Chama cha Mapinduzi
Member
- Aug 8, 2013
- 10
- 33
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
1. Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wa kuwachagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani imeandaliwa ikiwa ni mkataba kati ya CCM na wananchi.
Ilani hii imeandikwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mwelekeo wa Sera za CCM zenye lengo na nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020).2. Ilani hii ni tamko maalumukwa wapiga kura kuhusu nia ya CCM ya kuendelea kushika dola na kuwaongoza Watanzania kwa njia ya kidemokrasia, na hasa kuendelea kudumisha amani, umoja wa Kitaifa, usawa, ustawi wa wananchi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
3. Nia na uwezo wa CCM wa kuendelea kuongoza Taifa hili unajidhihirisha katika uzoefu ambao tumeupata kwa miaka 38 tangu kuanzishwa kwake na kuwa madarakani, ambapo katika kipindi chote hiki kimeiwezesha nchi yetu kupata mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
4. Katika miaka mitano ijayo (2015-2020),CCM ikiwa madarakani, itazielekeza Serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne:-
Kwanza kuondoa umaskini; pili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; tatu kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na nne kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.
Vipaumbele:
1. Elimu
2. Afya
3. Kilimo
4. Miundombinu
5. Utawala bora
6. Mawasiliano
Angalia attachment...