Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,922
- 33,366
Inasikitisha sana kuwa na Askari wanaolipwa mishahara, wamenunuliwa vitendeakazi, wamepewa magari mazuri na serikali lakini wapowapo tu hawafanyi kazi yao. Kuna matukio mawili yanafanana ambayo kikosi hicho kimeshindwa kabisa kuyatendea haki.
- Mwaka 2022 katika eneo la Kihonda VETA mwanafunzi mmoja wa chuo hicho alitumbukia kwenye maji akazama na kufia humo, Fire walipelekewa taarifa wakafika kwenye eneo la tukio, lakini wakajitetea kuwa hawaruhusiwi kuingia kumtafuta maiti kwenye maji baada ya saa 12 jioni, hivyo waliondoka na kurejea siku ya pili asubuhi, walipofika kama kawaida yao wakaanza kutupiana mpira na hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia kufanya uokoaji, vijana wa mtaani hapo wakajitosa na kufanikiwa kuibuka na mwili wa mwanafunzi huyo aliyekwenda kuzikwa kwao Moshi.
- Jana tarehe 1.3.2024, kijana mwingine aliyekuwa anafua kandokando ya mto Ngerengere aliteleza na kuzama majini karibu na daraja la mwendokasi Tungi Morogoro, kama kawaida Fire wakapigiwa simu wakafika majira ya saa 9 alasiri, lakini hawakuweza kufanya chochote zaidi ya kuvaa na kuvua life jackets zao na kuzunguka huku na kule wakiongea na simu, walipoulizwa mbona hawafanyi chochote wakasema wanataka kufunga mashine wavute maji yapungue, ndipo kijana yuleyule aliyeopoa mwili wa mwanachuo wa Veta mwaka 2022 akaamua kuzama mara kadhaa na kufanikiwa kutoka na mwili wa mhanga huyo.