Sijawahi kuchanganyikiwa maishani mwangu namna hii

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Wanaume wawili walikutana kwenye kituo cha basi na wakawa na mazungumzo. Mmoja wao aliendelea kulalamika kuhusu matatizo ya familia yake. Hatimaye yule mtu mwingine wa pili akasema, “unafikiri unayo matatizo ya kifamilia? Sikiliza hali yangu."

"Miaka michache iliyopita nilikutana na mjane mwenye umri mdofo na akiwa na binti yake ambaye ni wa makamo ya utu uzima na tukafunga ndoa. Baadaye baba yangu akamuoa yule binti wa yule mama yani binti yangu wa kambo.

Hilo lilimfanya binti yangu wa kambo kuwa mama yangu wa kambo
na baba yangu mzazi akawa mtoto wangu wa kambo kwa sababu kamuoa binti yangu wa kambo.

Pia mke wangu akawa mama mkwe wa baba mkwe wake (yani baba yangu ni baba mkwe wa mke wangu kwa sababu yangu, na pia mke wangu ni mama mkwe wa baba yangu kwa sababu ya binti yake aliyemuozesha).

Kisha binti wa mke wangu, akawa mama yangu wa kambo, na pia alijaaliwa kujifungua mtoto wa kiume. Hivyo Kijana huyu alikuwa kaka yangu wa kambo kwa sababu alikuwa ni mtoto wa baba yangu, lakini pia alikuwa mtoto wa binti wa mke wangu, ambayo inamfanya kuwa mjukuu wa mke wangu. Hiyo ilinifanya mimi pia kuwa babu wa kaka yangu wa kambo.

Hii haikuwa chochote hadi mimi na mke wangu nasi tukapata mtoto wa kiume. Sasa yule binti wa mke wangu kawa dada wa mwanangu kwa sababu mke wa wangu na mama mzazi wa wote wawili, ambaye pia kimsingi binti huyo ni mama yangu wa kambo kwa sababu kaolewa na baba yangu vilevile sasa binti huyo kawa bibi wa mwanangu kwa sababu kwa upande mwingine mimi ni mtoto wake wa kambo na mwanangu ni mjukuu wake.

Hii inamfanya baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu kwa sababu baba yangu kamuoa dada yake ambaye mke wangu ndio mama yao, ambaye pia dada wa mwanagu ni mke wa baba yangu. Hivyo mimi ni shemeji wa mama yangu wa kambo, mke wangu ni shangazi wa mtoto wake mwenyewe, na mwanangu ni mpwa wa baba yangu na mimi ni babu yangu mwenyewe."

Na unafikiri una matatizo ya familia?
 
Mbombo ngafu
 
Wabongo utafikiri matatizo hua ni mashindano,utasikia "Wewe hujateseka niulize mimi'

''Hujapitia shida wewe,ukisikia niliyo yapitia Mimi utabaki mdomo wazi'' Kila mmoja huona matatizo yake ni makubwa zaidi kuliko ya mwingine.

:D
 
ondoka huko dar naona umeshaanza kuchanganyikiwa
20240102_180605.jpg
 
Ati baba yako ni shemeji wa mtoto wako?🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom