Ilikuwa ni fedheha ambayo sitokuja kuisahau....

Mkubwa, Salaam!
Ni tukio la aina yake, lakini imetokea kama ajali tu
Kamwe usiache kujenga urafiki na watu wema
 
Nilifahamiana na huyu kijana mwaka 2004, tulipokutana pale kituo cha utamaduni cha Russia, akawa ni rafiki yangu wa karibu sana. Tulikuwa na mazoea ya kutembeleana mara kwa mara na hata pale kwao walitokea kunifahamu vizuri na hata wazazi wake pia walitokea kunipenda sana.
Huyu hakuwa mwingine bali ni rafiki yangu ambaye alikuwa na ulemavu wa ngozi (Albino) na tulikuwa tumezoeana sana, alikuwa bado anaishi na wazazi wake maeneo ya Ukonga, na mie nilikuwa naishi Tabata.

Ni tukio ambalo bado mpaka leo nalikumbuka, ilikuwa ni mwaka 2009, kipindi hicho lile wimbi la walemavu wa ngozi (alibino) kuuawa na kukatwa viungo ndio lilikuwa limeshika kasi kwelikweli hapa nchini. Siku moja alikuja nyumbani kwangu akanikosa, bali alimkuta mke wangu Mama Ngina. Hakukaa muda mrefu akaondoka lakini alimjulisha mke wangu kuwa simu yake imeibwa na hana mawasiliano labda mpaka hapo atakaponunua simu nyingine.

Niliporudi mke wangu alinipa zile salama, lakini kuna jambo alidai anataka tujadili juu ya rafiki yangu, mimi nikashtuka, na kumuuliza, ni jambo gani hilo? Akaniambia kuwa kutokana na hili wimbi la watu wenye lemavu wa ngozi kuuawa na kukatwa viungo vya mwili, inawezekana huyo rafiki yangu akapatwa na tatizo halafu ikatuletea shida, tukawa suspect……………….
Nilishtushwa sana na kauli ile ya mke wangu, nilikaa kimya kwa muda kidogo, nikitafakari kisha nikamuuliza, ‘Sasa unataka nimkataze asije hapa nyumbani'

‘Hapana, sio lengo langu kuvunja urafiki wenu, lakini jaribu kupunguza ukaribu wenu na hasa kutembeleana, ikiwezekana mwambie unasoma na utakuwa unaishi Hostel kwa muda ili asiwe anakuja hapa nyumbani, mwenzio mimi naogopa'
alijibu mke wangu kwa sauti ya upole. Sikukubaliana naye na tulibishana sana na hatukufikia muafaka wa jambo hilo. Haikupita wiki yule rafiki yangu alikuja na akashinda kwangu kutwa, ilikuwa ni siku ya jumamosi na tulizungumza mambo mengi sana kuhusiana na mradi ambao tulitaka kuuanzisha, lakini pia alinijulisha kuwa huenda wiki inayofuata angesafiri kwenda Morogoro mara moja kuna kitu anafuatilia kule kwa rafiki yake ambaye alisoma naye.

Siku iliyofuata asubuhi alikuja mdogo wake na yule rafiki yangu na kuniuliza kama kaka yake alikuwa pale kwangu, kwani tangu alipoondoka jana asubuhi kuja kwangu kama alivyoaga hakurejea hadi asubuhi, na simu yake haipatikani kabisa….. mke wangu alinitupia jicho kali kama la kunisuta, nilibabaika kidogo. Nilimjulisha kwamba ni kweli alikuja kwangu na aliondoka mchana kurudi nyumbani kwao. Basi yule kijana akaondoka, lakini huku nyuma mke wangu alinibadilikia na kuanza kunishambulia kuwa mimi sio msikivu na sana nitapata matatizo asipopatikana huyo kijana wa watu, nilibaki kimya na sikujibu aliendelea kunishambulia huku akilia kwa uchungu kuwa nimejitafutia matatizo. Ilibidi niwe mkali kidogo na kumuonya juu ya fikra zake potofu. Ghafla nikawa nimekumbuka kuwa yule rafiki yangu aliniaga kuwa huenda angesafiri kwenda Morogoro kwa rafikiye aliyesoma naye, hivyo nikamtoa mke wangu wasiwasi kuwa huenda kaenda Morogoro na simu yake imeisha chaji na ndio maana haipatikani.

