueleza wanataka nini Zaidi ya Uongozi wa juu wa CUF,

Kwa siasa za Tanzania zilivyo sasa zinahitaji nguvu kubwa sana Kuikomboa hii nchi, hakuna hata kitu kimoja kilichonyooka, na ni ukweli usiopingika kuwa Huwezi kuinyoosha hii nchi ukiwa ndani ya Serikali,

KAMA KUNA NCHI ZIMEFANIKIWA KWA KUWA NA COALITION BASI ILIKUWA NI COALITION ZA KIDEMOKRASIA, LAKINI SIO ZANZIBAR
 
:A S thumbs_down:Umejitahidi kusurf web kukusanya taarifa lakini it is all in vein kwa sababu motive yako siyo. Pole
 
Kwani kuungana ni lazima! Chadema wana haki ya kukubali au kukataa muungano na CUF coz wana sera tofauti! Kwa hiyo siyo lazima kuungana! ubaya uko wapi hapo? Kwani CUF wakiungana na Chadema ndiyo CUF itaipinga serikali kwa mambo ya msingi? Hata nje ya muungano CUF wanaweza kuipinga serikali kwa manufaa ya kitaifa siyo kutengemea muungano na chadema.

MASLAHI YA TAIFA HAYAKO KWENYE MUUNGANO WA CUF NA CHADEMA, YAPO KWENYE UELEWA WA WABUNGE WETU! K

ama hawaelewi maslahi ya taifa ni yapi hata huo muungano unaousemea ni sifuri. Kwa hiyo msitake kukichafua chama kingine sababu ya muungano, Tunachohitaji ni nguvu ya hoja bungeni wala siyo muungano kwanza, hii ni hatua ya pili utakuja automatic kwa kuvutwa na nguvu ya hoja.

Mbunge akitoa hoja nzuri bungeni wananchi tutamsikia na sisi ndiyo nguvu ya umma tutamrudisha 2015 mjengoni na wala siyo muungano utamrudisha mjengoni.
 
Najua pamoja na hali ilivyo si wengi inawagusa....mmelaaniwa mnaoneemeka kupitia jasho la wenzenu...mnaotumia uwezo wenu wa kufikiri vibaya kukanganya watu na kuwatoa kwenye mambo ya msingi....

CCM ilizaliwa, Ikakua na ni muda wake wakufa sasa kwa kua walikiuka miiko ya kutumikia watu...CCM si Chama cha siasa,ni NGO ya wakubwa! Si mtu mwenye akili za kawaida anayeweza kupoteza muda wake kutetea uozo km si tamaa ya kujaza matumbo inamsumbua....wananchi wasasa ni waelewa...elimu ya kuwadumaza iliyoletwa kupitia shule za kata zenye majina ya wanasiasa imewafumbua macho....

Mimi ni mpenda mabadiliko...vyovyote iwavyo...nachukia mfumo mzima wa utawala wa Chama Cha Mapinduzi chini ya kina JK.
 
Waberoya,

Wewe na kaka yako mkiishia kuishi kwenye KISIWA fulani na huko kuna Mwanamke mmoja, itabidi muanze kumchangia. Hiyo si kuwa ni wazo zuri ila kwa sababu HAKUNA NJIA NYINGINE.

USA akina Obama walikuwa wengi kwenye mabaraza yao na hawakutaka kusikiliza MJUSI yeyote. Mambo yamebadilika na wengine hata wanasema kuwa itakuwa rahisi kwake kufanya kazi maana Republicans nao sasa wana sauti. Ila kabla ya hapo asingelithubutu kwenda kuwapigia magoti.

Hata CCM wangelikuwa chama cha Maslahi ya TAIFA, basi wangelikuwa wamefanya mengi sana. Ila kwa kuwa ni Wezi na Vibaka wakubwa na wana madaraka makubwa, ndiyo wametufikisha hapa tulipo.

CHADEMA kama wangelikuwa hawana jinsi, ingelibidi waungane na hao Wake WA CCM. Ila kwa hali ilivyo sasa, they can go to hell.

Inatakuwa tu urudi siku Bunge wameanza vikao. Chadema waliachwa peke yao. Hao CUF walipiga kura na CCM kuchagua Spika. Chadema walipoondoka, CUF waliwazomea na kukimbilia viti vyao. Walikuwa kama vile maatahira hivi na huwezi amini MIJITU MIZIMA na akili kichwani ingeliweza kufanya vitu vya kitoto namna hiyo.

Baadaye akaja Dr. Hamad siku ile ya mdahalo. Akamwaga matusi yake na kuonyesha jinsi alivyo Dr. hadi wa kejeli na vijembe utafikiri Kaka pacha wa Khadija Kopa. Akasema wao wataanzisha Kambi ya upinzani isiyo rasmi akitegemea kwa hilo ataendelea kutanua kwa visenti kutoka CCM. Walipomgomea na kumwambia sheria hairuhusu, ndiyo akaja na wimbo wake wa kuingizwa kwenye ngome ya upinzani.

Watu kama hawa wewe ndiyo UNAWATETEA kweli?

Kwako wewe hawa ndiyo wanajali maslahi ya RAIFA?

Kwako wewe ni CCM inajali maslahi ya taifa?

Kama na wewe unataka ndoa na Dr, Hamad Rashid, si uende tu mkafunge?

Au hata NCCR Mageuzi na bwana Kashilila sijui? Kama siyo Mbatia, sisi poa. Hata Mrema ni sawa tu.

Hawa watu kama kweli watabadilika kwa vitendo, basi tutakuwa hapa KUWAPIGIA kelele Chadema wawaingize upinzani ila siyo leo. Waonyeshe kwa dhati kuwa wako kwa ajili ya UTAIFA na si matumbo yao. Kama wewe ndiyo Dr. Hamad basi rusha vijembe vikali na ukimalize basi visome mwenyewe na ndiyo uwe UJUMBE WAKO kwako maana kwa vijembe, Dr wee mkali.
 
Thread ndefu lakini ungesema na ukweli kidogo basi. Umesahau kuwa CDM walimuunga mkono Prof Lipumba mwaka 2000? Utasemaje eti CDM hawawezi kuunga mkono CUF kwa lolote? Acha hizo. Upinzani sio lazima mtu awe waziri kivuli, jenga hoja tu za kutetea maslahi ya watanzania nasi tutakuhesabu. Kuandika mi-thread mirefu kwa minajili ya kupigia spidi pesa ya kambi ya upinzani bara wakati visiwani unavuta ya serikali ni bure kabisa!
akili zenyewe kama ndo hizi, za kuwaza pesa tu na si maslahi ya nchi, no wonder we are where we are
 
Webs

Kwa mazingira yetu ulichoandika sehemu kubwa ni ndoto na binafsi sikubaliani sababu kubwa CCM na CUF wameungana (muafaka to me is like coalition hutakaa umsikie Maalimu Seif HaMad akiipinga serikali iliyo madarakani wakati yeye ni Makamu wa 4 wa raisi...balal, Shein yule mwingine na Sharif. That will be a grave mistake for CHADEMA main opposition to merge with CUF. Wanaweza ungana na wengine wakai-exclude CUF. Wasipofanya hivyo yote uliyopoteza muda kuandika itabakia ni Istilahi na Nadharia

I am sorry webs, ur long thread has no intellectual challenging umekuwa shabiki zaidi na ukasahau uhalisia wa siasa za kibongo bongo. CHADEMA kuunga na CUF ni kuuwa upinzani maana indirectly CHADEMA watakuwa wameungana na CCM kupitia CUF sasa hiyo ni akili ama tope?
 
mkuu... hapa unanichanganya...btn coalition government and government of national unity..... serikali ya mseto na serikali ya umoja wa kitaifa
 
..inawezekana ukawa na point, lakini lugha uliyotumia kuleta ujumbe huu siyo nzuri.

..ironically, umewashutumu kamati kuu ya CDM kwa kukosa ustaarabu[kuandika uozo] ktk matamshi yao, halafu na wewe mwenyewe ukatumia lugha isiyo nzuri ktk ujumbe wako.

..kwanini CUF wasiungane na CCM ktk kuunda serikali huku Tanganyika?

NB:

..katika wakati huu tuangalie QUALITY ya mchango wa wapinzani kuliko QUANTITY[their number] in the parliament.

..tuwaelekeze wabunge kuunga mkono hoja zenye maslahi ya nchi na kuachana na ushabiki wa vyama.

..CDM na CUF wanahitaji muda wa "CONFIDENCE BUILDING" ukizingatia ukweli kwamba CUF ni chama tawala Zenj ambayo ni sehemu ya muungano.

..mind you 99% ya wabunge wa CUF ktk bunge la Jamhuri wanatokea visiwani ambako chama chao kimeungana na CCM.
 
Kwa nini huwa inaundwa?;

The usual reason given for this arrangement is that no party on its own can achieve a majority in the parliament. A coalition government might also be created in a time of national difficulty or crisis, for example during wartime, to give a government the high degree of perceived political legitimacy it desires whilst also playing a role in diminishing internal political strife. In such times, parties have formed all-party coalitions (national unity governments, grand coalitions)1
Mkuu argument yako has got some flaws.... lakini kwa kuanzia hapo kwenye bold...

Since hata kama Chadema ikijoin na vyama vyote vya upinzani will it achieve majority? and if not doesnt this negate the main purpose?, Tarudi ukinijibu ili tuendelee

Even in UK Conservations would never in a million years make a coalition government ni kwamba they did not have majority and hence they had no choice
 
Mbona CUF walikataa huko visiwani vyama vingine vya upinzani visishirikishwe kwenye hiyo SUK na hakuna chama kingine kimelazimisha kuwepo? Tunakumbuka sote jinsi Jahazi Asilia na wengineo walivyoomba kujumuishwa kwenye serikali hiyo lakini CUF na CMM kwa mambo waliyoyajua wao walikataa. Iwaje leo CUF waje walazimishe kuwepo kwenye kambi ya Upinzani? Kwanza kwani ni lazima wapewe uwaziri kivuli au cheo chochote? Na kwa nini ni CUF tu wanaolilia kujumuishwa kwenye hiyo kambi ya Upinzani? Mbona vyama vingine kama TLP,NCCR,UDP hawapaazi sauti kubwa kama CUF?

Cuf wajilaumu wenyewe kwa yanayowakuta. Na kama vipi wasubiri 2015 wapate viti vingi bara waunde hiyo kambi peke yao!
 
Back
Top Bottom