IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Kama kweli serikali inawafahamu wamiliki wa Dowans haitoshi tu kusema kuwa JK siyo mmiliki wa Dowans na kwamba Dr. Slaa ni mwongo.

Je kutuambia wamiliki wa Dowans kutaigharimu nini serikali? kuna siri gani katika kuwataja hao wamilki?

Dk. Slaa aishika pabaya Ikulu

• Yatumia maneno ya kejeli, mtaani kujibu hoja zake

na Edward Kinabo

KURUGENZI ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumtaja rais Jakaya Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.

Taarifa kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu ‘aliyechanganyikiwa' na ‘mzabinazabina' ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.

Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima alikwenda mbele na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.

Sehemu ya maneno makali ya Rweyemamu kwa Dk. Slaa ni kama yale aliyosema, "Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii."

Rweyemamu aliendelea kueleza, "Kama Dk. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachane na tabia ya kutapatapa na uzabinazabina yenye lengo la kuwapaka watu watope."

Ikulu ambayo katika mazingira ambayo si rahisi kuyaeleza imekuwa na desturi ya kukanusha kwa nguvu kubwa kila wakati jina la Rais Kikwete linapohusishwa na sakata la kashfa ya Richmond/Dowans.

Hii ni mara ya pili kwa Ikulu kufanya hivyo baada ya mara ya kwanza kuchukua hatua kama hiyo wakati Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alipokanusha hoja zilizokuwa zikijaribu kumhusisha Rais Kikwete na uhusiano wake na mkataba wa Richmond.

Wakati Ikulu ikikanusha mara kwa mara kuhusishwa kwa Kikwete katika sakata la Richmond/Dowans kwa namna yoyote ile, upo ushahidi wa kibunge (rejea ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe) unaoonyesha kwamba, maamuzi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri lililokuwa chini ya uenyekiti wa rais mwenyewe.

Kama hiyo haitoshi, gazeti moja la kila wiki linalomilikiwa na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambalo Rweyemamu amepata kuwa mmiliki wake, limepata kuchapisha katika ukurasa wake wa mbele barua ikionyesha barua aliyoandika aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu suala la Richmond ambayo nakala yake ilikwenda pia kwa Rais Kikwete.

Uamuzi wa jana wa Rweyemamu kuandika taarifa kali dhidi ya Dk. Slaa unakuja siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya kibiashara hivi karibuni kuamuru Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kuilipa Dowans fidia kubwa baada ya kuvunja mkataba nayo kinyume cha taratibu.

Katika mahojiano maalum na gazeti Tanzania Daima Jumapili, la juzi Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala zima lililopelekea Dowans kutakiwa kulipwa fidia hiyo ni uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe kwani ndio waliohusika katika kuileta kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

Ikulu katika taarifa yake hiyo kwa sababu zisizojulikana ilijikuta ikipotoka ama kwa makusudi au kwa kutojua ilipoeleza kuwa gazeti la Tanzania Daima lililonukuu maelezo ya Dk. Slaa, linamilikiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati taarifa zilizopo kwa msajili wa magazeti zinaeleza bayana kwamba, gazeti hilo ni la watu binafsi.

Ikipinga maelezo ya Dk. Slaa kuhusu uhusiano wa rais Kikwete na Dowans, taarifa hiyo ya Ikulu ilisema, "Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dk. Slaa

"Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa kampuni hii." Ikitumia lugha kali dhidi yake Ikulu iliwataka wananchi wampuuze Dk. Slaa ikidai kuwa ni mzushi na amechanginyikiwa.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Dk.Slaa kuitwa mzushi na vigogo wa serikali kwani mara kwa mara anapoibua maovu amekuwa akipingwa kwa kuitwa jina hilo ingawa anayoibua huthibitika kuwa na ukweli ndani yake.

BARUA YA SALVA KWA VYOMBO VYA HABARI HII HAPA

From: "Salvator Rweyemamu" rweyemamu.salvator@gmail.com
Date: Sun, January 2, 2011 11:29 pm
Subject: On Dkt Slaa na Madai yake dhidi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu Dowans

Hi wakubwa

This is important in terms of kuweka ukweli sawa. Tunaomba msaada wenu kwa mujibu wa shughuli zetu za habari. Best regards na usiku mwema.


Salva




[FONT=Book Antiqua, serif]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU.



[FONT=Book Antiqua, serif]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilboard Slaa, leo, Jumapili, Januari 2, 2011, amekaririwa na Gazeti la Tanzania Daima, linalomikiwa na chama chake hicho, akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dkt. Slaa na hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Sababu ni rahisi sana. Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kama Dkt. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachae tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope. Tabia ya kuwasingizia na kusema uongo kuhusu viongozi wa taifa letu ni tabia ya hatari.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kiongozi huyo wa upinzani ametoa shutuma zake dhidi ya Rais Kikwete kufuatia Kampuni ya Dowans kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na Mahakama hiyo ikaamua kuwa Dowans ilipwe kiasi cha sh bilioni 185.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Dkt. Slaa amezomoko na kumshutumu Rais Kikwete eti kwa sababu Mheshimiwa Rais hakuzungumzia suala hilo katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Ijumaa iliyopita.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Imetolewa na Salva Rweyemamu – Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu[/FONT][/FONT]
 
sa huyo rweyemam, mkwere na mafisadi wenzao,kama hawahusiki basi si wawataje kwa majina wamiliki wa kampuni hiyo? Waache jazba waongee ukweli tu ndio tunao utaka kwa sasa.
 
Jiwe la Slaa limegonga palipotakiwa, watetezi wa ikulu watachoka kupaka rangi ukuta unaobomoka.
 
Hii habari kwenye gazeti la Tanzania Daima badala kusema Salvatory Rweyemamu aliwahi kuwa mhariri anayeheshimika, lingesema kuwa Salvatory Rweyemamu aliwahi kuajiriwa na Richmond kufanya kazi ya Public Relations kusaidia kuijenga Richmond/Dowans kwenye media ya Tanzania.

Salva pia alihojiwa na kamati ya Bunge iliyoongozwa ya Mwakyembe na kukiri kuwa yeye alitambulishwa kwa Richmond/Dowans na Rostam Aziz.

Hizi kumbukumbu zote ziko kwenye ripoti ya Mwakyembe.
 
Kumekucha!!!mwaka huu kitaeleweka mwanzo mgumu lakini tutafika. Wewe rweyemamu kama sio kikwete basi ni wewe!!tajeni wahusika mbona kigugumiza kwa sana. rweyemamu kasome document imetolewa na MM halafu uje hapa utueleze uongo wako nya......
 
Jamani mbona kila baya awe anasukuwa tu JK, tatizo ni nini hasa ndugu zetu?

Hii sasa inafika mahali mpaka inaudhi kweli. Ndiyo maana tangu sasa bora ikulu iwekiwaporomosheeni matusi ya nguoni hivyo ndiyo mkome na umbeambea wenu huo.
 
hawana jeuri hiyo, wataishia kutukana tu na kujifanya watakatifu,ila tumeshawasoma hata waseme Dr slaa ni kichaa wa kwanza duniani hatuwaamini,kwani huyo rweyemam na mkwere pamoja na mafisadi woote ndio vichaa,wezi, majangiri na wachakachuaji.
 
Saliva bado anazunguka zunguka kwenye anga za Dr? asubiri tuje tumuangushie kombora. Shauri yake. Ajipime ubavu wake kwanza na kifua chake kama kinalingana na DR wa ukweli!
 
Hawa wanahabari wa ikulu mbona wanapenda sana ngonjera? Kwa nini hawampeleki mahakamani Dr. Slaa na kuuthibitishia umma kwamba Slaa ni mwongo? Na lugha hiyo kama ni kweli imetumika basi kazi tunayo!
 
Wameibuka haraka sana katika kutetea, lakini kutwambia nani ni mmiliki/wamiliki wa Dowans inakuwa kizungumkuti. Kazi Kweli kweli!
 
Wameibuka haraka sana katika kutetea, lakini kutwambia nani ni mmiliki/wamiliki wa Dowans inakuwa kizungumkuti. Kazi Kweli kweli!

Hapo ndiyo kazi ilipo, ila inachekesha kuona kwamba hawa jamaa wa ikulu siku zote ni kuwa defensive tu hakuna kutoa ufafanuzi!
 
Silva is talking the obvious! Hakuna aliyetegemea aseme ni kweli Ikulu inathibitisha Mkwere ndiye mmiliki mkubwa wa Dowans! Hahahahahaahah
 
Ndiyo hapo Dr Slaa atakapoibuka na more info kuhusu kauli yake aliyoitoa.
 
Ndiyo hapo Dr Slaa atakapoibuka na more info kuhusu kauli yake aliyoitoa.

Unajua hawa akina Salva bado wanaishi kwenye fikra za kikomunisti wakati huu, they don't see kwamba mabadiliko ni makubwa sana leo hii na propaganda hazina nafasi na kama ipo basi it has to be carefully cultivated. Hawa jamaa nadhani bado wanafikiri watanzania wa leo wakisikia Ikulu wanaogopa kama ilivyokuwa enzi za Julius........ Kwamba ikulu ikisema ni mwisho hakuna wa kuhoji.
 
Hiyo wala si lugha kali kama watu wanavyotaka kusema. Lakini kama mtu angesoma ila Tz Daima between lines, hakuna sehem ambayo ilimuhusisha Kikwete kwamba ndiye mmliki zaidi ya Title.

Habari ilikuwa by implications na ile ilikuwa ni politics. Kwa bahati mbaya Ikulu nao wameingia na sasa watakuwa wanafanya kazi ya kukanusha. Wangekaa kimya na wakaishughulikia DOWANS kivingine wangepata heshma zaidi kuliko kuhangaika kukanusha.

Kiuhalisia Kikwete hawezi kuwa mmiliki ila by implications.
 
Hiyo wala si lugha kali kama watu wanavyotaka kusema. Lakini kama mtu angesoma ila Tz Daima between lines, hakuna sehem ambayo ilimuhusisha Kikwete kwamba ndiye mmliki zaidi ya Title.

Habari ilikuwa by implications na ile ilikuwa ni politics. Kwa bahati mbaya Ikulu nao wameingia na sasa watakuwa wanafanya kazi ya kukanusha. Wangekaa kimya na wakaishughulikia DOWANS kivingine wangepata heshma zaidi kuliko kuhangaika kukanusha.

Kiuhalisia Kikwete hawezi kuwa mmiliki ila by implications.

The genie is out of the bottle...they're simply clutching at straws!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom