Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
CCM wapo kazini. NCCR inatumika kuwadaka watu ambao ni tishio kwa ccm halafu inawamaliza na kuvuruga mamba mwishoni. Kafulila aangalie yasijemtokea ya Mrema, kina Marando bado wako kazini.
 
Kuna habari nyingine ambazo zinachochea migogoro zaidi. Kafulila ni mwanasiasa mchanga, nadhani hajui siasa ni nini. Kwa mwendo anaokwenda nao anaweza kujikuta anajimaliza mwenyewe bila kujua.

Tatizo ninaloliona, kijana anataka kuwa kwenye media akifikiri kwamba inampandisha chati, lakini ukweli ni kwamba media inamuongezea maadui badala ya kumjenga.

Ingekuwa ni busara angeenda huko Kigoma Kusini akasema na wananchi wa huko ambao ndiyo wapiga kura wake. Kuweka habari hizi kwenye magazeti ni kama vile anatumia jina la Zitto kuomba aungwe mkono na supporters wa CHADEMA jimboni. Pia in a way, ni kama anamchonganisha Zitto na CHADEMA.

Anaongelea kuchukua jimbo wakati serikali za mitaa viti 20 vimeenda CCM, na wao (CHADEMA + NCCR) walipata viti 23, je ana uhakika gani kwamba waliopigia kura CHADEMA na NCCR wote watampa kura yeye?

Hakutakiwa ku-reveal details za hiyo safari yake wala support anayoipata toka kwa Zitto. Pili, kutoa habari kama hiyo kunamfanya ajiweke kwenye mazingira ya utata kwa kuwa aligoma kurudisha kadi ya CHADEMA (kama taarifa hizo zilikuwa sahihi). Je, ana uhakika gani kwamba NCCR-Mageuzi watampa nafasi ya kugombea kwenye hilo jimbo? Asije akashangaa ikifika wakati wa uteuzi wakamtema kwa sababu nyepesi sana kwamba hawana imani naye.

Zitto, mshauri rafiki yako kwamba kwenye siasa na hasa kabla hujajenga jina unatakiwa kuwa makini sana. Jina linajengwa kuanzia jimboni kwako na siyo kuanzia kwenye magazeti. Wanaopiga kura ni wananchi wa jimboni, sio sisi wasoma magazeti. Hizo habari za kwenye magazeti zinatoa mwanya wa wapinzani wengine wanaonyemelea hilo jimbo kutafuta njia za kukumaliza kirahisi zaidi.

Atakuja kushangaa atakapokuja kujikuta jina lake limepigwa red na chama chake na wala asijue ilikuwaje. Kwani aliyegombea Ubunge 2005 kupitia NCCR amesema hataki tena kugombea?

Hizi siasa za kwenye magazeti tuwaachie wenyewe wanaojua, wengine naona tunazivamia tu bila kujua how to play the dirty game. Mimi sikumfahamu Zitto wala Mnyika kabla ya uchaguzi wa 2005, nimemfahamu Zitto baada ya kushinda na pia Mnyika nimemfahamu baada ya kuitikisa CCM jimboni Ubungo.

Kwa hiyo a good starting point ni sera zake huko jimboni kwake na siyo publicity kwenye magazeti. Atajimaliza kirahisi sana. Akomae na wapiga kura wa jimbo lake maana ndio watakaomchagua, sisi wengine ni wapiga domo tu.

Pia inahitaji understanding ya hali ya juu na ukomavu wa kisiasa CHADEMA kumwelewa Zitto kwamba hana nia ya kukihujumu chama chake. Pamoja na kwamba lengo ni kuimarisha upinzani, lakini ushirikiano wa dhati kati ya vyama vya upinzani haupo, wao wenyewe wanaonana kama maadui, lakini at personal level watu wanaweza kushirikiana lakini kwa njia za kimya kimya na siyo kuropoka magazetini kama jinsi dogo Kafulila anavyofanya.

Wewe ni wa ukweli sana kaka, hawa watoto wanakuja juzi juzi tu af wanaanza kurukaruka kama ndama, we mwache aendelee hvyo.

yeye anafikiri ujio wake NCCR-mageuzi umefurahiwa na nccr wenyewe?

ataundiwa zengwe humohumo anapofikiri ni salama.
 