Ilipofika jioni, nilipata wageni tena, na hawakuwa wengine, bali wazazi wa yule rafiki yangu, wakiwa wameambatana na watu wengine wawili, ambao sikuwafahamu, waliingia ndani na walinijulisha kuwa mtoto wao hajulikani alipo na wanahisi kuwa huenda nahusika na kutoweka kwake. Mimi niliwajulisha kwamba, ni kweli jana alifika kwangu na alikaa mpaka mchana akaondoka, na nikawajulisha kwamba mtoto wao alinidokeza kuwa angesafiri kwenda Morogoro kwa rafikie waliyesoma naye kwani kuna jambo analifuatilia huko. Wazazi wa yule kijana walikanusha kujua lolote juu ya safari hiyo. Lakini wakati bado wakiendelea kuniuliza, mama wa yule kijana alidakia kuwa nipelekwe kituoni nikatoe maelezo, kwani inawezekana nafahamu kilichompata mtoto wao. Nilipinga kupelekwa kituoni, likazuka zogo mle ndani mpaka majirani zangu wakaja kusikiliza kulikoni!

Miongoni mwa majirani zangu alikuwepo dada mmoja wa Kichaga, ambaye hakuwa na maelewano mazuri na mke wangu, na aliposikia zile tuhuma, alianza kusema kishabiki kuwa tupelekwe kituoni kwani lazima tunajua aliko mtoto wao. Alianza kulizungumza jambo lile kwa dhihaka akisema, 'watu wanajifanya wana hela na kujitia ufahari kumbe wanauza viungo vya albino!' Alikuwa anaongea kwa sauti na kwa ushabiki akitumia lafudhi ya Kizaramo iliyochanganyika na ya Kichaga, alinikera sana.

Baada ya mvutano mkali mke wangu alinishauri nikubali kwenda kituoni kutoa maelezo, kwa kuwa sikuhusika na kupotea kwa kijana yule. Nilitoka nje uso wangu ukiwa umesawajika kwa fedheha ile. Siku hiyo ndio niliwafahamu majirani zangu kwa rangi zao halisi.
Nilifuatana na wazazi wa yule kijana pamoja na baadhi ya majirani zangu waliokuwa wameguswa na jambo lile, kwani pia wapo waliokuwa wakinipa moyo kuwa nisiwe na wasiwasi kwa kuwa sikuhusika, basi kila kitu kitafahamika kule kituoni. Mke wangu mama Ngina alikuwa amefuatana na mimi akiwa analia na alionekana wazi akiwa na wasiwasi sana.

Wakati tuko njiani kuelekea kituo cha Polisi simu ya yule baba wa kijana iliita, alipoitoa mfukoni , alisita kidogo kuipokea, mkewe akamuuliza kuwa ni nani anapiga simu, yule mzee hakuipokea simu ile alibaki kuikodolea macho akiwa ameishika mkononi. Mmoja wa wale watu aliofuatana nao ambaye nilikuja kuambiwa kuwa ni shemejiye, aliichukua ile simu na kuipokea, ‘haloo, nani anaongea…………..aah mjomba, uko wapi?'
Wakati anaongea na simu ile wote pale tukajua kuwa alikuwa ni yule kijana aliyekuwa akitafutwa, na watu wote tulikuwa kimya………..yule mjomba hakumwambia kuwa anatafutwa, ila alimdanganya kuwa mama yake yu mgonjwa na anahitajika nyumbani haraka. Alikata simu na kusema, ‘Ni Msakuzi, ni kweli yuko Morogoro na simu yake iliisha chaji akawa amekosa chaji tangu jana na leo kutwa.' Wote tulishikwa na butwaa, na wazazi wa yule kijana waliniomba radhi kwa usumbufu wote uliotokea.

