Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Onyesha jambo moja tu awamu hii ililotekeleza kikamilifu.

REA II,
TASAF III,
Ujenzi wa flyover Dar,
Serikali kuhamia Dodoma,
Mikopo ya wanafunzi Elimu ya Juuu,
Elimu Bila Malipo (Shule za Msingi na Sekondari),

Ulinzi na Usalama wa Nchi,
Uwajibikaji kwa Taasisi za Umma,
Makusanyo ya Ndani/Mapato ya Serikali,
Ujenzi wa Barabara za Lami (Mikoa yote),
Ununuzi wa Ndege,
Kupunguza Matumizi Serikalini,


HIVI CDM kweli zinawatosha!
 
Kwa uchache tu nawakumbusha kwamba CCM kupitia Ilani yake imefanya mengi mazuri - kwa ufupi tu:-

REA II, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa umeme sababu ya kuwa upinzani)?
TASAF III, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa fedha za TASAF sababu ya kuwa upinzani)?

Ujenzi wa flyover Dar, (
Je, leo kuna Mwana CDM anayekatazwa kuzitumia sababu ya kuwa upinzani)?

Serikali kuhamia Dodoma, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa huduma sababu ya kuwa upinzani - hatuoni pia kiasi cha fedha kilichopungua sababu ya huduma kuwa karibu)?

Mikopo ya wanafunzi Elimu ya Juuu, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa mkopo sababu ya kuwa upinzani)?
Elimu Bila Malipo (Shule za Msingi na Sekondari), (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa fedha sababu ya kuwa upinzani)?


Ulinzi na Usalama wa Nchi, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa ulinzi sababu ya kuwa upinzani)?
Uwajibikaji kwa Taasisi za Umma, (Je, leo kuna Mwana CDM anayenyimwa huduma ofisini sababu ya kuwa upinzani)?

Makusanyo ya Ndani/Mapato ya Serikali, (Kuna Mwana CDM anayezuiwa kutumia miundombinu inayojengwa kwa kuwa ni mpinzani)?

Ujenzi wa Barabara za Lami (Mikoa yote), (Je, leo kuna Mwana CDM anayezuiwa kutumia barabara sababu ya kuwa upinzani)?

Ununuzi wa Ndege, (Je, leo kuna Mwana CDM anayezuiwa kusafiri au kusafirisha sababu ya kuwa upinzani)?

CHADEMA WEKENI AKIBA YA MANENO WAKATI CCM WAKITEKELEZA ILANI - NI KWA MANUFAA YA TAIFA (TANZANIA)
 
Kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2015-2020).

1. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi itatenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji, badala ya kupewa milioni 50 wamachinga ndio wanaichangia serikali elfu 20,000 kwa kila kitambulisho.

2. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi itahakikisha wananchi wanaopakana na miundombinu ya gesi na ambako bomba la gesi linapita wananufaika na gesi. Walichoambulia wananchi ni kuona alama za njano bomba linakopita na virungu vya polisi.

3. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kuhamia Dodoma kabla ya 2020 tukaambiwa kufikia Desemba 2018 Rais atakuwa Dodoma, hadi leo namuona bado yupo Dar.

4. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kuongeza kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati kutoka 1,300MW hadi 5,000MW ifikapo 2020. Sina uhakika hata megawati 2,000 zimefika.

5. Ilani ya CCM: Serikali inaahidi kipaumbele kitakuwa katika kukuza na kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Leo hata aliyeanzisha wimbo wa Tanzania ya viwanda anaona aibu kutamka mbele za watu.

6. Ilani ya CCM: Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, serikali ya CCM itaendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa na ufisadi. Leo CCM imerudi kuwakaribisha Mafisadi papa waliowakataa 2015 akiwepo fisadi mkuu Lowassa.

7. Ilani ya CCM: Serikali ya CCM itahakikisha thamani ya Shilingi yetu inatengamaa. Leo 1USD = 2400TZS.

8. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inaongeza mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi. Leo mazao ya Korosho na Mbaazi yamekosa soko.

9. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inasimamia Deni la Taifa liendelee kuwa himilivu. Leo Deni limekua toka 35T walivyolikuta hadi 50T.

10: Ilani ya CCM: Serikali itasimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria na miongozo ya ununuzi wa umma, ukaguzi na kusimamia mali za Serikali. Tumeshuhudia Issue ya CAG na 1.5t, ndege zimenunuliwa bila kufuata kanuni ya manunuzi, uwanja wa ndege wa chato umejengwa bila bunge kuidhinisha bajeti yake.

11. Ilani ya CCM: Serikali itahakikisha inajenga zahanati kila kijiji, kila kata kuwa na Kituo cha Afya na kujenga hospitali kila Wilaya. Hili sina uhakika ngoja nimtag Waziri Ummy Mwalimu anaweza kuwa na takwimu.

Kama huu sio ulaghai kwa wananchi ni nini.

Ngoja niishie hapa, Mambo ni Mengi, muda Mchache.

Hizi ni facts anayepinga aje na data.


Lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasambaratisha wapinzani wake, iwe kwa hiari au kwa lazima
 
Back
Top Bottom