Timu yenu ya mafisadi ndio unataka iyafaidi madini?Hakuna kitu hapo madini wanafaidi wakina Bush na Queen Elizabeth sisi tunasubiri misaada toka KUWAIT Kwa Sadam Hussein haaaaaaaaaaaaa haaaaaaa! shame on us!
Elimu gani walioisimamia kwa miaka 54 ikaleta maendeleo?
Huduma za afya ambazo hakuna hata madawa hospitali?
Watanzania tuamke, tuwe critical thinkers.
tuko busy na viwanda na wapinzani. yatatimia vuta subira.CCM ni matapeli sana.
Sawa.Ila msije na mbwembwe za kutaka kubinuka pushapu za sungusungu.W
tuko busy na viwanda na wapinzani. yatatimia vuta subira.
Kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2015-2020).
1. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi itatenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji, badala ya kupewa milioni 50 wamachinga ndio wanaichangia serikali elfu 2,000 kwa kila kitambulisho.
2. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi itahakikisha wananchi wanaopakana na miundombinu ya gesi na ambako bomba la gesi linapita wananufaika na gesi. Wananchi walichoambulia ni kuona alama za njano bomba linapopitia na virungu.
3. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kuhamia Dodoma kabla ya 2020 tukaambiwa kufikia Desemba2018 Rais atakuwa Dodoma, hadi leo namuona bado yupo Dar.
4. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kuongeza kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati kutoka 1,300MW hadi 5,000MW ifikapo 2020. Sina uhakika hata megawati 2,000 zimefika.
5. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kipaumbele kitakuwa katika kukuza na kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Leo hata aliyeanzisha wimbo wa Tanzania ya viwanda anaona aibu kutamka mbele za watu.
6. Ilani ya CCM: Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, serikali ya CCM itaendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa na ufisadi. Leo CCM imerudia kuwakaribisha Mafisadi papa waliowakataa 2015 akiwepo fisadi mkuu Lowassa.
7. Ilani ya CCM: Serikali ya CCM itahakikisha thamani ya Shilingi yetu inatengamaa. Leo 1USD = 2400TZS.
8. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inaongeza mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi. Leo mazao ya Korosho na Mbaazi yamekosa soko.
9. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inasimamia Deni la Taifa liendelee kuwa himilivu. Leo Deni limekua toka 35T walivyolikuta hadi 50T.
10: Ilani ya CCM: Serikali itasimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria na miongozo ya ununuzi wa umma, ukaguzi na kusimamia mali za Serikali. Tumeshuhudia Issue ya CAG na 1.5t, ndege zimenunuliwa bila kufuata kanuni ya manunuzi, uwanja wa ndege wa chato umejengwa bila bunge kuidhinisha bajeti yake.
11. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inajenga zahanati kila kijiji, Kata kuwa na Kituo cha Afya na kujenga hospitali Lila Wilaya. Hili sina uhakika ngoja nimtag Waziri Ummy Mwalimu.
Kama huu sio ulaghai kwa wananchi ni nini.
Ngoja niishie hapa, Mambo ni Mengi, muda Mchache.
Hizi ni facts anayepinga aje na data.