Sikuwajibu kitu, nilimshika mke wangu Mama Ngina na kurudi nyumbani. Ni fedheha ambayo sitokuja kuisahau………………………………
Naomba nitofautiane na walio wengi ...
kwanza kabisa nakupa pole kwa kadhia iliyokukuta mkuu..
Pili. mimi nadhani haikuwa sahihi kwa mazingira yale 2009 kujitwisha msalaba mkubwa namna hiyo kwa kigezo cha urafiki..
My take: Kwa kuwa ulijua huyu bwana ni Rafiki yako na anasafiri kwenda Moro..ulitakiwa at least uwe na wazo la kumuonea 'huruma' kwa kuwajulisha baadhi ya ndugu zake kuwa Jamaa yao anasafiri hasa ukizingatia kuwa kile kipindi 'wauaji walikuwa nje nje'..Kitendo cha wewe kuchukulia simple kingeweza kutafsrika kirahisi tu kuwa unayo ajenda ya siri na Rafiki yako..na kwa mantiki hiyo wale nduguze na rafiki yako walikuwa 'right' kukunyooshea kidole kwa vile hukuonyesha tangu mwanzo kuwa 'unamlinda'..
Somo nililolipata hapa ni kuwa mkeo alionyesha kuwa anajali zaidi yako..na hata alipokuwa anakuonya kuhusu urafiki wenu..binafsi sidhani kama alikuwa hampendi rafiki yako BUT alikuwa 'focused'..na alikuwa anajaribu kuku'alert' uwe makini..
wakati mwingine 'try to read between lines'....
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, lakini kumbuka kwamba sisi kama wanaadamu tunatofautiana namna ya kufikiri, hilo ni moja, la pili katika mazingira hayo hayo ya urafiki wetu, hivi ningewezaje kujitenga naye ghafla namna ile. kumbuka kwamba mke wangu alinipa tahadhari kama wiki moja iliyopita kabla ya tukio, ingawa nilitofautiana naye sana juu ya jambo hilo, lakini bado nilikuwa na nafasi ya kutafakari, si kila ushauri mtu anaopewa na mwenzi wake ni wa kuchukuliwa kwa kukurupuka. kunahitajika busara ya hali ya juu katika kufanya maamuzi. mimi nilijipa nafasi ya kutafakari ushauri huo.
lakini pia hebu tuliangalie tukio hili kwa jicho la tatu (naamini unanielewa). Mimi ni muumini wa kanuni za maumbile (Univeversal Law). Hivi nikikwambia kuwa mke wangu ndiye aliyelitengeneza hilo tukio utabisha? kumbuka kwamba kauli huumba na kila mtu aliwazalo humtokea, hata hizi dini zetu za mapokeo zinakiri hilo............. Wewe una maoni gani kuhusu hilo?
 
mtambuzi,u ar going too far with this. siamini wala sifikirii mke wako angeweza kusuka huo mpango unless she is a drama queen! kuhusu swali lako la kuwa ungefanyaje, ungeweza kujadiliana na mkeo jinsi gani ya kupunguza mawasiliano na huyo kijana bila kuumiza hisia zake. mngeweza kukubaliana kuwa badala ya yeye kuzurura na kuja kwako kila wakati ungeweza kuwa unamtembelea kwa wazazi wake. ni kitu cha haraka tu nimewaza,bt im sure ungeendeleza maongezi na mama ngina mngepata suluhu ya maana.
 
Ni mkasa amboa sitokuja kuusahau, lakini kubwa zaidi, niliwasaidia watu wengi kujifunza kupitia mkasa wangu huu.............

Pole mkuu. Pia mkasa huo ulisaidia kuwafahamu majirani zako vizuri. Kwa kweli ni funzo kwetu sote jinsi tunavyo-trade ktk shughuli za kila siku za maisha.
 
mtambuzi,u ar going too far with this. siamini wala sifikirii mke wako angeweza kusuka huo mpango unless she is a drama queen! kuhusu swali lako la kuwa ungefanyaje, ungeweza kujadiliana na mkeo jinsi gani ya kupunguza mawasiliano na huyo kijana bila kuumiza hisia zake. mngeweza kukubaliana kuwa badala ya yeye kuzurura na kuja kwako kila wakati ungeweza kuwa unamtembelea kwa wazazi wake. ni kitu cha haraka tu nimewaza,bt im sure ungeendeleza maongezi na mama ngina mngepata suluhu ya maana.