CCM wapo kazini. NCCR inatumika kuwadaka watu ambao ni tishio kwa ccm halafu inawamaliza na kuvuruga mamba mwishoni. Kafulila aangalie yasijemtokea ya Mrema, kina Marando bado wako kazini.
CCM haina haja ya mazagazaga toka katika vyama pinzani, ila pale wanapokili kuwa kuwepo kwao katika upinzani kulitokana na ulimbukeni wao wa siasa hukaribishwa na kupigwa msasa ili waendane vema na kanuni za CCM
 
Atakuja kushangaa atakapokuja kujikuta jina lake limepigwa red na chama chake na wala asijue ilikuwaje. Kwani aliyegombea Ubunge 2005 kupitia NCCR amesema hataki tena kugombea?

Keil umetoa point nzuri sana, mgombea wa NCCR 2005 alipata kura zaidi ya 40% endapo chadema wangekuwa wamemuunga mkono ndo angekuwa Mbunge. Aliyeshinda (CCM) alipata chini ya 50%. Kwa takwimu hizi huyo jamaa wa NCCR anakubalika sana jimboni pengine kuliko hata Kufulila, kwani Kufulila amepima vipi kwamba anakubalika?

Inakuwa ngumu kujenga upinzani wenye nguvu kwasababu ya siasa kama hizi. Definitely kuna mgogoro wa ndani kati ya kamb ya Kufulila na mgombea wa NCCR mwaka 2005. And it is very unfair kwa Kufulila kuanza kampeni kabla ya muda wake.
 
Mnapoteza maana ya demokrasia.... kama wapinzani wanaungana mkono kuiondoa CCM madarakani, kinawauma nini? Wawe wa CUF, CHADEMA, TLP au NCCR, wakiungana na kusaidiana, kuna tatizo? Mimi namuunga mkono Zitto kwa kumsaidia Kafulila, kwa kuwa ametamka wazi malengo yake... wapinzani walipokuwa wanahasimiana, mlilalamika. Sasa wanaungana, mnalalamika tena? MNATAKA NINI ninyi binadam MSIOTOSHEKA? Mkiletewa mvua, mnalalamika, mnataka jua! Mkiletewa jua, mnalalamika, mnataka mvua! Waacheni waungane!

Hongera Zitto na Kafulila kwa kuweka MFANO BORA wa ushirikiano katika mapinduzi ya kisiasa nchini! Na wengine nao wafuate mfano wenu!

./Mwana wa Haki

Safi sana kaka
 
Kuna habari nyingine ambazo zinachochea migogoro zaidi. Kafulila ni mwanasiasa mchanga, nadhani hajui siasa ni nini. Kwa mwendo anaokwenda nao anaweza kujikuta anajimaliza mwenyewe bila kujua.

Tatizo ninaloliona, kijana anataka kuwa kwenye media akifikiri kwamba inampandisha chati, lakini ukweli ni kwamba media inamuongezea maadui badala ya kumjenga.

Ingekuwa ni busara angeenda huko Kigoma Kusini akasema na wananchi wa huko ambao ndiyo wapiga kura wake. Kuweka habari hizi kwenye magazeti ni kama vile anatumia jina la Zitto kuomba aungwe mkono na supporters wa CHADEMA jimboni. Pia in a way, ni kama anamchonganisha Zitto na CHADEMA.

Anaongelea kuchukua jimbo wakati serikali za mitaa viti 20 vimeenda CCM, na wao (CHADEMA + NCCR) walipata viti 23, je ana uhakika gani kwamba waliopigia kura CHADEMA na NCCR wote watampa kura yeye?

Hakutakiwa ku-reveal details za hiyo safari yake wala support anayoipata toka kwa Zitto. Pili, kutoa habari kama hiyo kunamfanya ajiweke kwenye mazingira ya utata kwa kuwa aligoma kurudisha kadi ya CHADEMA (kama taarifa hizo zilikuwa sahihi). Je, ana uhakika gani kwamba NCCR-Mageuzi watampa nafasi ya kugombea kwenye hilo jimbo? Asije akashangaa ikifika wakati wa uteuzi wakamtema kwa sababu nyepesi sana kwamba hawana imani naye.

Zitto, mshauri rafiki yako kwamba kwenye siasa na hasa kabla hujajenga jina unatakiwa kuwa makini sana. Jina linajengwa kuanzia jimboni kwako na siyo kuanzia kwenye magazeti. Wanaopiga kura ni wananchi wa jimboni, sio sisi wasoma magazeti. Hizo habari za kwenye magazeti zinatoa mwanya wa wapinzani wengine wanaonyemelea hilo jimbo kutafuta njia za kukumaliza kirahisi zaidi.

Atakuja kushangaa atakapokuja kujikuta jina lake limepigwa red na chama chake na wala asijue ilikuwaje. Kwani aliyegombea Ubunge 2005 kupitia NCCR amesema hataki tena kugombea?

Hizi siasa za kwenye magazeti tuwaachie wenyewe wanaojua, wengine naona tunazivamia tu bila kujua how to play the dirty game. Mimi sikumfahamu Zitto wala Mnyika kabla ya uchaguzi wa 2005, nimemfahamu Zitto baada ya kushinda na pia Mnyika nimemfahamu baada ya kuitikisa CCM jimboni Ubungo.

Kwa hiyo a good starting point ni sera zake huko jimboni kwake na siyo publicity kwenye magazeti. Atajimaliza kirahisi sana. Akomae na wapiga kura wa jimbo lake maana ndio watakaomchagua, sisi wengine ni wapiga domo tu.

Pia inahitaji understanding ya hali ya juu na ukomavu wa kisiasa CHADEMA kumwelewa Zitto kwamba hana nia ya kukihujumu chama chake. Pamoja na kwamba lengo ni kuimarisha upinzani, lakini ushirikiano wa dhati kati ya vyama vya upinzani haupo, wao wenyewe wanaonana kama maadui, lakini at personal level watu wanaweza kushirikiana lakini kwa njia za kimya kimya na siyo kuropoka magazetini kama jinsi dogo Kafulila anavyofanya.

Ni bahati mbaya mimi siyo Mtu wa Kigoma pia ni bahati mbaya mimi siyo Mwana Chadema, vinginevyo ningekwenda kugombea Ubunge kwenye hilo kupitia CHEDEMA halafu huyo dogo nimtoe kamasi. Si mnajua Kampeni za CHADEMA zilivyo organized Jimbo kwa Jimbo?

Maneno ya Kafulila yatamtokea puani wakati Chopper iliyombeba Free, Slaa, Zitto na Mgombea wa Ubunge itakapotua kusaka hizo kura. Dogo Kafulia atajuta sana.

A point of correction! Kafulia hakuwa mwanasiasa alipokuwa CHADEMA! Kama angekuwa ni mwanasiasa asingedai taarifa za pesa au masuala ya kusaini cheki kwenye magazeti. Angesubiri vikao halali vya chama akajenga hoja zake halafu akapata watu wa kumuunga mkono. Vinginevyo, bwana mdogo huyo ni trouble maker tu na ataipata flesh kwenye uchaguzi ujao atakapoona jimbo hilo likichukuliwa na CHADEMA mbele ya macho yake!
 
NO,

Zitto yuko njiani kuelekea CCM.

and

Hell NO

Zitto ndiye amekutana na moto hadi anatishia kujiondoa JF. Ha ha ha, who is smiling now - burger king or McDonald?

Sitashangaa sana. He is now a prisoner of Rostam, atajiondoa JF lakini tutaanza kumwona kupitia makala zake atakazoandika kwenye gazeti ambalo litaanzishwa hivi karibuni. Mengi yako njiani yanakuja, lakini naweza kusema kwa uhakika kuwa NCCR haiwezi kuwa salama kwa kufadhiliwa na Mafisadi.
 
