IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Kikwete anatakiwa amtimue salva mara moja; asitake tumpe sababu..

Kwanza kamsemea mambo yake personal ya baadaye, kwa kusema Kikwete hajawahi, na wa wala hatakuja kuwa mmiliki wa Dowans. Amejuaje mipango binafsi ya Kikwete.

Salva sasa ajiangilie na matamshi yake itafika mahala kila mtu ataufahamu uwezo wake kwamba hatakiwi kufanya kazi ikulu na maamlaka husika zikishindwa kumuondoa kutoka katika ikulu ambayo kimsingi ni mali ya wananchi. Hii inaweza kupelekea watu wachukue sheria mikononi kwa kumuadhibu Salva anachefua sana kwanini hataki kukaa kimya ili heshima yake isichakachuliwe?.
 
Ndugu Nsiande,unapotosha mada,ingefaa uweke post yako na utueleze kwa uzuri ili sie watz tusiolewa tujue kila kitu kuhusu dowans. Unasema rais anaweza kumteua mkurugenzi wa tanesco,una maanisha kuwa Board ya Tanesco haina mamlaka kwa ilo?Kila mtu anajua kuwa rais ana power zote na pia hata kutamka Nsiande hakamatwe na kuwekwa kizuizini bila kutoa sababu kwa umma lakini haimaanishi kuwa atatumia iyo power kutenda atakapojisikia sawa mkuu? Alaf kama unasema Dowans unaijua vizuri na wewe ulihusika kwenye Commission,kwa nini usiwe huru kuwataja hata wamiliki?mpaka dr.Slaa aseme. Nyie ndo watu tunaotaka mliongoze taifa lakini mnakaa nyuma ya hoja za watu,je taifa liwaeleweje? Come on,tetea wananchi bila woga!
Sijasema naijua dowans vizuri kwa maana ya wamiliki, naijua kama mitambo kwa maana ya mtaalamu..naomba tutofautishe hapo...

Naomba usome articles of association zinazoiunda tanesco na unitajie ni nani ana mamlaka ya kumchagua mtendaji mkuu, board ya wakurugenzi inapendekeza na inaweza pia kuchagua ila Rais ndiye mwenye dhamana hiyo

Naomba usijibu kwa jazba jibu kutokana na yale niliyoyachambua ndugu yangu, polepole tutafika
 
RUTASHUBANYUMA, I would like to respond to your first post by giving facts ili tuwekane sawa tafadhali

A. Sheria inayounda mashirika ya umma inampa rais uwezo wa kuteua mtendaji mkuu wa shirika, hivyo uteuzi wa Dr Rashidi haukukiuka sheria yoyote, hoja kama ana uwezo ama hana ni nyingine

B. Dr Rashidi hakuidhinisha Richmond, aliingia jan 2007 na Richmond iliingia 2006 na walioiingiza si TANESCO ni Govenrment Negotiating Team, tume ya Mwakyembe imeainisha hilo.

C. Walichofanya Richmond baada ya kukosa uwezo ni kuwapa ile tender Dowans , na baraka zote from GNT

D. Dowans haikupitia kwenye Tanesco tender board bali GNT

E. TANESCO opted for Dowans because its already connected to the grid and cheaper than IPTL, all they did was to ask for permission to buy it and not 'kushinikiza' kwa mwenye kujua biashara ya umeme, kutembeza. IPTL ni billion 11 hali Dowans ni billion 2, kama mtu ni mfanyabiashara unaopt kilicho more reasonable cost ways..bei tajwa haikuwa mara 20 kwani haikuwa discussed sijui mwenzangu umepata wapi hii data ?? I commissioned Dowans and am involved in consulting change of IPTL from heavy fuel so I know what am talking about, DOWANS is better off (then )

F.ukiisoma judgement ya ICC utaona si TANESCO waliovunja mkataba ni dowans !! Walivunja na kushtaki TANESCO, thts why mitambo ilishikiliwa kwa kadhia ya kodi..

G, H and I siwezi kuyaongelea, Dr Rashidi amefanyia mengi TANESCO, ashtakiwe kwa mambo aliyofanya prior to TANESCO and not whilst there

Nimeona tu nirekebishee hii ili tujue ukweli uko vipi, kama una ya kuongezea karibu sana ila tunyooshane kwa amani
Mhandisi mifumo na njia kuu za umeme Nsiande.
Eng. Nsiande nimependa jinsi ulivyoeleza lakini, naomba nikuulize kitu hata kama rais hakuvunja kipengele chochote cha sheria kwa nini asiache sheria ikachukua mkondo katika upatikanaji wa Dr. Rashid mpaka amteue yeye mwenyewe. Hata JK hakuwa na lengo baya na Dr. Rashid lakini kutokana na mchakato ulivyo unaibua maswali mengi ingawaje Dr. Rashid ni mengi ameyafanya Tanesco na hata alipoondoka baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco walionyesha kusikitishwa.

Mpaka ifikiwe rais anasingiziwa kuwa ndiyo miliki wa Dowans, na yeye ikiwa hana maslahi inakuwaje hapo? Yaani ninavyofahamu, mtu ikifikia hatua ya mtu kukashifika kwa niaba ya watu wengine inatia mashaka, uubebe msalaba wa mtu mwingine wakati wewe wa kwako unakushinda!!!!! Eng jiulize kwa makini najua wewe unajua mengi kuliko mimi kutokana na jinsi ulivyoandika lakini hapa rais wetu lazima asikubali kuangikwa msalabani kwa kisingizio cha siri ya nchi, aweke wazi vinginevyo naye ataonekana ana maslahi.
NI MTAZAMO TU.
 
[FONT=Book Antiqua, serif]Sawa mkuu Salva tumekuelewa sasa ni nani mmiliki wa DOWANS atakayeenda kupokea sh 185bn?
[/FONT]

Nenda BRELA au Chamber of Commerce, hiyo si kazi ya Salva.
 
Kwa walaka huu, Tanzania imeishiwa . kama ilkulu inaweza kuandika kwa mtindo wa kusutana kama huu..

Mh naogopa huko tuendako!

Ni uchemfu wa hali ya juu!
NADHANI SI LAZIMA KUJIBU KILA HOJA, KAMA HUNA UWEZO WA KUTOA HOJA
 
Sometimes nashindwa kuelewa Ikulu yetu ina-operate vipi. Hivi nani anaweza kuwaweka sawa hawa jamaa?

Angalia anachoandika Salva:

....[FONT=Book Antiqua, serif]hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

Salva, angetoa kauli hiyo nani na ninyi mkubali kumjibu au kuja out clean?

You mean ukishagombea urais basi unatakiwa kukaa kimya kwenye mambo ya msingi ati unalinda Status Quo? Unataka kutwambia kuwa huelewi kwanini Slaa katumia njia hii mbadala kusababisha walau mtoe kauli yenu juu ya DOWANS?

[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]

Kauli hizi tulizisikia toka KWAKO wakati wa EPA, baadae mkaanza mazingaombwe! Mtu gani si wa hatari kwa taifa hili kwa upande wenu? Unataka 'kutunywesha' kuwa ili kuwa muungwana kwa taifa lako hutakiwi kumnyooshea kidole rais aliye madarakani?

[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]

Salva bro, WE will prove you wrong soon... Amini usiamini! Watch this space

[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]

Hizi kauli hizi...!

Sasa, ni upi msimamo wa rais (si wewe Salva) juu ya DOWANS?

Baada ya Dr. Slaa kumsingizia Mhe. Rais (kitu ambacho hata mimi kimenikera SANA), mheshimiwa Rais anatwambia nini juu ya dudu hili (DOWANS), ni la nani haswa? Ni nini hatma ya taifa katika mgawo ambao unaendelea nchi nzima?

Well, huu uzushi wa Slaa tuuweke kando, vipi mnatudanganya kama vile sisi hatujaiona hiyo hukumu ya ICC na mnataka kutuaminisha kuwa kinachotakiwa kulipwa ni Bil 185.85 Tshs (hatujui nani mpokeaji); salio ni la nini lililoongezwa?

Acheni siasa kwenye mambo ya msingi, come out clean mkuu. Taifa hili ni letu sote, mnapochemka mkakosolewa kama hamna majibu sawia kaeni kimya, tutadhania mnayafanyia kazi maoni/malalamiko ya wananchi lakini kujibu kisiasa na kwa kebehi haitatusaidia kama taifa!
 
Ukiona waraka toka ikulu imepambwa na matusi kama vile KIZABIZABINA basi usisubiri sana mtu akueleze kwamba madai husika ni ya kweli kiasi gani. Taasisi ya heshima kutumia lugha za kihuni?

Kama Dr Slaa kajianzia tu uongo usio na msingi wowote basi hata nayo ikulu inahaki ya kutafuta sheria mahamani kuilinda na wala si kuandika lugha pungufu ya STAHA na kuisambaza kwa vyombo vya habari.

Mwandishi wa habari mwandamizi na mwenye historia inayoheshimika katika taaluma yake kama Dr Salva Rweyemamu alishindwa vipi kujizua na roho yake kutilia sahihi yake lugha kali kiasi hicho kwenda kwa jamii!!!

Muongo lazima umsute kwa lugha kali, Slaa kuitwa kidhabidhabina si tusi. Kidhabi maana yake ni muongo na dhabina wa waongo. Kwa hiyo, kidhabidhabina ina maana muongo wa waongo. Au huoni uongo wake wa kuwazido waongo?

Leo kafikia mpaka kudanganya kuwa Rais ndie mmiliki wa Dowans? Haaa, anashangaza kidhabu mkubwa huyu.
 
wakuu mi nilijua nasoma lyrics za taarabu kumbe msemaji wa ikulu..tuhuma nzito kama hiyo haihitaji majibu ya mipasho,wamuweke hadharani mmiliki halisi watutoe kwenye hili giza,sio kumponda docta slaa bila kutupa majibu sahihi kwenye maswali magumu..kumbuka Epa,Eptl,kagoda..list ya top 10 ya mafisadi ..wanatoa majibu rahisi afu ukweli unawaumbua...
 
Huyu ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu yet he can't even spell jina la kwanza la DK. SLAA, eti anamuita "Dkt. Wilboard."

Pia kusema "Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana," ni ushabiki wa kitoto wa kisiasa ambao tulitarajia mtu kama Yusuf Makamba au Tambwe Hiza wa CCM wayasema, si mkurugenzi wa Ikulu. It's quite astonishing!
 
Ikulu imejaza wendawazimu?

Mtoto wangu wa miaka mitano anayesoma St. Joseph hapa Marekani hawezi kuandika upumbavu usio na mashiko kama huu wa Salva. Salva angesema Mumuiliki ni nani na akatoa sababu sahihi zenye kuchanganua masuala vizuri zinazoweza kutushawishi kuona kuwa Dr. Slaa kweli kapotosha Umma.

Salva ameonesha ujinga ulioko kichwani mwake na ameshindwa kushawishi watanzania kuhusu Dowans. ....
Salva amesahau kabisa kuwa Kikwete alihusika bila hofu kwenye maamuzi ya kuiweka Dowans. Watanzania hatusahau haraka hivyo ila naomba sana Rweyemamu arejee kwenye hotuba za Kikwete na rekodi za Bunge ndo ataona ushiriki wa Kikwete kwenye maamuzi ya Richmond na Dowans.

Ni uzembe kweli............
 
Ikulu ijishushe kiasi hiki kwa kufurumsha MATUSI, VITISHO, KEJELI na MASHAMBULIZI YA WAZI dhidi ya Dr Slaa kama raia aliye na uhuru wa kutoa mawazo yake?

Kama mawazo yake si ya kweli kwa nini ikulu itafute kuchukua sheria mkononi kutafuta KUMUADHIBU Dr Slaa kwa kumfanyia mashambulizi ya maneno yenye kutafuta kumdunisha na kudhalilisha mbele ya jamii ilhali mahakama ipo na Tanzania tunadai kufuata utawala wa sheria?

Kwa nini Ikulu haisemi Balozi Maajar alioko kwenye balozi yetu nchini Marekani uteuzi wake ni ZAO LA 'KAZI ZURI' ALIYOMFANYIA MHE KIKWETE kuwaibia Watanzania walipakodi fedha kupitia Dowans.

Sijui huko aliko ataficha wapi sura yake huyu mteule wa mgongo wa Dowans Wamarekani wakilifahamu hili!!!
 
Salva mdogo wangu - Ipo siku ukweli utafahamika na wewe utakuwa wa kwanza kupigwa pingu - Hiyo ndiyo tabia ya historia!
Amesahau ya Celina Kombani na Werema, wanakimbilia kutoa matamko huku mhusika yuko kimya anasikilizia. Salva atatafuta mahali pa kujificha siku JK atakapobanwa na kukubali kuwa ana hisa Dowans, kama alivyobanwa na kukubali katiba mpya na kuwaacha akina Selina wasielewe nini cha kusema tena!
 
Eng. Nsiande nimependa jinsi ulivyoeleza lakini, naomba nikuulize kitu hata kama rais hakuvunja kipengele chochote cha sheria kwa nini asiache sheria ikachukua mkondo katika upatikanaji wa Dr. Rashid mpaka amteue yeye mwenyewe. Hata JK hakuwa na lengo baya na Dr. Rashid lakini kutokana na mchakato ulivyo unaibua maswali mengi ingawaje Dr. Rashid ni mengi ameyafanya Tanesco na hata alipoondoka baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco walionyesha kusikitishwa.

Mpaka ifikiwe rais anasingiziwa kuwa ndiyo miliki wa Dowans, na yeye ikiwa hana maslahi inakuwaje hapo? Yaani ninavyofahamu, mtu ikifikia hatua ya mtu kukashifika kwa niaba ya watu wengine inatia mashaka, uubebe msalaba wa mtu mwingine wakati wewe wa kwako unakushinda!!!!! Eng jiulize kwa makini najua wewe unajua mengi kuliko mimi kutokana na jinsi ulivyoandika lakini hapa rais wetu lazima asikubali kuangikwa msalabani kwa kisingizio cha siri ya nchi, aweke wazi vinginevyo naye ataonekana ana maslahi.
NI MTAZAMO TU.

Mzee wa rula asante kwa maswali yako mazuri ambayo mimi kama mimi, sina majibu sahihi, ila nina majibu ya kifupi kama yalivyoainishwa na bodi baada ya uteuzi huo wa dr Rashidi,

Kilichosemwa ni kuwa rais amemteua mtanzania kuendesha shirika kutoka netgroup management , ili kurudisha imani kwa wafanyakazi na raia wanaofaidika na nishati, aidha rais alisitisha mpango wa kuibinafsisha tanesco hivyo aliamua kuteua mchumi kutoka nje ili alikwamue shirika lililokuwa linasuasua kiuendeshaji na linalojiendesha kwa hasara,

Ukiangalia baada ya uteuzi huu, hasara ya shirika imeshuka toka bil 65 (sina hakika ) mpaka bilioni 5 kufikia mwaka jana lakini tovuti ina maelezo sahihi

Mzee wa rula, mimi kama mtanzania mwenye uchungu na nchi siafiki dowans kulipwa, ila kama technical person naafiki ununuzi wa dowans ambayo tayari iko kwenye gridi na napinga kugeuza iptl kwa gharama kubwa ambayo ni chakavu zaidi ya dowans, hapa nimeongea tu kiufundi kwani nimefanya kazi kwenye mashine zote...naomba nieleweke tu kuwa ninachokiandika ninakiona kwa macho ya ufundi na kwa faida, ila sifagilii mafisadi katu.
Ni hayo tu baba,
 
Muongo lazima umsute kwa lugha kali, Slaa kuitwa kidhabidhabina si tusi. Kidhabi maana yake ni muongo na dhabina wa waongo. Kwa hiyo, kidhabidhabina ina maana muongo wa waongo. Au huoni uongo wake wa kuwazido waongo?

Leo kafikia mpaka kudanganya kuwa Rais ndie mmiliki wa Dowans? Haaa, anashangaza kidhabu mkubwa huyu.

We are talking about the true liberation of this poor nation BUT you are talking and fighting about your fanaticism! Dude Tanzania ni ya Watanzania siyo ya Wahuni wachache na wenye interest zenye hidden agendas like yours! time to be serious! you cannot refute the truth!
 
Mahali kama Ikulu na majibu yanayotoka kwa hawa watendaji napata mashaka na 'usafi' wa hii ofisi..
 
Ningependa wampeleke mahakamani wasiiyeyushie kwenye magazeti tu.. kama amechafuliwa raisi wao wampeleke Dr Slaa mahakani wamshtaki.
 
From: "Salvator Rweyemamu" rweyemamu.salvator@gmail.com
Date: Sun, January 2, 2011 11:29 pm
Subject: On Dkt Slaa na Madai yake dhidi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu Dowans


Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana.

Huyu kweli ni mkurugenzi wa habari wa ikulu?? Yaani hata mtiririko wa wakati unachakachuliwa kusisitiza upuuzi, navyofahamu mimi uchaguzi ulifanyika October 31, 2010.

 
Back
Top Bottom