King'asti nawe! hujanielewa bana.................nilikuwa nazungumzia kitu kinaitwa universal law, au kanuni za maumbile, nadhani niliyemjibu atanielewa vizuri zaidi. Iko hivi, kila kitu tunachokiwaza, huja kututokea, kwa maana, kama unawaza sana kuwa tajiri, ni dhahiri kwamba huko mbeleni utakuwa tajiri, na kama unawaza kuhusu maanguko, umasikini na talaka au hata magonjwa hayo ndiyo yatakuwa ni mavuno yako,,hiyo iko kwa kila mtu.......... Hivyo basi sio kwamba mke wangu alinifanyia njama......hapana...... Ila kama binadamu alijiwa na mawazo ya aina hiyo na akajenga hofu kisha akanitahadharisha. na kwa kuwa hatukuelewana juu ya jambo hilo, inawezekana aliendelea kujenga hofu, na hiyo ni njia rahisi sana katika kulivuta tukio....... namshukuru Mungu kwamba tukio hilo lilikuja kwa namna ya kujifunza na sio sisi tu kama wanandoa bali pia majirani na wazazi wa kijana nao pia walijifunza..............
 
Mkuu pole sana, kisa kinasikitisha. Shukran kwa mtitiko mzuri sana wa keleweka wa kisa.
Kuna mambo kadhaa:
1. Sikubaliani na wazo a kumkimbia mwaka 2009, nani angesimama na huyo mwenzetu kama si Mtambuzi, wewe na mimi.
Na je angekuwa dogo wako ungemkimbia

2. Kumsikiliza mkeo haina maana kukubalina na mawazo yake. Msimamo wa Mtambuzi uliegemea kwa kile alichodhani ni sahihi kama mkewe alivyosimamia upande wake. Bado Mtambuzi angejifanya anaishi Hosteli na balaa kubwa lingeweza kutokea kwa kukutana tu na kusaliamiana kusikopangwa. By the way watu walishajua kuwa ni rafiki yake.

3. Imekuonyesha majirani zako na mtazamo wao kwao. Adui si aliyetaka kukupeleka polisi bali aliyesherehekea matatizo. Sasa unawajua.

4. Endelea na urafiki kwani rafiki wa dhiki ndiye rafiki wa kweli, ukianza kumkimbia utamkimbia nduguyo siku moja. Na sasa unaaminika zaidi ya awali
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, lakini kumbuka kwamba sisi kama wanaadamu tunatofautiana namna ya kufikiri, hilo ni moja, la pili katika mazingira hayo hayo ya urafiki wetu, hivi ningewezaje kujitenga naye ghafla namna ile. kumbuka kwamba mke wangu alinipa tahadhari kama wiki moja iliyopita kabla ya tukio, ingawa nilitofautiana naye sana juu ya jambo hilo, lakini bado nilikuwa na nafasi ya kutafakari, si kila ushauri mtu anaopewa na mwenzi wake ni wa kuchukuliwa kwa kukurupuka. kunahitajika busara ya hali ya juu katika kufanya maamuzi. mimi nilijipa nafasi ya kutafakari ushauri huo.
lakini pia hebu tuliangalie tukio hili kwa jicho la tatu (naamini unanielewa). Mimi ni muumini wa kanuni za maumbile (Univeversal Law). Hivi nikikwambia kuwa mke wangu ndiye aliyelitengeneza hilo tukio utabisha? kumbuka kwamba kauli huumba na kila mtu aliwazalo humtokea, hata hizi dini zetu za mapokeo zinakiri hilo............. Wewe una maoni gani kuhusu hilo?

Mtambuzi, sijasema ungejitenga naye mara tu baada ya mkeo kukuambia kuwa 'ni hatari' la hasha!!..Nilichojaribu kusema ni kuwa Mkeo aliliona Tukio kama unavyosema wewe 'means she was so focused on what would probably happened' na wewe hukuliona tukio lililo mbele yako..Na kama mkeo aliamini pia tukio linalokugusa wewe na kwake lina athari kubwa pia..
Kwa mtazamo huo badala ya kukaa wiki nzima unafikiri nini cha kufanya..mnge'merge' hiyo hatari aliyokuwa anaihofia na 'mapenzi/urafiki' wako kwa huyo kijana ambapo mngepata namna nzuri ya kuishi na huyu rafiki bila kuathiriana..Na ikumbukwe pia 'that' guy was a mere friend of you' na sio ndugu au jamaa yako of which urafiki wenu ungeweza kuwa adjustable bila matatizo.
Kuhusu dhana ya 'universal law' ni kweli kwamba 'thoughts' za mkeo ultimately zilipelekea 'mtiririko' (flow) wa tukio kuonekana kama alivyokuwa anasema..Na ikumbukwe tu kuwa MTIRIRIKO wa tukio hauna nguvu sana kama 'FACTS' zitakuja kuonekana hazisupport huo mtiririko...kwa maana hiyo bado nasema ulitakiwa 'uchanganye worry ya mkeo na 'mapenzi mema' uliyokuwa nayo kwa rafiki yako ili kuzuia ule MTIRIRIKO ..ambao kwa kiasi fulani ndio umekuletea fedheha..japo facts zilikuja kuwa 'favourable' on your side
 
Nimeishiwa maneno kaka................... nimekusikia na ninakubaliana na wewe. ninakushukuru sana kwa darasa lako makini......... ahsante sana mkuu
 
mtambuzi,u ar going too far with this. siamini wala sifikirii mke wako angeweza kusuka huo mpango unless she is a drama queen! kuhusu swali lako la kuwa ungefanyaje, ungeweza kujadiliana na mkeo jinsi gani ya kupunguza mawasiliano na huyo kijana bila kuumiza hisia zake. mngeweza kukubaliana kuwa badala ya yeye kuzurura na kuja kwako kila wakati ungeweza kuwa unamtembelea kwa wazazi wake. ni kitu cha haraka tu nimewaza,bt im sure ungeendeleza maongezi na mama ngina mngepata suluhu ya maana.
king'ast, ndg. Kwanza napenda nikutaarifu kua naungana na mtoa mda kwa asilimia 100, hana maana ya kwamba wife wake ametengeneza ishu, ila ni kuwa kutokana na matamshi aliweza kutayarisha hilo tukio. Nadhani umenielewa na jaribu kuelewa mwandishi anaelezea nini. Hujaelewa ndo maana umejibu hayo ulo jibu tafakari kwa hekima kwanza na jaribu kuitafuta hekima utaweza kushinda/kukabiliana na mengi.
 
Pole sana ndg.
Imekupa fursa ya kuwatambu majirani zako.
 
Ni kumbukumbu mzuri sana, tafuta jinsi ya kuhiifadhi, yaana waweza andika kitabu ikawa ukumbusho mzuri na kuonyesha ujasili wa kutokuwa mbaguzi
 
Mkuu pole sana, kisa kinasikitisha. Shukran kwa mtitiko mzuri sana wa keleweka wa kisa.
Kuna mambo kadhaa:
1. Sikubaliani na wazo a kumkimbia mwaka 2009, nani angesimama na huyo mwenzetu kama si Mtambuzi, wewe na mimi.
Na je angekuwa dogo wako ungemkimbia

2. Kumsikiliza mkeo haina maana kukubalina na mawazo yake. Msimamo wa Mtambuzi uliegemea kwa kile alichodhani ni sahihi kama mkewe alivyosimamia upande wake. Bado Mtambuzi angejifanya anaishi Hosteli na balaa kubwa lingeweza kutokea kwa kukutana tu na kusaliamiana kusikopangwa. By the way watu walishajua kuwa ni rafiki yake.

3. Imekuonyesha majirani zako na mtazamo wao kwao. Adui si aliyetaka kukupeleka polisi bali aliyesherehekea matatizo. Sasa unawajua.

4. Endelea na urafiki kwani rafiki wa dhiki ndiye rafiki wa kweli, ukianza kumkimbia utamkimbia nduguyo siku moja. Na sasa unaaminika zaidi ya awali

Umegonga point 4 muhimu mkuu! Asante sana!
 
Back
Top Bottom