Habari hii imeelemewa na cheche za kishabiki za mwandishi kuliko uhalisia wake. Kwa mtu yeyote mwenye uwezo wa kupambanua atagundua kuwa kwa asilimia 75 ya hii habari ni maoni(mtizamo) binafsi wa mwandishi. Mapendekezo yangu kwa hii habari ingepewa heading 'NIONAVYO MIMI'
 
Hapa hakuna kilichokosewa, ni kweli Zitto amempa gari Kafulila ili aweze kushinda ubunge kupitia NCCR mageuzi, hili ni jambo jema, lengo hapa ni kuunganisha nguvu ili kuiondoa CCM, na Zitto kafanya hivyo, kosa lake nini

BIG UP Zitto
 
It is all political agenda there and I want to be smart sio kwa kusema CHADEMa but he is needed to sure kwa kusema kuwa atasema nini au kufanya nini juu ya jimbo hilo
 
Ni kweli wakuu, mikakati ya NCCR-Mageuzi kuelekea 2010 ni mikali na ina kasi ya kutisha. Inashangaza pia nguvu hii inatoka wapi.. huenda si ndani bali nje. Mtakumbuka Mhe. Mbatia amekaa nje ya nchi kwa miaka miwili mfululizo (alikuwa anakuja bongo kwa kubip) alichokuwa akifanya huko, ati shule, lakini tokea arudi rasmi mwezi Agosti, mambo yanabadilika. Si ajabu akachukua fomu ya kuelekea ikulu mwakani (wakati wenyeviti wenzake wanakimbilia ubunge)!
Wakati huo huo anaandaa safu yake vizuri, vijana kadhaa wa karibu yake wako (kawapeleka) nje wanakula kitabu (possibly na Zitto ni mmoja wao)Tusubiri kuona.
 
Nimesoma vichwa vya habari vya habari vya gazeti la mwanachi la leo,nimekutana na kichwa kinachosema hatuhitaji magri tu ya Zitto bali wanamhitaji na Zitto pia,asema Mbatia.Na waandishi ni wale wale Fidelis Butahe na Ester. Sijui ndani kimeandikwa nini.
 
Ni kweli wakuu, mikakati ya NCCR-Mageuzi kuelekea 2010 ni mikali na ina kasi ya kutisha. Inashangaza pia nguvu hii inatoka wapi.. huenda si ndani bali nje. Mtakumbuka Mhe. Mbatia amekaa nje ya nchi kwa miaka miwili mfululizo (alikuwa anakuja bongo kwa kubip) alichokuwa akifanya huko, ati shule, lakini tokea arudi rasmi mwezi Agosti, mambo yanabadilika. Si ajabu akachukua fomu ya kuelekea ikulu mwakani (wakati wenyeviti wenzake wanakimbilia ubunge)!
Wakati huo huo anaandaa safu yake vizuri, vijana kadhaa wa karibu yake wako (kawapeleka) nje wanakula kitabu (possibly na Zitto ni mmoja wao)Tusubiri kuona.

Mbatia alipelekwa nje kusoma na kugharimiwa na Rostam, Kuhusu Zitto kugharimiwa na Rostam, sina uhakika lakini ni kawaida kwa RA kumwagilia miche yote maana hana hakika na utakao chipua!! Lipumba, Mrema, Mtikila,Mbatia nk wote wako kwenye payroll yake.
 
Si magari yake tu, tunamtaka pia Zitto

Fidelis Butahe na Elizabeth Ernest

MWENYEKITI wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia amesema chama hicho hakihitaji msaada wa magari pekee kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe bali pia kinamhitaji yeye kujiunga nacho.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mbatia alisema licha ya msaada wake wa magari, Zitto akitaka kujiunga na NCCR-Mageuzi wanampokea kwa mikono miwili.

“Wapinzani tuna lengo moja kubwa; kuing’oa CCM sasa kama Zitto katoa magari kwa Kafulila (David) ubaya uko wapi? Sio magari tu hata yeye akija NCCR- Mageuzi, hii ndio demokrasia tunayoizungumzia,” alisema Mbatia na kuongeza;

“Zitto ameona kuwa Kafulila ana uwezo wa kuwawakilisha wananchi wa Kigoma Kusini bungeni, umefika wakati wapinzani tukapeana nafasi na kusaidiana kama hivi hii ndio demokrasia, huyu Zitto anaweka maslahi ya Watanzania mbele kuliko ya chama na hivyo ndivyo inavyotakiwa”

Alisema kuwa chama chake hakina kinyongo na kiongozi huyo wa Chadema na kwamba kinamkaribisha muda wowote akitaka kujiunga nacho.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema kuwa Zitto kumsaidia Kafulila ni jambo la kawaida na kusisitiza kuwa mbona Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumpigia kampeni mgombea wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Musoma Vijijini mbona hilo haliongelewi.

''Mwalimu Nyerere aliwahi kumpigia kampeni mgombea wa NCCR-Mageuzi , Balozi Paul Ndobho na kuwaambia wapiga kura kuwa wasimchague mgombea wa CCM kwa kuwa alikuwa hafai hivyo wamchague wa upinzani hilo Chadema vipi hawalioni,'' alisema Mrema na kuongeza;

''Unajua wapinzani lengo letu ni moja kwa hiyo tunapokuwa na urafiki wakati tuko vyama tofauti na kusaidiana kwa vitu vidogo kama magari na fedha kwa ajili ya kampeni hilo ni jambo la kheri, ndio umoja wa wapinzani huo,''

Alisema siasa za Zitto ni zaidi ya chama alichokuwa na kusisitiza kuwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ni kiongozi ambaye chama chochote kinaweza kumshawishi ajiunge nacho kutokana na tabia yake ya kujali na kuipenda demokrasia.

“Sisi TLP tulikuwa tukimtaka sana Zitto ajiunge katika chama chetu, siasa zake ni zaidi ya Chadema, hata mimi nilipokuwa nikipata matatizo yeye peke yake kutoka Chadema ndio alikuwa akinitafuta na kunijulia hali na yeye mpaka kesho anapigania niwe Mbunge wa Vunjo,” alisema Mrema ambaye ametangaza kuwania ubunge Jimbo la Vunjo.

Jana kulikuwa na taarifa za uhakika za Zitto kutangaza kuwa atamuunga mkono swahiba wake, David Kafulila kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi na tayari ametoa magari matatu kwa ajili ya kumsaidia kujiimarisha jimboni huko.

Vyanzo vya habari vilidokeza kuwa kiongozi huyo wa Chadema ameamua kumuunga mkono Kafulila ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoka mikononi mwa CCM na kubaki upinzani.

Katika Uchaguzi Mkuu w 2005, NCCR-Mageuzi ilishika nafasi ya pili huku Chadema ikishika nafasi ya tatu kwenye matokeo ya ubunge. Katika uchaguzi wa mwaka 2000, jimbo hilo lilichukuliwa na NCCR-Mageuzi kabla ya 2003 kuchukuliwa na CCM katika uchaguzi mdogo.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni, Chadema ilijizolea viti 12, NCCR-Mageuzi 11 na CCM ilipata viti 20. Kulingana na takwimu hizo, upinzani uliongoza.

Mwaka 2005 kama Chadema ambacho kilishika nafasi ya tatu kingeiunga mkono NCCR-Mageuzi, Jimbo hilo sasa lingekuwa katika mikono ya upinzani kwa kuwa kura za kambi hiyo zilikuwa nyingi kuliko za CCM.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Zitto anaamini kwamba, Kafulila ndiye aliyejenga Chadema kama chama ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano na NCCR-Mageuzi katika maeneo ambayo chama hicho kina nguvu.

“Zitto amekwisha weka bayana kuwa katika Uchaguzi Mkuu ujao upande wa jimbo hilo anamuunga mkono Kafulila kwa kuwa anaamini atashinda na kuimarisha upinzani,” kilisema chanzo cha kuaminika.

Maelezo hayo ya Kabwe yamekuja huku Kafulila akijiandaa kwenda jimboni humo kuhutubia mikutano ya hadhara akitumia magari ya Zitto katika ziara yake mkoani Kigoma itakayoanza Desemba 8, mwaka huu akiwa na viongozi wa kitaifa wa NCCR-Mageuzi.

Kafulila aliliambia gazeti hili jana kuwa atatumia magari ya Zitto kwa kuwa ni rafiki yake wa karibu.

''Mimi na Zitto ni marafiki wa siku nyingi, tayari nimezungumza naye na amekubali kunisaidia kama rafiki yake wala sijakodisha," alisema Kafulila juzi na kuongeza:

"Amenipa magari yake kwa ajili ya usafiri kwa sababu nitaondoka na watu wangu huku Dar kwenda Kigoma''.
Alifafanua kuwa jambo kubwa analokwenda kufanya Kigoma ni kuwaeleza wanachama wa Chadema sababu zilizomwondoa kwenye chama hicho na hatima yake kisiasa.

source; http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16383
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom